SIWEMA
Siwema ni msichana wa pekee katika familia ya mzee Kibonye toka kuzaliwa kwake siwema hajaijua shida alilelewa maisha ya kifahari sana ,Akiwa katika shule ya sekondari Nzenga kila mwanafunzi aliogopa kumsogelea kutokana na jinsi alivyojiweka ,Umbo na sura ya siwema ilikua ni kivutio kikubwa sana kwa wanaume ,kila alipokuwa akipita wanaume waligeuza macho kumuangalia jambo hili siwema alilijua fika na kwakutambua kuwa anasifika kwa uzuri ndipo alipoongeza mikogo na majivuno
“Hellow my lovely daughter mbona umenung`unika kuna tatizo kipenzi’’ilikua ni sauti ya mzee kibonye akizungumza na binti yake siwema ,,,Siwema alijibu kwa sauti ya kudeka ndio baba “tell me my daughter/niambie binti yangu , siwema alianza kuongea huku akideka baba wiki inaisha hujanipeleka shoping kwa nini ?? woooh samahani binti yangu nilisahau siunajua majukumu ya kikazi haya mwite Mwangi nimuagize akupeleke mjini ,kwani wahitaji kama shilingi ngapi binti yangu,Siwema alimwambia baba yake kama shilingi laki tatu,Mzee Kibonye bila kusita alitoa noti mfukoni kwake na kuzihesabu kimafungu mafungu na kumkabidhi Siwema ,Siwema alishukuru na kuchukuaana na mwangi kuelekea mjini,,,,
Maisha yalisonga hatimaye Siwema alimaliza kidato cha nne ,hivyo kwa muda wa miezi kadhaa ilimlazimu awepo nyumbani kwa wazazi wake,,uwepo wa siwema mahali pale uliwachosha ,kila wakati alikuwa akiwapelekesha wafanyakazi walioajiriwa na baba yake kama watoto wadogo,,,“We kirange mshenzi kweli vile viroba vya sukari vinakaa hapo ‘’ilikua ni sauti ya siwema akimfokea kirange mzee mwenye miaka takribani hamsini,siwema alisema maneno hayo bila kujali kuwa anaongea na baba yake,,,Kwa mikogo aliondoka huku akiviringisha tako lake bila kujali kuwa ajafanya vizuri,Alipofika sebuleni aliwakuta baadhi ya wafanyakazi wapo wamepumzika wakiangalia mpira ,,,siwema kwa dharau alisimama vyema na kuwakazia macho wafanyakazi wale ,“Nyie nguruwe mnafanya nini hapa hivi mmeletwa huku kuja kupumzika ‘’wafanyakazi walinyamaza kimya maneno yale yaliwachosha na kuwachoma mioyo yao ila hakuwemo hata mmoja aliyethubutu kumjibu siwema ,siwema alirudia kusema“ Nyie wapuzi si nina ongea na ninyi wapumbavu wakubwa kweli hamnijui’’
Baada ya kuona siwema amekua mkali wafanyakazi wote walitoka nje kwa haraka kuhofia kupoteza kazi ,,walipofika nje kila mmoja alikua akilalamika. Ama kweli fedha inatutesa namna hii ipo siku ,kila mmoja alilamika kwa uchungu mkubwa
Ilikua ni siku ya alhamisi asubuhi mzee Kibonye aliwahi sana kuamka hii ni kutokana na majukumu mengi aliyokuwa nayo ,kama hajaondoka aliaacha maagizo ya kazi kwa vijana wake ,,maagizo yote alipewa mwangi kijana mmoja ambaye alikuwa ni mchapa kazi sana katika kampuni ile ,Baada ya hapo mzee Kibonye alielekea dining kwa ajili ya kujipatia kifungua kinywa alipofika alimkuta mama siwema na siwema wakiwa tayari kabisa wanamsubiri yeye afike ili waanze kunywa chai ,,shikamoo baba ilikua ni sauti ya siwema akimsalimu baba yake mzee kibonye aliitikia kwa furaha marahaba mwanangu kipenzi hujambo ,Siwema alijibu sijambo baba waliendelea kunywa chai baada ya hapo mzee kibonye alisimama akawaaga kuwa anaelekea ofisini ,,,,
Siku hiyo kazi zilikua zimepamba moto kila mfanyakazi alikua anachachamaa huku wakitokwa na jasho mithili ya wafua vyuma,,,Siwema alikua akijipitisha sehemu ya shughuli akiangalia mzembe ni nani katika kazi siwema alikua kavalia kisketi kifupi kilichokuwa kimeacha mapaja yake wazi masikioni alikua amevalia headphone bila shaka alikua anasikiliza muziki,aliendelea kuzunguka zunguka sehemu ile ,Hali hii iliwaboa sana wafanyakazi walihisi kuchafukwa kwani binti huyu alikuwa anawakera sana,,Mzee mgosi alikua amechoka sana kwani mifuko ya sementi aliyokuwa amepakua ukilinganisha na umri wake kweli ni kazi nzito sana,duuuh ila kama siyo dhiki na shida mzee kama huyu angetakiwa awe amepumzika nyumbani ,,,,Kitendo cha mzee huyu kupumzika tu kilikua ni kosa kubwa kwa siwema looooo!!!!!
