JASMINE
Jasmine akiwa anatembea kwa madaha kuelekea nyumbani, kwa mbali alimwona kijana akija nyuma yake mbio sana ,jasmine hakuelewa ni nini kinaendelea aliendelea kujitembeza kwa madaha na mikogo kama yote,jasmine akiwa anaendelea kutembea alisikia sauti ikiita “jasmineeeeeeeeeeeeee subiri ‘’
Kwa dharau jasmine aligeuza shingo lake nyuma kumtizama ni nani anayemwita ,kijana Yule aliendelea kusogea karibu kabisa na jasmine kisha akapiga magoti chini na kuanza kusema
“jasmine mambo ,,uko salama sijui kama unanikumbuka mimi’’
“mhhh wewe ni nani na unataka nini’’
“jasmine umenisahau siku moja nilikufuata nikakuomba tuwe wapenzi ‘’
“ee kwahiyo umesahau nilikwambiaje ,,,siwezi kuwa na wanaume kama wewe ,mwanaume mwenyewe unanuka jasho wakupeleka wapi wewe unaona hii njia uliyokuja nayorudi ulikotoka maana nishaanza kusikia kichefu chefu’’
Hadson aliinama chini kwa uchungu machozi yake yalidondoka kwenye ardhi mithili ya matone ya mvua ,jasmine hakujali aliendelea mbele taratibu akiwa ameshikilia simu yake kubwa sana mkononi huku akiwa anaperuzi mtandaoni.
Jasmine ni msichana aliyezaliwa katika familia moja maskini sana iliyopo mbagala dar-es-salaam ila kutokana na shida nyingi katika familia yao jasmine akiwa mdogo alichukuliwa na familia moja ili alelewe
Miaka takribani kumi na mbili iliyopita katika mtaa wa mbagala watoto wawili walikua wakitembea ,watoto hao walikua wamekondeana sana ,walikua wakitokwa na kamasi ,mainzi yalikuwa ya kiwasonga na kuwang’ata kila kona ya miili yao ,,,hali watoto hao wakiwa wanatembe huku mikononi wakiwa wameshikilia madumu ya maji mikononi gari moja ya rava4 ilifunga breki mbele yao ,,Jasmine akiwa na kaka yake pita waliogopa sana na kuanza kutetemeka ,waliogopa sana kwani mama yao alishawaambia wanapaswa kuwa makini na watu wenye magari kwasababu watoto wadogo mara nyingi huibiwa katika mtaa wao
Watu wawili walishuka ndani ya gari lile na kuanza kuzungumza na wakina jasmine
“toto hamjambo jamaniii’’
“hatujambo shikamoo mama shikamoo baba’’
Jasmine na pita walisalimu kwa heshima ,wazazi wale waliitikia kisha waliendelea
“kwenu ni wapiii watoto wazuri’’
Pita kaka wa jasmine kwa ishara ya kidole aliwaelekeza
Kwa haraka waliwapakia ndani ya gari na kuelekea kwao ,walipofika baba na mama mzazi wa jasmine walishangazwa kuona gari likiingia nyumbani kwao
Mzee john aliwasalimu wazazi wa jasmine na kujitambulisha vyema sana ,baada ya kujitambulisha alimweleza baba mzazi wa jasmine kuwa amependezwa na jasmine anaomba akakae nae amtunze na kumsomesha
Kutokana na wingi wa shida katika familia ya jasmine wazazi wake hawakuwa na kipingamizi ,wote kwa pamoja walikubaliana jasmine alifungasha vijinguo vyake tayari kabisa kwa safari ya kuelekea ugenini kwa mzee john na mama sweet,ndani ya lisaa jasmine alifikishwa katika familia mpya sehemu ijulikanayo kama masaki ,masaki ni sehemu moja ya jiji la dar-es-salam sehemu wanayoishi matajiri wa mji.
