SEHEMU YA NNE
Turaendelea palepale amapo maria alikuwa amesema ” ananishikaje kiuno kama sio ukorofi”
Alisem hivo kisha akaamka na kwenda kumfunia mtoto wake si unajua mbu.Asije akaumwa halafu hela zenyewe ni ngumu
….biashara haziendi sana
Lakini alipokuwa anaondoka baada ya
kumfunika mwanae machozi yalikuwa yanamtoka . Unajua mpaka sasa hatujuwi baba wa mtoto yuko wapi lakini inaonyesha kuna jambo zito . Chozi la
mtu mzima liheshimiwe.
Akawa anaondoka akasikia sauti kutoka kwa mwanaye ” Mama Nakupenda sana kuliko kitu chochote dunia”
“Nakupenda pia mwanangu”
” usinilie utanifanya na mimi nilie”
“sawa mwanangu ngoja niende uwani nakuja”
” sawa mama uwahi naogopa peke yangu”
Mama aliufungua mlango lakini hakuwa
hata anaenda hata uwani alijibanza nje ya mlango na kulia kwa uchungu hadi
kukaa chini.lengo ni kutokutaka kumfanya mwanae aone licha ya futmraha yao
,moyoni mwa mama kuna makubwa .
Mwishowe aliingia ndani
kisha aliponyamaza, alirudi ndani hakusema kitu zaidi ya kulala usingizi mzito kachoka na maisha maria.
Kwa uande wangu , nilijihisi mimo ndiye niliyekuwa nampenda na kumuwaza Maria kuliko hata yeye alivyokuwa akinifikiria. Mawazo yalinizidi kiasi cha
kwamba nilijikuta napitiwa na usingizi
nikiwa nimelala kitandani huku mikono yangu ikiwa imeegemezwa kichwani.
Lakini licha ya usingizi huo mzito, nilikuwa nimejiwekea ahadi:
“kesho nitawahi mtoni, hata kama ni kumuona tu, Maria lazima nimuone”.
Asubuhi ilipofika, nilishtuka usingizini ghafla kabla hata ya jogoo kuwika.ilikuwa kama saa kumi na moja inaelekea saa kumi na mbili hivi niliwasha zile taa maarufu kama SOLATA.
Akiili mwangu au hata malengo yangu
nikuwajengea wazazi wangu nyumba nzuri na kuweka umeme . Ni lazima wazazi wangu waishi vizuri na hii ni ndoto yangu .Niliamka kisha ……
Nikafanya kazi zote za nyumbani kwa haraka nikafagia sebule, jikoni, kisha nikachukua ndoo yangu ya maji na kuelekea mtoni kwa matumaini ya kumuona Maria .
Akilini mwangu niliamini leo lazima nimuone Maria. Nilimweleze jinsi nilivyommis sana . Lakini akilini mwangu yaani sielewi hui ni ugonjwa gani wa
kumuwaza mtu hivi …nikitembea mpaka
kisimani
Nilipofika mtoni, sikumuona. Moyo ulipoa ghafla niiishiwa nguvu Nikajisemea:
“Kwanini hajaja leo? Shida ni nini tena Maria au alichota toka jana?”haya ndo maswali niliyokuwa najiuliza mimi mwenyewe hakika sikuwa na furaha hata kidogo
Nikaanza kulalamika kimoyomoyo, maneno yangu yakitoka bila kupanga:
“Au nimemkosea? Au anaumwa? Mbona leo kimya kabisa?”
” yaani haiwezekani ,atakuwa ananifanyia
makusudi huyu mdada toka nianze kumuwaza ndo simuoni hata kidogo ” huku nikiweka maji niliyochota pembeni yangu …
Wakati bado nipo katika dimbwi la mawazo, nilihisi kama mtu yupo nyuma yangu. Niligeuka kwa haraka, moyo ukidunda.Nilijuwa huenda ni yeye ndo aliyekuwa kaja kisimani . lakini kumbe alikuwa Mama Devotha, jirani yetu.
