PENZI LA KIKOMANDO
EPISODE YA 07
KUMBUKA NI MIAKA 20 NYUMA
TULIPOISHIA……..
“Jamani Kuna taarifa mbaya tumezipata, Ni kwamba nchi yetu inaelekea kuvamiwa na kundi la SK ambalo lipo milimani linakuja bila kupoteza mda inatakiwa twende tukawadhibiti kabla hawajaingia kwenye makazi ya raia, tumeelewana makomando?……” Aliongea general kwa sauti akiwa kizimbani.
“Maisha yetu kwa ajiri ya nchi yetu….” Waliitikia wanajeshi kwa sauti yenye kishindo.
ENDELEA….
“Jiandaeni kesho tunaanza safari kuelekea milimani na kaptain wenu atakuwa Ram. Na hakuna anayeruhusiwa kutoka nje ya kambi..”
Aliongea general akiwa anashuka pale kizimbani.
“Hongera sana Ram general anakuamini sana …” Askari walikuwa wakimpa pongezi Ramos baada ya general kuondoka.
“Asanteni sana ndugu zangu nyie wenyewe simnanijua nikishika silaha huwaga sikosei hahaha…” Aliongea Ram akiwa a naelekea ofisi ya general.
“ Mshikaji unaenda unaenda kufanya nini huko?….” Aliuliza Ramos alipoona Ram anaingia ofisi ya general.
“Nisubiri hapohapo nje mara moja….”
Ram aliingia mpaka kwenye ofisi ya general na kumkuta general akiwa anapanga nyaraka.
“ Samahani mkuu nilikuwa na shida na wewe…” Aliongea Ram akiwa amesimama mlangoni.
“Ingia Ram….”
Ram anaingia ndani na kutoa salute kwa heshima
“ General Asante sana kwa nafasi uliyonipa lakini nilikuwa naomba nikamuaga mke wangu mtarajiwa maana hana hizi taarifa….” Aliongea Ram kwa heshima sana.
“Nilipanga nitume watu waende kutangaza mjini kama Askari wao wanaenda vitani ila kivile umeomba unaweza ukaenda hakikisha unarudi haraka sana kupanga kikosi….” Aliongea general.
Ram alitoka nje akiwa na furaha moja kwa moja anaanza safari kuelekea mjini kumuaga Maria.
“Mshikaji usisahau kupitia kwa shemeji yako janeth…” Aliongea Ramos alipoona Ram ameruhusiwa kutoka nje ya kambi.
“ Siwezi nikasahau….” Ram aliongea akiwa anakimbia
Haikuchukua mda mrefu sana Ram anafika kituo cha watoto yatima, anamuona Maria akiwa amekaa kwenye bembea za watoto.
“Kipenzi umetoka kambini?….” Aliuliza Maria baada kumuona Ram .
“Ndiyo nimetoka huko lakini Kuna habari mbaya tumeambiwa leo!…. aliongea Ram akiwa ameshika kamba ya bembea.
“ Habari gani hizo mbaya?…”
“Ni kwamba kesho inatakiwa twende milimani tukalidhibiti kundi la SK linalotaka kuvamia mji. “
“Tumebakiza siku chache tufunge ndoa alafu inakuwa hivi jamani, vipi kama utapatwa na jambo baya nitaishije Mimi..” Maria aliongea akiwa amesimama.
“ Naenda huko kupambana ili wewe baba na watu wengine mbaki salama, nakuahidi nitarudi tena kwa ajiri yako endelea kunisubiri kipenzi changu… “ Aliongea Ram kwa hisia akiwa ameshika mikono ya Maria.
“Sawa nitakusubiri…..” Maria aliongea akitokwa na machozi.
Ram alimaliza kuongea na maria anamuga Maria moyoni akiwa anamaumivu makali Kisha anaondoka kuelekea nyumbani kwa Ramos ambapo anamkuta shemeji yake akiwa anafua nguo za Ramos.
“Shemeji pole na kazi lakini Ramos hatakuwepo kwa mda, kesho tunaenda vitani kikubwa maombi yenu tu …”
“ Mungu wangu mbona haraka hivyo ?…” Aliuliza janeth kwa mshituko akiwa ameacha kufua.
