DADA VUA BANAH..
Sehemu Ya 16
……….ilipoishia
Wakati baba na mama walikuwa wakiagana kwa kupeana mautamu vitu urojo urojo.
Huku sule huku sule mambo yalikuwa magumu balaa.
Lakini alipomuona Shangazi yake na helena alishtuka sana kwani alitokea ghafla tuu.Hali hiyo ilimpa mashaka sana Sule.
Wakati anaduwaa alishangaa kuona shangazi anawazuia wale wanyama ambao ni kina Helena.
Shangazi aliongea kwa sauti ya kutisha”Tabia yako ndio imekusababisha uko hukuuuu!!! na ulivyo na tamaa ulitaka kuzini na dada zako mbwa wewe……
Shangazi aliwakamata kina Helena kwa kitambaa cheupe na kuwazuia wasimdhuru Kijana sule.
Sule hakuamini kama mpaka dakika hiyo yuko mzima kwani alishaamini ndio mwisho wake.
Shangazi hakutaka kumficha alimpasulia sule japo sule hakuelewa moja kwa moja ni dada zake kivipi maana ni kitambo sana walifariki na hakuwaza kuhusu ushirikina.
Basi Shangazi Alimtazama Sule huku ameikunja sura yaani alikaa kikazi zaidi si unajua mambo ya kichawi tena.
Shangazi aliongea “Vijana wa siku hizi mnapenda kuvamia vamia wanawake ungezini na dada zako na hizo tamaa za kijinga,Na ulikuwa na nafasi nzuri sana kwani nyota yako ni ya bahati lakini hizo tamaa zimekuponza”.
Sule alimsikiliza Bi kidako lakini hakumuelewa kwani hajui chochote alibaki kumshangaa tuu.
Wakati huo dereva alifika mpaka hotel moja inaitwa MOMELA HOTEL maana aliambiwa apitie njia hiyo atakutana na sule njiani,Alizidi kuingia ndani zaidi yaani porini lakini hakuona mtu.
Kwa sababu ilikuwa ni usiku aliogopa kuendelea mbele kwani ni porini na alikuwa mwenyewe tuu.
Alifika mahali akasimama na kupark gari pembeni”
Sasa huyu mtu yuko wapi??”
Alijiuliza bila kupata majibu kisha akaegesha gari yake kando ya barabara na kumngoja.
Yaani dereva alibakiza mita chache eneo ambalo Sule,Shangazi na kina Helena walikuwepo.
Wakati huo Mama wa Sule alipomaliza kumfurahisha mzee wake aliomba ruhusa kwa mumewe atoke kidogo kwani mama anamdai hivyo kamwita akachukue pesa yake.
Mumewe kwa kuwa tayari alishapata haki yake hakuwa na hofu hata kidogo.
Alimruhusu bila shaka”Nenda lakini usikawie maana usiku saiz”Mama alienda parking na kuchukua gari safi na kutoka.
Mama aliondoka na kuelekea Mount meru hotel.
Alipofika alimchukulia mwanae chumba kizuri sana na ilikuwa ni chumba namba 15.
Wakati huo yule dereva aliyetumwa kumfuata Sule alikata tamaa kwani aliona kama anasubiri hewa tuu yaani hakuna mtu.
Aliwasha gari yake kisha akaenda mbele kidogo ili apate sehemu ya kugeuzia gari.
Sasa wakati anatafuta sehemu ya kugeuzia,Mwanga wa taa za gari ulikutana na macho ya wale wanyama ambao ni kina Helena,
Dereva presha,Woga vilianza kumuingia kwani yeye si mzoefu wa porini.
Aliigeuza gari kwa spidi ya haraka,Alirudi mpaka momela hoteli Alisimama na kumpigia simu mama yake Sule”
Haloo mama,Yaani mama hii ni adhabu mama yangu huwezi amini nimekutana na masimba huku.
Kiukweli mama mi siwezi narudi tuu Sule mwenyewe simuoni mimi”……..
Mama alimjibu”Hapana usifanye hivyo nakuomba sana usiache kuja na Sule nakuahidi nitakulipa mara mbili ya tulivyokubaliana”.
Dereva mwenyewe mchaga sasa ukimtajia mambo ya hela anachanganyikiwa kabisa,Alikubali lakini hakurudi tena kule alibaki pale pale hotelini.