Nikavuta pumzi, niliumia kimoyomoyo sio siri….unamsubiri mtu anakuja mwingine
” shikamoo mama devotha”
” marhaba Goodluck , umeamkaje”
” nimeamka salama kabisa .Vipi wewe?
” niko salama Mungu ni mwema’ ” Ngoja nikuchote mama”
” aaah – sante mwanangu nashukuru”
Nilimchotea maji lakini akili yangu ni
kuwa yuko wapi maria ? Na kwanini hajaja kisimani? Au katingwa sana ?.Nilijiuliza maswali mwisho nikapata jawabu la kuchota maji mara nne niki.kosa zote nitajuwa leo hajaja kisimani…
Nilichota maji mara nne lakini Maria hakuja. Nilirudi nyumbani na kumwagilia bustani yangu huku maji yakinilowesha nguo nilizovaa. Ilinibidi baada ya kumaliza
kumwagilia nilibadilisha na kuvaa pensi
nyeusi niliyonunua mjini na kitishet cheupe.
Nikajiangalia kwenye kioo nikachana nywele zangu angalau kidogo niwe nakamvuto japo maisha magumu nijivunie na nilichonacho .Kisha nikaamua kwenda kwa Mangi kuchukua mkate baada ya kuwa tayari nilishapika chai.
Nilimkuta Mangi mchangamfu kama kawaida, tukasalimiana kidogo.
” habari za asubuhi mangi” ” salam karibu sana “
“naomba mkate mmoja wa 1500”
” Haina shida akanipa nikamlipa hela na kuondoka”
Nilipoondoka dukani, njiani nikakutana na mtoto yule ambaye nilimfundisha ile siku na kumpa Pipi pamoja na biscuti.Ambaye dhairi shaili ni mtoto wa Maria lakini mpaka sasa bado sijalitambua hilo
Benson alionekana hana furaha sana.Ilibidi nimsimamishe maana hata hakuniona kama angeniona angeniita hata jina ” uncle ,uncle “
nilimwita” we sukari viwili na viberiti
robo,mbona unapita bila hata kunisalimia?”. Aligeuka haraka na kusema Uncle alinikumbuka, akanisalimia kwa adabu.
” Uncle shikamoo “
“marhaba unaendeleaje”. Alianza kulia baada ya kumuuliza swali hilo,hiyo ilinipa wasiwas”
” shida nini mtoto mbona unalia?”
“Nashida, mama anaumwa sana na hatuna hela ya dawa,” alisema kwa sauti ya huzuni.
Nikamwuliza kwa upole, “Mama anaumwa nini?”
“Anasumbuliwa na kichwa sana.”
Nilimwonea huruma sanana kusema “kama mtoto kama huyu analia yaosha mam ana hali mbaya” .
Nilimnyamazisha Na nikamshika mkono na kumpeleka hadi kwenye duka la dawa. Nikamnunulia dawa tatu pamoja na ya kutuliza maumivu ya kichwa.Yule mhudumu wa maabara akampa dawa na kuandika maelekezo
Na baadaye akatukabidhi dawa nikalipa haraka haraka huku nikiinama na kutoa
kitambaa kisha nikamfuta mtoto machozi
na Nikamwambia, “Nenda kampe mama yako hizi, atapona tu. Mwambie ni zawadi ya upendo na matumaini.”
Mtoto yule alitabasamu, akasema “Asante sana uncle!”
” unaitwa nani we mtoto?” ” Benson “
” haya nenda nyumbani benson nenda haraka kampe dawa” huku nikimshika usoni na kumuonea huruma sana
kisha akaondoka kwa furaha. Nilikuwa namsindikiza kwa macho mpaka
alivyopotelea kwenye kichochoro kimoja
hivi..
Nilitembea taratibu moyoni nikiwa nimejaa huruma na mapenzi ambayo sijawahi kuhisi hapo kabla. Sikujua kama mama yake ni Maria
Mtoto alipofika nyumbani, alimkuta mama yake kalala, akamwamsha kwa upole.
“Mama nimekutana na yule uncle, kaninunulia dawa kasema utapona tu ukitumia vizuri.”