“Shemeji ni hivyo tu ngoja niwai kurudi nikatoe maelekezo maana mimi ni kaptain…” Aliongea Ram akiwa anakimbia kuelekea kambini
MAJIRA YA ASUBUHI
Baada ya kushinda usiku mzima wakifanya mazoezi hatimaye majira ya saa kumi na moja za asuhi wanajeshi wanaanza safari kuelekea milimani wakiongozwa na Ram.
Safari yao ilikuwa ni ndefu sana iliyowaradhimu wapande na kushuka milima mikubwa wakiwa njiani.
Majira ya saa tatu za usiku wanafika mlima wa vita ambao kundi la SK waliweka kambi yao hapo.
“Ramos wewe pita huku na Hawa Askari alafu mimi naenda huku na hawa waliobaki tuwe kama tumeizunguka kambi ya SK….” Aliongea Ram kwa sauti ya chini akiwa anatembea kwa kunyata .
Ramos na askari wengine kadhaa walipita upande wa kushoto na Ram upande wa kulia akiwa na askari wenginekwa lengo la kuizunguka kambi ya SK.
Taratibu walianza kuingia ndani ya kambi wakiwa wameizunguka na kuiweka katikati, lakini Kuna onekana kukiwa na utulivu mkubwa kana kwambahakuna watu wanaoishi ndani ya hiyo kambi iliyokuwa imetapakaa mahema mengi.
Waliendelea kusogea taribu wakielekea yalipo mahema ya kulalia.
Ram alimuona Ramos yupo upande wa pili, akampa ishara ya kushambulia mahema yote yaliyokuwa katikati yao wakiamini ndani ya mahemakutakuwa na vikosi vya SK vimelala.
“Shambuliaaaaaaa” aliongea Ram kwa sauti kubwa askari wa pande zote wakaanza kupiga risasi yale mahema.
Baada ya kushambulia kwa mda mrefu ukimya unatawa eneo lile na Ram taratibu anasogea kwenda kufunua mahema waliyokuwa wakiyapiga risasi kwa muda mrefu.
“Haiwezekani …” Aliongea ram alipokuta ndani ya hema moja patupu akaendelea kufunua mengine haraka haraka nako anakuta patupu.
“Washenzi hawa wametuchezea mchezo tuwe makini hapa….” Aliongea Ram akiwaanarudi nyuma kwa haraka .
Ram akiwaanarudi nyuma mala taa nyingi zinawaka kutokea katika kila upande waliopo na kujikuta wapo katikati ya kundi la SK.
“Haiwezekaniiiiii hakuna kusalimu amri shambuliaaaaaaa..” Aliongea Ram kwa sauti kubwa baada ya kuona wamewekwa kati na SK.
**************************************************************************
*Hii vita walishinda kweli na sababu gani iliyomfanya Ram awe kiongozi wa waasi.
*HAPO TULIRUDI NYUMA KUPATA HISTORIA YA GENERAL RAMOS NA RAM ILI TWENDE SAMBAMBA NADHANI TUTAKUWA TUMEANZA KUELEWA KITU HAPO.👌
🔥🔥
*Kumbe Maria alikuwa mchumba wa Ram kwanini miaka hii tunamuona na General Ramos
*Na vipi kuhusu janeth mke wa zamani wa general Ramos yupo wapi mbona miaka hii hatumuoni
PENZI LA KIKOMANDO
EPISODE YA 08
TULIPOISHIA….
“ Haiwezekani hakuna kusalimu amri, shambuliaaaaaaa…”Ram aliwaambia Askari kwa sauti kubwa baada ya kuona wamezungukwa na kundi la SK.
ENDELEA….
Milio ya risasi ilianza kutawala milimani majira hayo ya usiku .
Kundi kubwa la Askari wanapoteza maisha, Askari waliosalia wanajibana kwenye shimo dogo na kuendelea kupambana na kundi la SK ambalo lilikuwa limewazunguka pande zote.
“Kaptain tumezidiwa sana tunafanyaje?….”
“Hakuna kukata tamaa tupambane kwa ajiri ya tuwapendao mpaka umauti utakapo tufika …” Aliongea Ram kwa sauti akiwahamasisha wenzake waliokuwa wameanza kukata tamaa akiwa anaendelea kufyatua risasi.
“Oya mshikaji nipe bomu haraka….” Aliongea Ramos akiwa mbali kidogo na alipo Ram.
Ram anaingiza mkono wake ndani ya kombati anatoa bomu na kumrushia Ramos .
“ Ngoja niwasambazie upendo washenzi hawa….” Aliongea Ramos baada ya kulidaka bomu akatoa lock na kulirusha nyuma walipokuwa watu wa SK.
