USIMDHARAU USIYEMJUA UNDANI WAKE
Msichana mmoja alikuwa amempenda
kijana mmoja mtanashati na mcha
Mungu..
Malengo yao ilikua waje kuoana
baada ya muda.
Kijana huyu alijitoa sana kwa binti huyu
hadi wenzie wakamuona mjinga, lakini
ukweli ni kuwa alimpenda msichana yule
kwa dhati.
Alimtafutia kazi alipomaliza
chuo, alimshauri kuhusu mipango ya
maisha na alikua akimuombea kila
alipopata nafasiya kuomba.
Siku moja binti alikua anasherehekea siku
yake ya kuzaliwa…hivyo akaalika marafiki
zake, na watu wengine muhimu akiwemo
mpenzi wake.
Wageni wote walifika kwa wakati isipokua
yule kijana alichelewa kidogo…
Hivyo msichana akatumia muda ule ambao mpenzi wake hajafika kuwaeleza wageni namna yule kijana alivyokua wa muhimu kwake..,
Akamsifia sana, akasema atamvalisha
pete ya uchumba soon, na akasema siku
hiyo ya birthday yake anategemea zawadi
kubwa sana kutoka kwa huyo mpenzi wa
nafsi yake,
Baadae kijana akaingia na kuketi high
table..
Muda wa zawadi ulipofika watu
wakamtunza binti zawadi mbalimbali na
kijana akawa wa mwisho…
Hivyo wageni wote wakawa na hamu ya kutaka kujua zawadi aliyoleta hasa baada ya yule msichana kumsifia sana.
Kijana akaamka na kutoa mfuko.. kila mtu
akataka kujua kilichokua ndani ya
mfuko..mara kijana akafungua mfuko na
kutoa mkate..!!
Lahaula… watu wote wakastaajabu..
mkate??? Lakini kabla hajasema lolote
kuhusu ule mkate, yule msichana akaanza kulia.. akapandwa hasira kwa kuwa mpenzi wake amemuaibisha..!!
Akiwa analia kwa kwikwi, akamkwida shati na kumvua tai yake, akamwagia juisi,
kisha akauchukua ule mkate na
kuutupa.!!
Maskini..yule kijana akaukimbilia ule
mkate na kuuokota.. Kisha akarudi high
table na kusema “baby nakushukuru kwa
yote..Huenda umenidharau kwa kuwa
nimekuletea zawadi hii ndogo kwenye
siku yako muhimu kama hii. Lakini kama
ungetambua thamani ya zawadi hii,
usingefanya haya..”
Kisha akafungua ule mkate na kutoa vitu
viwili alivyoficha ndani ya mkate..
Kwanza akatoa ufunguo wa gari, ambalo alikuwa amemnunulia mpenzi wake na alitaka amkabidhi siku hiyo ya birthday.
Kisha akatoa pete ya uchumba na
kusema “Nilimuomba Mungu anipe mwanamke atakayenipenda katika hali yoyote.
Nilipanga leo nikuvalishe pete hii ili
kuelekea ndoto yetu ya ndoa..
..Lakini kwa kuwa uliangalia nje, uliona
mkate, badala ya pete hii ya thamani
iliyokua ndani..
Naamini mwanamke niliyemuomba kwa Mungu bado sijampata..
Nashukuru kwa yote uliyonifanyia, nimekusamehe, nawe naomba unisamehe kama nimekukwaza..”
Kisha akachukua mkate wake, huyoo
akaondoka. Msichana akaomba msamaha lakini ilikua too late..,.
MORAL OF THE STORY..!
Usidharau kitu/mtu kwa kumtizama nje..
Mungu huangalia thamani ya kitu ndani
lakini Wanadamu huangalia nje..
Thamani ya kitu/mtu ipo ndani na si rahisi
kuonekana..
Usiwe mwepesi wa kuhukumu kwa
kutizama umbo la nje..
Wale wanaokudharau leo na kukuona mkate, ipo siku watagundua haukua mkate wa kawaida… kuna vingi vya thamani ndani yako,.
Wote wanaokudharau leo ipo siku
watakusalimia kwa heshima..!!,
1 Comment
Pingback: Hadithi Tamu za Mapenzi, Maisha na Uchawi - Raha Special