Huku kwa Sule Bi kidako aliamua kumsamehe lakini alimpa onyo”
Kuwa makini na zipu lako la sivyo utajua mi ni nani?, Na ukiondoka hapa uelekee nyumbani”Sule alivyosikia vile hakutaka kuchelewa hadi begi aliliacha.
Alitoka spidi ya hatari,Bi kidako alicheeeka kwa dharau kisha akawarudisha kina Helena katika hali yao ya kawaida.
Wakati Bi kidako anajiandaa kurudi na shangazi zake nyumbani simu yake iliita,
Aliichomoa pale kwenye kile kimfuko cha kuvaa shingoni,Aliangalia namba iliyopiga alifurahi na kumwambia
“Kazi imekwenda vizur sana mwanangu sasa mwambie huyo kijana aliyemfuata amngoje barabarani anapitia barabara kubwa ya Usa”……..
“Sawa mama yangu nashukuru sana na lile swala letu hakikisha kesho linakaa sawa”………
Bi kidako alijibu kwa dharau”Mwanangu hivi huniamini mie sasa akipanda tuu ndege utasikia habari yake muda mfupi tuu”……..
Mama wa sule alifurahi sana kisha akauliza tena,
“Vipi hali ya hao kina Lucy??”……
“Kina Lucy wako vizur ila tuu mwanao huyu Sule alitaka kuvuruga mambo kwani alitaka kuzini na nduguze bila kujua na ingekuwa ni hatari sana kwa upande wenu,Ila nashukuru nilifanikiwa kuzuia hali hiyo”.
Mama yake Sule alifurahi sana.
Baada ya mazungumzo Mama yake Sule alimpigia dereva na kumwambia awe makini Sule asipitilize maana anapita pale muda si mrefu”Wewe Dereva kuwa makini asikupite amevaa kaushi nyeupe na suruali ya blue”…..
Sawa mama niko makini kuliko unavyofikiria,Ebu ngoja!!!!! subiri!!!!”……..
Wakati wanaongea na simu kwa mbali aliona mtu anakimbia kwa kasi sana.
Kwa kuwa dereva aliipaki gari ikiwa imeelekea huko alipoambiwa sule yupo,Basi aliwasha taa ili ajue kama ni sule ndiye anayekuja.
Ni kweli alikuwa ni sule na alikuwa akikimbia sana,Sule alipoona anapigwa na mwanga wa gari alisimama kwanza kwani alishajua kuwa Bi kidako ni mchawi hivyo kila kinachomtokea alijua ni uchawi.
Sule alijishauri”
Niende au nisiende!!?”Mara dereva yule alimpigia honi”
Piiiipiiii!!”,Kisha akashuka na kumuita
“Suuule!!!”.
Ukweli ni kwamba sule aliingiwa na woga alisimama kwa muda mrefu sana pale.
Dereva kwa kuwa alishajua huyu ni Sule alimfuata aliamua kumfuata.
Wakati huo Bi kidako alikuwa anarejea kwenye nyumba yake akiwa na kina Lucy,Wakiwa wanatembea Lucy aliona begi la Sule”Heee!! Shangazi nini kimetokea mbona begi la sule liko hapa na linaonekana limetupwa!!?”……
Kina helena wakibadilika huwa hawajui kilichoendelea hivyo hawajui nini kimeendelea baada ya kugezwa wanyama labda shangazi yao awasimulie,Shangazi alijibu
“Achaneni na huyu kichaa”
Lucy alibeba begi hilo kaenda nalo mpaka ndani.
Kwa kuwa Lucy na Helena wanalala chumba kimoja basi walianza kupekua begi lile kwa pamoja na kukuta mapicha mengi Sule akiwa katika majumba ya kifahari na warembo.
Walikuta business card yenye anwani na namba za simu zenye jina SULEIMANI.
Helena alichukua ile business card na kwenda kuichukua simu ya shangazi yao ili wajaribu kupiga ile namba……
.Nini kitaendelea,Usikose kigongo hichi kitamuuu kesho maana story yetu yote imebebwa na episod ya 17,
DADA VUA BANAH..
Sehemu ya 17
……ilipoishia
Dereva kwa kuwa alishajua huyu ni Sule aliamua kumfuata.
Wakati huo Bi kidako alikuwa anarejea Owen’s nyumba yake akiwa na kina Lucy,Wakiwa wanatembea Lucy aliona begi la Sule”Heee!! Shangazi nini kimetokea mbona begi la sule liko hapa na linaonekana limetupwa!!?”……
Kina helena wakibadilika huwa hawajui kilichoendelea hivyo hawajui nini kimeendelea baada ya kugezwa wanyama labda Shanghai yao awasimulie,Shangazi alijibu”Achaneni na huyu kichaa”Lucy alibeba begi hilo kaenda nalo mpaka ndani.
