PISI YA KIJIJI
EPISODE 4
Alishtuka sana baada ya kusikia sauti nzito lakini alifurahi baada ya kugundua kuwa mtu aliyemwita ni kelvin . Mwanaume anayempenda na kumuwaza sana .Basi walibaki wanatazamana sana na kila ntu akionyesha tabasamu ,utofauti ni kwamba tabasamu la kelvin nila kirafiki lakini tabasamu la Olesta ni la
upendo patamu hapo ..lakini kelvin
aligundua kuna kajani kametua kwenye nguo ya olesta alimsogelea ..
Kisha akamtoa kile kijan ile kumsogelea yaani huwezi amini kamoyo ka olesta kariridhika sana yaani alihisi raha ya ajabu.kelvin anafanya kwa utu lakini olesta anajua kelvin huenda labda anampenda kumbe hakuna chochote zaidi ya kufanya au kumsaidia kama binadamu.
“kelvin umeamkaje ???”huki
akimtazama kwa kujali na upendo mzito
“niko salama vipi wewe”. “mimi pia niko salama “
“nakuona unachota chotq maji”
‘yaah kazi ndo nguzo yetu si unajua ..”
“okay but kuna kitu nataka kukwambia kelvin”
“kitu gani hicho olestaaaa”almkazia macho…
“Na………….” mara ghafla kabla hajamalizia kusema sauti ilisikika “we olesta uko wapi njoo ulishie kuku huku
,maji gani unachoka huko alikuwa ni
mama yake na olesta. Ndo alisema
hivo
“kelvin mama kaniita tutaongea siku nyingine tukionana “alijitwisha ndoo na kuondoka haraka sana lakini alijilaumu kimoyomoyo”mama naye ananikata stimu nilikuwa naweka hisia zangu wazi sasa anadhani ujasiri nitautoa wapii??? ila ipo siku nitakwambia kelvin”
Kelvin yeye alipeleka maji nyumbani na kuwatembelea baadhi ya rafiki zake basi mizunguko ilikuwa mingi sana
sababu ilipita muda toka awatembelee
baada ya ukimya wa muda mrefu huko hakusema neno bila kutaja jina la mariamu kila atakachosema mfano wa kwanza ni mariamu mpaka marafiki zake wakamuuliza kwani mariamu yukoje maana unavompamba kama malaika ……
Kelvin alicheka sana yaani alikosa neno la kuwambia washikajizake walipomuuliza umemfungukia kelvin alianza visingizo ooooh mara nimekutana naye mara moja maro oooohooo pisi iko bize hapo ndipo marafiki zake wakamwamwambia
“chelewa chelewa mwana utakuta
mwana si wako …. ooooooho! utabaki unamsifia wenzako ndo wanapita naye.
Maneno yalimuingia kelvin vizuri akaona kuna ulazima wa kumuweka wazi yule nesi mpya kelvin alimpa jina la “PISI YA KIJIJI”
Basi aliondoka ile sehemu chapuchapu kuelekea nyumbani maana muda ulikuwa umesogea kidogo lakini katika pita pita zake kuna dada alikuwa mbele yake ghafla alipawa na watu walioonekana
wanafukuzana na kumwaga nyanya
zake zilizokuwa kwenye kimfumko chake … tukio hilo kelvin the golden boy aliliona …….
Na nyanya nyingine zilizoanguka zilifika mpaka miguu kwake aliamua
kumsaidi kuokota moja , mbili , tatu
,nne na ya tano wote wakaishika kelvin alikuja kupandisha uso taratibu na kukutana ana kwa ana …. na yule binti alitabasamu sana yaani meno yote na kusema “kumbe ni wewe mariamu”
Mariam naye alicheka na kuziweka
nywele zake vizuri namna anaziweka na kuzirusha rusha huku anaushika mtandio wake wa kijana kelvin ndo anadata hachoki kumtazama yaaani jamani mapenzi akitabasamu kelvin anamtazama kuanzia kwenye midomo
,tushavu na macho mpaka binti akamshtua “unawaza nini kelvin ???”