Jasmine alishangazwa sana na mazingira yale aliona vitu vya kifahari ambavyo kamwe hajawahi viona maishani,alilelewa pale kwa miaka kadhaa ndani ya siku chache tu aliweza kuyamudu mazingira na kuwa mzoefu kabisa wa jiji
Baada ya miaka sita kupita jasmine alinawiri sana mwili wa kisichana ulianza kuumbika ,jasmine alikua na shepu nzuri sana iliyokuwa ikiwavutia kila waliokuwa wakimtizama ,uzuri wake ulijionyesha waziwazi kwa watu waliokuwa wakimtizama ,jasmine alipomaliza darasa la saba hakufanikiwa kuendelea na masomo yake kutokana na ufaulu wake kutokuwa mzuri
Siku zilienda miaka ilikata umbo na shepu ya jasmine viliendelea kuwapumbaza vijana si madereva taksi si wafanya kazi wa serikali kila mmoja alikua akimtamani jasmine
Jasmine alielewa fika kuwa yeye ni mzuri hivyo aliringa kupindukia macho yake alikua akiyarembesha mwili wake aliuviringisha kwa makusudi kabisa ili tu kuwapagawisha vijana,na kweli alifanikiwa kwani kila aliyemwona alihisi kuchanganyikiwa alijikuta akimfuata nakuanza kumtongoza
Mzee john mlezi wa jasmine alimfungulia jasmine duka kubwa la nguo za kisasa kutoka dubai ,jasmine alifurahi sana na kuanza kazi hiyo,,,
Haikupita mwezi jasmine aliingiza shoti kubwa sana katika biashara ile mama sweet mama mlezi wake alimshauri jasmine na kumweleza wazi kuwa asichanganye mapenzi na kazi ,pia alimweleza kwa kina kuwa wanaume ni watapeli ,jasmine hakujali aliitikia kishingo upande tu ,vijana mbali mbali walifunga breki nyumbani kwa mzee john kwa ajili ya kumtaka jasmine ,jasmine alikua akiringa sana na hakutaka kuwaelewa kabisa ,hakuweza kutofautisha kati ya mwanaume wa kweli na mwanaume wauongo kwa upande wa jasmine mwanaume mwenye hela kwake ndio mwanaume wa thamani
jasmine akiwa anatembea kwa madaha kuelekea kazini, kwa mbali alimwona kijana akija nyuma yake mbio sana ,jasmine hakuelewa ni nini kinaendelea aliendelea kujitembeza kwa madaha na mikogo kama yote,jasmine akiwa anaendelea kutembea alisikia sauti ikiita “jasmineeeeeeeeeeeeee subiri ‘’
Kwa dharau jasmine aligeuza shingo lake nyuma kumtizama ni nani anayemwita ,kijana Yule aliendelea kusogea karibu kabisa na jasmine kisha akapiga magoti chini na kuanza kusema
“jasmine mambo ,,uko salama sijui kama unanikumbuka mimi’’
“mhhh wewe ni nani na unataka nini’’
“jasmine umenisahau siku moja nilikufuata nikakuomba tuwe wapenzi ‘’
“ee kwahiyo umesahau nilikwambiaje ,,,siwezi kuwa na wanaume kama wewe ,mwanaume mwenyewe unanuka jasho wakupeleka wapi wewe unaona hii njia uliyokuja nayorudi ulikotoka maana nishaanza kusikia kichefu chefu’’
Ndivyo jasmine alivyokuwa akikatalia wanaume
Siku moja jasmine akiwa dukani kwake aliona gari limefunga breki mbele ya duka lake
Alishuka kijana mmoja wa kihindi mwenye mvuto wa kipekee jasmine alipomwona moyo wake ulidunda kwa woga na matamanio alitamani sana kijana Yule angekuwa wake ,kwanza kijana ni mtanashati pili anaonyesha kuwa anahela ,kijana Yule alisogea pale alipokuwa jasmine ,
“hellow habari gani’’
“salama mambo’’
“muzuri habari ya wewe ‘’
“nzuri karibu’’
“mimi taka hii suruali pesa ngapi’’
“sawa suruali 30 elfu’’
“haha pesa ndogo hiyo chukua hamsini kwanza wewe toto zuri sana unaitwa nani’’
“`jasmine ‘’
“jasmine penda sana wewe nataka kukuoa wewe tuende Mumbai india ‘’
Jasmine hakuamini alichoambiwa jasmine siku zote alikua akipendelea wanaume matajiri hivyo kwake hiyo aliona ni fursa kubwa sana alifurahi kupita maelezo
Aliondoka haraka kwenda nyumbani kwa walezi wake aliwatupia funguo za duka na kuwaambia kwaherini asanteni kwa kunitunza
Mama sweet mlezi wa jasmine hakuamini aliita kwa sauti “jasmineeeeee mwanangu ‘’ ila jasmine alikua kama mtu aliyewekewa pamba maskioni alikimbia kuelekea alipo muhindi Yule
“ahaaa jasmine toto zuri sana umerudi twende tuondoke ‘’
Feraz alimchukua jasmine na kumpakisha kwenye gari alimpeleka mpaka kwa wazazi wake ,,mzee Mohamed alifurahi sna alipomwona jasmine mama wa feraz pia alifurahi sana wote walijisemea binti huyu atatufaa ‘
Ilipofika asubuhi jasmine alipanda meli tayari kabisa kwa safari kuelekea india ,ilipofika saa mbili usiku jasmine alifika jiji la Mumbai
Kwa haraka aliingizwa katika chumba kizuri kilichopambwa feraz waliingia nae ,feruz alilala na jasmine usiku kucha alimchezea na kumfanyia vitimbi vyote alivyoweza ,ilipofika asubuhi jasmine alipelekwa nje feruz alianza kumtambulisha mbele ya wakina dada wa kihindi
“hii mutu nimeitoa Tanzania itatusaidia usafi na kazi za ndani’’
Jasmine aliposikia hivyo alishtuka sana alilia kwa uchungu sana hakuamini maneno aliyoyasema feraz ,,mwanzo feraz alimwambia kuwa atamwoa ila hali haikuwa vile
Jasmine alianza kukondeana ndani ya siku chache tu ,feraz alikua akimtumia jasmine apendavyo kila akimwitaji alimchukua na kulala nae hayo ndio yalikua maisha ya jasmine.
Jasmine alilemewa sana na majukumu akiwa nchini india aliyakumbuka sana maisha aliyokuwa Tanzania aliwakumbuka vijana wengi sana waliokuwa wakimtongoza Tanzania na kuwakatalia ,alilia sana ila alikua ameshachelewaa