Maria alishtuka, akajiuliza kimoyomoyo:
“Uncle gani huyo? Kwa nini ana moyo wa huruma kiasi hiki? Mbona anajali hivi bila hata kuwajua kwa undani?”
Hajui kabisa kuwa uncle huyo ni mimi, akaanza kuhisi labda huenda ni baba yake Benson ,Moses lakini alikumbuka kuwa Benson aliwakataa yeye na mtoto na alikimbilia mjini sasa. Huyo uncle ni Uncle gani .
Dont miss Sehemu inayofuata……
SEHEMU YA 5
Tunaendelea pale pale tulipoishia baada ya Maria kujiuliza sana maswali kuhusu mwanaume anayemsaidia mtoto wake ambaye kichwani mwa mwanaye anafahamika kama mjomba .
Alijiuliza sana Maria kuhusu huyo mwanaume mwenye huruma,mwenye kujali mtoto wake na mwenye kumjali yeye ingawa hata hamfahamu. Alijisemea
” MUNGU akuzishie baraka na akupe maisha marefu ,maana katika dunia hii ni ngumu mtu kumjali mtu asiyemfahamu. Natumai siku moja nitakuona kaka”
Basi asijuwe kuwa mimi ndo
ninayemsaidia mwanaye na hata dawa vyote nimefanya mimi. Huku hata akili yangu inawaza nitaona na maria lini na nilijiuliza kwa nini namsaidia sana yule mtoto? Na kwa nini sipendi awe katika shida ? .Ni maswali ambayo nilijiuliza nikiwa kitandani majira hayo ya mchana .
SIKU TATU BAADAYE……
Kama kawaida yangu niliamka mapema siku hiyo ilikuwa jumapili niliamka mapema nakufanya shughuli zangu . Na baadaye nikabeba ndoo kueleka mtoni kuchota maji. Kichwani kwangu nilifuta
mawazo kuhusu Maria nilijuwa huenda
kasafiri.
Nilishuka taratibu kwenye njia yenye migomba na kushuka mtoni nikiwa na mawazo yangu mwenyewe kuhisu maisha. Nilikuwa natazama simu yangu tu .Nikiwa nasogea taratibu karibu na kisima nilisikia mwanamke akiimba ..
” ni kwa uwezo wa Mungu ,ni kwa uwezo wa roho mtakatifu…..” Baada ya kusikia ile sauti niliacha kuchezea simu
Sauti za ndege zilikuwa zinasikika na hata chura pamoja na upepo kwa mbali kwa sababu maeneo tunayo ishia ni karibu
sana na milima . Alikuwa kanipa mgongo
tu ile anainuka na kunigeukia niliangusha mpaka ndoo chini mwili na hata mikono vyote viliishiwa nguvu….
” Mariaa!!! ” niliita kwa sauti ya mshangao na ya uoga kama siamini aliyekuwa mbele yangu kweli ni maria ?
Naye alishusha pumzi na kuniita
” Gooodluck ” Basi niliacha ndoo pale pale nikamsogelea karibu zaidi .
” Ulikuwa wapi maria?” nilimuuliza kwa sauti ya kuonyesha sijamuona kwa muda mrefu
” mbona mimi nipo Goodluck”
” mmmh uko wakati hata mtoni ulikuwa huji?”
” hapana, nilipata kashida kidogo ” ” kah shida gani tena jamani”
“We elewa kashida si unajuwa sisi ni binadamuna tumeumbiwa shida”
” Sawa ila niliku……..” nilikuwa nashindwa kumaliza aliitikia kwa mshangao
” Ulini nini ? Mbon unasita kusema ?”
” Nilikumis Maria ” Nilisema kwa kujiamini then nilimsogelea na kumkumbatia
Alishtuka sana na haki hii niliinmgundua baada ya kumkumbatia alikuwa anatetemeka na mapigo ya moyo yalikuwa yanaenda mbio sana.Akaniuliza nikiwa bado nimemkumbatia ..
” kwanini umenikumbatia? Huwezi kusema bila kunikumbatia ????”
