SINGLE MOTHER
Changamoto ni kupata Mwanaume atakayekupenda
wewe na Mtoto wako!
Unapokuwa na mtoto, changamoto kubwa katika kuingia kwenye mahusiano siyo
kupata mwanaume wa kukupenda — hao wapo tu. Utatongozwa kwa sababu si kwamba
unatoka na bango usoni linalosema “Mimi ni single mother.”
Lakini changamoto kubwa ni kumpata mwanaume ambaye atakupenda wewe na mtoto
wako. Yaani, kukukubali wewe kama wewe na pia kukubali kuwa mtoto wako ni
sehemu ya maisha yako.
Changamoto Kubwa Zinazowakumba Wanawake Wenye Watoto
1. Kumuambia Mwanaume Kuwa Una Mtoto
Shida ya kwanza ni hali ya kujiuliza: “Ni wakati gani muafaka wa
kumuambia mwanaume kuwa nina mtoto?” Swali kubwa hapa ni:
• Je, ni siku ya kwanza ya kukutana naye?
• Je, ni baada ya kuzoeana?
• Vipi ni baada ya kulala naye au baada ya mahusiano kuimarika?
• Ni lini hasa nimuambie ili asinikimbie?
•
2. Kumpata Mwanaume Atakayempenda Mtoto Wako
Hata mwanaume akijua kuwa una mtoto — iwe ulimwambia au alijua kabla ya
kutongoza — changamoto kubwa ni kumpenda mtoto wako. Jambo ni:
• Atachukuliana na mtoto wako kama sehemu ya maisha yenu?
• Atamwona mtoto wako kama mzigo, kwamba hatamlea au hata kumjali?
• Je, ataweza kumchukulia mtoto wako kama wa kwake, hata bila wewe kumuomba
msaada wa kifedha?
Katika mazungumzo na wanawake wengi wenye watoto, nimegundua kwamba hizi ndizo
changamoto kubwa wanazokutana nazo. Hii ndiyo sababu, katika kitabu changu
“SINGLE MOTHER,” nimeandika mbinu za kukabiliana na changamoto