Ni bora siwema asingeliona kwa hasira siwema alisimama kuelekea alipo mzee Yule alimtizama kwa dharau na kumzaba kofi zito PAAAAAAAH!!!!! “We kiumbe wewe umekuja kulala hapa mpuzi kabisa ‘’Mlio wa kofi uliwafikia wafanyakazi waliokuwa wakiendelea na shughuli pia baadhi ya wafanyakazi walishuhudia tukio lile lilivyokuwa limetokea ,kitendo hiki kiliwachafua wengi sana na wengine walidiriki kuacha kazi ,Kwa bahati nzuri mama siwema alikua pembeni kabisa sehemu lilipo duka lao la jumla ,na alifanikiwa kuona kitendo mwanae alichomfanyia mzee mgosi taratibu alimwita siwema ,siwema bila hofu yoyote alimfuata mam yake .
Mama siwema alimkanya mwanae sana na kumwambia maisha hayaendi hivi pia alimweleza kuwa hata baba yake mzazi hakuwai kufanya kitendo kama hicho.
Kwa siku siwema alizokuwa pale nyumbani mwili wake ulipendeza sana kwa uzuri wake na shepu aliyojaliwa na mungu ni wazi kabisa kila kijana aliyemwona lazima hisia za mapenzi ziliwaka juu yake ,,,mazingira aliyokulia siwema yalikua ni mazingira ya kazi mzee kibonye aliajiri takribani vijana mia tatu katika kampuni yake,,,Vijana wengi walijitoa ufahamu kwa kujaribu kumtongoza siwema lakini walichoambulia ni kufukuzwa kazi na kuzalilishwa haya yalikua ni maneno ya siwema kwa kijan mmoja aliyejulikana kwa jina la Simioni “mpumbavu kweli wewe yaani kati ya maboya wewe ni wa kwanza yaani wewe kabisa wakunitongoza mimi muone alivyo kwanza mwenyewe kuoga huogi maskini mkubwa wewe ukome adabu yako kwanza kuanzia kesho kazi huna umenivunjia heshima’’ Simioni alimwomba sana siwema asimshitaki kwa baba yake simioni alilia kama mtoto mdogo,kilio cha simioni kiliwafanya mpaka vijana wengine waingilie kati..wewe siwema si umsamehe mwenzio khaaa kaeleza tu hisia zake kwako mbona unakuwa hivyo Kipesa alidakia ,,,HAHAHAHAH Siwema alitabasamu kwa dharau eti kaeleza hisia zake kwangu.
Siwema alielekea ndani huku akijizungusha kwa maringo yote kuwaacha vijana wote wakimtumbulia macho
Ilipofika asubuhi ripoti iliyokuja ni kuwa Simioni kafukuzwa kazi kila mmoja alisikitika na wote walitambua kuwa ni njama za siwema,Maskini kijana Yule aliyetoka katika familia masikini amepoteza kazi yake kisa binti huyu wafanyakazi wengi walisikika wakilalamika ,,Wafanyakazi walichukia sana na kuahidi kulipiza kisasi kwa hili
Ilikua ni siku ya jumamosi mzee Kibonye aliagiza vijana nane kuelekea mjini kufuatilia vifaa vya electronics kwa ajili ya ujenzi ambavyo vilikua vinagaharimu takribani milioni ishirini Mwangi alipangwa kama kiongozi wa msafara ule alikabidhiwa hela kwa ajili ya shughuli hiyo,,,Siwema akiwa ndani alitoka njee haraka na kumsihi bab yake anataka kuambatana na vijana hawa kuelekea mjini kwa ajili ya manunuzi ,,baba yake na mama yake walimkatalia lakini siwema alifanya ugumu na kulazimisha kwenda baba na mama yake walimsihi sana ila mwishoe walimwacha kutokana na kunang`ania kwake, Siwema aliingia ndani na kuvaa nguo fupi na iliyoonyesha baadhi ya sehemu zake ,nguo aliyovalia siwema ilikua haina maadili kabisa ,aliingia ndani ya gari na kukaa sehemu ya mbele ,safari ilianza kuelekea mjini walipofika vichakani mwangi alishuka ndani ya gari na kuwaambia wenzake kuwa anakwenda kujisaidia alivyoshuka alitumia simu ya mkononi kuwataarifu wenzake watoke nje ,walipotoka nje Mwangi alianza kwa kusema “Hivi mnaonaje hii milioni ishirini tukigawana wote hapa alafu kila mmoja wetu akapotelea mitini hii ni hela ndefu sana ujue,Kwa uroho wa hela waliokuwa nao vijana wale waligawana fedha zile ,Siwema akiwa ndani ya gari aliona takribani dakika kumi zimekata bila mwangi na wenzake kurudi alishuka ndani ya gari huku akinyoosha mdomo wapuzi wakubwa hawa hawanijui alivyotoka nje aliwaona vijana wale vichakani wakigawana hela alicheka kwa dharau “Wapuzi wakubwa nyie mnafanyaje hahahahah’’Kijana mmoja aliropoka mwache aje lazima tumbake hawezi kutufanyia hivi kwanza katutesa sana kazini lazima tulipe kisasi, vijana wanne baada ya mgawanyo wa hela walikimbia na kumwacha siwema akiwafuatilia wale wanne waliobakia.
Siwema alivyowafikia alisimama wima huku akishika kiuno nyie wajinga mnafanya nini ……kabla hajamalzia kauli yake vijana wale walimkamata na kumpeleka vichakani ,Maskini siwema alibakwa mpaka kupoteza fahamu.Baada ya vijana hao kumaliza hazma yao waliondoka na kumwacha siwema akiwa amezimia.
FUNZO USIMDHARAU MWENZIO,PIA NI VYEMA KUWAHESHIMU WAZAZI