DADA VUA BWANAH
Sehemu Ya 13
……….ilipoishia
Huku kwa kina Helena tayari Lucy alisharejea katika hali yake ya kibinadamu na wakati huohuo Sule alionekana anaondoka.
Kwa kuwa helena alikuwa amepewa kazi ya kumzuia sule asiondoke bila kunywa kinywaji kile alichopewa na Shangazi,Basi alimfuata sule akiwa na kile kinywaji kujaribu kama hilo litawezekana…..
Endelea……
NAOMBA LIKE YAKO MTU WANGU ILI TUENDELEE CHAP ….
Basi Helena aliutumia tena usichana wake kumshawishi Sule anywe kinywaji kile.
Basi helena alimfuata sule mpaka alipo kisha akamwambia”
sule naomba unisamehe mimi pamoja na shangazi yangu,
Na pia shangazi kasema haina haja ya wewe kuondoka kwani umeshakuwa mtu wa karibu katika familia yetu”.
Sule alimtazama kwa umakini kisha akajiuliza,”Mmmmmh!! inawezekana vipi shangazi anifume na wote hawa na bado aniambie nimekuwa mwana familia!!?”
Sule kwa akili yake fupi aliwaza kisha akagundua kuwa shangazi alikuwa anamchora pengine anamuitia polisi.
Helena hakuishia hapo alizidi kuongea”
Aaaamh! na pia kama umeamua kuondoka basi chukua kinywaji hiki kunywa ili uendako usinisahau”.
Sule alipokea kikombe kile kikiwa na kinywaji ndani tayari kabisa kwa kunywa.
Sule alishangaa kuona helena anabembeleza sana ili anywe kinywaji hicho.
Sule machale yalimcheza akamrudishia helena kile kikombe na hakutaka kunywa kabisa”
Helena pleas siwezi kunywa kinywaji hiki”……..”
Sule inamaana hunipendi kabisa babaaa!! mbona yale yashapita jamouny”……..
Sule taaratibu maneno ya mtoto wa kike yalianza kumuingia lakini nafsi yake ikawa na mashaka kwani mazingira anayopewa hicho kinywaji yalimpa hofu sule alijiuliza”
Sasa kwa nini wasinipe wakati ule nilipokuja saizi nataka kuondoka ndio wanipe!! hapana hapa kuna kamchezo,
“Sule aliangalia kwa mbali alimuona Lucy na shangazi yake wakitazama jinsi anavyopewa kinywaji kile na dada helena,Na hapo ndipo Sule alipoghairi kabisa swala la yeye kunywa hicho kinywaji.
HUKU NYUMBANI ALIPO MAMA YAKE SULE MAMBO YALIKUWA HIVI,
Mama yake sule baada ya kuona anakabidhiwa nyaraka na hati miliki za mali zao alianza kuingiwa na tamaa.
Alitoka nje na kuanza kuzitazama gari zilivyopark pamoja na nyumba ilivyo nzuri,
Aliangalia huku akionekana kama kuna jambo analitafakari kichwani.
Mama yake sule aliingia ndani kisha akachukua simu yake na kuanza kutafuta namba,
Alipofika kwenye namba ya Bi kidako aliitazama huku akionekana kujishauri kuipiga,Lakini aliikaza roho na kupiga.
“Haloo!! shikamoo bibi!!?”
marhaba mwanangu habari zenu huko
“Hatujambo kabisa vipi kuhusu swala la sule?”
Sule niko naye hapa ndio nafanya mpango jinsi ya kumfanya arudi
“Ooooooh!! ahsante sana kumbe tayari uko naye sasa tutampata vipi”
Atakuja usiku huu huu haitafika saa nne
“Sasa bibi naomba unisaidie kitu”
Mama yake sule aliongea huku akipepesa macho kuangalia kama yuko mwenyewe.
Aligundua kuwa yuko mwenyewe na ndipo alipomwambia maneno haya bi kidako.
sema tuu mwanangu
“Aaaamh!! unajua mi sitaki kabisa kuishi na huyu mwanaume na nataka ufanye jambo hapo”
kwa hiyo wataka tufanye nini?,
“Kesho anasafiri sasa nataka akienda huko iwe ndio mwisho kuiona tanzania na ukikubali kunifanyia hivyo nitakupatia milioni 20 kama zawadi na nitakujengea nyumba nzuri hapa mjini kama utataka ila kama utataka huko huko pia sawa”
Sawa lakini ni ngumu sana ila nitajitahidi lakini uwe makini sana kwani ni hatari,
Nitafanya hivyo lakini nakusihi tena kuwa makini na naomba akishaondoka tuu uje huku na pia chakula cha wanao kimekwisha uje nacho.
