SEHEMU YA 7
Tunaanzia pale pale alipokunja shuka kwa hasira huku akionyeshwa kukunja shuka kwa hasira zaidi. Na kulitaja jina la mwanaume ambaye mpaka sasa
hatujuwi mwanaume huyo ni nani? Na
nini alifanya mpaka achukiwe kiasi hicho
☆⋅━━━━━━━━━━━━━━━━
━━━━━━━━☆
Sehemu ya saba inaanza Baada ya kurejea nyumbani kwa kuwa ilikuwa siku ya mapumziko wazazi wangu walitoka kutembea tembea . Basi mara ghafla nilipigiwa simu na jamaa yangu moja anafanya kazi kwenye zahanati ya kijiji.
Nilipokea akanambya pale kwenye zahanati wanahitaji mtu wa kukaa mapokezi na yeye kwa kuwa ananijuwa ndo kaniona nafaa..
Hivyo ilibidi niharakishe na kwenda
kwenye ile zahanati haraka haraka
.nilikimbia kwa kuwa nilikuwa natafuta cha kufanya walau hata nyumbani maisha yawe mazuri kiasi .walau tuwe tunabadilisha mboga sio kila siku majani ya maboga kama sio maharage tembele.
Nilitembea haraka huku nikitoka jasho . Lakini nililutana na Benson mtoto aliyenipenda sana kutokana na namna navyo mjali . Bila kujua mima na mama yake ni marafiki sana .
” Uncle shikamoo”
” Oooh marhaba benson mama hajambo”
“Mzma anakusalimia kasem siku
ukamtembelee “
” Haya nitakuja mtoto mzuri kuna sehemu naenda “
.” Byee unclee byee”
Basi niriharakisha hadi kwenye zahanati ya kijiji nikakutana na rafiki yangu akaniambiya nasubiliwa ofisini . Nilihema kidogo nikajua wataanza kuniuliza maswali mengi
” Karibu sana Goodluck” “Asante sana baba pole na kazi” ” Tumepoa kijana karibu sana “
” Rafiki yako ametupa taarifa zako zote,hivyo sina haja ya kukihoji vitu
jiandae kesho unatakiwa uanze kazi .
Muda wa kurepoti saa kumi na mbili asubuhi na muda wa kuondoka saa kumi na moja jioni ,,”
” Asante kwa ukalimu wako na vipi kuhusu malipo” niliuliza kwa sauti ya upole, ya kujiamini na unyenyekevu .
” Ooooh tutakupa laki moja tu je upo tayari”
” Sawa mi niko tayari kabisa “
” Okay karibu sana mazingira yetu kama unavyoyaona . Rafiki yake Colince atakuzungusha na kukuonyesha maeneo yote.
Basi nilifurahi sio siri toka nimezaliwa leo
ndo nimepata kazi ambayo nachoingiza naamini kitawasaidia wazazi hata kama ni kidogo . Kwa sababu naamini 100 inaanza na 1.Nilimshukuru sana rafiki yangu Colince
” Kaka “
” Nambie kaka ‘
” Nashukuru sana umeonyesha maana ya urafiki”
“Usijali tunaishi kwa kutegemeana’
” Okay naomba niwahi nyumbani kaka tutaongea maana baba na mama hata hawajuwi haya”
” Haya kaka tutakuwa wote hapa “
“Okay kwa heri Colince nikaondoka na
kurudi nyumbani.
Lakini Nyumbani kwa kina Maria .alikuwa kakaa chini anasukwa na mama mmoja huku wakipiga soga ..
” Shoga kweli mwaka mzma” ” Mwaka mzima umefanyaje”
“Umekosa hata bwana na uzuri huo”
” Mmmh ! Uzuri gani wakati wanaume hawataki ma single mama”
,”aah! Sio kweli bwana we hujaamua tu ” ” Hapana kwa sasa siko tayari”
” Enhew tena nimekumbuka” ” Kukumbuka iyo vipi shoga “
“Leo nimekuona na yule kijana
aliyemaliza chuo”
” Mmmh Goodluck au ?”
