NILIVYOBEBA MIMBA YA KAKA YANGU WA DAMU
Sehemu 8 – 9
Ilipoishia…… “Kwahiyo kaka yako anahitaji akuoe, au si kaka wa damu” Sauti hiyo ikapenya mpaka kwenye ngoma za masikio yangu nikaanza kujiuliza nani huyo aliyejua siri hiyo… Taratibu nikaanza kuinua uso wangu kutazama ninani ambaye amezungumza maneno hayo… Songa nayo… Nikatazama viatu vya mtu huyo vilikuwa ni viatu vyeusi vya kiume, nikazidi kupanda na kukutana na sulual ya kiume.. Nilipomtazama usoni nikakutana na sura ya kijana muhuni pale chuo.. Mara nyingi amekuwa akinihitaji ila mimi sijawahi kumkubalia hata siku moja, ninamjua vizuri ana makundi mawili, moja la wadada lingine la vijana.. Hili la vijana lilikuwa linateka watu waliokosana na kijana huyo, huku la kike likiwa la kutangaza kila uvumi ambao kijana huyo alitaka ujulikane.. Walikuwa na group lako WhatApp, hili group lilikuwa na robo tatu ya wanafunzi wote pale chuo… Kila mwanafunzi aliyejiunga na chuo hicho alipewa link kwahiyo wale wapenzi wa matukio ya chuo lazima wajiunge..
Nami nilikuwa miongoni mwa member waliomo kwenye group hilo.. Kuna zaidi ya wanafunzi 800, huku watu wa kawaida wa mtaani wakiwa 2000, jumla walikua 2800, sasa taarifa ikiwekwa humo lazima wengi wajue.. Na kama ujuavyo hakuna kituo bora cha kusambaza habari mbali mbali za kweli na za uongo kama mdomo..Sasa walio kwenye group wakishapata taarifa lazima watasambaza habari hadi kila mwana huo ajue.. Taratibu nikanyanyuka pale chini huku nikiwa nimetazama sana kijana huyo, “Bonsina” Nikamuita ila yeye hakuitika badala yake akaprey video iliyokuwa inaonyesha matukio mawili.. Tukio la kwanza ni lile la kaka kumpiga mpenzi wangu na kila kilichozungumzwa lilisikika.. Tukio la pili ni lile la mimi kutamkiwa na kaka kubwa lazima anioe, baada ya video ile kuisha akasema “Jiandae, maana hii habari ni ya moto sana, kwahiyo itasambaa, kufika jioni watakuwa wamekula wanachuo wote na wale wa mtaani pia” Nikabaki namtazama sana maana huwa hatanii husema akiwa anacheka kumbe ndio yupo Sirius… Nikawaza kumpa pesa ni ngumu maana anapesa kuliko wanachuo wote… Nikawaza nimuuombeje asiweke taarifa hizo kwenye group lao ila sikielewa kabisa, moyo wangu ukapatwa na umivu kali sana, nikatazama sana na kusema “Naomba usitangaze” Nikasema hivyo huku taratibu nikipiga magoti… “Ahaaaaa!!! Mrembo acha kupiga magoti, maana maamuzi unayo wewe, chagua, unipe penzi kila ninapo kuhitaji nisipost au niipost video hii kwenye group la kundi, harafu nimetengeneza page mpya juzi Whatsapp wewe hukuwepo maana ulikuwa bado kwenye maombolezo, ohooo pole sana kwa msiba, sasa mpaka mda huu kuna wanafunzi zaidi ya 1000, na laia wanaopenda habari za hapa chuo ili wapost kwenye page zao pia wapo zaidi ya watu 4000 kwahiyo mpaka sasa kuna watu 5000” Akameza mate na kuendelea “Chagua unipe mapenzi au niipost hii video kwenye group na page hiyo mpya” Akasema maneno yale, harafu mda huo huo akaanza kubonyeza simu yake, mara ujumbe ukaingia kwenye Whatsapp yangu, nilipomtazama alikuwa ametuma link ya page mpya..