Kwa kuwa Lucy na Helena wanalala chumba kimoja basi walianza kupekua begi lile kwa pamoja na kukuta mapicha mengi Sule akiwa katika majumba ya kifahari na warembo.
Walikuta business card yenye anwani na namba za simu zenye jina SULEIMANI.
Helena alichukua ile business card na kwenda kuichukua simu ya shangazi yao ili wajaribu kupiga ile namba.
ENDELEA NA NAOMBA UDONDOSHE LIKE YAKO MAANA NI MUHIMU.
Wakina Helena baada ya kuchukua simu waliipiga ile namba lakini haikuwa hewani.
Walitamani kutuma ujumbe lakini kwa kuwa hawakusoma basi hawakuwa na uwezo wa kuandika,Helena na dada yake Lucy walitoa zile kondom kwenye begi la sule na kuanza kuzicheze mara waingize vidole mara michezo ya ajabu ajabu ilimradi tuu wafurahi.
Wakati huo Sule tayari alishapanda kwenye gari kwani dereva alijaribu kumuelewesha kuwa ametumwa na mama yake na si vinginevyo.
Mama yake sule alifurahi sana kuisikia sauti ya mwanae,Aliwaambia wakifika philips wasimame kwanza kwani yeye yuko hapo.
Baada ya dakika kama 15 walifika maeneo ya philips,Mama alishangaa kuona mwanae yuko rafu rafu,hana kiatu kimoja,Manywele yako hovyo hovyo.
Mama yake sule alimtazama mwanae akaanza kumuone huruma.
Alimchukua na kumuingiza kwenye gari yake kisha akalipia ile tax na kuondoka akiwa na mwanae.
Walienda mpaka NAKUMATT SHOPPRITE kisha akamchukulia nguo na viatu kisha akampeleka hoteli alikomchukulia chumba kwa ajili ya kulala.
Mama alipofika akamuagizia chakula VEGETABLE TOSTADA chakula safi sana.
Wakati wanaendelea kusubiri chakula Sule alianza kumsimulia mama yake mkasa wote kule alikokuwa,Mama aliposikia majina ya watoto wake alianza kutamani kuwarejesha ili wafurahie pesa na mali atakazokuwa nazo bila kufikiria kuwa chanzo cha pesa hizo ni hao watoto.
Mama alimwambia sule”Kwanza pole sana mwanangu halafu nia na madhumuni ya kukufikisha hapa ni”..
Mama aliongea huku akizitoa hati na nyaraka zote za mali ya familia”Tazama hizi mwanangu”Alimpa mwanae azione.
Basi sule alizitazama huku akionyesha mshangao kwani hakuwahi kufikiria suala la kumiliki vitu vingi hivyo.
Sule kakopi tabia ya mama yake yaani wana tamaa hakuna mfano.
Basi sule alimuuliza mama yake”Kwanini umekuja nazo huku”
Mwanangu kusoma hujui hata picha huoni!!? hizi siku si nyingi zitakuwa chini yetu,
Naomba upumzike kesho asubuh nakujua tuongee vizuri.
SIKU ILIYOFUATA Mzee Nassor aliamka asubuhi na mapema ili awahi airport ya KILIMANJARO INTERNATIONAL AIRPORT(KIA) Tayari kabisa kuanza safari yake.
Hakuenda mwenyewe bali aliongozana na wanae pamoja na mama.
Mama alipofika tuu airport alimpigia simu Bi kidako na kumpa kinachoendelea
“Bi kidako tayari tuko airport na mzee kashapanda ndege kwa hiyo muda mfupi tuu wanaondoka”……..
“Mwanangu mimi hapa nawaona na nawafuatilia kwa kila hatua na nimeshaanza kazi hivyo muda wowote utapata majibu”Bi kidako aliongea huku akijiamini sana.
Ndege iliruka na wakati huo watoto wa mzee Nassor pamoja na mama yao wa kambo walikuwa njiani kurejea nyumbani.
Walipofika tuu nyumbani kabla hawajakaa Simu ya wedi iliita namba ni ya mzee wao,Wedi alishangaa “Inawezekana vipi mzee kupiga simu na yuko kwenye ndege muda huu!!!?”
