PISI YA KIJIJI
EPISODE 10
Basi ni pale pale tulipoishia baada ya
kelvin kuambiwa ukweli na olesta kuwa anampenda sana maneno yaliyomfanya kelvin kuangusha zile ndooo maana mikono ilikufa ganzi
kabisa kwa maneno hayo . sio kwamba alishtuka kwa sababu hakutegemea kuambiwa hivyo hapana sababu ni kwamba naye ashawahi kumpenda sana olesta lakini kwa sasa moyo wake upo kwa Mariamu hivyo alimuonea huruma na kuwaza nini atamjibu ……..
Basi alimsogelea Olesta akiwa serious sana na alipotaka kumwambia kitu Olesta alimwekea kidole mdomoni na
kimwambia usinijibu saizi lisije likawa
jibu baya naomba nijibu siku nyingine tafadhali naomba ufikilie mara mbili ujuwe mwanamke ni mdhaifu sana kumwambia mwanaume anampenda lakini maji yakikufika shingoni lazima useme
kelvin niko hoi kwa penzi lako yaani sijielewi nahisi naenda kuwa chizi mimi . huku machozi yakimtoks kelvin anawaza amjibu jibu gani aeleweke bila kumuumiza ……
Ghafla kabla hajaongea sana ilisikika sauti “we olesta ilibidiii aitike maana
aliyemuita alikuwa mama yake
“abeee mama nakujaaaa” kisha akamgeukia kelvin na kumshika mikono yote miwilo please think twice naumia baba kisha akajitwisha ndoo na kuondoka muda huo kelvin bado kagannda kana thanamu la kuchongwa hajuwi afanye nini … mpaka naye alipohisi jirani mmoja akipita lakini matukio yote hayo mwamba
Au waweza mwita MMBEYA WA MTAA mr cholo aliyaona maana muda huo alitoka nje kupiga mswakiiiiiiiii…………..
Alivunga hakusema kitu sababu bado
ana kusanya takwimu au ushahidi basi kelvin aliingia ndani kwake na kujifunhia yale maneno maana hajuwi nini amjibu binti ili angalau asimuumize hisia zake na jibu liwe angalau linamfariji na kumfanya aelewe kuwa kwa sasa kelvin naye anampenda mtu mwingine naye hana uhakika anayempenda kama anampenda ….,..
Siku iliyofuata majira ya mchana mida kama ya saa nane hivi mchana Dr samwel baada ya kutoka kazini alikuwa akiongoza sehemu anayokaa
macho yake yalikuwa yakitazama
upande fulani wa watu ile kugeuka kishoto alikutana na Lucy yeye hajuwi kuwa lucy ni kama gari la taka lina beba kila kitu iwe makopo , mawe yaani ni jamvi la wageni na kilichofanya awadatishe watu wengi ni Uzuri wake … ni pisi ya kwenda na kama unamvomjua dokta sam au mr Romantic ni mzee wa totoz na anajiamini anajua hakuna kitu anachoshindwa kumpa mwanamke sio pesa ,sio nini vyote anavyo yaani ni kama gari liko full tank …..
Basi naye kwa nini asidate na urembo
wa lucy bila kujua ni jamvi la wageni mr Romantic alimsimashi na kumwambia amsubiri na kisha kwa kuwa walikuwa wanaend njia moja ilikuwa raisi kumsubiri na walianza kupiga hatua huku wakiongea .
“Mmmmmh kumbe warembo kama nyinyi bado mpo??’
“hahah kwa nini???”
“kwa sababu sijawahi ona msichana mrembo kukuzidi wewe ????”
“mmmmmmh mbona wapo hafu mi sistahili sifa hizo”
“nikiwa na wewe hata nguvu za
kucheat nazitoa wapi’ “mmmmmh naijua hiyo sema
unaonekana mchangamfu unaitwa
nani ?
“naitw dokta samweli nina siku chache katika hospitali hiii”
Lucy kusikia ni daktari akajua hapa ndo pakuchumaa maokoto akaanza kumtega na kulegeza sauti ili angalau amweli aingie
” mi naitwa lucy nimefurahi kusikia sauti yako na kuongea na wewe hakika umeifanya siku yangu kuwa bomba
zaidi japo ni mara yetu ya kwanza
kuonana umekuwa mcheshi muongeaji hafu kingine …….. akakatisha .
