HANDSOME WA SHULE 9
Songa nayo
Anitha hakujali hali ya John kutoonekana pale nyumbani ila aliendelea na kazi zake za kila siku.
Mama John alipatwa na wasiwasi sana alianzaa kulia utafikili kuna msiba pale nyumbani.
(Uchungu wa mwana haujuaye mzazi)
**********
John huku yeye akiwa pangoni hajui sehemu ya kutoka wala kuingia.
John alizinduka usiku sana huku mbwa mwitu akiwa amelala na kunyata ili akimbie.
Ghafla alisikia sauti ikisema
“Huwezi kukimbia wala kutoka katika hili pango mpaka utakapo kuwa fit”
John alisimama hakuendelea kukimbia Bali alijipa moyo na kugeuka kuifuata sauti ilipotokea.
John alitembea mpaka pale alipokuwepo mbwamwitu na kumkuta binadamu wa kawaida. John alishtuka sana huku akirudi nyuma.
Yule mtu alimuambia usiniogope Mimi ni binadamu kama wewe ila nimechagua maisha ya kuishi porini kama mbwamwitu.
John alikaa chini iliapate kumuuliza kisa cha yeye kuwepo porini halafu ni binadamu ila unabadilika kutokana na mazingira.
John alipata ujasiri wa ghafla sana huku damu yake ikiwa imechanganyikana na ya mbwamwitu.
John alimuuliza
“Kwanini wewe unabadilika?.
Mbwamwitu: Mimi ni binadamu ila ni nusu mbwamwitu na nusu binadamu.
John: Kama wewe ni binadamu ulipataje umbwamwitu?.
Mbwamwitu:Niling’atwa na mbwamwitu ambaye anauwezo wa kuambukiza virusi vyake.
John: Inamaana na Mimi nimepata uumbwamwitu?.
Mbwamwitu:Ndiyo,yule aliyekung’ata anauwezo wa kumbukiza virusi vyake,undo maana umewahi kupona na kovu hauna.
John: Lini nitatoka humu pangoni?.
Mbwamwitu:wewe sasa ni jamii yetu inakupasa ujifunze mbinu za kujizuia pindi ukasirikapo ili usije kudhuru mtu.
John: sawa,Ila mama yangu atakuwa na hofu na Mimi?
Mbwamwitu:utajifunza taklibani wiki moja halafu utarudi kwenu.Kwanini umeingia katika hili pori bila hata na silaha ya kujikinga?.
John: Nilichanganyikiwa nilipopigiwa simu kuwa ametekwa na yupo katika hili pori.
Mbwamwitu:Basi walikudanganya hakuna ambaye anaweza kuingia katika pori bila Mimi kujua Mimi nika
HANDSOME WA SHULE 10
Songa nayo…..
Mbwamwitu:Basi walikudanganya hakuna mtu ambaye anaweza kuingia bila Mimi kujua Mimi ni kama mfalme wao.Labda huyo mwanamke alitaka kukuua maana ukiingia katika pori hili huwezi toka wanakutafuna unabaki mifupa tu.ila wewe umekuwa na bahati nilikuonea huruma.
Mbwamwitu aliongea sana mpaka John alianza kulia huku akimkumbuka mama yake aliyemuacha nyumbani.
Asubuhi na mapema John akiwa katika pango akimsubiri yule mbwamwitu arudi.
Baada ya muda mbwamwitu alifika akiwa na sungura pori
Mbwamwitu alimchoma vizuri na kumpa John amle
John alimpokea na kuanza kumtafuna John aliona mabadiliko katika meno yake.meno yake yalikuwa makali Sana baada ya dakika mbili yule sungura alikuwa ameisha.
Mazoezi yaliendelea jinsi ya kucontrol nguvu zake asimdhuru mtu.
Upande wa mama John yeye aliamua aende kutangaza katika redio na maruninga.
Marry yeye alipoteza matumaini akaanza kutembea(akampenda)kijana mmoja aitwae Joel ili amliwaze mapenzi ya hao wawili yalishamili sana mpaka wanafunzi wa Xhule wakajua kuwa marry kapata mvulana mwengine pale shuleni.
(BAADA YA WIKI MOJA KUPITA)
JOHN aliruhusiwa kuondoka pale porini kwenda kujumuika na nduguze kwao.
John alipewa cheo cha kuwa mlinzi msaidizi wa mbwamwitu na kuwa mbwamwitu wote wakochini ya John.
John alikuwa mbwamwitu wa kwanza kupewa cheo akiwa ni binadamu pia mwenye umri mdogo kabisa kama nusu binadamu nusu mbwamwitu.
John alikuwa na miaka 17 ya kibinadamu,mwenye uwezo wa kipekee Sana kuliko wote pale msituni.
Mbwamwitu yule alimwambia uwe makini huko uendako pia usiwasahau hawa ndugu zako kumbuka kuwalinda binadamu dhidi ya mbwamwitu wenye rangi ya bluu na nyekundu hawa ni hatari kwa binadamu na hata mbwamwitu jamii yetu sisi usisahau usimwambie mtu yeyote hata mama yako asijue kabisa kuhusu msitu huu ili mbwamwitu waendelee kuishi.