” Swadakta ndo huyohuyo ” ” Enhe! unataka kusemaje “
“ukitoka na yule kijana utakuwa mbali mbali sana “
“mmh hakuna kitu kama hicho yule ni best tu”
” Haya bhana mbona hata moses ilikuwa hivo hivo ulisema ni rafiki tu mwisho Benson na mwisho akakubwaga na kukuacha single mama”
” Unavotaja jina lake mpaka kichefu chefu hebu tuyaache hayo . Endelea kunisuka
shoga yangu mapenzi sio tiketi ya kwenda
mbinguni”
“Alooooo ooooooh” alisema Shoga yake Maria kwa jina la Vivian
Nilifika nyumbani na kumkuta baba na mama wanazungumza niliwambia yaliyojiri walifurahi sana na kuona kwamba kidogo sasa kama nimeaanza kupata vikazi vidogo vidogo kazi kubwa inakuja walifurahi sana
Muda huo baba akanambiya kuna maziwa mgando yapo hapo kwenye jagi natakiwa niyanywe .nilikaa na kuanza kuyanywa
huku baba na mama wakionesh furaha .
Kila nikiwa watazama napandwa na hasira na machozi yananitoka .
Sababu ni kwamba nachukia kuwa nimesoma lakini mpaka sasa sijawasaidia wazazi wangu na wao wamejitoa sadaja mpaka nimemaliza but still bado nawategemea wao sio.siri suala hili kinaniumiza sana . Nilianza kutokwa na machozi nikawa nayafuta taratibu …
Baba alishangaa na kuniuliza ” unalilia nini mwanangu mbona sikuelew?i”
Mama naye ” mwanangu usilie bhana
kuwa jasiri basi unaniogopesha shida nini?
” Baba na mama nakumbuka mmenisomesha sana, mmeshindwa kufanya yenu mmelala na njaa muda mwingine ili nisome ,mmeteseka ili nisome but still nawategemea mpaka sasa japo nimemaliza elimu mliyotaka nimalize.
” Mwanangu Goodluck mimi ni baba yako hata ukiwa na ndege mi nane lazima unitegemee mimi ni baba yako faraja yako ni yangu na uwepo wako mimi na mama
yako tunaufurahia sana .tunaamini
utafanikiwa kwa uwezo wa mungu”
Hapo kidogo kwa hayo maneno moyo wangu ulipowa ndipo nikanywa maziwa na kuingia chumbani kwangu.
Nilipoushika mkono wangu nikakumbuka namna tulivyoshikana na maria …
” Maria leo nimelipata jibu la swali ambalo nilijiuliza sana ni lini nitapata jibu,”
Nilitembea mpaka kwenye kioo changu kikubwa nikawa najitazama na kusema
” Nimegundua kuwa nakupenda Maria ….
WE UNADHANI ITAKUWAJE SASA
SEHEMU YA 8
Tunaanzia pale pale nilipokuwa najitazama kwenye kioo changu kikubwa nkiwa chumbani. Nlikuwa bado na nguo nlizozivaa kwenda zahanati, lakini akili yangu haikuwa pale ilikuwa kwa Maria.
Niiinama kidogo, nikaweka mkono kifuani na kusema kwa sauti ya chini,
“Nimegundua kuwa nakupenda Maria… lakini je, utanielewa? Na kama utanielewa, utanipokea au utaniona kama wanaume wengine waliokuumiza au uliowahi kuwa nao?”
Nilifikilia sana mpaka nikafikia kugundua
kuwa nina hisia na maria bila hata kumjua kiundani zaidi. Nilisogea mbele tena nikisema kwa ujasiri mkubwa…
“Siku moja nitakuambia Maria, si kwa maneno ya mdomo tu, bali kwa matendo. Siku hiyo haitakuwa mbali. Nitakufanya uamini katika upendo.i.”
Nilitoka nje na kuingia jikoni nikafungua chungu na kuchota maji na kunywa kisha kurudi chumbani kwangu .Basi na usiku ulikuwa ushaingia ni muda wa kulala sasa
Kwa kuwa kesho ni siku yangu ya kwanza kwenye zahanati ….
LAKINI
Maria akiwa chumbani kwake , alikuwa anamtazama sana mwanaye aliyekuwa tayari amepitiwa na usingizi.
” Hivi wewe mosea ulipata wapi ujasiri wa kunikataa mimi na mwanangu ili hali unajua sisi ni familia yako na Benson ni mwanao”
ANATUKUMBUSHA !!!!!!
MAria na Benson walikuwa ni wapenzi na walikuwa wanapendana sio siri na hakuna hajuwi jinsi wanavyopendana. Na kila mwanakijiji marafiki wa karibu wa Maria walijua ndoa hii hapa .
