NILIVYOBEBA MIMBA YA KAKA YANGU WA DAMU
Sehemu 12 – 13
Ilipoishia…… Daktari akanipeleka maabara na kuanza vipimo vyake, baada ya kumaliza akawa ameniambia nitoke nje amalizie, nikatoka nje nikiwa nimemuacha anafanya uchunguzi wake… Nikawa nje kwa muda mrefu sana, baada ya muda akaniita nikaingia ndani huku nikiwa na shauku kubwa ya kujua kilichoendelea… Songa nayo…Nilipofika nikaketi kwenye kiti kisha kumtazama kungoja majibu ya uchunguzi wake, “Binti unamme?” Nikajiuliza kwanini ameniuliza hivyo ila sikuelewa kabisa, nikawaza nilimwambia sina ataniona Malaya kama nikiwa na mimba.. “Ndio ninae ila leo asubuhi amesafiri kwenda mkoani kikazi” “Ohoooooo!! Hongera sana, maana jana usiku aliacha ameweka historia mpya ” “Kwanini dokta ” “Sijajua inawezekanaje, mimba changa ambayo ndio inaanza kutunga kuonyesha dalili zake?, jana yai lako na mbegu ya mmeo zilikutana na hatimaye kutingisha mimba .” “Jana???” Sio kwamba nilimuuliza sijaelewa alichozungumuza ila ni kwasababu jana nimelala na kaka yangu wa damu, kwahiyo nina mimba ya kaka.. Palepale daktari akanipatia ripoti ya majibu yangu….
Nikatoka nje nikiwa na mawazo mengi sana, nikawa najiuliza imekuwaje mimi na kaka tukutane jana harafu leo mimba ionyeshe dalili hapo nikatambua kama laana imeanza kunitafuna mapema… Taratibu za mimi kuondoka zikaanza, nikamlipa daktari kwa huduma yake nzuri kwangu… Nikaondoka huku mawazo yakiwa mengi sana kichwani kwangu, nikaelekea chuo na kukaa kwenye garden ya chuo iliyokuwa karibu… “Haya, umebana mimba ya kaka yako wa damu, unajisikia je ” Nikageuza kichwa changu kumtazama huyo aliyenisemesha maneno hayo na amekua vipi.. Nilipogeuka ilikuwa uso kwa uso na mpenzi wangu Brown, “Brown” “Nini!! Kwamba nadanganya, nimekufuatilia mpaka hospitali na yale maelezo ya dakitari nineyasikia yote, nikaunganisha na ile video niliyo itazama kwa kijana wa taarifa za chuo ” Kijana mwenyewe wa taarifa za chuo ndie yule kijana aliye narekod na kuniambia kama sitakubali kulala naye basi ataisambaza video ile..
Brown akaendelea kuongea baada ya kuona nipo kimya.. “Upo huru, nimeisha ifuta ile video kwenye simu ya kijana wa taarifa za chuo, na haipo kabisa””Asante sana Brown ” “Ok!! Kuanzia leo mimi na wewe mahusiano yetu basi, nenda kapambane na laana yako upo huru sasa” Baada ya kuongea hivyo, ghafla simu yangu ikaita.. “Hallow, wewe ndie Victoria nduguye na Amani” Sauti kwenye simu akauliza hivyo “Ndio mimi!!” “Ok haraka wahi hapa hospitali, kaka yako amepata ajari mbaya sana ya gari” “Hospitali gani ” “Washa location kisha fuatilia location ninayo kutumia sasa hivi ” “Sawa” Haraka nikaelekea hospitali huku nyuma nikifuatiwa na Brown, tukapanda bodaboda ili tuwahi haraka… Tulipofika hospitali, nikawa nimekutana na daktari.. “Samahani daktari ndugu yangu anaendeleaje” “Hapa tunawagojwa wengi sana ndugu yako nani” “anaitwa Amani, nimeambiwa amepata ajari na amefikishwa hapa mda sio mrefu ” Daktari hakashtuka kiasi, kisha akanikamata mkono huku akitazama wodi moja . Na mimi nikaitazama sana, palepale mlango ukafunguka.. Nilichokiona!!!!
Sehemu 14 – 15
Ilipoishia…… Daktari hakashtuka kiasi, kisha akanikamata mkono huku akitazama wodi moja . Na mimi nikaitazama sana, palepale mlango ukafunguka.. Nilichokiona!!!! Songa nayo… Mbele ya macho yangu nikashuhudia, maiti ikitolewa kwenye kile chumba, hapo nikaunganisha matukio na ile hali ya dakitari kutazama wodi ile kishaa kunikamata, hapo nikajua chungu imekua chungu mara mbili..Wakati maness wanausafirisha mwili ule ambao nilikuwa nahisi itakuwa ni mwili wa kaka, palepale kitambaa kikaanguka na mwili wa kaka nikashuhudia mbele ya macho yangu.. Moyo yakaripuka kwa maumivu, nikataka kuukimbilia ila ikawa ngumu maana daktari alikuwa amenikata kwa nguvu.. Nikaendelea kuleta vurugu hapo ndipo Brown naye akanikamata kwa nguvu sana , hapo ndipo nguvu za kukimbia zikaisha kabisa maana nilibanwa..