Ndipo akili yangu ikarudi maana nilifabya
kitendo ambacho moyo ukiamua bila kuushirikisha ubongo wangu.Niliona aibu
Huku nainama chini kuokota ndoo yangu
” Am sorry Maria hata sikutarajia imetokea tu ghafla “
Alicheka ” imetokea tu ghafla ? . Mh acha uongo Mr.”
” kweli tena ujuwe nilitaka nikwambie tu lakini mwisho wa siku nimekukumbatia kabisa”.
” okay hakuna shida ! Nataka niwahi
nyumbani ili nijiandae niende kanisani”.
Alisema maria
” oooh wewe ni dhehebu lipi”nilimuuliza maria
” mimi ni mkatoliki ,wewe je ? ” hata mimi pia ni mkatotiki
” leo hauendi kanisani ??”
” Naenda ndo maana nafanya mambo yangu yote asubuhi “
” aaah apo sawa ngoja niwahi “
” Naomba niwe kampani yako leo” ” mmmmh jamani “
” mbona unaguna Maria? “
” Noo hakuna shida tukutane mbele kidogo ya duka la mangi kuna mti mkubwa nitakusubiri pale usichelewe”
” haha asante, na kwanini nichelewe? Wakati leo naongozana na Ua moja zuri “
” haya sawa mi naenda “
Basi alijitwisha ndoo mwenyewe akawa anaobdoka na mimi nilijitwisha yangu.kulikuwa na umande umande lakini nashukuru MUngu nilirudi nyumbani kwetu salama.
Nilimwagilia bustani harak haraka . Na kufanya kazi zote haraka haraka lakini kwa umakini . Kisha niliingia kuoga. Baada ya muda mfupi nilitoka bafuni na kuingia chumbani kwangu .
Nilijifuta kila sehemu nikajipaka mafuta
nikavaa vizuri kiatu kishapigwa kiwi.Vaa saa yangu yaani nilijicheki kwenye kioo nikasema ” kioo hakidanganyi sana “
Nilijipuliza pafyumu nikijisemea ” mmmmh kweli maria atanisifia hivi nilivovaa sijuwi?
Niliwambia wazazi wangu kuwa natangulia kanisani wataweza kunikuta huko .Nilitoka nikiwa natembea taratibu tu. Kila mwanmke niliyekutana naye alikuwa akigeuka kunitazama . Mpaka nikawaza nawashangaza au nawavutia?
Nilitembea nikampungia mkono mangi
alikuwa akiendelea na shughuli zake za kila siku. Nilifika hadi tulipokubaliani lakini sikuweza kumuona mtu yoyote yule
Ikabidi nicheki saa bado dakika mbili muda wa makubaliano ufike …..
” Enheee siku ya kwanza tu anataka avunje ahadi mmh! Huyu mwanamke ” lakini kabla sijaongea zaidi nilishikwa bega niligeuka taratibu kutazama nani kanishika bega
Mashalaaah nilitahamaki kwa nilichokiona mmmmh kweli mungu ni fundi sana ….
Nilibaki nimekodooa macho yangu yaani
siamini ninachokiona. Niliswma ni wewe kweli????????
Mapigo ya moyo wangu yalizidi kwenda kasi, nikajua leo ni siku isiyo ya kawaida.
SEHEMU YA 6
Niligeuka taratibu baada ya kushikwa bega, nikatumbukia kwenye dimbwi zito la mawazo . Baada ya kugeuka na mbele yangu alisimama Maria lakini hakuwa
yule Maria wa kawaida niliyekuwa
namjua.
Hakuwa Maria yule wa kuvaa kawaida
….mara vitenge mara nguo kuu kuu…kutokana na shughuli za kijiji chetu………
Aliyesimama mbele yangu ni kama malaika si usoni si kwenye ngozi yake kilikuwa ni kifaa kifaa haswa. Nilizidi kumtazama mrembo aliyevaa gauni la bluu lililompendezesha na kumfanya avutie zaidi sio siri nilidata nilizidi kumtazama …
Gauni lake lilimkaa sawasawa, unaweza
ukasema fundi alitengeneza kwa ajili yake yeye. Lilikuwa ni la mikono mifupi, na sehemu ya kifua ilishonwa kwa mpangilio wa maua madogo madogo meupe yaliyopamba kama almasi.