Nikaingia na kutazama nikashangaa nakutana na habari za kifo cha wazazi wangu, emog za kulia na kuhuzunika zilikuwa 3000 chini ya taarifa hiyo… “Kama ni msiba wako umepata watu walioweka hisia kwenye post hiyo elfu tatu, unadhani page yangu haiwezi kukua nikiweka video hii na nikapiga pesa kwa wale wambea wa facebook”Nikashtuka sana kisha nikasema “Hapana naomba usinifanyie hivyo” Akaanza kwa kucheka kisha akasema “Nimesubiri jibu lako, unanipa penzi au niipost” Hapo sasa dada nimebanwa kona mbaya sana, hivi nitaweza kupona kweli?? Nilimtazama usoni nikiwa sina majibu kabisa “Na hesabu moja mpaka kumi nataka uwe umesha nipatia majibu” Akasema hivyo kisha akaanza kuhesabu… Hapo na mimi nikiwa nawaza nimjibuje nikubali au nikatae
Sehemu 10 – 11
Ilipoishia…… “Na hesabu moja mpaka kumi nataka uwe umesha nipatia majibu” Akasema hivyo kisha akaanza kuhesabu… Hapo na mimi nikiwa nawaza nimjibuje nikubali au nikatae 😥😥🤔🤔 Songa nayo… Nikajiuliza kama nikikataa basi lazima ayaanike hadharani, na akiyaweka hadharani lazima nitapata aibu na fedheha kubwa sana.. Nikamtazama alivyo kuwa anaendelea kuhesabu, nikamngoja mpaka alipofika tisa, ile anataka kusema kumi nikawa nimekubali sharti lake.. “Umechagua fungu jema Victoria” Nikanyanyuka nilipokuwa nimepiga magoti kisha nikaelekea darasani huku nikiwa na mawazo mengi sana ndani ya kichwa changu.. Nilijiuliza maisha yangu yatakuwaje, wakati nipo darasani naendelea kujisomea na mwalimu akiendelea kufundisha, ghafla nikapatwa na kichefuchefu, haraka nikatoka nje na kwenda kutapika nje. .
Hapo ndipo mdomo wangu ukawa mchungu ukawa na kichefuchefu kikubwa, nikawa nahisi kutamani vimaembe vibichi vibichi, nikazidi kuhisi natamani sana ndimu na machungwa.. Nikawa najiuliza mboga hali hiyo imenikuta ghafla, nini shida jamani…Darasani mwalimu alikuwa akiendelea kufundisha ila mimi nikawa simuelewi kabisa… Haraka nikachukua kila kilicho changu, nikakunja laptop yangu na kuitunza kwenye mkoba, kisha nikachukua simu yangu na kutoka nje bila kuaga… Safari yangu nilitaka niwlekeee hospitali kupata vipimo maana dalili zote ni za ujauzito.. Nilikuwa na mawazo mengi sana huku nikijiuliza kama ni mimba ni tani, maana siwezi kuamini eti kaka amenipatia mimba jana harafu leo nione dalili… Wazo moja kwa moja likamuwaza mpenzi wangu, nikawaza na kukishauri kama ikitokea nikakuta ninaujauzito basi mmiliki ni mpenzi wangu hakuna mwingine kabisa… Basi nikafanikiwa kufika hospital maana haikuwa mbali na kilipo chuo chetu… Basi nipofika nikawaeleza hali niliyo nayo, hali ya kutapika hali ya kuhisi kutamani kmkula vitu vichachu sana mfano maembe mabichi na marimau ndimu na machungwa..
Daktari akaniomba nimletee kiasi kidogo cha mkojo, baada ya kumletea akaanza vipimo vyake mimi nikiwa nimetoka toka nje kumpisha aendelee na uchunguzi wake, baada ya muda akaniita kunipatia majibu… “Binti” “Abee” “Sijaona tatizo, hapo inatakiwa tufanye vipimo vingine” Sikuwa na neno, nikakubali.. Daktari akanipeleka maabara na kuanza vipimo vyake, baada ya kumaliza akawa ameniambia nitoke nje amalizie, nikatoka nje nikiwa nimemuacha anafanya uchunguzi wake… Nikawa nje kwa muda mrefu sana, baada ya muda akaniita nikaingia ndani huku nikiwa na shauku kubwa ya kujua kilichoendelea…