Alizuga “khaaaaaa amna basi nilipenda nikutazame tu” huku wakiinuka wote na kelvin alimwomba amsaidie kubeba lengo ni kujua wapi binti anakaa moyoni mwake “jamani
huyu mdada nikiwa naye nahisi kabisa
ana ramani ya moyo wangu “
Binti naye “mmmmmmmh huyu kaka hata jina simjuwi tutakaa kimya mpaka saa ngapi ngoja nimchokoze “
“kaka ujuwe hujawahi niambia jina lako”
“naitwa kelvin we ni mariam sio ” “mmmmmmh nani kakwambia ” “si uliitwa siku ile jamani”
“oooooho nawe ungeitwa ningekujua tu”
“hahahha watu wengi hawanijuwi” “mmmmmh kweli “
“ndiyo nikwambie kitu”
“nambie “
“sema nilikusahau kukwambia toka muda “
“mmmmmh sema basi”
“umependeza sana yaani we ni mrembo sana lakini hizo nguo zimeuongeza urembo wako”
“kelvin acha kunipamba mi ni wa kawa….” kabla hajasema kelvin alimsogelea na kumuweka kidole mdomo na kusema
“kshhhhhhhhhhhhhhhhhhh, usijikose heshima malkia wangu “
kwa namna alivyomsogelea yule binti
kijasho chembamba kilikuwa kina mtiririka na macho yao yanatazamana huku yakizindikizwa na upepo mzuri sana wa kuvutia sambamba na sauti za ndege…..
Muda huo huo Gabriel naye alikuwa anakatiza njia ile ile ambayo mariam na kelvin wapo katika pozi tamu la mahaba lakini sio mahaba lakini Gabriel atawaelewa akiwakuta hivo maana naye anampenda yule binti bila kujua ndo huyo binti ambaye rafiki yake anampenda
Alikuwa akikatisha akiimba wimbo fulani wa msanii mmoja anaitwa ben will wimbo unaitwa najitoa … ile anaanza kuimba tu
nimechagua kuzama kwako,kwenye di…….alikatisha nyimbo hapo hapo alishtushwa na alichokiona mbele yake na alikunja ngumi kwa hasira huku kakunja ngumi yake je aliona nini
?????
Usikose sehemu ya 5
Sehemu inayofuata (Episode 5)
inaonekana itakuwa na hali ya sintofahamu na huenda Gabriel akachukua hatua kutokana na wivu wake. Je, atamkabili Kelvin? Au ataamua kumfuata Mariam kwa njia ya hila? Pia, Mariam ataanza kuhisi kitu kwa Kelvin, au atabaki na ukaribu wa kawaida
EPISODE 5
Olesta alikasirika sana baada ya kelvin kumuita jina la mwanamke mwingine yaani ni kama dharau alivoitafsiri yeye
na kelvin akaja kugundua kuwa
amemuita jina la meanamke mwingine tena kwa hisia
Olesta alisema kwa hasira ,” unawezekanaje mwanaume anayemoenda ataje jina la mwanamke mwingine tena kwako ina maana anaishi na ww akiwa kwenye hisia na mwanamke mwingine huko ni kunikosea heshima “
“samahani olesta nina mawazo aana naomba nisamehe jamani najua umejisikia vibaya tena sana na hii imekuja kutokana na ujinga wangu ,am
sorry oleata naomba unisamehe eti
nakuahidi hili halitokuja kutokea” lakini Olesta hakujibu aliondoka kwa hasira kelvin alijaribu kumuita Olesta Olesta Olesta lakini ni wimbo usio na maana kwa olesta
Aliondoka tena akiwa anakimbia huku machozi yakimtiririka kelvin nyuma kashika kichwa chake na kusema nimefanya nini mimi mbona kma sijitambuwi akawa anaondoka huku anajilaumu.
kwa Olesta naye kwa hasira zake
alikuwa anakimbia akiangalia nyuma bila kujua kuwa mbele kuna kijana alipokatisha ikabidi kijana amdake na kutokana na hali ya uoga aliokuwa nao Olesta wakajikuta wanadondoka chini katika pose fulani amazing huku nywele za olesta zikimfunika yule kijana olesta kutoa toa nywele zikawa zinapigwa na upepo kuja kumtazama yule kijana huwezi amini alikuwa ni Gabriel ……….
Olesta na Gabriel macho yao yakawa yanatizamana na nyumba ya jirani
kulikuwa kuna piga kale ka nyimbo ka
benwill najitoa
“zikikutana zetu mboni,mioyo inashibana na penzi letu samson hatuumii kwa miiba hatawaseme kulikoni siwezi sikiliza aaaaa….
Basi watu wanatazamana lakini Gabtiel asijuwe huyu binti kafa kaoza kwa kelvin yaani humwambiii kitu aiseeee naiona vita ya tatu ya dunia huko mbele yaani kila alipopaona Gabriel pana kelvin na Gabriel hakujua kabisa kama kelvin na olesta wanafahamiana …..
