TATIZO LA KUWAPENDA SANA WATU AMBAO
HAWAKUTAKI NA KUWACHUKIA SANA WATU AMBAO WANAKUPENDA SANA
LIMERENCE ni neno la kiingereza lenye maana ya hali isiyoweza kuzuilika ya
kiakili na kihisia ambayo husababishwa na hisia za mapenzi kwa mtu mwingine
ambapo mtu hujikuta anatumia muda mrefu sana kumfikiria sana mwanaume au
mwanamke huku akitamani mtu huyo aonyeshe kiwango kilekile cha upendo ambacho
yeye anakuwa nacho kwa mtu huyo.
Kwa maana kwamba unamuona mwanaume au mwanamke popote pale kisha unakuwa na
hisia kali sana za mapenzi juu yake mpaka unaanza kujenga taswira ukiwa na mtu
huyo kitandani au ukiwa umemuoa au umeolewa naye.Lakini mtu huyo anakuwa hajui
chochote.
Vilevile hata pale ambapo unakuwa umejenga naye mahusiano unajikuta unakuwa na
hisia kali sana za mapenzi juu yake kiasi kwamba unakuwa na hofu ya kuachwa
muda wote.
kwa leo tuangalie viashiria vya tatizo la kisaikolojia la LIMERENCE,kisha
tuangalie athari za LIMERENCE namna husababisha mtu kuumizwa sana kwenye
mahusiano.
VIASHIRIA VYA TATIZO LA
LIMERENCE
Mtu yeyote ambaye anasumbuliwa na tatizo la kisaikolojia la LIMERENCE huwa
anaonyesha viashiria vifuatavyo
-Unakuwa na hisia kali sana za mapenzi kwake kuliko kwa mtu yeyote
– Unatumia muda mrefu sana kumfikiria sana mtu huyo,mara kwa mara unakuwa
unafikiria namna utamuokoa endapo atakuwa kwenye matatizo
-Unakuwa unatafuta kiashiria chochote kama anakupenda mfano akionyesha tabasamu
au akicheka unahisi anakupenda sana
-Unapata utulivu mkubwa sana kwake ukiwa naye karibu kuliko ukiwa na mtu yeyote
-Kama ukimuona anazungumza na mtu mwengine unapata wivu mkali sana na unaweza
kuingilia mazungumzo yao
-Unatafuta mazingira kwa nguvu zote ili upate kuonana naye au kuwasiliana naye.
-Unaona mazuri yake tu na kupuuza mabaya yake na mapungufu yake,mazuri yake
unaona ni makubwa sana kuliko mtu yeyote na makosa yake unayapuuza kuliko
makosa ya watu wengine,unavumilia tabia zake zenye maudhi ambazo awali ulikuwa
hauwezi kuvumilia kutoka kwa watu wengine.
-Unakuwa na wasiwasi muda wote,kama hakuna mawasiliano baina yenu unahisi
tayari amekuacha na amekwenda kumpenda mtu mwingine,endapo akikaa kimya bila
mawasiliano.
-Unaamini hauwezi kuishi bila yeye, hali hii inaweza kukufanya ujitoe mhanga
kwake ili akuone mtu muhimu sana kwenye maisha yake ili iwe rahisi kukupenda
kama vile ambavyo ûnampenda,unataka uwe naye karibu muda wote,ukiwa mbali naye
unakosa furaha.
-Unafanya juhudi kubwa sana ili muwe pamoja lakini yeye hafanyi juhudi zozote
ili muwe pamoja
ATHARI ZA LIMERENCE
LIMERENCE inaweza kusababisha athari zifuatazo katika mahusiano
1. KUTAKA KUMBADILISHA TABIA ILI AJE KUWA MWENZA WA NDOTO ZAKO
a.Mwanamke hugeuka mama mzazi kwa mwenza wake
Mwanamke mwenye kusumbuliwa na LIMERENCE hufanya mambo yafuatayo
-Anavutiwa kimapenzi na mwanaume ambaye hana kazi yoyote wala hataki kufanya
kazi,hapo Mwanamke huamua kumtafutia kazi lakini anakataa,atampa mtaji kisha
mwanaume anakula,atamchukulia mkopo lakini mwanaume anakwenda kulewa na kuhonga
pesa inakwisha anarudi nyumbani kukaa sebuleni akitazama Tv
-Mwanamke atahudumia watoto,atajenga kwa pesa zake, lakini mwanaume yupo tu
nyumbani hana MSAADA wowote lakini Mwanamke anakuwa hana ujasiri wa kumuacha
mwanaume huyo
-Mwanamke atafanya kazi ya kumbadilisha tabia mwanaume kama vile kuacha
pombe,kuacha wizi,kuacha uvutaji bangi,kuacha uhalifu lakini mwanaume anakuwa
hivyo hivyo miaka yote na mwanamke anakosa ujasiri wa kumuacha mwanaume huyo.
