BINTI NGUVA
EPISODE 13
Tunaanzia nyuma kidogo baada ya
Goodluck kuvaa taswira ya bibi mzee alielekea kwenye kikao cha kijiji kuhusu mauaji yanayoendelea katika kijiji hicho , kutokana na vifo viwili vilivyotokea na vilikuwa vya kutatanisha sana ambapo kila mtu alikuwa akijiuliza ni nini chanzo mwenyekiti akawa anazungumzia vifo hivyo ……
Mwenyekiti”Wanakijiji cha kasongo mauaji haya yamezidi sana watu wanauawa vibaya yaani kila siku mtu anakufa daaaah inasikisha sana mpaka najiuliza maisha haya yanaendaje pasina amani”
Lakini Alice kutazama vizuri alimuona yule bibi kizee ambaye ni Goodluck
amechukua taswira yake baada ya
kumaliza maisha yake ………..”
Alichukua kitambaa na kuanza kukiviringisha ghafla mwenyekiti akaanza kukabwa shingoni alikuwa akiishika hukua akiweka mkono wake shingoni mara macho yakaanza kumtoa na kadri alivyozidi kukiviringa mwenyekiti damu zilimtoka nyingi mdomoni alianguka chini na kufa hapo hapo mwisho . wanakijiji walirudi nyuma na kusema maneno mbalimbali mara oooooiioh jamani nini kimemkuta mwenyekiti wetu ,wengine maraaa ooooh kijiji ctu kitakuwa kina laana baadaye ilikuwa ni kama kelele .
Goodluck katika taswira ya bibi kizee
aliondoka kipindi watu wanazozana na kupiga kelele zisizo na mpangilio hofu zikiwatawala Alice alipoona bibi kizee yule akiondoka aliamya kumfuata kwa nyuma na alipofika mbele hakuweza kumuona mtu. lakini alihisi upepo ukivuma na majani yakipepeleka .
akahisi kuna mtu nyuma yake kugeuka aliliona jini hajakaa sawa likapotea na kumtokea kwa mbele yaani lilimtisha kila namna lakini alibaki akitazama.
mwisho wa siku macho yeke yalubadilika na kuwa ya rangi ya bue na alikamata moja ya majini yakiyokuwa yakimzunguka na kulipigiza ukutani na muda huo kelvin
anamtazama Alice kila sehemu
waliyokuwako watu lakini hakuweza kumwona akajisemea “kaenda wapi huyi mwanamke mbona anataka kunitia presha aliendelea kumtafuta kila sehemu lakini hakuweza kumuona ….
UPANDE WA ALICE ………
Alizidi kupambana na wale majini akiwa amesimama ghafla jini la kwanza likataka kumchoma na makucha alilikwepa na kulitupia moto likaungua na kuyeyuka hajakaa sawa likaja lingine likitokea juu ya mti likishuka kama kimbiunga alilikwepa na likajipigiza chini alichofanya nikulitupia na moto nalo likaungua na kuyeyuka hapo hapo chini .
hajakaa sawa yakawa yanakuja mawili
kwa kasi aliyakwepa na kupiga kelele moja nzito ambayo ilifanya hadi wanakijiji Masikio ya waume na yalikuwa kama yameziba fulani hivi kila mtu alichuchumaa chini na kulalamika hata kelvin naye wale majini katika vitu ambavyo hawawezi kuhimili ni hiyo sauti ya nguva ni sauti ambayo nguva hutumia kujilinda kipindi cha hatari na kipindi anafanya yote hayo huwezi amini magamba yalikuwa yameshamuota mwili mzima sema tu hakubadilika kuwa nguva kabisa ……….
***””””
Kelvin alijikaza na kufuata sauti ilikosikia maana alihisi sauti ile ilikuwa ya mtu
anayemjua lakini akiwa njiani alipishana
na mtu kavaa mavazi meusi kafunika mpaka sura yake akajisemea kimoyo moyo “mbona mtu huyu kama namjua ???” ila akasema huenda naweza nikawa nimewachanganya ngoja niendelee mbele tu
Mtu yule kufika mbele tu alivua koti lake lililokuwa na kofia ,huwezi amini alikuwa ni Goodluck . Goodluck alicheka na kusema
“hhahahahaha kelvin rafiki yangu wewe nataka nikuue kifo cha mateso yaani utakufa huku nakutazama yaaani lazima uteseke mbwa wewe” huku akafunika kofia yake na kuondoka huku akipiga Makofi kila alipokanyaga majani
yalisambaratika matawi yalianguka
kutoka juu ya mito iliyokuwa karibu na eneo alilopita ………..
