PENZI LA KIKOMANDO
EPISODE YA 10
TULIPOISHIA…..
Ramos alirejea nyumbani kwake akiwa na askari kadhaa waliomlinda. Janeth mke wa Ramos alimkimbilia mmewe kwa furaha lakini Ramos alimkwepa mkewe na kuelekea ndani. Janeth alimfuata Ramos chumbani amuulize kwa nini amebadilika lakini Ramos anatoa kauli inayomfanya Janeth akose nguvu
“Chukua mabegi yako ondoka nyumbani kwangu…..” Aliongea Ramos baada ya kufika chumbani.
ENDELEA…..
“Ramos umesemaje…”
“Chukua mabegi yako uende….” Alirudia kwa hasira sana janeth taratibu akiwa anaanza kudondosha machozi.
“ Nimekukosea nini mpaka unifukuze Ramos….” Aliongea janeth kwa uchungu.
“Hakuna ulichonikosea ila kwa kweli sijawahi kukupenda hata siku moja….”
“Sasa ni kwa nini uliniowa…”
“Kwa sababu nilikutamani tu Janeth, sitaki tena uanze kuuliza uliza maswali yako ya kijinga nimekwambia chukua vitu vyako uende….”Aliongea Ramos tena kwa msisitizo.
“Sawa mimi naenda, uwe na maisha marefu mume wangu…” aliongea Janeth akiwa anachuka begi lake na kutoka nje uso wake ukiwa umetapakaa machozi.
Janeth hakuwa na sehemu ya kwenda sababu wazazi wake walifaliki miaka miwili nyuma. Maisha ya janeth yalikuwa yakitegemea jitihada za mmewe hivyo baada ya janeth kufukuzwa moja kwa moja alielekea baharini kujiuwa akiwa na maumivu makali.
Siku mbili baadae maiti ya janeth inaonekana pembezoni mwa mto watu waliokuwa pale waligundua kama ile ni maiti ya mke wa kamanda Ramos.
Ramos alifikishiwa taarifa kuwa maiti ya mkewe imepatiaka pembezoni mwa mto.
Ramos alichukua maiti na kuanza kufanya taratibu za mazishi.siku iliyofuata Watu wengi waliudhuria katika msiba ule ikiwemo viongozi wa juu wa serikali kama General.
“Ramos ilikuwaje mpaka mkeo amefariki ndani ya maji?…” Aliuliza General akiwa amevalia mavazi meupe.
“Alitoloka nyumbani na kwenda kujiuwa sielewi hata ni kwa nini!….” Ramos alimuongopea general akiwa anafuta machozi usoni.
“Usilie bwana wote tupo hapa kukutia moyo….” Aliongea general akimshika Ramos begani.
Msiba ulimalizika watu wote waliondoka. Ramos alipewa likizo ya siku 40 na general.
Siku iliyofuta baada ya msiba Majira ya saa tatu usiku Ramos akiwa ndani mala anasikia kelele za Askari wanaoweka ulinzi kwenye nyumba yake.
“ Binti huruhusiwi kuingia kamanda Ramos anapumzika..”
“Niachieni bwana nataka kuongea nae…” Alikuwa ni Maria akibishana na walinzi.
“Muacheni aingie ndani…” Aliongea Ramos akiwa amesimama mlangoni.
Maria aliachiwa na kuingia ndani.
“Karibu maria…..” Aliongea Ramos akiwa anakaa kwenye kiti.
“Asante shemeji Ramos pole na msiba….” Maria aliongea akiwa anakaa.
“Tayari nimepoa….”
“Unajua Ramos niliumia sana nilipopata habari kama Ram amefariki lakini nashindwa kuamini kama kweli aliwasaliti wenzake vitani maana alikuwa ni mzalendo sana na nchi yake….”
“Maria kila mtu anatunza siri zake moyoni hata sisi wenzake hatukutegemea hilo tulimuamini sana…..”
“Ukweli nilitokea kumpenda sana Ram lakini kumbe alikuwa anaficha makucha yake kwangu na kuonekana mwema ili anipate! Mpaka naona aibu kwa nini nililala naye mara ya mwisho msaliti yule…”aliongea Maria alionekana kumchukia sana Ram
“Pole sana Maria, Naisi Ram alikuwa anataka akutumie tu. Ngoja nikupe kitu utakipenda….” Aliongea Ramos akiwa anasimama pale na kuelekea chumbani.
