EPISODE 13
Nilipofika nyumbani, nilimkuta mama yangu akiwa amekaa sebuleni, macho yakiwa yamejaa mshangao na wasiwasi. Aliniangalia kwa macho yaliyoniambia kila kitu kabla hajazungumza.
Mama: (kwa sauti ya upole lakini yenye mzigo wa hasira)
“Kelvin… nimeambiwa yote. Kijiji kizima kimeshajua. Hivi kweli una uhusiano na Maria? Yule mwanamke mwenye mtoto?”
Nilinyamaza. Niliinama kidogo na kuchukua pumzi nzito.
Kisha nikasema kwa sauti ya uthabiti:
“Nampenda mama. Nampenda kweli. Na sitamwacha.”
Mama alisimama ghafla. Machozi yakimlenga.
Mama:
“Unaelewa maana ya unachokisema? Wanakijiji hawatakuelewa.
Hawatakusamehe. Na wewe ni kijana wetu wa heshima. Baba yako alikuwa mtu wa maana hapa kijijini. Usiharibu jina lake kwa mapenzi ya muda tu!”
Nilimwangalia mama kwa uchungu lakini nikiwa na msimamo.
“Mapenzi haya si ya muda mama. Niko tayari kwa lolote. Hata kama ni kufa.”
Mama alitetemeka kwa hasira na huzuni. Akaketi chini akisema kwa sauti ya chini:
“Basi jua umeshanivunja moyo, Goodluck
. Umekosea.”
Sikujibu niliondoka kwa hasira na kuelekea chumbani. Nilingi chumbani, nikajifungia na kutazama dari nikijiuliza maswali mengi. Je, kweli nitapambana na kijiji kizima? Je, Maria atakuwa salama?
Nilichoweza kufanya ni kumuombea usalama.
Sikuishia hapo kufikiria ” hivi wanakijiji wanawaza nini mpaka kupitisha sheria zisizo na maana hapa kijijini. Et mama mwenye mtoto ana laana na analeta mikosi imeandikwa wapi tena kwenye
kitabu gani? Kama sio kuendekeza
mambo ya kizamani ? Nasemaje huu mwaka nitasimamia haki nitasimamia na kutoa dhana ya mila potofu bila kujali chochote kile .
Nilichukua shuka langu na kujifunika huwezi amini mpka machozi yalikuwa yananitoka penzi halina hata siku mbili tayari kirusi kishaingia kuharibu penzi jipya . Nilikunja mto na kuuma meno kwa hasira nikisema” MOSES
…………najua hauwezi kuishi hapa lazima utakuwa na plan
Wakati huohuo…
Moses akiwa ameketi katika nyumba ya kifahari pamoja na Natasha, aliketi kwenye kochi kubwa la ngozi huku akivuta sigara kwa mikono mitetemeko ya hasira. Vijana wanne wenye miili ya kisoka walikuwa wamesimama mbele yake.
Ni baada ya kutoka kijijini kwetu alienda kijiji kinachofuata ambapo kule maisha yao ni mazuri kuliko yetu na hata
matajiri wapo wapo kule ndo maana hata yeye kajenga nyumba huko na ni mtu anayependwa sana na watu. Ukiwa na pesa unaweza kujipaka kinyesi lakini bado ukaambiwa unanukia . TUENDELEE
Moses:
“Kesho alfajiri… mnanielewa? Hakikisheni huyo kijana hatatokea tena mbele yangu.
Mlete hapa akiwa amepigwa kiasi cha kujifunza kuwa pesa ndio mungu.”
Kijana mmoja akauliza:
“Tumuue au tumfikidhe kwenye kiwanda cha zamani?”
Moses:
“Sitaki afe leo. Nataka aishi na maumivu. Mkimaliza, mtelekezeni porini. Aumie polepole.”
Natasha alicheka kwa dharau huku akishikilia glasi ya divai.
Natasha:
“Maskini jeuri. Atajifunza kuwa tajiri ndo anatakiwa kuheshimiwa .”
Kisha wale watu wakatoka Nje na kesho ndo siku ya kuja kunikama.ta mimi na kuniteka kwa kadri Mosea alivyowaagiza
Natasha na moses walielekea chumbani
.wakiwa na nguo za kulalia
mara walipigana mabusu na kushikana kisha taa ikazimwa .Watu na mambo yao ni kelele za mahaba ..
Kesho yake alfajiri…
Saa kumi na mbili na nusu asubuhi, nilikuwa njiani kuelekea kazini kwenye Zahanati. Kijiji kilikuwa kimya, milio ya ndege wachache tu ikiashiria mwanzo wa siku mpya.