Nywele zake zilikuwa zimefungwa vizuri nyuma kwa utepe wa rangi hiyo hiyo ya bluu, macho yake yakiwa makubwa ya mviringo yenye rangi ya kahawia, yenye kuvutia.
Midomo yake ilikuwa imepakwa rangi ya waridi , na uso wake uking’aa kwa mafuta ya asili, ulionyesha usafi, utulivu na haiba
ya kipekee. Hadi alishindwa kuongea.
Nilimtazama tu
Siku sita nilimwambia ” Mungu naamini alitumia muda mrefu sana”
” Mmmh muda mrefu kufanya nini” ” Kukuumba wewe Maria”
” Haha!(Kwa aibu) Kwanini sasa” ” Unaniruhusu niseme ?”
” Ndiyo sema nakuruhusu” ” Wewe ni mrembo sana “
“Mmh wapiii ila wanaume waongo”
” Hakya laaahi nakwambia wewe ni mzuri” ” Jamani asante Goodluck “
” Umefanya niamini kitu kimoja”
” Haa! Kitu gani tena ?
” Kwamba malaika wapo “
” Kwani mimi nimekuaminishaje?”
” Kwa huo uzuri ulionao jamani”.Maria aliachia tabasamu ambalo lilinifanya nishindwe kuacha kumtaza
Maria alitabasamu kwa upole kuniambia,
“Mbona unanitazama sana Goodluck?”
Nikamjibu kwa sauti ya chini,
“kwa sababu unastahili kutazamwa…”
Tukagundua kuwa tunachelewa
kanisani,ilibidi tuanze kutembea mdogo mdogo kuelekea kanisani.
Kila mmoja wetu alikuwa kimya kwa dakika kadhaa, lakini si kimya cha kawaida kilikuwa kimya chenye maneno mengi moyoni.
” Kwani kwa sasa nawaza ninj kuhusu maria mbona moyo wangu sielewi toka nimemuona siku ya kwanza ” niliendelea
” Kwanini mimi namuwaza sana japo hatuna ukaribu kivile .Na mbona kama yeye hana muda na mimi” Basi akili inanirudi nipo nje ya mlango wa kanisa
Tulipofika kanisani, kila mmoja wetu alikuwa akimtazama mwenzake kwa jicho la fulani la * njoo tukae wote”. Tukikaa kwenye viti vya mbao, tulikaa karibu sana kiasi kwamba mapigo ya moyo wangu yaliweza kusikia pumzi ya mwenzake
Misa iliendelea, na kila mara macho yetu yalikutana kisha wote tukainama haraka kwa aibu. Hata wakati wa kuimba, sauti ya Maria ilikuwa inayatesa masikio yangu lakinj piz ilituliza moyo, iliyonifanya nisahau hata mstari wa wimbo.
Nilitamani muda usonge polepole, lakini kama kawaida, saa haimsikilizi mpenda.
Baada ya misa kwisha, tulitembea pamoja kurudi. Safari ya kurudi haikuwa na maneno mengi, lakini macho yalizungumza kuliko midomo.
Lakini tukiwa tunatembea niliusogeza mkono wangu karibu na wake nikaishika kwa kuunganisha na wangu tukawa tumeahikana lakini hakuna aliyeongea zaidi ya hatua tu pekee kusikika baina yetu.
Nikikuwa namtazama kwa jicho la kuibia ibia kilichonichanganya zaido ni namna mikono yake ilivyokuwa milaini sana . Na
the way tulivyokuwa tumeshikana . Sio
mimi sio yeye ila mioyo ndo iliamuru tushikane .
” Misa kwako imeendaje Goodluck “
” Mmmh kwangu imeenda vizuri sijuw kwako” nilimjibu kwa kujiamini.
” Sawa siku moja uje mpaka kwetu” ” Mmh kwenu nitakuja tu “
” Kweli???? “
” Yeah kwanini nikudanganye , sehemu nayoijuwa ni sokoni unapouzia”
” Mmmh umepajuaje wewe”
‘ kuna siku nilikuona ulikuwa unauza vitu” ” Mbona mimi sikukuona Goodluck?”