“Kitu gani hicho?….” Aliuliza Maria kwa bashasha.
Ram anaingia chumbani kwake anachukua Pete iliyokuwa kwenye kibox kidogo Kisha anarudi sebureni.
“”Ni kitu gani icho ulitaka kunipa?..”aliuliza Maria alipoona Ramos amerudi kutoka chumbani.
Ramos alipiga goti moja chini na kutoa Pete.
“Maria naomba uwe mke wangu….” Aliongea Ramos kwa hisia kali akiwa amenyosha mkono mbele ulioshika Pete akitaka kumvisha Maria.
“Hiii! Lakini wewe mke wako si amefariki juzi leo tena unataka kunioa Mimi hapana!…” Aliongea maria kwa mshangao sana.
“Kwani shida ipo wapi Maria Mimi nilikuwa nakupenda wewe mda mrefu sana kabla hata sijamuowa janeth…”
“Sasa mbona hukuwai kuniambia uliacha mpaka nikachumbiwa na Rafiki yako?.
Ngoja mi niende afande…”Aliongea Maria akiwa anasimama, anaondoka anamuacha Ramos pale chini akiwa na Pete mkononi.
“Analeta ugumu lazima tu siku moja awe mkewangu…..” Ramos aliongea akiwa anasimama .
Siku iliyofuata Ramos alifungasafari yeye na walinzi wake wakielekea kwa kina Maria, anakoishi Maria na wazazi wake.
Ramos anafika pale na kupewa heshima kubwa sana na watu walikuwa lile eneo wakijua fika kwamba Ramos ndiye general ajaye .
“Karibu sana kijana wetu……” Aliongea baba yake Maria baada kumuona Ramos.
“Asante baba, Maria yupo?…”
“Hapana kiongozi, mwanangu ameenda kazini kwake huko, kwani mwanangu amefanya kitu gani mkuu mbona unamuulizia …”Aliuliza baba baba yake Maria kwa woga ndugu wengine wa Maria wakiwa pembeni.
“Hakuna tatizo baba ila nilikuwa nataka kumuowa binti yenu Maria lakini yeye anaonekana kutoridhia jambo hili…” Aliongea Ramos nyuma akiwa na walinzi.
“Mama Maria umesikia hili general anataka kumuowa binti yetu …”Aliongea baba Maria kwa furaha akimuangalia mkewe ambaye na yeye alikuwa akitabasam.
“Baba umeridhia hili jambo…”Aliuliza Ramos akiwa amesimama.
“Kwanini nikatae kijana wangu? Nimekubali asilimia zote ….”
“Basi mzee nisaidie kumshawishi binti yako maana nataka nimuowe haraka sana….”
“Usijali mimi ni baba yake, atake asitake lazima ataolewa ili tufiche aibu ya yule kijana msaliti kumchumbia binti yetu…”aliongea baba yake maria kwa furaha .
Ramos aliondoka pale kwa kina Maria na kuelekea kambi ya jeshi kuwatembelea Askari wenzake.
Majira ya jioni Maria aliporudi kutoka kazini anakutana na habari mpya za yeye kuolewa na Ramos.
“Baba Mimi sitaki kuolewa sasa…”aliongea maria kwa hasira.
“Utake usitake lazima uolewe na Kamanda Ramos lasivyo ukajenge nyumba yako na ukatafute wazazi wengine …”Aliongea baba Maria kwa hasira Maria akiwa ameshika kichwa chake .
Maria hakuwa na jinsi ilimbidi akubali tu kuolewa na Ramos kwa shindikizo la wazazi wake.
Ramos alifikishiwa taarifa kwamba Maria yupo tayari kuwa mkewe kilichobaki nikupanga siku yao ya kufunga ndoa.
Siku ilipendekezwa na wote waliridhia ndoa ifanyike mwezi mmoja baadae.
