Haya
1. Hujaolewa tu?
2. Kwanini Huna Watoto?
3. Utazaa lini, umri unaenda!
4. Unafanya kazi wapi?
5. Kwanini Umenenepa/Umekonda?
Watu wanapitia mambo mengi magumu ambayo huna taarifa nayo wala hujawahi
kuyasikia, jitahidi kuwa mwenye ufikirio unapozungumza na wengine.
Ikiwa wewe umefanikiwa kupata vyote jitahidi kutoropoka maneno unayodhani yako
sawa kwa upande wako.
Kuna watu wanapitia changamoto za mahusiano, uzazi, uchumi na mambo mengine ya
kifamilia, try to be kind!
Nakumbuka kuna siku sikuwa najua lolote lile nikapata mawasiliano kwenye group
na school mate mmoja hivi, maana miaka mingi ilipita bila mawasiliano, mule
kwenye group wakasema kaolewa. Mimi bila kujali na usingo wangu nikauliza ana
watoto wangapi?
Sikuwa na nia mbaya nilitaka tu kujua kwa wema tu ili nimpongeze. Yule dada
alileft group, ndio nikapata maelezo ya changamoto nyingi anazopitia, kusema
ule ukweli nilijilaumu sana.
Nilijifunza wapo watu wanajitenga na jamii sio kwa sababu hawapendi watu, hapana!
Ni kwa sababu wanepuka kero na mazingira ya kuongezewa stress kwenye maisha yao
ambayo tayari yanawahangaisha, wapo watu hata sherehe na mikusanyiko mingi
hawashiriki sababu ya maswali kama hayo hapo juu.
Tunakosa ushirikiano wa watu wengi sababu ya midomo yetu. Kuna mtu haji kwako
kukusalimia sio sababu hakupendi, ni huo mdomo wako huchelewi kuanza kutoa
ushauri au masimango kibao, mtu anakuja kukusalimia we unaanza kumfanyia
interview
Maisha sio mashindano! Kila mtu ana mzigo wake anahangaika nao kimya kimya
tusiwaongezee uzito.
Unaweza kumuona mtu yuko vizuri kiuchumi lakini kuna mwiba wake anahangaika
nao, na kadhalika yule unayemuona ana mahusiano yenye furaha naye ana mwiba
wake