Usiku huo hakika ulikuwa ni usiku wa kibabe uliotawaliwa mianga ya risasi na Moto wa mabomu.
Askari waliendelea kuuwawa wengi kwa kupigwa risasi , wanabakia askari sita Ram, Ramos na wengine wanne wanaendelea kupambana wakiwa wamejibana ndani ya shimo.
“Wamebakia wachache tujitahidi tuwamalize wasisogee eneo letu watatuwai ….”aliongea Ram akiwa anapiga risasi kwa wingi .
Jitihada za Ram na Ramos zinapelekea kuangusha kundi kubwa la maadui .
Kundi la SK lililo salia liliendelea kuwakaribia askari waliojibana kwenye lile shimo .
“Mtafia humo humo nyie wajinga….” Aliongea SK mwenyew akiwa anasogea na watu wake eneo walilo jificha Ram na wenzake watano mkononi mwake yakionekana mabomu .
“Kimbieni bomu hilo ….” Ram aliongea kwa sauti baada ya kuona SK anarusha bomu wenzake wote wakaruka kutoka mle ndani ya shimo.
Ram alikuwa wa mwisho kutoka ndani shimo ilipelekea bomu limtupe mbali zadi ya wenzake.
“Haya vijana mlijiona nyinyi ni wajanja baada ya kuniulia vijana wangu hahahaha mmeingia kwenye mtego wangu leo wote mtakufa…”
Aliongea SK Askari wote wakiwa chini wamechafuka moshi usoni na Ram akionekana kuwa na hali mbaya kushinda wenzake .
“ kaptain upo sawa?… Aliuliza Askari mmoja alipoona Ram amelala chini mwili wake ukiwa kama wa mtu aliyekufa .
Ram hakuweza kuchezesha hata kiungo kimoja wenzake wakapigwa na butwaa wakiamini tayari kaptain wao amekufa.
“Ram amka basi unatuachaje hivi …” Ramos aliongea akiwa amelala chini mbali kidogo na mwili wa Ram.
“Hahahahaha huyu kaptain wenu tayari amekufa mmebakia nyinyi tu..” aliongea SK kwa kucheka akiwa anaeleka ulipo mwili wa Ram ili ahakikishe kama kweli Ram amekufa.
SK anaugeuza mwili wa Ram ambao mgongo ulikuwa juu na tumbo chini.
“Kaptain wenu ameshakufa vijana….” Aliongea SK baada ya kuona Ram amefumba macho lakini ghafla Ram anafumbua macho, anasimama kwa haraka na kumkaba SK kisha anachomoa kisu kiunoni kwa haraka sana na kumuwekea SK shingoni.
“Hahaha kijana kumbe ulikuwa ukinichezea mchezo…” Aliongea SK akiwa amenyosha mikono juu Kundi lake likiwa limeelekeza siraha kwa Ram.
“Shusheni siraha zenu lasivyo nitamuuwa kiongozi wenu…” Aliongea Ram akiwa anarudi nyuma na SK.
Watu wote wa SK wakashusha siraha zao wakihofia kiongozi wao anaweza akauliwa.
“Haya rudini nyuma …” Aliongea Ram watu wa SK wakaanza kurudi nyuma taratibu.
Askari wengine waliokuwa wamelala chini taratibu wananza kupata nguvu.
“Nilijua tu mshikaje huwezi kufa kizembe wewe unaakili nyingi sana!….” Aliongea Ramos akiwa anasimama na wenzake wanne waliobaki.
“ nyie ondokeni hapa kwanza ….” Ram aliwaambia wenzake akiwa amembana shingo SK .
Ramos na askari wengine wanne wanaondoka pale mbele ya watu wa SK, wanamuacha Ram pekeyake kwenye kizahazaha.
“Nimewambia msinisogelee…..” Aliongea Ram alipoona watu wa SK wanasogea mbele.
“Kijana kama unaweza kunia niuwe uone…”aliongea SK kwa kujiamini sana alipo maliza kuongea hapohapo Ram alipitisha kisu chake kwenye shingo ya SK na kuitenganisha shingo na kiwiliwili.
Watu wa SK kwa hasira sana walianza kufyatua risasi wakitaka kumuuwa Ram lakini Ram aliutumia mwili wa SK kama ngao ya kuzuilia risasi,
Mda huohuo anatokea Ramos nyuma ya watu wa SK akiwa na mtutu uliotoa risasi kama maji na kuwaangamiza watu wa SK kwa haraka sana.