SIKU 30 BAADAE(mwezi mmoja)
Ramos na Maria wanafunga ndoa majira ya mchana . Ilipofika usiku kulikuwa na sherehe kubwa ambayo alianda general wa nchi kama zawadi kwa Ramos.
Sherehe ilifana sana huo usiku kulikuwa Kuna kila aina ya chakula na vinyaji na kila mtu alienjoy Ramos na mkewe walikuwa mbele kabisa wamekaa kwa mahaba wakiangalia show mbalimbali zinazofanya na Askari .
Wakati Sherehe ikiwa inaendelea usiku huo Kuna mtu anaonekana kuingia ndani ya hiyo kumbi akiwa amevalia koti kubwa lililofunika sura yake kwa kofia.
“Kipenzi changu Maria ukweli hadi wewe umeamua kunisaliti mimi na kuolewa na Rafiki yangu…..” Aliongea yule mtu akitazama mbele Kisha anageuka nyuma na kuondoka akiwa na machungu.
INAENDELEA…..
Ram kasambaziwa taarifa mbaya mji mzima unajua yeye ni msaliti alafu Ramos kapita na shemeji yake..
Mambo ndiyo hayo sasa 🔥
PENZI LA KIKOMANDO
EPISODE YA 11
TULIISHIA…..
Sherehe ikiwa inaendelea usiku huo Kuna mtu anaonekana kuingia ndani ya hiyo kumbi akiwa amevaa koti kubwa lililofunika sura yake kwa kofia.
“Kipenzi changu Maria ukweli hadi wewe umeamua kunisaliti mimi na kuolewa na Rafiki yangu…..” Aliongea yule mtu akitazama mbele Kisha anageuka nyuma na kuondoka akiwa na machungu.
INAENDELEA…….
Sherehe zilimalizika wazazi wa Maria walimuaga binti yao na kumuacha akaanze maisha mapya ndani ya ndoa na Ramos.
Maria na Ramos waliishi pamoja kuanzia iyo siku kama mke na mume.
Baada ya wiki mbili Maria anaanza kuwa na dalili zinazo mfanya Ramos awe na mashaka kidogo na kupelekea kwenda kumuuliza Maria.
“Mke wangu siku mbili tatu hizi ni kama vile haupo sawa unatapika ovyo tatizo nini?”
“”Leo nimeenda kwa daktari mmoja amesema ninamimba..” alijibu Maria akiwa amekaa chini
“Hahaha Asante Mungu hatimaye tutapata mtoto wetu. Furahi basi mke wangu mbona umenuna wakati hili ni jambo la kheri….”aliongea Ramos akiwa anacheka . Maria alionekana kutokuwa sawa kabisa alisimama pale na kwenda kujifungia chumbani.
“Maria umepatwa na nini wewe?…” Aliuza Ramos kwa wasiwasi Maria akiwa tayari ameshajifungia chumbani.
.
“Ram Ni kweli umekufa hata bila kumuona mwanao akizaliwa!..najua ungefurahi sana kupata hizi taarifa kama ulivyofurahi siku uliyosema unanipenda…”Aliongea Maria akiwa ameshika tumbo lake machozi yakimtoka taratibu akiwa chumbani.
Ramos alitunza ile mimba kipindi chote cha ujauzito akiamini ni mimba yake mpaka miezi tisa inakamilika hatimaye maria anajifungua mtoto wa kike.
Ramos anaandaa sherehe kubwa ya kumkaribisha binti yake duniani na kumpa mtoto jina WONDER.
Miaka miwili baadae general wa nchi alifariki kutokana na ugonjwa wa moyo hivyo nafasi yake moja kwa moja ilichokuliwa na Ramos. Hatimaye Ramos alikuwa General ., gold key aliifadhiwa kwenye nyumba yake kuanzia siku hiyo.
Ram alikuwa hai lakini aliogopa kutokea mjini sababu watu wote walikuwa wanaamini alikuwa ni msaliti wa nchi yake hivyo alienda kuishi milimani pekeyake taratibu akiwa anatengeneza kikosi cha waasi ili siku moja akafanye mapinduzi katika nchi yake iliyomkatili vibaya.
*****************************”*************
HIYO JUU ILIKUWA NI STORY YA MIAKA 20 NYUMA.