“kingine nini lucy”
“your so handsome huku akimuweka kola vizuri kisha akaondoka . Saa ngapi jamaa asidate bila kujuwa huyu ndo mtoa utamu maarufu hakuna asiyemjua ………..
Lakini kipindi muda huo wote wanaongea rafiki wa Isabella kwa jina la Tina aliliona hilo na ukichukulia
kuwa ana jua fika rafiki yake kampenda
sana Samweli Pia anajua tabia zote za lucy cha utyammmmu……Alikimbia haraka na kumkuta shoga yake isabella akipika alimshtua na kumwambia
“Daaaaaaaaaah rafiki yangu ” huku anahema
“kheeeeee kuna nini ” akiwa anashangaa
“pole lakini jamani”
“pole ya nini tena mbona sikuelewi??” “pole shoga yangu “
“kuna msiba ‘ “hapana”
“kuna ndugu yangu anaumwa “
“hapana “
“kuna nini sasa si useme”
“nimemkuta samweli na lucy wakitembea wanaonekana ni wenye furaha maana tabasamu kama lote ….
kusema hivo kikombe alichoshika kiliangua chini na kuoasuka paaaa. mikono imekufa ganzi akili imepotea
Alibaki anamtazama Tinah
EPISODE 11
Isabella kusikia hivo aliumia sana
alikosa hata nguvu ya kusema chochote mapigo ya moyo wake yalikuwa yanaenda kasi sana yaani alihisi maumivu makali mno . Unajua isabella anampenda sana Samweli lakini tatizo ni kwamba anaogopa kwa kuwa ana maisha ya kawaida hivyo hawezi kukidhi au kuwa hadhi ya samweli hivyo akisikia yupo na mwanamke mwingine Roho inamuua sana sio siri…..
Tina alimwambia “rafiki yangu ni bora umwambie ukweli maana chelewa chelewa utamkuta mwana si wako.
karaga bao na ujinga wako kila siku
nakwambiya mwambie huelewi mbona huuonei huruma moyo wako
????? unadhani mapenzi ni suala la mchezo mchezo sio we endelea mpaka uoewe kadi ya harusi.
huku akifuta machozi”sio kwamba nashindwa kumwambia samweli kuwa nampenda tatizo kwa kijana kama yule handsome si handsome tu pia ni mtu mwenye kazi yake unadhani atakubali kuwa na maskini kama mimo. Angalia mavazi yangu ya wauza migahawa yaaani sina mvuto wa kuwa naye ……..
Hapana usiseme hivo shoga yangu
mapenzi hayapo hivo mapenzi hayaangalii vitu kama hivyo mapenzi yanaangalia moyo wa mtu na sio hadhi sawa kuwa muelewa pia acha kulia sawa ?????
“sawa nimekuelewa Tina ” akachukua kitambaaa na kumfuta machozi shoga yake ujuwe Tina na isabella ni marafiki sana na wanapendana unaweza kusema ni ndugu lakini wapi…..ni marafiki tuuuuuuuu…..
*************
Basi majira ya saa nane mchana kelvin naye alitoka ndani mwakw na kumkuta
Olesta kasimama karibu na mwembe
uliokuwa karibu alionekana na mawazo ikabidi amfuate ajuwe anawaza nini maaana hii hali imeanza hivi karibuni na inashangaza . Kelvin alimfuata na kukaa karibu yake na kuzungumza naye
“Olesta!!!”
“aaaaaaabe kelvin umefi a saa ngapi” “nimefika sasa hivi tu “
“mmmmmh hata sijakuona”
“tatizo una mawazo sana nambie nini shida “
Olesta alimtazama kelvin na kusema
kwa userious mkubwa ” Tatzo ni wewe kelvin “
“mimi tena ??? kwani nmefanyaje olesta “
“Unatembea na moyo wangu unajua, nakupenda lakini unajifanyisha kama huelewi chochote kelvin I love you “
Kelvin aliishiwa nguvu maana hajuwi hata amjibu vipi maaana anachanganyikiwa ……
“Najua unanipenda sana Olesta na sidhani kwa namna ulivyo mremmbo atatokea mwanaume akatae kuwa na wewe…..Nashukuru sana kwa
kuniweka wazi kuhusu hisia zako tatizo
…
Alidakia Olesta tatizo nni sasa hivi hunionei huruma kelvin nateseka yaani wewe unanikondesha sana lakini hata hujali nambie tatizo sasa
…..