Wedi aliipokea lakini kitu alichokisikia alishtuka na simu ikadondoka chini.
Wote walishangaa kuona Wedi kajitwika mikono kichwani,Wakati huo mama alikuwepo hapo na alishajua tuu tayari mission complete!!.
Wedi aliongea maneno matatu tuu
“BABA AMEFARIKI DUNIA”.
Ni kweli Wedi alipewa taarifa za mzee wake kuwa amefariki akiwa kwenye siti yake ya ndege walisema na inawezeka ni Presha.
Ndege ilisimama kwa dharura Nairobi ili kuushusha mwili.
Nyumba ilikuwa chungu watoto walilia sana hakuna aliyeamini kuwa mzee nassor kafariki.
Mama akiwa pale pale Bi kidako alipiga simu,Mama yake sule aliipokea huku akilia kwa nguvu na kusema
“Muuuume wangu amefariiikiiii!!!!”
Ilikuwa ni zuga tuu ila ukweli ni kwamba alikuwa anampa taarifa kuwa mpango umeenda kama walivyopanga na Bi kidako alimwambia
“Nimekuelewa ila nawe fanya mpango mzigo wangu uje”Bibi aliongea akimaanisha anataka pesa aliyoahidiwa na Mama yake sule.
Mama yake Sule alijifanya amepaniki kisha akatoka kwa jazba na kuchukua gari yake na kuondoka,Alienda mpaka Hotelini aliko Sule Alifika hotelini lakini alishangaa kumkuta Sule yuko na kidemu”
Heeee!!! we sule huyu nani!??”……..
“Mama huyu ni rafiki yangu tuu hana shida”…….
“Ok ila take care,
Hujambo dada”
Alimsalimia kisha akamwambia sule”
Naomba niongee na wewe pale chini garden”
Aliongea kisha akashuka.
Sule alimfuata mama yake nyuma kisha mama akamwambia
“Mwanangu yaani mimi nahangaika kwa ajili yako,Namkosea mungu ili wewe upate maisha bora lakini wewe umeamu kufanya ujinga kama huu”
Sule alikaa kimya lakini mama aliongeza”
Yaani ungejua kitu nafikiria kwenye akili yangu ungetuliza na kuitumia akili yako,kwanza wewe ni msomi mzuri kwa nini unajishusha hivyoo,
Na nimepata taarifa zako juu ya kile ulichokifanya huko ulikokuwa.
Halafu Baba yako amekufa akiwa kwenye ndege”
Aliongea kama hataki na hajali kabisa,
Mama yake Sule alishtuka kusikia “puuuuh,”
Sule alidondoka chini kwani mama alimshtukiza kwa taarifa ile……
unadhani itakuwa aje, nini hatima ya sulle!!? like page twende sawa,.
DADA VUA BANA
Sehemu Ya 17B
…….Ilipoishia
Sule alimfuata mama yake nyuma kisha mama akamwambia
“Mwanangu yaani mimi nahangaika kwa ajili yako,Namkosea mungu ili wewe upate maisha bora lakini wewe umeamu kufanya ujinga kama huu
“Sule alikaa kimya lakini mama aliongeza
“Yaani ungejua kitu nafikiria kwenye akili yangu ungetuliza na kuitumia akili yako,kwanza wewe ni msomi mzuri kwa nini unajishusha hivyoo,Na nimepata taarifa zako juu ya kile ulichokifanya huko ulikokuwa.
Halafu Baba yako amekufa akiwa kwenye ndege”Aliongea kama hataki na hajali kabisa,Mama yake Sule alishtuka kusikia “puuuuh,” Sule alidondoka chini kwani mama alimshtukiza kwa taarifa ile..
Mama yake sule alipata kiwewe kwani hasira zake na kupaniki kwake kumepelekea kuongea bila kujua ile ni taarifa ya kushtua.Walinzi wa hoteli walipata taarifa kisha haraka wakawahi kutoa msaada na kumpeleka hospitali.
Wakati huo Lucy na Helena walikuwa ndio wanaamka amka na ilikuwa ni mida ya saa 4 asubuh.Helena alitangulia kuamka kisha akamuamsha mwenzake Lucy,Helena alimwambia Lucy”Dada unajua kuna kitu kinanijia kwenye ufahamu wangu sasa sijui ni ndoto au nilivyobadilishwa kuwa mnyama ilitokea kweli!!”…….
“Kitu gani mdogo wangu?”…..