Lakini hali nilikuwa naona kama haiko sawa .yaani sipo huru na wala hakuna shida yoyote. Bado sijiamini nikiangalia kichakani naona kama majani yanacheza cheza niliogopa ….
Ghafla, kutoka vichakani, vijana watatu waliruka na kunikaba, wakinishika mikono
na kunifunga mdomo kwa kitambaa.
Nilijaribu kupambana lakini walikuwa wengi na wenye nguvu.
Na hapo hapo likaja gari ,haraka haraka na kunibeba mzobe mzobe
Nilisukumwa ndani ya gari aina ya Toyota Harrier nyeusi yenye vioo vya tinted .
” nyie mnanipeleka wapi!?” niliuliza kwa sauti ya hasira na mshangao……
Nilipowatazama niliona bora nikae kimya maana vijana walikuwa wamejazia vifua na wana sura ngumu kama ngozi ya mambo .Na mmoja wao akachomoa bastora na kunionyesha. Nulishtuka
Kisha akaanza kuipitisha kwenye mashavu yangu kwenye kichwa kwenye macho akisema” tulia dogo si unapenda wake za watu na kutaka sifa sasa leo zimekuponza “
Lakini kumbe kipindi tukio lile limetokea Vivian shoga yake Maria
aliliona. Yeye alikuwa katika harakati zake za mazoezi ya asubuhi hivyo alilisguhudia lile tukio.Aliziba mdomo na
kuondoka ….
Nilipelekwa mpaka kwenye kiwanda cha zamani kilichoachwa miaka mingi
iliyopita, pembeni ya msitu. Walinivua
shati langu, wakaanza kunipiga kwa virungu na mateke.
Kijana mmoja akasema:
“Ulipaswa kujua mwenye pesa hashindani na maskini.”
Damu ilinitoka puani, kichwa kikaanza kuuma. Lakini sikulilia huruma. Sikuwaza chochote zaidi ya Maria na familia yangu. Nilijiambia, “Kama nikifa leo nitakuwa na deni kubwa sana kwa wazazi wangu hakuna nilichowafanyia zaidi ya kuwapa mawazo kitu walichokipambania toka nipo shule ya msingi mpaka chuo kikuu.”
” leo kimeonekana ni kazi bure nakufa nikiwa maskini sina hela na mtu nisiye namsaada kwa familia . Uchungu ulinishika na machozi yanatiririka tu
..”.lakini wao wanachokifanya nikunipiga tu bila huruma
Baada ya mateso ya takribani saa moja, walinifunga nakusubiri bossi wao aje na nilijuwa si mwingine lazima awe moses maana ndo mtu ambaye nimwgombana na yeye juzi tu ….
Wakati huohuo, Maria akiwa nyumbani…
Viviano alikuja akiwa anahem sana
“Maria ,maria, Maria njoo nje haraka alionekana ni mtu anayetetemeka
” Go….. Gooodluck ( huku akinyosga kidole”)
“( kwa wasiwasi) Goodluck kafanya tena mbona sikuelewi shoga ya!mngu”
“Maria, Goodluck katekwa nilikuwa nafanya mazoezi kuounguza unene yeye alikuwa anaelekea kazini.Garu likaja na kumteka …
Maria alijikuta akitetemeka. nabkupata wasiwssi” jamani Goodluck atakuwa
kaenda wapi mikono akaweka kichwani
na kuanza kulia …
Huku nikiwa nimefungwa kamba sina hili wala lile nipo kifua wazi yaani nimeanza kujuta kumpenda maria .maana mambo yashakuwa magumu na najiona narnda kupoteza maisha kizembe kabisa ….
Daah nilikuwa nalia huku viboko vikishula mwiini mwangu machozi yakinitoka ….
Nilijuwa huenda nitapoteza maisha ” Mungu nisamehe kwa kuwa
nimeshindwa kuilinda na kuijali familia
yangu naomba uwalinde hata kama siku
nikiwa sipo lakini nawapenda sana
wazazi wangu.
Muda ulikuwa ushaenda na sasa ni saa moja usiku .nilijuwa wazazi sasa wan wasiwasi sana
EPISODE YA 14
Tunaendelea palepale ambapo nilikuwa tayari nishakata tamaa nikiona kifo kipo mikononi mwangu.Niliwaz sana wazazi wangu watakuwa na hali gani…
Lakini yaliyojiri nyumbani sasa Wazazi
wangu walikuwa na wasiwasi sana kuhusu mimi walimpigia rafiki yangu Colince wanajua kuwa nafanya naye kazi.