“Tatzo hata nikikwambia hilo tatizo nitakuwa nimekuongezea tatizo naomba ujuwe tu kuwa kwa sasa sitaki kumumiza mtu naona bora hata niwe peke yangu kisha kelvin akaondoka . Olesta alikazana kuita lakini kelvin hakugeuka alijuwa
anamuumiza lakini aliona hii ndo njia
sahihi ya kufanya ……
***”*********
Yalipotimia majira ya saa mbili usiku maeneo kwenye mgahawa wa kawaida tu . tunamuona mariamu akiwa kaketi anamsubiri mtu. Baada ya muda
alifika Gabriel rafiki yake kelvin kapendeza kaazima viwalo na vimemtoa chichaaaaaa yaaani kapendeza ….
Mariamu alimpa maua yake na Gabriel alikuja na swaga za kizungu “samahani kwa kukukalisha “.”okay usijali ni
kawaida wote tunatingwa na
majukumu basi shukuru uko hapa ….
Basi waliongea lakini kimya kizito kililindimaa ndani humo Gabriel akimtazama Mariamu moyoni akasema “leo nitamwambia nampenda sitaficha … akakunja na ngumi .. ujuwe kumtongoza mwanamke kuna hitaji ujasiri na kujaribu ….
Alisem kwa sauti ya kujiamini “mariamu mama “.
“NAKUPENDA SANA huku akamkazia macho mariam je mariam atakubali au atakataaa???
EPISODE 12
Mariamu hakumjibu kitu kelvin alibaki akimtazama tu maana kama jambo alilosema limemshtua kabisa alibaki akitahamaki tu huku akiichezea mikono yako muda huo moyo wa Gabriel unaenda mbio akichukulia kwamba ndo kafunguka kuhusu hisia zake kwa Mariamu kwenye moyo wake tayari kamtanguliza mtu ….
Alijibu “nashukuru kwa upendo wako Gabriel na nami nilitamani sana
ningekuwa na wewe tatzo tayari nipo
kwenye mapenzi na mtu na nampenda sio siri samahani kwa hilo”
Gabriel alienda kushuka verse lakini wapi jibu analopewa ni kuwa vyumba vimejaa kabisa hakuna nafasi ya mwanaume mwingine .
Lakini naye ana wasiwasi hajuwi kama kweli kelvin atakuwa anampenda maana hajawahi kusema na hawajawahi kuambiana …
Gabriel aliondoka zake kwa hasira maeneo hayo ya Mgahawa na Mariamu hakusema kitu maana alijuwa kamdis
appoint sana Gabriel . Lakini Gabriel
kipindi anainuka kwa hasira na kutoka mlangoni aliweza kupamiana na Tinna
,Rafiki yake Issabela wale wafanyakazi kwenye cafteria ya Hospitali ..
“oooooh samahani dada sikuweza kutazama mbele”alisema Gabriel
“usijali ndo maisha kaka ” alijibu Tinna mwisho Gabriel akaondoka zake
Majira ya saa tatu Isabella alikuwa anarejea nyumbani baada ya kazi nzito licha ya kazi pia mwanaume
anayempenda yupo ana hangaika na
malaya sugu wa mtaaa LUCY yaaani ni shida sana alikuwa na mawazo sana
Hali iliyomfanya ashindwe kabisa kufocus na kutazama mbele . Kulikuwa na pikipiki inakuja kwa kasi sana na dereva alikuwa kaonekana amepiga maji yaani kalewa
Hakuna asiyezijua tabia zake anaitwa Sudi anatembeza pikipiki kama katumwa Isabella anakuja kutahamaki pikipiki ipo karibu baada ya mwanga kummulika machoni akajua tayari ashagongwa lakini alivutwa mkono
kwa haraka na kujikuta kichwa chake
kinatua kifuani kwa mwanaume ambaye sura yake hatukuweza kuona alikuwa anahema sana Isabella ..