“Yaani nitashukuru sana kama hilo jambo litafanikiwa sasa mimi kesho nakuja huko lakini hakikisha sule aje huku leo ili kesho tufanye hii niliyokuambia”
Yaani hapa wamekutana Mganga ana tamaa na mama yake sule ndio balaa.
Walikubaliana kisha mama yake sule alikata simu,Wakati anageuka tuu alikutana uso kwa uso na kijana wake Wedi,Mama alishtuka sana alionekana kama ana wasiwasi kutokana na kile alichokuwa anazungumza kwenye simu.
Alivuta pumzi kisha akaongea
“Hujambo mwanangu??”….
..Wedi alimjibu
“Yaani mama una bahati nilikuwa nije nikufumbe macho sema umewahi kugeuka
“Wedi aliongea kisha akanyanyua funguo ya gari juu huku akimwambia mama yake
“Supriseee!!!!!”……
“Mama alishangaa sana
“Whaaat!!”.
…Wedi alimwambia
“Njoo uone huku nje.
Mama alivyotoka nje alishangaa kukuta gari 2 zimepark nje moja ina plat namba imeandikwa MAMA na nyingine imeandikwa BABA.
Wakati huo mzee alikuwa ndani anajiandaa andaa kwa ajili ya safari yake.
Mama alipigwa butwaa kwani ni jambo linaloshtua sana kitendo cha watoto kuwapa magari sio kitendo kidogo.
Wakati wanashangaa mara sudi alitoka ndani akiwa amemziba baba yake macho mzee alikuwa anaongea ongea huku anacheka
“Halafu nyie watoto mna masihara mjue huuhuuhu!! angalia usinigongeze mlangoni oohooo!!”
Sudi aliwaambia”Shiiiiiii!!
“Yaani wanyamaze kisha akampeleka mpaka pale mbele ya gari na kumwambia “Ebu papasa hapo”
Mzee alipoligusa tuu lile gari na Sudi akamuachia macho,Basi mzee aliangalia kisha Sudi akamkabdhi ufunguo huku akisema”
Tumefurahi sana kitendo cha nyie kuona umuhimu wetu hasa hasa mama kwani bila yeye nahisi usingewaza kutufanyia hivi baba yetu,
Na tumeona tufanye hivi kabla haujasafiri baba yetu”.
Basi ilikuwa ni furaha kubwa kwenye familia ile,Kwanza walipiga picha nyingi mno mavinywaji nyalitolewa ndani walikunywa na mpaka basi.
Upande wa pili kule Sule aligomea kabisa kunywa kinywaji cha Helena.
Sule alimwambia”
Mbona unaning’ang’aniza sana kwanza sitaki hicho kinywaji hata wewe pia sikutaki tena
“Sule aliongea kwa hasira kisha akawa anaondoka.
Shangazi yake Helena alikuwa kwa mbali anatazama,
Alivyoona sule amekataa alisema,
“Ahaaaaa!! unajifanya mjuaji eeeeh!!
ngoja nikuonyeshe adabu”
Aliongea huku akiingia ndani………..
Je unadhani Bi, KIDAKO atamfanyia nini SULLE usidhubutu kuikosa sehemu ijayo ,.
DADA VUA BANA
Sehemu Ya 14
……….ilipoishia
Upande wa pili kule Sule aligomea kabisa kunywa kinywaji cha Helena.
Sule alimwambia”
Mbona unaning’ang’aniza sana kwanza sitaki hicho kinywaji hata wewe pia sikutaki tena”Sule aliongea kwa hasira kisha akawa anaondoka.
Shangazi yake Helena alikuwa kwa mbali anatazama,Alivyoona sule amekataa alisema “Ahaaaaa!! unajifanya mjuaji eeeeh!! ngoja nikuonyeshe adabu” Aliongea huku akiingia ndani………
Endelea………
#Hakikisha unailike ili nilete vitu mubashara pia kumbuka ukilike UKURASA HUU utafikiwa na CHOMBEZO zake popote ulipo usidhubutu kuzikosa kwa jinsi zilivyo TAMU LIKE PAGE SASA.
Shangazi alionekana amekasirika sana kitendo cha sule kukataa kunywa kile kinywaji.
Aliingia ndani akiwa na jazba sana.
Wakati huo Helena alibaki akimtazama sule anavyoondoka kwani kiukweli alimpenda sana ila siku zote kisicho riziki hakiliki.