” Ungeniona vipi na ukikuwa umetingwa”
” Ooh sawa ! Si ungeniite hiyo ni tabia
mbaya”
” Tabia mbaya tena ila Maria ?” Nilimwambia huku namgeukia kumtazama.
” Ndiyo basi hukutaka tu” akaonyesha kununa
” Mmmh jamani basi nisamehe maria “
” Sitaki ,sitaki sitaki” akaniachia mkono wangu
Ikabidi nimsogelee karibu zaidi nisimpe nafasi ya kupumua tukawa tuko zero distance macho yanatazamana
” Naomba nisamehe maria “
“( Kwa aibu ) Sawa nimekusamehe lakini
umenisogela zaidi mpaka naona aibu ” “Sasa si hutaki kunisamehe”
” Nimekusamehe rudi nyuma basi “
Nilirudi nyuma huku nikichek nikimuacha na kaaibu fulani hivi akasema
” Jamani uli isogelea karibu hivi na watu wanapita unadhani wayanifikiliaje ?
” Kwa hiyo unaishi kwa kuogopa watu”
” Hapana kwanza nishafika tutaonge siky nyingine ” Aliondoka mbio mbio kwa aibu nilibaki namtazama nikakumbuka sijachukua namba yake nilimwita
” Maria ! Maria maria !” Lakini hakugeuka
niliamini nitampata tu bila shida yoyote ile .muda ni rafiki wa kila mtu
Tulitengana hapo. Nilielekea kwetu na Maria alikuwa kashaenda kwao . Lakini mambo hayakuwa tulivu kwa upande wake.
Alipofika ndani, alimkuta Benson akiwa amekaa sebuleni, na walikubaliana kuwa wataenda wote kanisani.lakini muda ulipofika Benson aliingia mitini
Maria alimsogelea na kumuuliza:
“Kwanini hujaenda kanisani mwanangu?
Mbona nilikwambia twende wote?Umeanza kiburi?
Benson akajibu kwa sauti ya hofu:
“Mama samahani… nilienda kwakina Edgar nikawa sivioni viatu vyangu nisamehe usinichape tafadhali”
Maria alikasirika. Alimwambia,
“Nimekuchoka na uzembe wako. Siku nyingine utanifanya nikose baraka!”ujuwe mtoto umleavyo ndivyo akuavyo sitaki uwe mhuni au mzembe mwanangu”
Kwa hasira maria akamwambia aende
alete kiboko. Benson alikwenda kwa hofu na kurudi na kiboko, kisha Maria akamuadhibu. Benson alianza kulia kwa uchungu, machozi yakitiririka usoni mwake, akilia:
“Mama nisamehe… sitarudia tena…”
Lakini Maria akiwa bado na hasira, alimtazama mwanawe na kusema kwa sauti ya ukali iliyojaa mchanganyiko wa uchungu na hasira:
“Hii ni kwa faida yako, usije ukaja kuishi maisha ya hovyo kama nayoishi mimi!”
Benson aliendelea kulia sana… tena
sana. Kilio kilichochoma moyo wa jirani aliyepita nje na kusimama kwa sekunde chache kusikiliza, lakini akaendelea na safari yake, kwa kuwa alijua hasira za mama si jambo la kuingiliwa kirahisi.
Hasa hasa pale mtoto anapokosea
Basi baada ya kupiga tena akaanza kumnyamazisha tena mwenyewe. Na baada ya muda akanyamaza mama alimpa 500 akale biscuit angalau apoze hasira na hapo alifanikisha kumpoza mwanaye …..
Maria iingia ndani na kuanza kulia kwa
sauti huku akilaumu na kusema ” moses wewe ndo chanzo cha sisi kuishi maisha haya nakuchukia sana na katika maisha yangu wewe ni adui yangu mkubwa
NAKUCHUKIA MOSES HUKU AKIKUNJA SHUKA ALILOTANDIKA KITANDANI …