Maisha yalizidi kuwa mazuri na walikuwa wanaishi pamoja. Na zao la tendo ni mimba hivyo Maria alipata ujauzito.
Lakini kipindi Moses hana chochote na hata hakujipanga . Baada ya Maria kumwambia kuwa ana mimba yake .
Huwezi amini Moses alimwambia hayupo tayari kulea . Na kwamba sio jukumu lake na kapata mchumba mwenye hela mjini hivyo kila mtu ajitafute
” Moses una uhakika na unachosema”
” Yaani sitaki kusikia kwanza mi na wewe hatujawah lala pamoja’
” Muogope Mungu we mwanaume! Si
ulikuwa mpaka unasimamia”
” Haha! We mwanamke unaota sio siri”
” Mimi nilifanya na wewe ? Lini saa ngapi? Kwa lengo gani ? Na kwa nn?
“
Huku Maria machozi yakimtoka haamini anachoambiwa na Moses
” Moses huyu ni mtoto wako jamani” ” Mtoto gan? Au umechanganyikiwa” ” Si ulisema unanipenda moses?
” Mmmj labda pacha wangu sio mimi” “Jamani hayo ndo malipo ya upendo?”
” Hilo halinihusu mimi ni wewe na moyo wako”
Mara ghafla simu yake ikaita aliitazama na kusema ooh! Kumbe mahabuba kapiga tena anasema mbele ya Maria
.aliipokea na kuongea kwa sauti kubwa ili tu maria asikie
” honey “
” Yes honey , uko wapi”
” Niko home vipi unaendeleaje?” ” Mi mzma hofu yangu kwako”
” Uzima wangu ni uzima wako Irene”.Moses anajibebisha mbele ya Maria
Maria alikuwa akitokwa machozi,haamini maneno anayoyasikia kutoka kwa
mwanaume anayempenda. Basi baada ya
Moses kumaliza yale mazungumzo waliahidi kukutana ili wayafanye mamboziii ya kikubwa .
Lile suala lilimuumiza sana Maria aliondoka analia. Na baadaye mama yake aligundua kuwa mwanaye ni mjamzito. Alihangaika sana mpaka siku anajifungua na siku hiyo ya kujifungua ndipo alipokufa mama yake .
Ilikuwa ni pigo sana kwake sio hivyo tu pia miezi michache baadaye kaka zake na wajomba zake pamoja na ndugu wengine walimpora kila kitu ndo mpaka sasa
anaishia nyumba ya kupanga na kuteseka
namna hii
Xxxxxxxxmwisho wa kumbukumbuXxxxxx
Basi alikuwa akilia baada ya kuyakumbuka yote mpaka usingizi ukamchukua. Na alilala bila hata kutarajia bil hata kujifunika lakini mwanaye Benson kuna muda aliamka na kumfunika mama yake akarudi tena kulala.
Siku iliyofuata niliamka mapema na kujihimu kuelekea katika zahanati ya kijiji.kwa ajili ya kuianza kazi rasmi .
Nilifanya kazi zangu zote mapema na
kujiandaa kuelekea kazini .lakinj akilini
mwangu naamini siku nitakayokutana na Maria nitamwambia kuhusu hisia zangu…
Nilifika kwenye zahanati ya kijiji nikakutana na rafiki yangu Colince alikuw alinisubiri ili anipe jografia ya eneo lote la zahanati hiyo…
“Karibu sana kaka. Leo ndo siku,” alisema Colince kwa furaha.
Nilitabasamu na kusema “Nashukuru kaka. Mungu mwema wacha tulinge “
Tulizunguka pamoja kila chumba.
Nlionyeshwa mapokezi, ofisi ya wauguzi, chumba cha dharura na hata duka dogo la dawa. Baada ya maelezo, nililikaa mapokezi rasmi kama mhudumu wa kwanza wa siku hiyo.
Ugeni wa siku ya kwanza ulinitesa na hata pia uzoefu vyote ni changamotp kwa myu yoyote ambaye hajazoea kazi. Na niliamini nitafanya vizuri na nitatimiza malengo yangu.