Lucy aliamua kumfuata Helena pale na kumuuliza “
Hivi helena huyu kaka hujachukua hata namba yake??”……
“Lucy nawe namba ya nini na hata nikiichukua inakuhusu nini sasa!!?”……” Heee!!Weee vipi kukuuliza imekua nongwa!!?”.
Helena na Lucy walianza kubishana pale mpaka ikawa kama ugomvi,Lakini kwa mbali walimuona shangazi yao anakuja kwa kasi sana.
Helena na Lucy walianza kutazamana kwa hasira sana na hakuna anayemsemesha mwenzake kwani wakikutwa wanagombana itakuwa kesi nyingine kwa shangazi yao.
Shangazi alifika pale kisha akuliza
“Huyu kikaragosi yuko wapi??
“Akimaanisha Sule.
Basi Sule aliondoka kabisa na nia yake ilikuwa ni kwenda huko ngare lakini sasa kutokana na tamaa alijikuta amekaa kwa kina Helena mpaka giza limeingia.
Sule akiwa anatembea alisikia mlio wa pikipiki,Kwa kuwa alikuwa bado hajafika kwenye barabara kubwa inakopita hiyo pikipiki aliamua kukimbia ili awahi hiyo pikipiki.
Ni kweli aliwahi kisha akaisimamisha
“Samahani kaka unaelekea wapi unipe lift”…….”Mi siendi mbali ni hapo tuu hata nikikubeba ni bure tuu maana mi nshafika”…….
“oukey basi naomba unisaidie simu yako nimpigie mtu nyumbani anifuate samahani lakini”.
Sule alipewa simu na kuingiza namba na kupiga alionekana anaongea na mama yake huku akimuelekeza pale alipo.
Alimaliza kuongea kisha akamrudishia simu yule jamaa na yeye taratibu akawa anatembea kurudi nyumbani.
Wakati harakati za shangazi au bi kidako akihangaika namna ya kumteka sule ili amrudishe nyumbani kwao huku nyumbani kwa kina Sule watu walikuwa wamelewa sana,Walilewa wote kasoro mzee tuu kwani hakutaka kuuchosha mwili kwani anasafiri asubuh.
Pamoja na watoto kumjali mama yao wa kambo wazo la mama lilikuwa pale pale,Alipanga kumpoteza mume wake ili aweze kumiliki mali zote kwani hati miliki zote kaachiwa yeye.
Wakati huo mama alishawasiiana na Sule na hakumuambia yeyote kama amewasiliana na sule.
Mama alienda pembeni kisha akampigia mtu na kumuelekeza kule aliko Sule na alimwambia asimlete nyumbani bali ampeleke MOUNT MERU HOTEL.
Huku kwa sule Kumbe hata ile pikipiki aliyoiona ilikuwa ni mauzauza tuu ilikuwa ni kazi ya bi kidako kuhakikisha sule anarudi kwao.
Shangazi aliwafuata kina Helena kisha akawabadilisha wote kuwa wanyama na lengo lake ni kuwaamrisha kina Helena wamfuate Sule na kumtisha ili aogope huo msitu kabisa.
Bi kidako tayari alishawabadili kina Lucy kuwa madubwasha ili yakaifanye kazi hiyo aliyoikusudia,Akili ya Bi kidako iliwazia ile Milioni 20 alizoahidiwa na mama yake sule alijisemesha kimoyo moyo”Ooooh! mizimu yangu asante sana,Hiyo kazi ni ndogo sana kesho namaliza kila kitu”
Aliongea Bi kidako huku akiwaachia wanyama wake wamfuate Sule.
Lucy na Helena waliachiwa wakaanza kutimua mbio kama vile wanashindana huku ndimi zao zikiwa nje.
Wakati huo huku watoto wa mzee Nassor waliitana ndani na kuanza kuongea kwa furaha”
Yaani leo tumewafanyia wazee wetu bonge la suprise,
Hebu cheki wanavyofurahia pale njee
“Walikuwa wakiwatazama wanavyoshangilia kila mmoja anafurahi.
Kumbe mama moyoni anamkejeli tuu mzee wa watu masikini wa mungu.
Basi usilolijua ni giza nene,Basi baada ya hapo mama na mzee waliingia ndani kila mmoja akaendelea na shughuli yake.
Mama cha kwanza alipiga simu Mount meru hotel na kumfanyia mwanae booking Ili akae pale kwa siku kadhaa wakati yeye anaweka mambo sawa ili amiliki kila kitu kutoka kwa mume wake.