Hayo yqlikuwa ni maneno ya yule mbwamwitu ambaye alimsaidia John.
John alishika…
HANDSOME WA SHULE 11
Yale yalikuwa ni maneno ya mbwamwitu akimsisitiza asije akasahau wajibu wake WA kulinda mbwamwitu
John alishika mwiba na kujichoma nao katika kidole kama kiapo.
*****
John alianza safari ya kuelekea nyumbani kwao huku mawazo yakiwa kwa mama yakr atakuwaje alia za kukimbia kiumbwa mwitu ili afike haraka.
John aliwasili nyumbani kwao na kugonga Mara Tatu huku akiwa na hofu sana aliyefungua alikuwa ni mama yake.
Mama John hakuamini kama ni yeye mwanae alimpampasa mwili wake lakini ukweli haufichiki alia mini kuwa ni yeye.
*****
Upande WA marry yeye alikuwa anajitanua na mpenzi wake joely kila sehemu club,beach kila kona wao.
****-
John aliingia ndani na kuambiwa kwanza akaoge ,John aliinuka na kuelekea chumbani wake kupata maji ya mvua.
Baada ya kumaliza kuoga John alivaa T-shirt yake ambalo iliandikwa WHY ALWAYS ME(KWANINI KILA SIKU /MARA MIMI) ambayo ni msemo wa mchezaji mtukutu ndani na nje ya uwanja Super Mario Balloteli
Mama John alia za kumuuliza mwanaye.
Mama John: John mwanangu ulikuwepo hizi siku.
John: mama hata Mimi sijui nilikuwepo wapi
Mama John:hawajakuumiza
John: sio sana nikidogo tu wameniumiza.
Mama John; pole mwanangu sasa inatubidi twende polisi kuwataarifu.
John: sawa
Walifunga safari hadi kituo cha polisi njiani John alimuona marry akiwa na mwanaume mwingine wakishikana viuno na kupeana makiss njiani
John alikasirika mpaka macho yakawa ya bluu na kucha zikawa ndefu sana ila alijizuia ili mama yake asijue kama yeye ni mbwa nwitu.
Basi safari ilisonga mpaka kituo cha polisi,mapolisi walimuulizq maswali lakini aliyajibu yote John katika kichwa chake vitu viliongezeka maana aliyajibu vizuri na upeo wa kufikili ulikuwa umeongezeka sana John alijiona sio mtu wa kawaida kabisa.
Basi maaskari wakasema kuwa watamsaka jambazi yeyote aliyehusika lakini John alicheka tu maana hakukatekwa na jambazi Bali mbwa mwitu.
Waliruhusiwa kurudi nyumbani kupumzika.
Anitha………
HANDSOME WA SHULE 12
Songa nayo
Waliruhusiwa kwenda nyumbani kupumzika ili mapolisi wafanye uchunguzi wao.
Anitha yeye hakuwa amemuona John maana alitumwa supermarket.
Aliporudi kutoka supermarket alimkuta John akiwa amekaa kwenye sofa.
Anitha alimuangalia sana John nakumfyonya huku akiwa amekasirika kumuona pale.
Anitha hakufurahishwa na John kuwepo pale alitamani John angeuwawa sehemu alipokuwepo..
*******
Huku mapenzi mazito yakiwa yqnaendelea marry alimsahau kabisa John Bali alikuwa anakula raha na mpenzi wake.
*****-
John alikabidhiwa gari gari aina ya Prado na leseni ambayo ilifojiwa miaka John alikuwa na miaka 17 ila leseni imeandikwa ana miaka 18.
Gari aliyopewa aliyenunua alikuwa ni baba yake John ambaye alifariki katika ajali ya gari akiwa ametoka safarini.
John yeye ni chotara baba yake ni mzungu wa uingereza na mama yake ni mwarabu.
Hiyo gari iliandaliwa mahususi kwaajili ya John pekee na hakuna aliyejua kama kuna gari aina ya Prado pale nyumbani kwao zaidi ya wawili baba na mama yake John.
John alipokea zawadi ile ambayo ni maalum kwa ajili yake.
**********
John alianza mafunzo ya gari mpaka alipohitimu .Mafunzo Yale ya udereva. ¶
Baada ya siku mbili baadae John alianza kwenda Xhule na Prado yake, Mama yake aliacha kumlipia school bus.
Kwaajili ya usalama wake John
John alifika shuleni na Prado lake jeusi ambayo vioo vyake ni tinted.
Wanafunzi walishangaa kuliona gari limepaki pale nje ya Xhule ambapo kuna parking cars
John alishuka kwenye gari na kuelekea getini alionesha kitambulisho cha shule na kuruhusiwa kuingia ndani.
John alipokelewa na rafiki yake pheston.
John alikuwa siyo muongeaji alitulia kimya kama bubu akiulizwa maswali hajibu.
John alikuwa anadili na kusoma kuhusu wasichana alikuwa awazi juu yao maana siku nyingi hakuwepo shuleni aliandika notes tu.
Marry yeye alikuwa anamuangalia Sana John ambaye alifika shuleni Sikh hiyo.
John alimpotezea kabisa marry nahakuwa anaongea naye.
John hakuwa anawapenda
INAENDELEA