Kazi iliendelea mpaka ilipofika saa 10 jioni ambapo alikuja mwenzangu na mimi nikaambiwa nikapumzike kwanza lakini
ule muda nataka kuondoka Colince
aliniita
‘ oya Goodluck”
Nilisimama na kugeuka kumsililiza ila mkononi alishika 10000
” Kaka chukua hii basi’
” Mmh kaka asante sana, umekuwa mwema sana kwangu sijuw nitakulipa lini,”
” Hapana mi sihitaji malipo ila nachohitaji tubadilishe maisha yetu “
” Asante sana kaka mpaka naona aibu”
” Hahah ila Goodluck bwana we nenda nyumbani”
Nilitembea nikiwa naelekea nyumbani
nimechoka sana si unajuwa siku ya kwanza kazini mambo yanavyokuwa.
Nilipitia kwa mangi ….
” Mangi habari yako kaka” ” Aisee salama ndugu”
” Naomba soda tatu milinda nyeusi zote” ” Hakuna wasiwasi, saizi uko wapi?”
” Aaah! Nipo nasaidia saidia kazi kwenye zahanati ya kijiji”
” Aisee ndo hatua ya maisha”
” Mwenyewe naona ndugu MUNGU NI MWEMA “.
Nilimalizana na mangi muda huo huo
baada ya mimi kuondoka Maria naye alienda dukani kwa mangi ..
” Mangi nikopeshe mchele ,hela leo sina” ” Eeh nawewe unakopa yaani “
” Nitafanyaje mangi nisaidie nitakulipa” ” Sawa unataka kiasi gani?
” Nusu tu mangi si unajua nakula na mwanangu tu”
” Oooh benson ?”
” Ndiyo huyo huyo .huku anapokea mchele
” Uwahi kurudisha hela zangu nadhani unanijua?
” Mmmh mangi na wewe tena utanijazia
nzi”
” Hahah sikawii kamuulize mama Leila hata nisahau”
” Haya kwa heri Mangi nataka nikachote maji..”
Aliondok Maria pale dukani kwa mangi na kuelekea nyumbani alipofika nyumban aliweka mchele na kuchukua kata na ndoo kuelekea mtoni.
Upande wangu baada ya kufika nyumbani niligundua maji ya kuoga hayapo nilivaa hovyo na kuchukia ndoo kuelekea mtoni.
Akilini namuwaza Maria . Maana
sijamuona siku nzima ….
Nisijue kumbe naye anakuja mtoni patamu hapo usikose sehemu ya 9
SEHEMU YA 9
tunaanzia pale pale ulipoishia, Goodluck akiwa njiani kwenda mtoni kuchota maji, huku Maria naye akiwa anaelekea huko huko.)
Siku hiyo ilikuwa kimya sana, upepo mwanana ukipuliza taratibu ukichanganyika na harufu ya majani
mabichi na maji safi ya mto. Nilipofika
mtoni, nikaiweka ndoo chini kando ya jiwe kubwa lililokuwa pembezoni mwa maji, nikapiga magoti na kuanza kuchota maji.
Mara nikasikia sauti ya miguu nyuma yangu, ilikuwa ya haraka kidogo, lakini ya mtu mwepesi. Niligeuka taratibu…
Alikuwa ni Maria.
Moyo wangu ulishtuka sio mchezo,sijuwi ni furaha sijuwi ni hofu lakini nilijikuta nikitetemeka ni tu baada ya kumuona mwanamke nayempenda. Na niliapa
lazima nimwambie kuhusu hisia zangu
kwake.
Nilimtazama taratibu nikiinuka na kuacha kikombe cha kuchotea maji chini.
Mikono yake ilishika kata upande mmoja na ndoo mkononi. Alikuwa na kanga iliyomfunika vizuri juu kavaa tshirt nyeusi.
Naye alikuwa akinitazama na kusogea mwisho tukakutana macho yetu yalitazamana huku kila mmoja akionekana anashauku na mwenzake
.Maria aliangusha mpaka kata yake chini ” maria “
” Goodluck “
” umeshindaje leo”
” salama sijuwi wewe”
” nimeshinda salama maria sema na uchovu tu”
” mmmmh uchovu gan?”
” Nilikuwa zahanati si unajua ,nimepata kazi pale mapokezi”
Alinishika mkono nilisisimka sio siri ujuwe nampenda huyu mwanamke srma nashindwa kumwambia
Akasema” hongeara Goodluck na hayo ndo maisha “
” Asante sana Maria “
Wote tuliinama na kukishika kikombe
badala ya kukishika kikombe tukashikana mikono na kila mtu akamtazama mwenzie aisee ilikuwa ni moment tamu balaa ambayo ilifanya hata mazingira ya mtoni kuwa yanavutia sana .