.”Kama vile nimeota kuwa wewe na sule mlikuwa mnafanya mapenzi halafu mimi nikaenda kumuita shangazi ili msifanye hicho kitu halafu tena iko kama baada ya shangazi kuwakurupua mimi na wewe tulimkimbiza Sule na nakumbuka jana tuliokota begi la sule tena linaonekana alikuwa akikimbizwa”…….
Lucy alikumbuka kweli shangazi alikuja kumkurupua alipokuwa akitaka kusex na Sule na pia hali ya kumkimbiza Sule hata yeye inamjia kwa mbali lakini hakumbuki vyema.Lucy aliongea”Hilo la kumkimbiza Sule Inaweza kuwa hivyo lakini mimi na Sule hatukufanya mapenzi hiyo ni ndoto tuu”Helena Alimwambia Lucy”Tuachane na hayo ebu tumpigie Sule tena”…….
“Sawa lakini shangazi aliichukua simu yake usiku”.
Lucy alienda kuichukua simu ya shangazi.
Wakati Lucy anarudi Helena alipata Line ya simu kwenye begi lile la sule”Yees tukimkosa hewani humu hatutakosa namba ya mtu anayemfahamu”
Aliongea Helena.Lucy aliingia huku akionekana kuweka simu masikioni”Oooh my god simu ya sule inaita”…..
Mara simu ya sule ikapokelewa,Lakini Lucy alikata kwani alisikia sauti ya mwanamke”Mmmmmh!! au hizi namba sio za sule”Aliongea hivyo bila kujua kuwa yule aliongea ni mama yake Sule na ni mama yao.
Helena alimwambia”Sasa kuna line ya simu hii hapa tuangalie majina yaliyoko tunaweza kupata mtu anayemjua sule
“Waliiweka ile line kwenye simu kisha wakaingia sehemu ya majina,Line haikuwa na majina mengi sana lakini waliona jina (MY MOM) Wakajua moja kwa moja huyu ni mama yake sule.
Waliinakili ile namba pembeni ili wapige kwa line ya shangazi yao.Wakati wanajiandaa kupiga meseji iliingia ikisema “Samahani sule amefiwa na baba yake na amepata mshtuko kwa hiyo hawezi kuongea na simu” Kwa kuwa kina lucy hawajui kusoma hawakuhangaika na sms.
Lucy alipiga simu kwenda kwa mama yake Sule,Ilipokelewa lakini Lucy alishtuka kuisikia sauti ile ile aliyoisikia kwenye simu ya Sule,Mama yake sule aliongea akiwa na jazba bila kujua anaongea na watoto wake na sio bi kidako”Haloo mama afadhali umepiga simu,Yaani huku ni balaa sule aliposikia taarifa za msiba amezimia dakika ya 10 sasa.Lucy na Helena walidata kwani hawakujua nini kinaendelea baina ya Sule,Shangazi na mama yake Sule.
Wakati huo watoto wa Mzee Nassor walianza kumtilia shaka mama yao
.Kwani dalili zinaonyesha kuna utata kulingana na mazingira ya kifo cha baba yao.Waliamua kumpigia yule mtaalam wao wa nigeria na na kitu walichoambiwa ni kama walivyohisi.
Na mtaalamu aliwaambia”Mimi siwezi kumfufua baba yenu kitu ninachoweza kufanya ni kuwaadhibu wote walihusika.Watoto walimpa mtaalamu wao uhuru wa kufanya chochote ilimradi waone adui yao akiteseka.
Upande wa pili Sule alizinduka akiwa hospital pembeni yuko mama yake.Baada ya muda mfupi waliruhusiwa,Lakin mama alionekana kuumia kwa sule alivyozimia ila suala la kifo cha mumewe hakuwaza kabisa kwani ilikuwa ni mipango yake.Walirudi hotelini,Walipoingia ndani waliona vitu vimekaa shaghala baghala,Mama alipovuta picha akakumbuka ndani walimuacha yule binti na hayupo,Mama alianza kuingiwa na hofu.Kwanza kabisa alienda pale walipohifadhi zile documenti na hati za mali walizotaka kuiba,Kiukwelie hawakukuta kitu binti yule aliondoka na makaratasi yote mama alimgeukia sule”Wewe sule huyu msichana uliyekuwa naye hapa ulimtoa wapi”…….
Sule aliongea kwa unyonge kwani mwili ulikuwa umechoka kwa kilichomkuta”Ma
ma bwana maswali gani hayo huyu mi simjui vizuri nimekutana naye tuu”…….