Basi Baadaye kwa aibu wote walisimama huku kila mtu akiangalia chini …
“mambo ” “powa vipi”
“safi tu pole kwa ajali” “hahahahammmh kawaida tu “
” uwe una angalia mbele ,mbona kama ulikuwa unalia”
Akazuga na kusema “hapana hata sikuwa nalia”
“oooho apo sawa ua zuri kama wewe
huhitaji kulia . atakayekuliza moja kwa moja jehanamu”
“mmmmmmh kwa nini ???” “sababu ya uzuri wako”
kwa aibu”bhana acha uongo unaitwa nani??”
“naitwa Gabriel sijuwi wewe unaitwa nan?i’
“Mi naitwa Olesta”
“Wow una jina zuri la kuombea mkopo kabisa”
Walicheka wote kisha wakapeana mikono ya kwa heri
Lakini Gabriel kila anavopiga hatua anakumbuka moment za kuangukiana kutazamana kusalimia na kadhalika yaani kichwani kwako kuna kazi nzito lakini alipotezea huku akipiga mikono yake na kusema “Mungu anaumba wewe utajikuya kila mwanamke unataka kuoa . Ngoja nikajilie zangu birian bhana “
Kwa binti naye ameenda sokoni kununua vitu mara anasahau chenji mawazo ni kwa kelvin kwa nini amtaje mwanamke mwingine ina maana
anaongea na mimi mawazo yake yapo
kwa malaya wake . Akabeba vya kupika kisha akaondoka zakeeeeee
Lakini Mangi alimuita “olesta olesta!!!!!’
Aligeuka na kupiga hatua kadhaa mpaka gengeni pale na kusema “kuna nini mangi??”
“umesahau chenji yako ,inaonekana una mawazo sana???”
“oooooh asante jaman daaah”
“Au shemeji kakuzingua ,maana watoto wa saizi mapenzi yanawapelekea moto”
“hhaha Hapana mapenzi gani bhana”
“oooho sawa basi kazi njema na siku
njema”
“na kwako pia mangi”
Basi Olesta Alifunga safari mpaka nyumbani kwao akiwa anajilaumu laumu tu ‘hivi kelvin ananichululiaje mimi???yaani hiki kitendo cha kumtaja mwanamke mwingine kimenikera
kweli lakini tatizo mi mwenyewe sikusema ukweli mapema ” Akafika nyumbani ile anafungua mlango alimkuta kelvin kakaaa sebuleni kwao alishtuka na kuangusha vitu vyote alivyovibeba baada ya kupata
mshtuko alikunja sura na alionekana
mtu mwenye jazba
Alishtuka baada ya kutazama upande wa kushoto je aliona nini usikose inayofuata ……
EPISODE 6
Baada ya kelvin kukaa katika pose la mahaba kila mtu akiwa anamtazama mwenzake kaaibu kaka mshika mariamu na alizuga na kusema “tumefika karibu ndani “
“aaaaaaaaha asante mariam” alisema kelvin
Kwa sababu walikuwa washafika
nyumbani hivyo waliingia ndani lakini kipindi Gabriel anatokea alikutana na jamaa mmoja mwenye uhasama naye ila sio kelvin na mariam maana walikuwa tayari washaingia ndani
……..
MAZUNGUMZO YAO SASA…….
“Wewe! Si umesahau deni langu eeh?”
“Deni gani tena?” Gabriel aliuliza kwa sauti ya kujidai, lakini ndani ya moyo wake, hofu ilianza kupanda.
“Usijifanye hujui, Gabriel. Nilikuazima
pesa ili ulete mzigo wako wa biashara, ukaniambia utanirudishia baada ya wiki mbili. Leo ni mwezi mzima na hujasema chochote. Unajua mimi sipendi watu wasio waaminifu “
Gabriel alimeza mate. Alikuwa amesahau kabisa kuhusu deni hilo kwa sababu akili yake ilikuwa imejaa mawazo mengi yaani deni acha liitwe deni…..
“Wewe unadhani nitakimbia?” Gabriel alisema huku akijaribu kutabasamu.
“Nipe muda kidogo tu, nitakurudishia
pesa zako.”
Jamaa huyo alimsogelea na kumshika mkono kwa nguvu.
“Hakuna muda tena. Leo nataka pesa yangu, au nitakufundisha adabu.”
Wakati hayo yakiendelea nje, ndani ya nyumba Mariam na Kelvin walikuwa wamekaa karibu kwenye kochi mariamu akichambua mboga. Kelvin alikuwa na tabasamu la fulani hivi
usoni mwake huku akimtazama
Mariam kwa macho ya uchangamfu.
“Mariam, nahisi kama nakufahamu kwa muda mrefu sana,” Kelvin alisema huku akimtazama kwa makini.