Nikatoka pale kwenda nyumbani, ndugu zangu upande wa baba na mama wakaja, marafiki na kaka nao wakasogea pia ili kushirikiana na mimi kumpumzisha kaka Amani… “Ilikuwaje ukalala na kaka yako” Lilikuwa swali kutoka kwa mpenzi wangu Brown.. Nilimtazama na kuanza kumsimulia kila kitu kuanzia mazishi ya wazazi mpaka kulala na kaka yangu.. “Pole sana inaoneka huna kosa ndio maana Mungu kamadhibu kaka yako kwa kifo, ila wewe nawe kakuadhibu kwa fedheha maana ulikuwa unatakiwa ukatae” “Sikuwa na uwezo Brown ” “Nitakuoa kwasababu nakupenda ila kwa sharti moja ” “Sharti??” “Yaa sharti ” “Sharti gani Brown ” “Tafuta kanusa kisha nenda katubie dhambi zako kwa kuweka wazi yote mbele za watumishi wa Mungu, kisha waombe wafute laana ya Mungu kwako, ukimaliza mimi ndie nitakuwa baba wa mtoto wako” Nilifurahi sana kusikia vile maana nilikuwa nadhani atanipa sharti la kutoa mimba ila imekuwa tofauti…
Basi baada ya mazishi ya kumtunza kaka yangu, nilielekea kanisani kwenye dhehebu la TAG (Tanzania Assemblies of God).. Nikakutana na mtumishi wa Mungu, nikaeleza kila kitu mbele ya wazee na wachungaji wa kanisa hilo, baada ya kumaliza kuelezea nikaona kumpokea Yesu kisha nikaombewa sara ya toba .. Baada ya hapo, wanaomba na kulia kwa Mungu wakiomba laana ambazo Mungu alikuwa amezitayarisha kwaajili yangu ili kujutia na kuteseka katika laana, wanaomba sana kuwaabatilishe.. Kweli baada ya maombi nikawa najihisi mpya, mwenye amani tele ndani ya moyo wangu.. Nikaore wa na Brown huku ya kale tukitmyasahau, mtoto wa kiume akazaliwa baba na mama wa mtoto huyo akiwa ni mimi na Brown… Maisha yanaendelea tukapata mtoto wa pili wa kiume tena, na huo ndio ukawa uzao wa kwanza wa Brown lakini licha ya kumpata huyo ila bado upendo wa kweli kwa mtoto wa Marehemu Amani kaka yangu hakupunguza..
Nikapata mtoto wa tatu ikiwa imeshakatika miaka kumi na saba, tayari tulikuwa na watoto watatu, wakwanza anaitwa Alex huyu ndie mtoto wa kaka yangu aliyezaa na mimi, kwa maajabu Mungu aliyoyaonyesha, huyo mtoto alifanana sana na Brown mtu alinitazama utanisema ni mtoto wa Brown ishu inakuja wakati wa vinasaba hapo ndipo utajua hawana uhusiano wa baba na mwana, tayari alikuwa na miaka kumi na saba.. Wapili anaitwa Daudi, huyu anamiKa kumi na mbili, na wa mwisho anaitwa Lisa huyu bado anamiezi mitatu pekee yangu azaliwe.. Mungu ametusaidia mpaka sasa tunayo maisha mazuri sana, tunapendana sana.. Mwisho…
FUNDISHO UNAPO KOSEA NA KUFANYA JAMBO AMBALO KILA ANAYE LISIKIA ANASEMA HAKIKA WEWE U MJAA LAANA, SOGEA KWA MUNGU MAANA YEYE NDIE MWENYE KUSAMEHE NA KUUWISHA.. ATAKUFANYA KIUMBE KIPYA NA WALE AMBAO VINYWA VYAO VILIKUWA VINAKUDHIHAKI VITAANZA KUKUHESHIMU NA KUKUTAMKIA BARAKA.. >>MAANA YEYE HUSAMEHE NA KUKUFANYA KAMA MTU ASIYE NA HATIA.. Hesabu 14:18 BWANA ni mpole wa hasira, mwingi wa rehema, mwenye kusamehe uovu na makosa, naye hatamfanya mwenye hatia kuwa hana makosa kwa njia yo yote; mwenye kuwapatiliza wana kwa uovu wa baba zao, katika kizazi cha tatu na cha nne. >> KILICHO BORA NI KUUNGAMA DHAMBI ZAKO KWA KUTUBU, NAYE ATAKUSAMEHE, KAMA ALIVYOMSAMEHE VICTORIA KATIKA SIMULIZI YETU HII, MAANA YEYE NI MWAMINIFU.. 1 Yohana 1:9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na