Mama alimfuata akiwa na hasira tele”We mbwa umefanya niiini!!!?
Hati zangu ziko wapi!!??”
mama alianza kulia sule naye alinyanyuka na kuanza kupekua kila mahali lakini hati hazikuonekana.
Wakiwa wanatapatapa pale ndani simu ya mama iliita na aliyepiga ni Wedi,Wedi aliongea”
MAMA UMEAMUA KUFANYA HIVI KWELI,HAKIAMUNGU SIAMINI SAWA TUU LAKINI UJUE YA KWAMBA DOCUMENT TUNAZO SISI NA BABA TUTAMZIKA KESHO HALAFU WEWE TUTAKUZIKA KESHO KUTWA
“Aliongea wedi kwa hisia kali sana,Mama aizidi kuchanganyikiwa kwa maneno aliyoyapata.
Kumbe wakati mama amemtuma dereva amfuate sule kina Wedi walikuwa wanafuatilia kupitia yule dereva kwani wanafahamiana vema tuu.
Na waliamua kumtuma msichana ili wapate taarifa nini kitaendelea kwani kitendo cha mama kumficha Sule kiliwapa mashaka japokuwa hawakujua mipango iliyopangwa kumuua baba yao laiti wangejua mwanzo wangeweza kuzuia.Lakini waliamua kumtumia mganga wao wa kule Nigeria ili mambo yaende sawa.
Wakati mama anaendelea kuduwaa simu iliingia tena kutazama ni Bi kidako”Haloo mwanangu,Kazi yako nimeshaimaliza mzee nimeshamuondosha sasa unatakiwa unilipe pesa yangu kama ulivyoniahidi
“Mama hakuongea alikata simu ya bi kidako kwani aliamini kuwa misheni zote zimefeli.
Mama aliwaza ni wapi atatoa pesa ya huyu bibi na alimuahidi hela nyingi sana kama milioni 20.
Mara Sule alimuuliza mama yake”Hivi mama mbona yule bibi kule aliniambia kuwa wale ni dada zangu inawezekanaje sasa”.
Sule alianza kutamani kuwasaidia lakini anataka kujjua ukweli kwanza kama kweli lile alilosema bi kidako ni la kweli au laa.Mama hakujibu kitu bali alionekana kuanza kushangaa mazingira ya pale ndani kama vile ni mgeni.Sule alimtazama mama yake hakuelewa nini kinamsibu.
Mara mama alianza kucheka cheka hovyo huku akivuruga vitu pale ndani,Mama alitoka mpaka nje ya hoteli,Ukweli ni kwamba mama yake sule aliingiwa na uwendawazimu ghafla.
Sule alitoka kumfuata mama yake,Watu walishangaa kuona mama msafi kabisa akiongea kama kichaa,Masikini wa mungu mama wa watu kichaa kilimuanza ghafla tuu lakini hii yote inasababishwa na tamaa,Aliongea hovyo hovyo.
Wakati anatembea aliingia barabara ya Moshi,Arusha na kwa bahati mbaya kulikuwa na gari ya tours inakuja kwa kasi sana dereva alijitahidi kumkwepa lakini kwa bahati mbaya mama yake sule aligongwa huku sule akishuhudia.Damu ilitapakaa barabarani hakuna aliyeweza kuutazama mwili wa mama yake sule mara mbili kwani uliharibika vibaya mno.
Sule hakuamini macho yake alihisi kama ni ndoto lakini ndio hivyo mama kashafariki.
WIKI KADHAA BAADA YA VIFO VYA WAZAZI WA SULE.
Sule aliamua kujichanganya stand angalau awe mpiga debe wa mabasi yaendayo mikoani.Lakini akili yake ilijutia bahati aliyoipoteza kwani saivi angekuwa Tajiri mkubwa hapa mjini.Mbali ni hayo alianza kupanga mikakati ya namna ya kuwarejesha wadogo zake katika hali ya kawaida na mara kadhaa amekuwa akihudhuria nyumba ya ibada na kuwashirikisha viongozi wa dini ili kufanikisha jambo hilo.Lakini aliamini mbele za mungu hakuna kitakachoshindi
kana maana mungu anasema
“NIAMINI MIMI NAMI NITAKUVUSHA KWENYE MAMBO YALIYOSHINDIKANA”……….
NA HUO MWISHO WA SIMULIZI HII SHUKRANI!!?