Mariam alitabasamu, akakunja vidole vyake kwa aibu.
“Unanifurahisha Kelvin,” alisema kwa sauti ya upole. “Lakini mbona unaniambia hivyo?”
“Kwa sababu kila ninapokuwa na
wewe, nahisi kama moyo wangu unapumzika.”
Mariam aliona aibu, akashusha macho chini.
“Nashukuru kwa maneno yako, lakini unajua hatujajuana kwa muda mrefu ni siku tano sijuwi nne sijakuzoea hujanisoea kifupi hatujazoeana.”
“Sijali,” Kelvin alisema kwa upole. “Wakati mwingine, moyo huamua kabla ya akili.”
Mariam alitaka kujibu, lakini kabla hajafungua mdomo, mlango uligongwa kwa nguvu.
NGO ! NGO! NGO!
Kelvin na Mariam walirushwa na mshangao.na ikafanya maongezi yao yaishie palepale na kila mtu aliwaza nani kaugonga ule mlango tena kwa fujo sana
“Mariam, nani huyo?” Kelvin aliuliza huku akisimama.
“Nadhani ni mtu tu ,” Mariam alisema
huku akiinuka taratibu kwenda kufungua.
Mariamu alipiga hatua moja mbili tatu sauti ya viatu zilisikika koh koh koh akawa ashafika mlango alishika kitasa na kukizungusha Alipofungua, aliyegonga alikuwa kijana mmoja aliyekuwa akihema kwa uchovu, kana kwamba ametoka mbio. Uso wake ulikuwa na wasiwasi mkubwa.
” Huko nje kuna ugomvi mkubwa! Watu wanapigana vibaya sana!” kijana huyo alisema kwa sauti ya juu.
Kelvin alimtazama Mariam kisha akasema kwa upole, “Mariam, kaa ndani. Nitakwenda kuangalia kinachoendelea.”
Mariam alitaka kumzuia lakini Kelvin tayari alikuwa ameshatoka nje kwa kasi.
Alipofika eneo la tukio, aliona kundi la watu wakizunguka wawili waliokuwa wakizozana vikali. Mmoja alikuwa rafiki yake wa karibu Gabriel na mwingine alikuwa mwanaume mnene na
mwenye mwili wa miraba minne.
Gabriel alikuwa amekunja ngumi kwa hasira, huku yule mwanaume akimpigia kelele kwa jazba.
Kelvin alipenya kati ya watu na kuwasogelea.
“Jamani, jamani! Kuna shida gani?” Kelvin aliuliza huku akiweka mkono kati yao.
“Kelvin, huyu jamaa ananidai pesa kwa nguvu na anataka kunivunjia heshima
mbele ya watu!” Gabriel alisema kwa
hasira.
“Heshima gani unayoongelea?” yule mwanaume alimkatisha kwa sauti nzito. “Uliniahidi utanilipa baada ya wiki mbili, sasa ni mwezi mzima! Mimi si mtu wa masihara!”
Kelvin alimtazama Gabriel kwa macho makali, kisha akageukia yule jamaa.
“Rafiki yangu anaweza kulipa deni lako, lakini si kwa fujo kama hizi,” alisema kwa sauti ya utulivu lakini
yenye mamlaka. “Tunaweza kutatua
hili kwa amani.”
Watu waliokuwa wakitazama walipunguza kelele zao, wakisikiliza jinsi Kelvin alivyoshughulikia hali hiyo kwa hekima.
Yule mwanaume akavuta pumzi kwa nguvu kisha akasema, “Sawa, lakini nataka pesa zangu haraka. Msinifanye nionekane mjinga hapa mtaani.”
Kelvin alimtazama Gabriel, kisha akamvuta pembeni kidogo.
“Unajua kama una deni, unapaswa kulipa. Sasa kuna mpango gani?” aliuliza kwa sauti ya chini.
Gabriel alishusha pumzi ndefu. “Nina mpango wa kulipa, Kelvin, lakini mambo hayajakaa sawa. Nitahitaji muda kidogo.”
Kelvin alifikiria kwa muda mfupi, kisha akamgeukia yule jamaa.
“Sikia, rafiki yangu ana shida kidogo
kwa sasa. Naomba umpe muda wa ziada, tutahakikisha anakulipa.”
Yule jamaa alimtazama Kelvin kwa macho makali, lakini akaonekana kutulia kidogo.
“Naamini maneno yako, Kelvin. Lakini akichelewesha zaidi, itabidi nishughulikie mwenyewe,” alisema kabla hajageuka na kuondoka.