“Hatimaye tumefanikisha ….” Aliongea Ram kwa furaha akiwa anapeleka mkono wake ndani ya suruhali aliyokuwa amevaa SK Kisha anatoa Gold key na kuuangusha mwili wa SK chini.
“Hiyo ni gold key?….” Aliuliza Ramos akiwa mbali kidogo
“Ndiyo mshikaji nimeipata lazima nitakuwa General kwa kuupata huu ufunguo wa dhahabu…..”aliongea Ram uso wake ukiwa na tabasamu zuri licha ya kuchafuka moshi.
“Hongera sana mshikaji tumefanikisha misheni….”
“Licha ya kwamba tumepoteza wenzetu wengi ila umoja wetu ndiyo uliofanya tufanikishe hili, wengine wapo wapi niwape pongezi? .. “ aliongea Ram akiwa anatembea kwa furaha anasogea alipokuwa Ramos mkononi akiwa na gold key.
“Nimewauwa wenzetu wote… “ Aliongea Ramos sura yake ikiwa imebadilika na akionekana mwenye hasira sana, hapohapo anasimamisha mtutu wake na kuelekeza alipo Ram, Ram anasimama na kubaki akitaharuki kama aamini amini kitu anachokiona.
******************************************************************
*Balaaaaa ndo hilo bwana kama kawaida yetu mambo ni Moto kila siku.
USIKOSE IJAYO TUTATOKA MPAKA KWENYE HII STORY YA RAMOS NA RAM TUTARUDI MAISHA YA SASA TUNAKOMUONA JAMES YUPO MAUTUTI.
PENZI LA KIKOMANDO
EPISODE YA 09
TULIISHIA
Ramos anamgeka Ram mwenzake na kumnyoshea siraha . Ram alishangaa sana baada ya kugundua kuwa Ramos ameuwa Askari wenzake wote alafu akitaka kumuuwa na Ram .
ENDELEA……..
Ramos umepatwa na nini mshikaji unataka kuniuwa!, mbona umebadilika hivyo ?. aliongea Ram kwa mashaka akiwa amenyoshewa Siraha na ramos
“Umechukua vitu vyangu vingi sana Ram na hii siku nilikuwa naisubiri kwa hamu sana nikumalize mshenzi wewe…”
Aliongea Ramos akiwa anaendelea kumnyoshea siraha Ram.
“Mshikaji nimekutendea kitu gani kibaya?..mbona tuliishi pamoja kwa upendo….”
Aliongea Ram furaha yote ya kushinda vita ikiwa imepotea usoni mwake.
“Ram unajua kosa kubwa ulilofanya ni kutaka kufunga ndoa na Maria…” Aliongea Ramos kwa hasira.
“Kwanini nisimuowe Maria sasa?…”
“Maria Ni mwanamke ambaye ninampenda sana lakini sikuwahi kupata nafasi ya kumuelezea hisia zangu, nilihisi hawezi kunikubali sababu tayari nilikuwa na janeth….” Aliongea Ramos, ram alishituka baada ya kusikia hayo maneno.
“Kumbe na wewe ulikuwa unampenda maria! Sasa hiyo ndiyo sababu umeuwa Askari wenzako na mimi unataka kuniuwa kwa lengo hilo ety….” Aliongea Ram kwa hasira sana.
“Sio hilo tu, pia naitaka hiyo gold key uliyochukua kwa SK, mimi ndo nastahili kuwa general na wala sio wewe…” Ramos aliongea akiwa mbali kidogo na Ram.
“Ahaaa kumbe hiyo ndiyo nia yako msaliti mkubwa wewe hupati kitu hapa…” Aliongea Ram akiwa anageuka na kuanza kukimbia.
Ramos anaanza kumimina risasi kama kichaa akiwa anamkimbiza Ram . Risasi moja inampiga Ram mguu wa kushoto na kupelekea kasi yake kupungua. Ram anaendelea kujikokota akiwa anachechemea mguu mmoja lakini mbele yake anakutana na bonde kubwa lililoenda chini kina kirefu sana.
“Hahaha Rafiki yangu kipenzi ulikuwa unajaribu kunikimbia Mimi hahaha. “ Aliongea Ramos akiwa anahema kwa nguvu mkononi akiwa na bunduki Ram akiwa amesimama kwenye lile bonde ambalo chini kabisa kulikuwa na maji.