-Mwanaume kazi yake ni kumpiga, kumtukana, kumkashifu, kumkaripia, kumgombeza,
kumtangaza vibaya, kumlaumu, kumdhalilisha, kumuingilia kinguvu wakati huohuo
mwanaume huyo anaishi kwa kutegemea fedha za Mwanamke.
b.Nice guy
hapa ni eneo la mwanaume, LIMERENCE husababisha mwanaume anavutiwa kimapenzi na
Mwanamke mwenye hulka ya kiume (Masculine woman) – mwanamke anakuwa na tabia za
ubabe, ukali kupitiliza, kiburi, majivuno, jeuri, ujuaji, misimamo mikali sana,
mwanamke anakuwa hashauriki, haambiliki, anakuwa hataki kuambiwa makosa yake,
hataki kuambiwa cha kufanya,anakuwa na lugha ya udhalilishaji,
mwanaume anakuwa anapangiwa sheria,anapelekeshwa , anagombezwa lakini mwanaume
anakuwa hana sauti yoyote ya kujitetea.
2. KUWEKEZA FEDHA NYINGI SANA ILI KUBORESHA MAISHA YAKE LAKINI ANAKUGEUKA
BAADAYE
Hapa mwanaume ambaye anasumbuliwa na tatizo la kisaikolojia la LIMERENCE huwa
anafanya uwekezaji mkubwa sana kwa mwanamke kama ifuatavyo
-Atakutana na mwanamke ambaye ameumizwa kwenye mahusiano labda amemtendwa au
ametelekezwa na ujauzito au watoto kisha mwanaume anafanya kazi ya kumfariji,
kumlinda, kumliwaza, kumtetea lakini Mwanamke anakuwa hana huruma,hana
shukurani,anakuwa na masharti magumu sana na misimamo mikali sana,anampangia
mwanaume sheria kisha mwanaume anakubali
baada ya hapo mwanaume anafanya uwekezaji mkubwa sana kama vile kumsomesha,
kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumnunulia zawadi za gharama kubwa
sana,kumjengea nyumba, kusomesha watoto ambao Mwanamke alitelekezwa nao
lakini katika hali ya kustaajabisha mwanamke huyohuyo baada ya kuanza
kupendeza,kusimama vizuri kiuchumi anarudiana na mzazi mwenzie (Ex wake) kisha
anamuacha Nice guy bila kumuonea huruma hata chembe kisha akifika kwa mzazi
mwenzie anakabidhi fedha zote na mali zako alizopewa na huyu Nice guy kisha
baada ya muda anapewa ujauzito kisha anafukuzwa kwa mara ya pili, kisha
Mwanamke huyohuyo anarudi kuomba msamaha kwa yule Nice guy aliejitoa mhanga
kumfariji na kubadilisha maisha yake mara ya kwanza .
3. KUVUMILIA MATESO NA MANYANYASO KWENYE MAHUSIANO
madhara ya LIMERENCE ni uvumilivu uliopitiliza wa manyanyaso na mateso kwenye
mahusiano.
mwanamke anaweza kuvumilia unyanyasaji wa kimwili kama vile vipigo
-Vipigo hapa kunahusisha -kubamizwa ukutani,kupigwa vibao usoni,kuvutwa nywele,
kuburuzwa sakafuni,kuchomwa moto,kuchomwa pasi ya umeme,kubanwa na
plaizi,kupigwa mateke,kulazwa kwenye miiba,kufungiwa ndani, kufukuzwa nyumbani
usiku wa manane,kukojolewa mwilini,kukabwa kooni,kutishiwa kuuawa.
-Manyanyaso ya kihisia anaweza kufanyiwa yeyote
ambapo kunakuwa na mfululizo wa kauli zenye kuumiza kama vile ,-kufokewa,
kutukanwa, kujibiwa vibaya, kudhalilishwa hadharani, kufanywa kichekesho,
kugombezwa, kukaripiwa, kupelekeshwa,kutukanwa wazazi wako, kumshambulia kwa
maneno makali sana,
kuitwa majina ya udhalilishaji kama vile “mbwa”,au kuambiwa
“Hauna akili”,
“Unanuka sehemu za siri usinisogelee”
“wewe ni laana”
“wewe ni mkosi”
“Hauna hadhi ya kuwa na mimi”
“Mimi nikikuacha haupati mtu kama mimi”