Baba alipiga simu na ilianza kuita kisha ikapokelewa
” hello baba ” sauti ya Colince ilisikika ” hello colince “
” baba shikamoo”.
” marhaba pole na majukumu”
” Asante sana lakini Goodluck leo hajaja na hajatoa taarifa”
” we Colince hajaja wakati ameondoka saa kumi na mbili asubuhi na mpaka sasa saa nne haonekani?
” Enhe basi hata huku hajafika baba
yangu”
” ulijaribu kumpiga ?”
” nilimpigia lakini akawa hapatikani
,nimejaribu mara kadhaa lakini hakuna chochote tulichopata”
Baba alikata simu kachanganyikiwa haelewi nini kinaendelea kuhusu mimi wanaojua ni Maria na Vivian ambao nao wamempelekea mwenyekiti taarifa.
Mwenyekiti akawaambia atalifanyia kazi.
Mama alianza kulia sana ” mwanangu Goodluck uko wapi? Mbona unatupa wasiwasi wazazi wako?” jamani sijuwi
utakuwa mzima au umekufa? Angalau
nikuone mwanangu …
Mzee alisema kuwa ” usilie mke wangu mtoto wetu ashakua na anauwezo wa kufanya maamuzi. Si alituambia ana mchumba na ni mwanamke mwenye mtoto anaitwa Maria pengine yupo huko si unajua mapenzi ni upofu labda kapofoka
Wanaume wengi hupenda kurahisisha sana mambo hususani wakiwa hawana uhakika nayo. Na baba yangu yupo katika kundi hilo la kurahisisha mambo .
Alimfariju mama yangu na kumwambia
walale kesho watajua cha kufanya lakini mama usingizi hata hauji mawazo yote kwangu.
Kwa Upande wangu wangu mambo ni moto hali yangu ni mbaya .nimeachwa kifua wazi na kuna baridi sana .
Nimefungwa kitambaa cheusi sioni kitu chochote kile zaidi ya kuhisi .Nilikuwa natetemeka muda huo mikono nimefungwa kwa nyuma na miguu pia …
Mwisho nilidondoka chini na kuzimia ilionyesha ndani mule hakukuwa na mtu yeyote wote waliniacha mule na
kuondoka na walivyonifunga ilikuwa sio
rahisi kufungua au kutikisika ilikuwa ni unyama wa hali ya juuu….
………………….SIKU ILIYOFUATA
……………………..
Nilishtuka baada ya kumwagiwa maji ya baridi.Yaani kuna baridi lakini bado walinimwagia maji ya baridi. Na hatimaye nilisikia sauti ya Moses
” Kijana unampiga ngumi tajiri , jambazi unajua kwanini nimekimbia mjini? “
” Sijuwi lakini naomba unisamehe”
” Haha! Unaomba msamaha wakati ushaingia kwenye anga zangu? Nimeua
wengi mpaka sasa na wewe sio wa
kwanza “
“Kwanini umeua sasa walikukosea nini?
” Wengine walikuwa watovu wanidhamu kama wewe na wengine walikuwa wanapita kwenye njia zangu”
” Naomba nisamehe Moses*
” Ukiona nimekueleza kuwa mimi ni nani ujuwe basi huna maisha tena. Kitu unachostahili nikufa na utakufa ngoja kwanza wazazi wako wahangaike “
Kisha akanipiga kofi zito nilihisi masikio kuziba akanipiga ngumi mbili za tumbo nilihisi haja ikinitoka sio kwa yale
maumivu alinigeuza kama Punching Beg
alinipiga sio siri.
Kisha akawambia watu wake kuwa waniangalie atakuja kufanya mazoezi ya kung fu kwenye mwili wangu kuna staili mpya kaziona mtandaoni hivyo atazijaribishia kwenye mwili wangu.kisha akatoka na kwenda zake huwezi amini kwa yale maumivu nilizimia tena …
Kwa mwenyekiti Maria na Vivian walikuwa wa kwanza kufika na muda mfupi baba ,mama na rafiki yangu Colince nao walifika . Unajua M wazazi wangi hawamjuwi Maria na wana hasira
naye kwa kuwa wanaona ndo sababu ya
yote hayo
Maria kumuona baba alimsogelea na kumsalimia ” shikamoo baba “
” Marahaba mwanangu “
” Pole na yaliyomkuta mwanao” ” Pole ya nini na wewe ni nani?