Kelvin alipumua kwa utulivu, akageukia Gabriel.
“Bro, lazima ujipange. Usiruhusu deni likuharibie maisha,” alimwambia kwa sauti ya ushauri.
Gabriel alitikisa kichwa kwa aibu, akijua kwamba Kelvin alikuwa sahihi.
Baada ya hali kutulia, Kelvin alirudi kwa Mariam, ambaye alikuwa akisubiri kwa hamu ndani ya nyumba.
“Nini kimetokea?” Mariam aliuliza mara tu Kelvin alipoingia.
“Sawa tu, nilifanikiwa kuwaachanisha. Yalikuwa mambo ya deni tu,” Kelvin alisema huku akitabasamu.
Mariam alimtazama kwa muda mrefu, kisha akatabasamu taratibu.
“Wewe ni mtu mzuri sana, Kelvin.”
Kelvin alitabasamu, akimtazama Mariam kwa macho yenye hisia. na kusema wewe ni mzuri zaidi mariam yaani sichoki kukutazama ujuwe ….
Mariamu kwa aibu “acha mambo yako
kelvin na wewe unanisifia mno muda mwingine unanipa sifa zisizonistahili
…….”
“hakuna ambacho hustahili mrembo kama wewe jamani tabasamu jamani moyo wangu uridhike”
“kwa aibu” kelvin bhana mie siwezi jaribu kwa ajili yangu “
“okay sawa ” mariamu alimjibu kelvin
Mariam alimtazama Kelvin kwa macho ya mvuto ya uchokozi akawa yuko serious kidogo muda huo kelvin anamtazama pia , kisha taratibu
akaliachia tabasamu lake. Lilikuwa
tabasamu lililotoka ndani kabisa ya moyo wake, likitengeneza mistari midogo pembezoni mwa midomo yake myembamba, ikichanua kama maua yanavyofunguka taratibu asubuhi.
Mashavu yake yalinyanyuka taratibu na dimples mbili ndogo zilizoonekana kwa mbali, . Macho yake nayo yakionyesha uhalisia wa tabasamu hilo,
Nyusi zake zilipinda kidogo, zikampa sura ya msichana aliyekuwa na furaha ya kweli, lakini pia aliyekuwa akificha
kitu kitu ambacho hakutaka kusema
kwa maneno, bali kwa tabasamu lake. kwa sababu ndio kitu kelvin aling’an’gania kukiona na mariamu ilibidi amuonyeshe …
Ghafla dirisha lilifungua na upepo ulivuma mpaka mule ndani nywele chache zilizokuwa zimeangukia usoni pake, zikapepea taratibu huku akiziondoa kwa vidole vyake laini.
Katika sekunde chache hizo, Kelvin alihisi kana kwamba dunia nzima imesimama—hakukuwa na kelele zozote, hakukuwa na kitu kingine cha
maana… kilichokuwepo tu ni Mariam
na tabasamu lake.
Kelvin alizinduka kwa mshangao, macho yake yakiwa bado yameganda kwa Mariam, huku mapigo ya moyo yanaenda mbio …….
Alijisemea moyoni………. “Jamani! Mbona kama vile nipo
ndotoni? Hivi huyu msichana ana nini?
Mbona tabasamu lake linanifanya nihisi namna hii?” aliwaza kwa mshangao.
Mariam alicheka kwa sauti nyororo,
halafu akakunja mikono kifuani, akimtazama Kelvin kwa macho ya utani.
“Kelvin, mbona unaonekana kama mtu aliyepigwa na butwaa?” aliuliza huku akimkodolea macho.
Kwani kelvin anasikia hata anachoulizwa tayri kawa kiziwi hasikii na mdomo tayari kuna vifusi kumi vya mchanga kadata kwa mariamu …..Basi mariamu akimshitua na kumuita mara tatu we kelvini ! we kelvin ,we kelvin na
alishtuka na kusema namu madamu
naona muda umeenda aliinuka na kuvaa viatu kisha akaondoka mariamu alipigwa na butwaaa
“huyu kapatwa na nini??? kelvin yeye aliendelea na safari yake ya kurudi nyumbani lakini alikutana na Olesta
” kelvin mambo”Ujue Olwsta anampenda sana kelvin lakini kelvin sasa humwambii kitu kwa mariamu ….
“poa mzima mariamu ” badala ya olesta yaani kachanganyikiwa Olesta alikunja uso kwa hasira sana maumivu
aliyoyapata kuitwa jina la msichana
mwingine aisee ilimuuma sana
Unadhani nini kitatokea usikose bonge la love story hiii ..