kelvin alizidi kutembea kumtafuta Alice . alikuwa akitembea na kumuita kila sehemu lakini wapi alizidi kumuita lakini haikusaidia kitu Aice muda huo yupo na magamba na kabadilika na nguvu zimemuisha naogopa asije kelvin akamkuta na magamba itatakiwa ajibu maswali ambayo ilibidi ayajibu toka muda mrefu sana ….
na muda huo kelvin alikuwa akielekea kule kule aliko Alice . Kelvin alifika hadi alipo Alice hakuamini kile alichokiona je alikiona nini
EPISODE 14
Basi tunaendelea pale pale tulipoishia sehemu ya kumi na tatu ambapo kelvin alikuwa anashangaa . kilichomfanya ashangae ni baada ya kumuona Alice kalala chini …Alimsogelea kwa haraka jambo ambalo zuri ni kwamba Alice magamba yake yalipotea hivyo akarudi katika umbile la ubinadamu .Na kufanya siri yake iendelee kuwa siri lakini wanasema siri labda iwe yako peke yako ya wawili sio siri tena zaidi zaidi lazima ifichuke tumuone Alics anaweza akawa mtu wa kwanza kuficha japokuwa mzee Isnaili anajua kila kitu …….
Basi alimsogelea na kumuamsha lakini
haikusaidia kitu zaidi zaidi ilikuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gita alimbeba mpaka nyumbani kwake
Alijaribu kila namna kumtibia lakini ilishindikana ikabidi amfuate mzee ismaili na kumueleza kila kitu …..
Mzee Ismaili aliingia ndani kwake na kwenda kuchukua kitabu kimoja kilichokuwa na vumbi akakikun’guta na kumkabidhi
“Baba kitabu hiki cha nini ????” aliuliza kelvin kwa nzee ismaili. Alimwambia tu jibu fupi na la kueleweka ,” naamini hiki
kitasaidia kumrudisha Alice katika hali
yake ……
Kuja kufungua kitabu alikuta kimeandikwa mermaids (Nguva) alishtuka ina maana Alice ni nguva akajibiwa na mzee ismail
“ndiyo ni nguva na ni mtu ambaye ndo kakusaidia wewe ndo maana unaishi hadi leo”
kelvin alishtuka na kusema “mbona hukuniambia ” . ndipo mzee alipomwambia kuwa ilikuwa ni ombi la Alice kukufanya wewe usijuwe jambo hili
!!!!!!!!
Basi kama ni ombi lake hakilisha humwambiii kama nimejua kuwa yeye ni
nguva yaani ficha hii siri kama ulivoficha
kwake na usimwambie kwamba nimejua
….mzee ismail hakuwa na hiyana alimwambia sawa na yeye hatajuwa chochote lakini nikwambiye tu kijiji hiki kimevamiwa na majini sijuwi hata tutakiokoaje ……….
kelvin hakuamini habari za majini alimwambia habari hizo ni za vitabu hata hii ya binti kuwa ni nguva naifanyia uchunguzi nikibaini ni kweli nitaamini na hiyo ya majini
“ngoja nimuandalie maji ya moto kama walivyoandika kwenye kitabu nimpake upande wa mgongoni nione kama ataamka kisha sitamwambia chochote
nitasema umemtibu wewe “. ili asije
akahisi nimemtibu mimi na nimegundua kila kitu hivyo ili kuficha mi nitamtibu na kukuachia kila kitu wewe “
Basi alifanya taratibu zote za kumfanyia matibabu kama kitabu kilivyosema . alichemsha maji , akatia chumvi kidogo akachukua kitambaa safi na kutia kwenye yale maji ya moto baada ya kuyapooza na akakikamua na kujaribu kumpakaza maeneo ya mgongo lakini baada ya kumgusisha kitambaa cha maji ya vuguvugu huwezi amini kama magamba yalitokea na kupotea alishtuka na kila akiendelea kumgusisha kile kitambaa .. Ndivyo magamba yalivyozidi kuonekana
baada ya kumaliza alitoka mpaka kwa
mzee Ismaili na kumwambia
“baba nimeamini uliyoyasema Alice kweli ni Nguva huku akikaa chini maana hakuamini kuwa mwanamke ambaye wanapendana naye ni Nguva .
*******
Kisha kelvin akamwambia mzee Ismail Aende ndani baada ya kusikia sauti ya Alice akikohoa
“nenda jifanye kama wewe ndo umemtibia ili asijue chochote” kelvin huku akimsukuma mzee Ismail aingie ndani yeye akawa anasikiliza tu alijibanza kwenye mlango
Alice kwa sauti ya uchovu sana “,we ndo
umenitibia mzee ismaili au ni kelvin
….????”