“Ramos ni kweli unataka kuniuwa mimi Rafiki yako, kumbuka Kuna watu wananiitaji mimi tafadhali naomba uwe mpole?…” Aliongea Ram kwa uchungu akishika sehemu ya paja aliyopigwa risasi.
“ Nitafikilia hilo mshikaji lakini nipe kwanza hiyo gold key uliyoishika….” Aliongea Ramos akiwa ameelekeza bunduki kwa Ram aliye simama pembeni na bonde. Ram alirusha gold key mpaka alipokuwa Ramos Kisha anaidaka na kuibana kiunoni.
“Nimekupa gold key unaweza kwenda kuwa kiongozi badala yangu lakini naomba usifanye hicho unachotaka kufanya…”
“Hahaha Pole sana mshika ndiyo nakuuwa hivi …” Aliongea Ramos akiwa anataka kufyatua risasi lakini kwa haraka sana Ram aliona ni bora ajitupe kwenye lile bonde kuliko kuuliwa na rafiki yake.
“Mpumbavu sana huyu ameamua kujiuwa mwenyewe.. “ Aliongea Ramos akiwa anasogea kuangalia chini alipo dondoka Ram.
“Kwisha habari yake ….” Aliongea Ramos akiwa anaondoka .
KAMBINI
Ramos anarudi pekeyake kambini akiwa amechafuka damu mwili wote.
“Kamanda amerudi!…” Aliongea Askari mmoja baada kumuona Ramos.
Moja kwa moja watu wanakusanyika kambini baada ya kumuona Ramos wakitaka kujua nini kilichotokea vitani.
General alipatiwa habari njema na Ramos ya kwamba SK gaidi aliyeisumbua nchi kwa miaka mingi ameuwawa.
Watu wote waliokusanyika pale, walipiga kelele nyingi za furaha baada ya kusikia SK ameuliwa
“Sasa vipi kuhusu kaptain na Askari wengine, wote wameuwawa?…”aliuliza general akiwa pale nje watu wengine wakiendelea kushangilia ushindi.
“Ndio wote wameuliwa lakini cha kushangazwa ni kwamba kaptain Ram kumbe alikuwa anamakubaliano na SK tulipokuwa katikati ya vita alitugeuka na kuwa upande wa adui lakini hatukukata tamaa Mimi na wenzangu tulipambana mpaka mwisho na tukafanikiwa licha wenzangu kupoteza maisha, na nimefanikiwa kupata gold key aliyoibiwa gavana wetu wa zamani na SK…”aliongea Ramos akiwa anatoa Gold key kiunoni.
“Huyu ndiye shujaa wetu mpya, na ndiye atakaye ongoza baada yangu……” Aliongea general kwa sauti kubwa baada ya kuona gold key watu wote walipiga kelele za shangwe wakiwa wanambeba Ramos juu juu.
Baada ya hapo kila sehemu ya mji ilitangaziwa habari hizo za ushindi, na habari mbaya zilisambazwa kuhusu usaliti aliofanya kaptain Ram akiwa vitani.
Wananchi wenye hasira kali walienda kubomoa nyumba ya Ram wakiamini alikuwa ni msaliti wa nchi yake.
NYUMBANI KWA RAMOS
Ramos anarudi nyumbani kwake kisindikizwa na kundi la Askari waliokuwa wakimlinda sababu general Alisha toa tamko kwamba Ramos ndiye atakaye beba mikoba yake.
“Mme wangu huyo…..”aliongea Janeth kwa furaha akiwa anamkimbilia Ramos ili amkumbatie, cha kushanga Ramos anampisha Janeth bila hata ya salamu na kuelekea ndani.
“Kipenzi mbona kama haupo sawa unajua nilikumiss mwenzako ….” Aliongea janeth akiwa anamfuata Ramos ndani, Askari wengine wakiwa wamesimama nje.
“ Chukua mabegi yako ondoka nyumbani kwangu …..” Aliongea Ramos baada ya kufika chumbani na janeth
INAENDELEA…..
USIKOSE IJAYO…..
Kifo kibaya chamtokea binti mrembo…Nani huyo? Usikose episode ijayo
• Baada ya Ram kuanguka katika like bonde alikuwaje kuwaje kwa usalama wake.
*Ndoa ya Ramos yafungwa