………………………………………………….
MIAKA YA SASA
TULIISHIA….
Mara ya mwisho tulimuona wonder akiwa ametekwa na Aboku ambaye ni mtu wa Ram. Abuku alimpeleka wonder moja kwa moja mpaka kwenye kambi yao ya waasi ambayo iliongozwa na Ram mwenyewe.
Ram alipatiwa taarifa na Aboku kama wameshinda vita vya msituni dhidi ya wanajeshi na wamefanikiwa kupata gold key pamoja na binti wa general Ramos.
“Hahaha safi sana Aboku umefanya kazi nzuri lazima nimuuwe binti yake kama ambavyo aliuwa maisha yangu..”
Aliongea Ram akiwa anatoa maski aliyoivaa usoni sura yake ikionekana kuwa na makovu ya vidonda aliyopata miaka ishirini nyuma baada ya kudondoka kwenye lile bonde na akiwa ameanza kuota mvi za uzee.
Ram alitoka kwenye ofisi yake na kuelekea vyumba vya mateka akiwa na msaidizi wake Aboku.
Anafika anamuona Wonder akiwa bado hajapata fahamu tangia alipozimishwa njiani na Aboku.
“Woow binti mrembo amefanana sana na mama yake, lakini lazima nitamuuwa tu…” Aliongea Ram baada ya kuingia vyumba vya mateka na Aboku.
“Mkuu tumuuwe hata saizi akiwa akiwa bado ajazinduka, akiamka huyu ni msumbufu sana …”
Aliongea aboku.
“Hapana huyu hatuta muuwa sasa, tutamtumia ili tupate nafasi ya kumuuwa baba yake general Ramos Kisha na yeyeatakufa baada ya baba yake” Aliongea Ram akiwa ana uangalia mwili wa wonder.
“Kivipi mkuu mbona aijaelewa..”
Aliuliza Aboku.
“Aboku huelewi kitu gani sasa. Baba yake lazima atakuja huku milimani kumchukua binti yake kutoka kwetu hiyo itakuwa nafasi yetu ya kuuwa ndege wawili kwa jiwe moja …”
“Hahaha kweli kiongozi baba na mtoto wote watakufa….”
“Hahaha ndiyo hivyo kijana..” aliongea Ram kwa kucheka akiwa antoka kwenye kile chumba.
MSITUNI
Mara ya mwisho………
Tulimuona James akiwa kwenye
Hali mbaya amelala chini pumzi yake ikitoka shida akisubiri tu umauti umfike.
General Ramos na askari wengine walimuona James akiwa kwenye ile hali walimuuliza sehemu waliyoelekea waasi, James aliwaambia kwa shida sana haraka sana wote waliondoka pale kwenda kumtafuta wonder wakimuacha James anaangaika pale chini bila msaada.
ENDELEA……
General Ramos na askari wake baada ya kumkosa mwanae wanapitia ile sehemu waliyo muacha James maututi
“Mkuu Mwili wa James haupo hapa!…” Aliongea Jordan akiwa amesimama eneo ambalo mwanzo kulikuwa na mwili wa James.
“Achana nao utakuwa umeliwa na wanyama turudini kambini tukajipange upya namna ya kumsaidia mwanangu…”
“Sawa mkuu …”
General Ramos na askari wote waliondoka kwenye ile misitu na kurudi mjini.
SIKU MBILI MBELE
Ni katika kinyumba kidogo kilichopo pembezoni mwa msitu.
Mwili wa James unaonekana ukiwa umelala kitandani, ukiwa umezungushiwa vitambaa sehemu za kifua ambazo alipigwa risasi .
“Hapana msimuuwe huyo binti,, msimuuwe huyo binti ,, msimuuweeee….” James alikuwa akiongea pekeyake usingizini Kisha akashtuka na kujikuta yupo sehemu tofauti sana.
“Nipo wapi hapa?…” James aliongea pekeyake akiwa anatazama pembeni.
Hapohapo Kuna mzee anafungua mlango na kuingia ndani.
“Kijana umeaka Asante Mungu..”
Aliongea mzee akiwa ameshika dawa za mimea mkononi.
