Mwenye Kujiheshimu
Kwa asili mwanaume tangu enzi na enzi alikuwa na sifa ya kupambana na hatari
misituni kukabiliana na wanyama wakali,alikuwa na tabia ya kulinda familia,
kuihudumia familia kwa kuwinda wanyama porini hivyo basi kwa Mwanamke alikuwa
na tabia ya kulea watoto nyumbani huku mwanaume anakwenda kupambana kwa ajili
ya kuleta chakula nyumbani.
Asili hiyo ipo kwa miaka na miaka na itaendelea kuwa hivyo haijalishi
mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
kwa asili Mwanamke huwa anaongozwa sio kumuongoza mwanaume,hata ukiangalia
vitabu vya dini utakuta mitume wote na manabii walikuwa wanaume kwa sababu ya
uwezo wa kukabiliana na matatizo,kulinda na kuhudumia.
kwa asili Mwanamke huwa anapokea sio mtoaji,ndiyo maana Mwanamke huwa anapenda
kupewa zawadi,kupewa fedha,kusifiwa, kupongezwa n.k lakini asili ya mwanaume ni
kutoa,kulinda na kuhudumia.
Ikitokea mwanaume hana sifa ya kulinda, kuhudumia,kutoa,kuongoza familia moja
kwa moja mwanaume huyo ataonyesha tabia za upole kupitiliza, kunyenyekea sana,
kusamehe makosa haraka,kujali sana,kuogopa ugomvi na migogoro, kujishusha sana
,kutaka kumfurahisha kila mtu,kutaka kupendwa na kila mtu.
Kwa asili Mwanamke ameumbwa kwa ajili ya kutii maagizo na muongozo,hivyo basi
pale ambapo mwanaume anakuwa hajiamini mbele ya Mwanamke huanza kutetemeka,
kumnyenyekea, kuomba msamaha, kumpa ushauri, kumbembeleza, kumkumbusha wema
amefanya zamani n.k lakini hizi siyo sifa za mwanaume ni sifa za mwanamke.
Kutokana na hali hiyo Mwanamke automatically ataanza kuonyesha dharau
waziwazi,atamjibu vibaya,atamgombeza,atamdhambulia kwa maneno makali sana kwa
sababu Mwanamke hawezi kumuongoza mwanaume hata siku moja katika familia kisha
amani ipatikane.
Mwanamke akiwa na furaha,amani na utulivu anakuwa na sifa ya huruma, kujali,
kunyenyekea, kusamehe,anakuwa mpole,anakuwa mtiifu,anakuwa msikivu.
huo utulivu unakuja pale ambapo anakuwa analindwa na kupewa uhakika wa maisha
na usalama wake.
pale ambapo anakuwa hapati ulinzi,wala hana uhakika wa maisha yake hulazimika
kupambana kutafuta mwanaume ambaye anaweza kumlinda, kumuongoza na kumpa
maagizo kwa sababu ni hulka ya Mwanamke kufuata maagizo ya mwanaume toka enzi
na enzi.
Kwanini wanaume ambao ni “bad boy na play boy” wanapata wanawake
wenye tabia ya upole, huruma, kujali, kunyenyekea, kusamehe makosa na
uvumilivu?
jibu lake ni rahisi kwamba mwanaume ambaye ni bad boy anakuwa mkali pale ambapo
kuna hatari,anakuwa tayari kugombana na kupambana na mtu yeyote ili kujilinda.
bad boy hawezi kuvumilia dharau,bad boy hawezi kukubali kugombezwa,bad boy
anaweza kuleta madhara endapo haki zake zitakiukwa na heshima yake itavunjwa.
kwanini mwanaume mstaarabu sana hana mvuto kwa Mwanamke ? jibu lake ni kwa
sababu mwanaume mpole kupitiliza, mvumilivu sana, mnyenyekevu kupitiliza,
king’ang’anizi,muoga,anaogopa mahusiano kuvunjika,anaogopa kuachwa
mpweke,anaogopa ugomvi na migogoro huwa anaonyesha tabia za kike badala ya
tabia za kiume.
kwa asili mwanaume haridhiki na Mwanamke mmoja ,hivyo basi kwa mwanaume
mstaarabu sana anakuwa king’ang’anizi kwa Mwanamke mmoja jambo ambalo linaonyesha
kwamba huyu siyo mwanaume kamili.