Baada ya hapo aliongea na dereva kujua amefika wapi.
Wakati huo Sule alikuwa anatembea huku hofu na mashaka vikiwa vimemtawala kwani giza lilikuwa limetanda na isitoshe ni porini.
Wakati anaendelea na safari zake alihisi mchakacho kwa mbali kama vile kuna kitu kinakuja kwa kasi ,Aligeuka nyuma kuangalia ni nini kinakuja,Aliona wanyama kama chui wanakuja kwa kasi tena wawili,Sule alivuta pumzi akatupa begi lake kisha akaanza kutimka mbio……..
Unafikiri nini kitafuata hapo,Usikose sehem inayofuata hapo kesho,.
DADA VUA BANAH.
Sehemu Ya 15
……….ilipoishia
Wakati huo Sule alikuwa anatembea huku hofu na mashaka vikiwa vimemtawala kwani giza lilikuwa limetanda na isitoshe ni porini.
Wakati anaendelea na safari zake alihisi mchakacho kwa mbali kama vile kuna kitu kinakuja kwa kasi ,Aligeuka nyuma kuangalia ni nini kinakuja,Aliona wanyama kama chui wanakuja kwa kasi tena wawili,Sule alivuta pumzi akatupa begi lake kisha akaanza kutimka mbio.
Endelea…
Ilikuwa ni kama ndoto kwa sule kwani alichokiona ilikuwa ni hatari hatari.
Alijuta hata kukimbia nyumbani kwao,Sule alianza kuikumbuka sala ya toba maana aliiona njia ya kuzimu imefunguliwa.
Wakati huo bi kidako alikuwa akicheka tuu kwani alianza kuisikia sauti ya sule ikiomba msaada
“Ndio ukome mshenzi wewe yaani unataka kuzini na ndugu zako!!?
“Bi kidako alijisemea maneno hayo.
Kumbe huyu bi kidako anamjua vizuri sana Sule na amejuana siku nyingi sana mama yake Sule na yeye ndio aliyemleta mumewe kwa huyu bi kidako.
Kwahiyo Bibi huyu anamsikiliza zaidi mwanamke na sio mwanaume.
Upande wa pili huku watoto wamzee Nassor walikuwa wamekaa meza moja huku wakishauriana jinsi ya kuendesha biashara zao.
Shukuru alinyanyuka na kuongea
“Mnajua nyie ni kaka zangu ebu naomba niwaambie kitu
“Wote walitega masikio kumsikiliza Shukuru ambaye ndiyo kijana mdogo kuliko wote kwa mzee Nassor.
Shukuru aliongea
“Naomba tusiamini hizi chale tulizochanjwa kule nigeria,Sawa labda zinasaidia lakini tuna uhakika gani kuwa hii ni kinga dhidi ya wabaya wetu
“Sudi alimkatisha Shukuru”Shukuru sikia nikuambie Hivi unadhanji baba ni mjinga kutupeleka Nigeria kutusafishia nyota!?Jaribu kufikiria umeishi miaka mingapi ukiwa masikini na hujiulizi kwa nini baba yetu ni zaidi ya tajiri hapa mtaani??,
Ukikuua utaelewa ila kwa sasa wewe angalia tuu na usifikiri hawa matajiri unaowaona wamepata mali kama unavyofikiria wewe,
“Sudi aliongea huku akicheka cheka.
Kumbe siku ile wakina Sudi wanarudi kutoka masomoni walipitishwa Nigeria na mzee wao.
Nia na kusudi la mzee huyu kuwapitisha huko ni kuwaweka vizur kwanguvu za kishirikina.
Mzee Nassor baada ya kuona watoto wanafanikiwa kwa haraka aliona ni bora naye abadili mganga kwani aliona kama bi kidako bado yuko chini kiutaalamu ni bora aende Nigeria.
Na hakumwambia mkewe kuwa anakwenda Nigeria kwani hata safar yenyewe kaipanga ghafla hivyo alimwambia anasafiri kikazi.
Basi Mzee alikuwa akiwaza namna ya kuendeleza mali zake na mama aliwaza namna ya kumfilisi mumewe mali zote.
Unahisi nini kitatokea??
Endelea….
Huku aliko Sule mambo yalizidi kuwa magumu zaid kwani wale wanyama walikuwa wanazidi kumkimbiza.
Ghafla wakati anakimbizwa alishangaa kuona barabara inajaa maji na hakuna hata mvua.
Kutokana na yale maji sule alishindwa kabisa kukimbia,Cha ajabu zaid alivyogeuka nyuma alishangaa kuona wale wanyama wanakimbia juu ya maji.