“ni mimi nimekutibia yeye kelvin alikuacha akasema akakutafutie tiba bila kujua wewe ni nguva na nilipoona hayupo ilinipasa nikutibe Binti nguva ” Alisema mzee ismail kwa sauti ya kujiamini
“Nashukuru mungu kelvin yaani akijuwa huyo mi nayeye basi sijuwi ata kama atanipenda kiumbe cha ajabu kama mimi namlinda kwa nguvu zangu zote hata kama ataniacha saw ila nampenda na nitamlinda dhidi ya chuki ya rafiki yake
ambaye yeye ndo anaendesha ushetani
wote.
kelvin alishtuka na kusema “ina maana kelvin rafiki niliyemuamini ndo wakunifanyia yote haya au nimesikia vibaya …………
Mara ghafla kelvin kwa bahati mbaya akakanyaga kimti kilichofanya ashtuke Alice na kusema
“nani huyo hapo nje “?????????kelvin ikabidi aitike ni mimi mama watoto ” umeamka aliingia kwa furaha lakini akilini mwake akisema huyu kelvin ni kelvin yupi
…..??????
Mwisho wa siku walizungumza watu hao
watatu wakiwa na furaha Alice akidhani anamficha kelvin kumbe kelvin anajua kila kitu kihusu Alice . Basi Mzee Ismail alitoka na kelvin alibaki na Alice kamkumbatia lakini kila mtu kichwani ana mawazo yake
MAWAZO YA KELVIN
“hivi Alice kwa hiyo kwao ni baharini na kama ndo hivyo mbona siku zote hajarudi kwao kuna nini ? kuna tatzo au amefukuzwa na kwanini ameniokoa mara zote hizo toka siku ya nyumba yangu kuchomwa moto na sio hapo kaniokoa mara wa kadha hii ina maana kwamba she my guardian angel(malaika mlinzi
).Lakini vipi huyu kelvin ni kG yupi au rafiki
yangu ????? daah kama ni yeye ndo
kasabisha kila kitu nitaumia bora asiwe yeye ….”
MAWAZO YA ALICE
“Daaah nawaza sana kelvin akijuwa kuwa mimi ni nguva atanipenda kweli na kingine huyu Goodluck kwa sasa nahisi atafanya shambulio la kummaliza mbaya wake kabla ya kuitawala dunia asijuwe hata ulimwengu wa majini unamtumia yeye kutawala dunia hivyo inabidi nimzuie hata kwa kumuua tu ….”
Mara ghafla wakasikia vilio walipotoka nje walimkuta yule babu ismail kakatwa
kichwa damu zinatililika na moshi
ukitawala kila sehemu ya kijiji hicho ,ikiwa na maana tayari ulimwengu wao ushashambuliwa na majini na sasa hakuna namna ya kulikwepa hilo ghafla kikasikika kicheko kutoka nyuma yake kelvin aligeuka hakuweza kuamini mtu aliyemuona baada ya kugeuka
Je aliona nini usikose sehemu inayofuata
……
BINTI NGUVA
EPISODE 15
Kelvin aligeuka na alishtuka baada ya
kumuona mtu aliyenyuma yake tena alikuwa akipiga makofi na kusema oooooh rafiki yangu ,ndugu yangu ,classmate wangu huku akicheka kwa dharau nadhani leo ni siku ya kukuonyesha sura yangu halisi kwa sababu natumai leo ndo mwisho wa maisha yako na huyu binti Alice maana kana kihere here sidhani kama unajuwa kama haka kabinti ni kakiumbe kaajabu et kanguva wale watu walioongozana naye ambao walikuwa ni men with black jacket huku sura zao zikifunikwa ….
Kelvin hata hakushtuka baada ya kujua kuwa Alice ni nguva kwa sababu alijua
toka ile siku mzee ismail alipomwambia
….
“ilo nalijuw muda mrefu sana kuwa Alice ni nguva ambacho nilikuwa sikijuwi kuwa wewe ni mchawi wangu nikiwa na maana kumbe baada ya kukaa kuwaombea wagonjwa nakuombea mtu ambaye unachuki na mimi na hata sijuwi nimekosea wapi mimi…..???