Kutokana na hali hiyo ni rahisi kuona wanawake wengi sana wanamgombania
mwanaume mmoja ambaye hajali mapenzi kwa sababu ni hulka ya mwanaume
kutoridhika na Mwanamke mmoja.
Hii maana yake ni kwamba pale ambapo mwanaume anapoonyesha tabia zenye
kupingana na asili ya mwanaume husababisha Mwanamke kutilia shaka uanaume wa
mwanaume huyo.
Hii ndiyo sababu mwanaume ambaye tabia zake zipo kinyume na asili ya wanaume wa
zamani huwa hana mvuto kwa Mwanamke.
Mwanamke akiona mwanaume ni mpole kupitiliza, hulazimika yeye mwenyewe Mwanamke
kuwa mkali kupitiliza kama njia ya kujilinda.
Mwanamke akiona mwanaume anajali sana analazimika yeye mwenyewe Mwanamke kuacha
kujali kwa sababu hana cha kufanya .
Mwanamke akiona mwanaume anamnyenyekea sana huamua kuacha kuonyesha unyenyekevu
kwa sababu anakuwa hana cha kufanya.
Mwanamke akiona kila agizo ambalo anampa mwanaume -Anaona mwanaume wake anatii
papohapo hupoteza hisia kwa mwanaume huyo kwa sababu anaona huyu si mwanaume
kamili
Mwanamke yeyote akifanya makosa makubwa kisha akiona anapewa msamaha haraka
huanza kuonyesha dharau waziwazi kwa mwanaume huyo kwa sababu hata nyakati za
utotoni -mtoto akifanya makosa huwa anapewa onyo kali kutoka kwa baba ,hivyo
akiona hakuna onyo wala karipio anajua huyu siyo mwanaume kamili.
Mwanaume ambaye hajiamini mbele ya Mwanamke huvutiwa kimapenzi na Mwanamke
mwenye kiburi, majivuno, jeuri na dharau kwa sababu yeye Mwanamke anakuwa
anajiamini kupitiliza lakini mwanaume anakuwa hajiamini.
kwa asili Mwanamke anakuwa hajiamini mbele ya mwanaume ndiyo maana anaweza
kuvaa,kuongea kwa lengo la kumvutia mwanaume, vilevile Mwanamke anakuwa anataka
kusifiwa ili apate kujiamini lakini mwanaume haitaji kusifiwa ili apate
kujiamini.
Maana yake mwanaume ambaye hajiamini ataishi kwa kutaka kumfurahisha Mwanamke
saa 24 lakini Mwanamke atajiona yupo na nguvu na mamlaka ya juu kwa mwanaume
huyo hivyo atamuacha ghafla aende kwa mwanaume ambaye hana hisia naye ili yeye
Mwanamke apate kujitutumua ili kumvutia mwanaume husika.
Mwanaume hauwezi kukwepa uongozi maishani mwako,ukiona hauwezi kuongoza basi
utaongozwa na mwenza wako kisha atakugeuza mtumwa kwa sababu siyo hulka ya
Mwanamke kumuongoza mwanaume ndani ya familia.
Mwanamke akiona haujiamini vilevile hawezi kukuamini vilevile hawezi kukubali
kuongozwa na mwanaume asiejiamini.Unawezaje kuruhusu mtu ambaye unamzidi uwezo
akuongoze?
Unawezje kuruhusu mtu ambaye hajiamini mbele yako akuongoze si atakupoteza?
bad boy wanajiamini sana hivyo wanavutia kwa Mwanamke kuliko wanaume wastaarabu
sana ambao huonekana kama bendera .Hauwezi kumheshimu kiongozi ambaye
anatetemeka mbele yako hata siku moja.
Silaha ya mwanaume ni uanaume wake yaani kuongoza sio kuongozwa.
Ukitaka 50/50 unapata mwanamke ambaye ni feminist,ukitaka kuongoza familia
unapata Mwanamke ambaye ni mtiifu, mpole, mstaarabu, mnyenyekevu.
Mwanamke mkali kupitiliza,mbabe,mwenye kauli za mkato, mwenye hasira kupitiliza
hawezi kupata mwanaume mwenye sifa za kiume (Masculine behavior) bali atapata
player wanampa ujauzito na kumtelekeza au waume za watu tu , vilevile wanaume
legelege ambao kwake hawana mvuto.