Masikini wa mungu sule alikiona kifo kile kinakuja,
Hakuwa na njia nyingine ya kujisaidia.
Wakati mguu uko ndani ya maji alihisi kama kuna kitu kimemshika mguuni,Sule alijitahidi kuutoa mguu lakini alishachelewa tayari wale wanyama wakali walishafika pale na walikuwa wameachama midomo kama wanataka kummeza.
Sule alifumba macho ishara ya kukata tamaa kwani aliamini huo ndio mwisho wa maisha yake.
mara alipofumbua macho alimuona shangazi yake na Helena na hakujua kafika vipi pale.
Wakati Sule anasubiri kifo Huku mama yake alikuwa anakusanya hati zote nia yake ni kuzitoa pale ndani ya nyumba na kumpelekea mwanae pindi atakapofika Mount meru hotel.
Mama alimpigia simu yule dereva akiamini tayari kashafika na kumchukua Sule”
Habari yako derevaumeshamuona??”……..
“Hapana mama ndio niko Usa hapa naelekea hapo uliponielekeza mama”.
Basi Mama alimuharakisha dereva kwani aliona kama anachelewa kufika.
Wakati huo huo Mzee alikuwa tayar kashapanga vitu vyake na anakuja pale alipo mkewe,Mama alikuwa bize kama vile anaiba kwani alikuwa na harakati za kuhamisha hati za umiliki wa nyumba na mali zingine.
Basi mzee alifika mlangoni kwa bahati alikohoa kabla hajaingia ndani,Mama alishtuka na alikuwa na makaratasi mkononi,Aliwaza pa kuficha kwa haraka haraka alizikusanya na kuziweka ndani ya nguo ya ndani/
Chupi”
Hahaaa! karibu mume wangu”
Alijichekesha pale kiuongo uongo,Mzee alimuangalia mkewe na kuona kama kuna utofauti lakini akachukulia poa
“Aaaamh!! nilikuwa nakusisitizia hakikisha unakuwa makini na kazi niliyokuachia mke wangu.
Basi mzee aliongea kisha akamwambia”Sasa mke wangu unajua nitakumiss eti”
Aliongea huku akimsogelea karibu na kutaka kumkumbatia,
Mwanamke aliogopa sana kwani alikuwa ameficha zile karatasi pale kwenye chupi,Mama aliamua kumpotezea
“Baby sory leo sijisikii vizur”…….
“Sasa mke wangu nitasafiri vipi na ukata huu nakuomba sana mke wangu”.
Mwanamke alifikiria sana na kuona ni haki mumewe kupata Sunnah kwani safari ni ndefu,Basi mama alimuomba kitu”
Sawa nakupa lakini naomba niende bafuni mara moja nikajiweke vizuri
“Baba hakuwa na kipingamizi bali alifurahi kwani kweli mzee alikuwa na ukata wa kweli alimiss chitumbua cha mkewe sana.
Basi mama alitoka na hakuelekea bafuni kama alivyomwambia mumewe aliingia kwenye chumba cha Sule na kuzihifadhi zile karatasi kisha akaingia bafuni na kutoa nguo zake akabaki na khanga tuu.
Mzee alikuwa ndani alisubiri ujio wa mkewe,Mwanamke aliingia kisha akaufunga mlango.
Taaratibu aliifungua khanga ile na kuitupa chini,mzee alianza kufungua mkanda wa suruali yake.
Basi mama alimfuata mumewe huku akimuangalia kwa kurembua rembua na kumlaza baba watoto wale kitandani naye kufuatia kwa juu.
Lengo la mama ni kuzidi kumchanganya kabisa mzee wa watu.
Basi mzee alimega tunda lake lakini kama unavyojua umri umeenda sana hivyo hakutumia mda mrefu sana babu aliomba poo!!.
Wakati baba na mama walikuwa wakiagana kwa kupeana mautamu vitu urojo urojo.
Huku sule huku mambo yalikuwa magumu balaa.
Lakini alipomuona Shangazi yake na helena alishtuka sana kwani alitokea ghafla tuu.
Hali hiyo ilimpa mashaka sana Sule.
Wakati anaduwaa alishangaa kuona shangazi anawazuia wale wanyama ambao ni kina Helena.
Shangazi aliongea kwa sauti ya kutisha,
“Tabia yako ndio imekusababisha!!! na ulivyo na tamaa ulitaka kuzini na dada zako mbwa wewe…………
“Usikose sehemu inayofuata hapo kesho unadhani itakuwa aje,