Alice alishangaa kelvin amejuaje kuwa yeye ni nguva na kuficha bila kumwambia lKini kelvin alimjibu nilimficha kwa sababu nilijua kama wewe hujanambia basi kuna sababu ndo maana sikutaka nikufanye
ujuwe kuwa najua ,hata kukutibia
nilikutibia mimi lakini mzee Ismaili alikuwa amezuga ili usijuwe kuwa naelewa kila kitu……na nilipomsikia kuwa wewe Goodluck ni msaliti nikagundua kuwa inawezekana na labda umesahau ulimchoma moto mwalimu wa mathematics yeyw na nyumba yake yaaani nakukumbuka Goodluck sio matukio hayo tu ila ni mengi ndo maana nilijuwa unaweza ukawa ni wewe unayehusika ………..
Basi Goodluck akatuma wapambe wake kama wanne hivi Alice alimuweka pembeni Kelvin kisha macho yake yalibadilika rangi na kuwa ya rangi ya blue kisha akawatazama wale wapambe
wanne huwezi amini walidondoka kama
kifurushi ,tuma wengine majibu yalikuwa tale yale wapigwa na kuandika kama. kipeto puuuuuh
Vita ilikuwa ni kubwa sana kiasi kwamba mpaka Goodluck aliingia mwenyewe walishindana nguvu na Alice mpaka kila mtu akiwa hoi.. hapo kelvin alikuwa hawezi kuingilia chochote lakini alipotazama vizuri aligundua kuwa kuna cheni ipo shingoni kwa Goodluck ilikuwa inawaka sana na sasa siti ni kwamba ukifanikisha kuikata ile cheni na kuweza kuisambaratisha hapo utakuwa umefunga lile geti lililopo ambalo lililowatenganisha
nguva na binadamu wa kawaida sasa ishu
utaitoaje ….
Na katika siri ambazo , Majini ni kuhakikisha ile cheni hawaioni binadamy na kama wataiona na kufanikisha kumvua atakuwa binadamu wa kawaida kama kawaida sema ndo atatokea kwenye ulimwengu wao na ka atatokea huko ina maana kuwa hataweza kurudi dunia na watamuulia kule kule .
yaani Kwa bahati mbaya Alice alipigwa shambulizi moja kubwa sana kiasi kwamba hakujua atatokea wapi alianguka chini kama mzigoo puuuuuuh
Kelvin aliita Alice akawa anamkimbilia
kwenda kumuona lakini wapi kabla hajafika Goodluck alimshambulia na yeye akaanguka chini mwisho akamwangukia Alce kila mtu yuko hoi hajuwi afanye nini ili kukomboa maisha ya mwenzie yaani haelewi nini afanye.
Lakini kelvin akakumbuka ndani ya kile kitabu cha mermaids alichopewa na mzee Ismaili aliiona ile cheni shingoni na akakumbuka cheni ni ileile na akakuta kuna maneno yameandikwa ili kutoa hii laaana lazima cheni hiii ivunjwe vunjwe na akakumbuka kuna aya Alisoma nayeye anakumbuka alisoma kama gazeti maana alijuwa ndani mule zimeandikwa stori za kubuni tu …. ….
Akawa amepata akili kwamba ili aweze
kushinda inatakiwa amvue ile cheni na kitu kingine alitazama kwa makini hata wale majini wengine wanaongizwa na ile cheni maana ili awatume lazima ashike ile cheni na kuwambia nendeni . basi akawa anatafuta namna ya kumvizia akamilishe kila kitu kuja kumtazama Alice amekata moto yaani kazimia .Goodlck akawa ana msogelea kelvin kosha kumkwida na kumwambia
“we mbuzi yaani nilikuwa shetani kwa ajili yako wewe kelvin kumbe ni mdebwedo hivo ??? ningejua nisingejiunga ningekuua kawaida tu kama nachinja kuku…..
Lakini Goodluck unajua kwangu wewe ni
kama ndugu kwangu lakini siamini kama umekuwa mnyama kiasi hicho mbona unanifanya mimi kama roboti. Ulinambia mtoto wako anaumwa nilipambana kumbe hata ulikuwa haumwi hata kidogo
,ilikuwa ni mbinu yako ya kuniangamiza
Maskini ya mungu hukuishia hapo, hata Emanuel na familia yake ilikukosea nini Goodluck kwa kutuma watu wawachinje chinje na hata watu uliowauwa hapa wamekukosea nini kweli wewe no shetani Goodluck siamini kama una roho mbaya kiasi hicho daaa hili limeniumiza sana
.muda huo kashaiweka cheni kwenye
tageti …..”