“Wewe ni Nani?…” Aliuliza James
“Kijana mimi ni mganga, nilienda msituni kutafuta baadhi ya dawa nikakuona ukiwa kwenye hali mbaya nikaona nikusaidie sababu ulikuwa bado unapumua haya kijana kunywa maji haya alafu upumzike
INAENDELEA……
Ram ambaya Ni gaidi mkubwa miaka ya sasa anataka kumuuwa Wonder bila kujua ya kwamba ni ……………..
Haya jamani James bado anapumua sasa Mambo yanaenda kuwa 🔥
Ijayo……RAM NA RAMOS WAKUTANA TENA BAADA YA MIAKA MINGI!!!!!
Lazima utaucheza mziki hata kama ujui step
PENZI LA KIKOMANDO
EPISODE 12
TULIISHIA
Mara ya mwisho tulimuona James anapata fahamu akijikuta yupo sehemu tofauti sana,
Akiwa anaendelea kujiuliza ndipo anatokea mzee mmoja kikongwa ambaye ni mganga na kumwambie
“Kijana nilikuokota msituni nilipokuwa natafuta dawa ulikuwa na hali mbaya sana nikaona nikusaidie Asante mungu umeamka…”
Aliongea yule mzee akiwa anasogeza kikombe cha maji kwa James.
ENDELEA…….
“Asante sana mzee ngoja niende Kuna mambo mengi sijakamilisha…” Aliongea James akiwa anajaribu kusimama kitandani lakini alishindwa sababu alikuwa na majeraha makubwa.
“Pumzika kwanza kijana bado ujapona..” Mzee mganga aliongea akiwa anamlaza James vizuri.
OFISINI KWA GENERAL
General Ramos yupo ofisini kwake akiwa na mawazo mengi kuhusu binti yake wonder.mala Kuna mtu anagonga mlango
“Ingia….”
“Mkuu ujumbe wako …” Aliongea
Askari baada ya kuingia akiwa na barua mkononi.
“Unaweza ukaenda…” Aliongea general Ramos akiwa tayari ameshapokea ile barua. Anafungua barua na kuanza kusoma.
“”Mshikaji wangu nilikumiss, vipi mambo huko yanaendaje? Najua yapo vizuri sababu upo na mwanamke uliye mchukua kutoka kwangu, Sisi huku mambo ni mazuri sana kwa sababu tupo na binti yako kipenzi, na habari njema ni kwamba kesho jioni atauliwa .
Ni mimi
Rafiki
Yako kipenzi
RAM””
Hayo yalikuwa ni maneno yaliyoa andikwa kwenye barua yaliyomfanya general Ramos akose nguvu na kuanguka..
Bila kupoteza mda general Ramos alitoka nje na kwenda sehemu lilipokuwa jeshi lake
“Wote kusanyikeni…” Aliongea kwa sauti wanajeshi wote wakakaa sawia kumsikiliza general.
“Leo jioni tunaanza safari ya kwenda milimani kuitafuta kambi ya Ram , mashenzi yule anataka kuniulia binti yangu. Hakikisheni mnafanya maandalizi haraka jioni safari inaanza….”
“Sawa mkuu….” Waliitikia wanajeshi kwa kishindo.
“Jordan hakikisha unawaandaa askari vizuri na mimi nitakuwa miongoni mwenu…”
“Sawa kiongozi …”aliitikia Jordan kamanda anaye aminika sana na Ramos.
General Ramos aliondoka pale na kuelekea kwenye jumba lake. Anamkuta Maria akiwa bado kwenye hali ya mawazo, taratibu anamsogelea
“Maria Leo jioni naondoka naenda milimani kumkomboa binti yetu, ondoa shaka mke wangu Wonder nitameudisha salama…”
“Umejua sehemu alipo binti yangu?….” aliuliza Maria akitokwa na machozi.
“Ndiyo ametekwa na Ram. Na nimetumiwa barua ifikapo jioni ya kesho Wonder atauliwa…”
“Ram gani huyo?….” Maria aliuliza kwa mshangao sana aliposikia Ram.
“Ram Rafiki yangu wa zamani…”
“Ram si alifaliki kwenye vita ya SK….”