Pembeni na katikati yetu walikuwa wanapita vipepeo na wadudu wadogo wadogo tulizidi kutazamana mwishowe kila mtu alijikuta akitabasamu . Lakini baadaye kwa aibu nilimsaidia kuchota maji
Mwishowe tukawa tukaondoka wote na kupandisha tukipiga stori
mbalimbali.Hadithi zilikuwa nyingi lakini
bado nilitamani kumwambia kuwa nampenda sema nashindwa kumwambia jamani .
Lakini kuna ujasiri ulinijia moyoni mwangu nakusema ” mwambie akikukataa au akikubali basi usikubali kuteseka Goodluck .Wewe ni mwanaume na mwanaume lazima uwe na moyo wa kiume”
“Maria…” nilimwita kwa sauti ya chini, isiyo na kiburi wala haraka.
“Ningefanya hata kazi ya kulima, kama
ingekuwa ni kwa ajili yako…” nilijikuta nikisema bila kufikiria sana.
Maria akavuta pumzi, akaniangalia. Uso wake ulionyesha mshangao. “Una maana gani?”
“Namaanisha… Maria, kila nikikuona, najisikia tofauti. Sijui ni mapenzi au kitu gani, lakini najua kuna kitu ndani yangu kinapiga kelele kunituma niseme…”
Alinitazama kwa makini bila hata kusema kitu chochote kile .
Niliendelea, kwa sauti ya utulivu,
“Samahani kama nimekosea. Sikupaswa kusema hivyo. Ila… sitaki kuficha tena.”
Maria alinyanyuka,alinigeukia na kunitazama kwa jicho la kina, halafu akasema taratibu, “Watu wanaposema maneno mazuri, mara nyingi huwa si kwa sababu ya moyo… ila kwa sababu ya tamaa au huruma.”
“Sio huruma,” nilimjibu, “Na si tamaa. Sijawahi kumtamani mwanamke kwa namna hiyo upo moyoni Maria. Natamani kukuona ukitabasamu , ukiheshimika, na ukifurahia maisha yako.”
Kimya kilitawala kwa sekunde kadhaa.
Kisha Maria alisema, “Tafadhali , naomba usinitazame sana. Kuna watu hukosea maana ya macho kama yako. Sihitaji kupendwa na sihitaji mwanaume kwa sababu maisha yangu ni yangu tu.
Nilipata maumivu makali baada ya kusikia yale maneno kinywani mwake. “Sawa, nitatembea upande mwingine wa barabara… lakini moyo wangu bado utakuwa karibu na wewe.”
Hatukuzungumza tena. Tulitembea
kimya, lakini kwa mara ya kwanza, hakukuwa na ukakasi. Ukimya ulikuwa wa utulivu Nilikuwa nikimtazama lakini alionekana kukasirika sana .
Huwezi amini sikuongea naye alikuwa kakasirika sana. Mwishowe njia panda kila mtu alienda kwake . Nikiwa naelekea nyumbani mawazo yamejaa kichwa kizima
‘” bora nisingemwambia ona sasa nimemkera ona sasa nimemuudhi
sababu ya hisia tunaweza tukapoteza kila kitu “
Nilifika nyumbani nikiwa na mawazo
niliingia kuoga . Na baad ya hapo nililala kidogo na nilikuja kuamka saa kumi na mbili jioni.Na muda huo niliamka nikiwa bado na mawazo sana .
Niliondoka na safari ilikuwa kwa rafiki yangu Colince tulikuwa tunaenda kuangalia mechi kati ya LIVERPOOL VS MANCHESTER UNITED. Colince ni shabiki mkubwa sana wa Manchester united toka tupo wadogo lakini mimj ni Liverpool .
nilipitia kwa mangi lengo nikunywa angalau ata mirinda ya baridi kabla sijaenda kupigizana kelele na Colince .
” mangi naomba mirinda nyeusi”
” yachupa ya kopo”
” naomba ya kopo ya baridi”
” haya sawa chukua hii hapa”
Ile naifungua tu nikasikia sauti ” mjomba” Alikuwa ni Benson mtoto wa Maria .
Tambua mpaka leo sijatambua kuwa
Benson ni mtoto wa Maria . Nilimkumbatia yule mtoto na damu zetu zilikuwa zinaendana .
Lakni nikiwa nimemkumbatia Benson hatua za mwanamke zilisikika na akawa kasimama mbele yangu ile nainuka tu
Nilishangaa kwa kile nilichikiona ………
INAENDELEA …………