Yule jamaa alimtoa na kumwambia kwa hasira hivi wewe unatembeaje barabarani kama uko uwani ??
Unataka uvunjwe miguu au ? Mbona hujionei huruma wew?? alisema yule mwanaume kwa hasira lakini Isabella kuja kutazama sura alikuwa ni Samweli
. Alitahamaki na kumtazama yaani jamaa analalamika lakini binti anahisi anabembelezwa anampenda sana Samweli tena sana ..
Samweli mpaka alipomtikisa ndo akashtuka kutoka kwenye mawazo mazito mawazo magumu
“samahani samweli sijafanya makusudi nilikuwa nimechoka sana
,am very sorry” alionyesha kujutia uzembe . Samweli alimuelewa na kumwambia “hakuna shida ,unaelekea wapi ??
“naenda nyumbani”
“twende nikupeleke”Moyo wake ulidunda ghafla yaani anasindikizwa na mtu anayempenda ….
Basi walikuwa wakipiga stori za hapa
na pale Isabela alijikuta anafuraha sana anapokua na mtaalamu wa mambo. Lakini kwenye moja ya kona kuna mtu alipita na baiskeli nusura amgonge binti lakini Samweli alimvuta wakajikuta wanaanguka wote mpaka kwenye nyasi isabelaa juu ya kifua cha samweli .
Isabella akajikuta anayasika mapigo ya samweli moja kwa moja na mwishowe macho yao yakawa yanatazama kila mtu anamtazama mwenzake jamani mapenzi kikohozi hayafichiki …
Walipoangukia ilikuwa karibu na
bustani ya mzee mmoja aliitwa KIKOTI
. naye anatoka nje anakuta watu wamelala kwenye bustani alisema kwa hasira ” shenzi kabisa kwahiyo
bustani yangu ndo sehemu ya mapenzi yenu umalaya tu mme kosa gest muda huo isabela na samwel wanatoka mbiambio walikuwa wakikimbia huku wakicheka ilikuwa bonge la moment…..
Mpaka walipofika karibu na nyumbani kwa isabela anapokaa isabella hapakuwa pazuri sana hata umeme haupo jambo lililomuumiza sana Samweli hajaelewa kwanini anaumia
juu ya yule mwanamke na kwann
kafurahia sana siku hii ya leo . Basi waliongea mwishowe aliondoka samweli lakini kila mtu akimtazama mwenzie huku akimwambia kimoyomoyo”baki na mimi????” lakini ndo mapenzi yalivyo…
Upande wa mariamu anakatisha katisha mtaani kuelekea nyumbani mara ghafla anahisi kuna mtu anamfuata kwa nyuma anageuka hayupo ikavidi aendelee kutembea haraka huku mapigo ya moyo yanaenda kasi sana … “mungu wangu shida za kutembea usiku ndo hizi yaani
naweza kuchinjwa leo ” muda huo ana
harakisha kwenda nyumbani kwake
Lakini ghafla alivutwa na mtu asiyemjua na kumbana kwenye chemba na kumuwekea kidole mdomoni “shhhhhhh”
Kuja kumtazama ni kelvin.
Mariamu alichofanya ni kumkumbatia mpaka yule mtu aliyekuwa akimfuatilia akapita bila hata kumuona mtu yoyote yule akasema”ningemkamata na ule uzuri ningempelekea moto kabla sijamuibia ..” kisha akasepa alimkumbatia kelvin na kumwambia “
kwanza asante pia nimekumiss na leo
sitoficha chochote kama utanikataa nikatae tu”
“unamaanisha nini mariamu,maana na mimi natamani nikwambie kitun ambacho nimechoka kuficha …
” Basi niruhusu mimi nianze kusema ” ” okay sema nakusikiliza “
Mariamu alimshika shingo kelvin na kuanza kumpa romance na kelvin akalipoa mmmmmmmmh mwaaaa…..
Kila mtu anamwangalia mwenzake nakupenda mariamu nakupenda kelvin na tukio hilo Gabriel analiona hilo tukio….
Unadhani nini kitatokea Gabriel atafanya ninina vipi kuhusu ukaribu uliopo kati ya Samweli na isabela usikose sehemu inayofuata ….