“Hapana mke wangu, alikimbilia milimani na kwenda kuanzisha kundi la waasi na yeye ndo kiongozi wa hao watu …”
“Haiwezekani …” Alisimama maria kwa haraka.
“Shida nini Maria tulia tulia mke wangu ..”
“Hapana twende wote huko milimani nataka niongee nae huyo Ram hawezi akamuuwa binti yangu..”
Aliongea kwa jazba akijua fika kuwa Wonder sio mtoto wa general Ramos ni mtoto wa Ram.
“Siwezi kuruhusu uende huko,unajua kama tunaenda kupigana vita . we baki hapa mke wangu nitamleta binti yetu salama kabisa nakuahidi..”alimkalisha mkewe chini taratibu.
“Sawa nenda hakikisha binti yangu hadhuriki…”
“Nakuahidi namrudisha binti yetu salama kabisa…” Aliongea general kisha anambusu Maria kwenye paji la uso na kuondoka.
“Haiwezekani lazima niende huko milimani nikaonane na Ram…” Maria aliongea pekeyake akiwa anaingia ndani haraka kujiandaa baada ya Ramos kuondoka.
JIONI
General Ramos alichukua kundi la Askari zaidi ya mia tano na kuelekea nao milimani.
Yule mzee mganga aliye muhifadhi James nyumbani kwake akiwa msituni kutafuta baadhi ya dawa analiona jeshi kwa mbali likiwa linaelekea milimani.
“Mmmh Nchi yetu ni vita kila siku..” aliongea yule mganga akiwa anarudi kwake.
“Kijana umelala..” aliongea mganga alipofika kwenye kijumba chake.
“Hapana babu…” Alijibu James akiwa amejiegesha kitandani.
“Kuna kundi la Askari nimeliona linaelekea milimani alafu nilimuona kama na general hivi…”
“ Kweli mzee?..” alishituka na kuinuka kitandani.
“Ndiyo kijana ila tuliza jazba kwanza bado ujapona vizuri…”
Safari ya general Ramos na kundi lake la Askari ilichukua karibu siku nzima mpaka kuanza kukaribia milima ambayo Kuna kambi ya Ram.
“Mkuu pale mbele ndo Kuna kambi …”aliongea Jordan wote wakiwa wamesimama wakitizama mbele yalikuwa ni majira ya saa tisa alasili
“Inatakiwa muwe makini sana mtu tunayeenda kupigana nae ni hatari tofauti na mnavyozania nyie, Mimi nitajitokeza na Askari wachache kwenda kuongea na Ram akishanikabidhi tu binti yangu nyie wengine huku mtaanza kushambulia……” Ramos Alichukua Askari kadhaa na kuingia nao kwenye lango la kambi ya Ram, Askari wengi aliwaacha nje.
Ram tayari alikuwa ameweka mpelelezi atakaye toa taarifa baada ya kuliona jeshi la General Ramos.
General Ramos aliingia ndani ya kambi akiwa na Askari wachache, waasi wakamuweka chini ya ulinzi
“Bosi Askari na general wao wamefika tayari wanakusubiri nje…” Muasi mmoja alipeleka taarifa kwa Ram.
“Hahaha siku yenyewe imewadia” Ram Alitabasam na kutoka nje.
Ram anafika nje anakuta general Ramos akiwa na askari wachache wamewekwa chini ya ulinzi mkali .
“Aaaa Rafiki yangu kipenzi huyo hatujaonana siku nyingi sana …”
Aliongea Ram kiskaji sana baada kumuona Ramos.
“Nimekuja hapa kumchukua binti yangu nisingependa tuanzishe mazungumzo nje ya mada…”… Aliongea general akiwa chini ya ulinzi mkali wa waasi.
“Aboku mleteni huyo binti haraka …” ilitoa amri Ram macho yake yakiwa yanamtazama general Ramos kwa tabasam lakini Ramos alikuwa anaona aibu kumtazama Ram.
“babaaaaaaaa”
“Mwanangu hawajakuumiza…”
INAENDELEA……..
Bwana Leo sitaki kuongea maana inajieleza wazawazi moto utakao tokea hapo!!!!!!