Goodluck alicheka sana na kusema “yaani ulivokuwa unasimulia matukio ya nyuma yaani ni kama mchambuzi wa nbc priemere legue baada ya dakika tisini tukapata uchambuzi kutoka kwako asante si tulikuwa tumeiona kaama movie hivi
…………hongera sana kelvin lakini ukweli kwamba ,weee ndo umenifanya mpaka leo niwe hivi . Kwanini ufanikiwe zaidi yangu
??? ikiwa umeishia Fom 4 mi nipo mpaka chuo nimemaliza nimeajiliwa lakini wewe ndo una maisha mazuri……
Tena una bahati sana yaani nilitamani ufe
toka zamani kuna siku nilikununulia kinywaji nikaweka sumu ufe hiyo ilikuwa zamani sana lakini sijuwi una bahati gani haukuinywa …mbona ulikuwa umekufa kitambo we mjinga ….
Ghafla kelvin aliivuta ile cheni na kuikata kisha akairusha karibu na ukuta ilikuwa sio ngumu sana hivyo ilipasuka paaah …..
Goodluck alikimbilia kuiwahi lakini ashachelewa alianza kulia mara ghafla wale majini waliyeyuka hata Goodluck naye yalitokea mawimbi makali yaliyopiga baharini mwisho lile geti la ulimwengu wa kina Aluce lilifunguliwa na dada Alice ambaye ni sabrina hakutaka kuchelewa
safari duniana kwa mdogo wake maana
matukio yote aliyoyafanya waliyaona kwenye video yao ya kichawi na walijuwa kwa sasa wao ndo wanahitajika kumtibia
KWA KELVIN
Muda huo Kelvin kamshika Aluce akiwa anamtazama na dunia kwa sasa haitavamiwa na ulimwengu wa majini mpaka mtu aje akosee tena masharti na aingie makubaliano .
Basi kelvin akiwa hajuwi namna ya kumuamsha Alice alisikia sauti ikisema
“kwa sasa anahitajika akatibiwe nyumbani kwao ambako waliko nguva na amini akipona atarudi ……
Kelvin hakuwa na pingamizi hata kidogo
alimuacha Alice abebwe na Sabrina lakini Sabrina kabla hajaondoka alimwambia kelvin kuwa ” Nguva wote wanakushukuru kwa msaada wako kwa sababu bila wewe wote tungefia mle tunasema Asante “
Basi baada ya hayo maneno Sabrina alipotea na Alice lakin kijiji cha kasongo kilikuwa tayari kipo salama …..
KWA UPANDE WA GOODLUCK
Alijikuta ametokea katika ulimwengu wa majini akiwa hajuwi nini akifanye mara ghafla alitokea Roy na kusema mfalme hataki kukuona tena hivyo una stahili hiki alitupiwa kama minyororo iliyokuwa kama
ina muunguza na kumpa maumivu
makali. kisha akambiwa utateseka mpaka pale atakapotokea mtu wa kufungua hili lango kisha akafungiwa kwenye chumba zilizokuwa zikisikika ni kelele
MWAKA MMOJA BAADAYE
kelvin alimsubiri Alice kwa muda mrefu lakini Alice hakuweza kuonekana mpaka akakata tamaaa sasa siku moja Alice alitoka katika ulimwengu wao maana matibabu yake yalikuwa ni ya miezi nane na kuridi katika hali ya kawaida ni miezi minne hivyo kwa hesabu ya jumla ni mwaka mzima . Basi alipofika kijiji kila mtu alimtambua kama mke wa kelvin japo wengi walijuwa kuwa binti huyo ni nguva
na walimuheshimi kwa sababu kelvin
aliwambia huyu ndo kapigania maisha yenu ..
Basi aliwauliza kuhusu kelvin walimjibu alishakufa zamani sana ni kipindi kile kile ulichoondoka kumbe alikuwa ana majeraha makubwa ……….
Alice alichanganyikiwa na akaondoka na kuingia njia ya sokoni akiwa analia sana kila mtu alimtazama huyu vipi mara ghafla mvua ikaanza kunyesha oooh anaweza akageuka kuwa nguva barabarani
,akaanza kujificha sehemu za mwili wake ili maji yasimmwagikie ata kidogo maana ni hatari kwa afya yake aliinama na kujaribu kujjfunika . mara ghafla
alishangaa kijana mmoja aliyekuwa
kapendenza sana amemwekea mwamvuli alipomtazama usoni alitabasamu na kusema kelvin ….
kelvin aliitika “rebekhaaaa Alice huku akitabasamu na kumtazama ..
Alice ” michezo gani ya kunichezea et umejufa na unajuwa siwezi ishi bila wewe hafu unafanya utani basi Kelvin alicheka na kusema its suprise to you
Alimuinua na kumkumbatia wanakijiji na watu pale sokoni walipiga makofi na kushangilia na hapa ndio mwisho wa hadithi hii ya Binti nguva …………
……… MWISHO ………………