” Mimi naitwa maria “
Baba hakuongea sana zaidi ya kumpiga kibao na nguvu na kusema ” shetani wewe haya niambir mwanangu yuko wapi?
Maria alikuwa anajishika shavu huku
analia ” Goodluck ametekwa toka jana nimemletea taarifa mwenyekiti alisema atawajulisha na kulifanyia kazi
Baba alimgeukia mwenyekiti” hivi mwenyekiti namba yangu unayo au hauna”
” Ninayo namba yako “
” Kwanini hukunipigia kunijulisha ?” “Nisamehe mzee ni majukumu”
” Majukumu?” Akawa anataka kumsogelea amfumue pia lakini Colince alimzuia
Baba alikuwa kavurugwa akili kawa mbogo hataki utani na mtu yoyote yule
Alivuta simu na kumpigia jamaa moja
ambaye ni mwanajeshi mstaafu maana kama mwenyekiti anampotezea muda
….
Simu iliita muda huo anamtazama Maria kwa hasira lakini mama yangu hana nguvu hata ya kuongea kakaa tu chini mwishowe simu ilipokelewa
” Habari Mzee Mlowe “
” Habari kamanda Issack “
” Rafiki yangu za siku nyingi”
” Salama kabisa sijuwi kwako?”
” Siko salama ndugu yangi na matatizo” ” Matatizo ! Matatizo gani tena ?
” Yule mtoto wangu wa kiume “
” Anha si Goodkuck ?”
” Eeeh kapata tatizo kubwa “
” Tatizo gani kama hana ajira sema namuunganisha haraka anapata kazi”
” Sio hivyo katekwa jana usiku “
” Katekwa ? Hivi hadi kijijini kwenu kuna watekaji ?mbona kijiji chenu kina amani ?
” Ndiyo kuna mtu amekuja kutoka mjini aliishi hapa hapa ndo anahisiwa ndiyo kafanya utekaji
” Nani tena huyo maana si ubakumbuka nimeishi sana hapo “
” Kuna tajiri mmoja anaitwa Moses ni kijana wa hapa hapa lakini alienda mjini alivyorudi ndo yote yakatokea.
” Moses ? Si umemsema huyo”
” Ndiyo unamfahamu “
” Yaani huyo ni jambazi kila sehemu huku kuna mabango yake tena afadhali umenipa taarifa nitawajulisha polisu na watafika huko mara moja …..
Kisha akakata simu na kuongea na polisi ambao hawakuwa mbali sana na kijiji chetu na baada ya kupata taarifa walijiandaa na kuanza safari ya kufika kijijini kwetu..
Wazazi wangu walirudi nyumbani baada ya kusikia kuwa suala hilo lipo mikononi mwa polisi ….
Polisi walianza upelelezi haraka sana .
Waliuliza kila mtu kama aliliona gari jeusi lenye tinted lakini kial aliyeulizwa hajuwi kitu. Siku zilizidi kwenda nipo ndani mule nateseka na tabia ya Moses anakuja kunipiga piga mwisho ananiacha Baba mama , maria na watu wengi walikuwa wanajiuliza niko wapi na hata Benson anamuuliza mama yake nitarudi lini …..
Sikuwahi kufikiri kama napendwa hivyo
Baada ya siku tatu Polisi waligundua nilipokuwa nimehifadhiwa waliomba makao makuu iongeze idadi ya askari maana wanaoenda kuwavamia ni majambazi sio vibaka au wezi wa pipi
…Basi idadi iliongezeka mambo yalienda
kimya kimya bila Moses kugundua
Jioni ya siku hiyo Moses alikuja na kuniambia amenivumilia sana anaona sasa ni muda wangu wa kufa kachoka kunitesa. Alichukua kamba muda huo nimekarishwa kwenye kiti sina .
Akaniviringisha kamba ngumu shingoni na kuanza kuninyonga huku anacheka na kusema
” KUFA ! KUFA! ” Nilianza kuishiwa pumzi lakini ghafla alipigwa risasi ya bega ….
Alijikuta akirudi nyuma huku akilishika bega
” Sauti ilisikika mpo chini ya ulinzi”
EPISODE YA 15
Mara tu baada ya risasi kupigwa, sauti nzito ya kikomando ilisikika kwa ukali:
“Tupa silaha chini! Mikono juu! Wote mko chini ya ulinzi!”
Angalau sasa nilipata matumaini wazazi wangu nitawaona hapo ndipo faraja ya moyo ikaja …..
Moses alitetemeka. Hakutegemea hata
kidogo kuwa polisi wangekuwa wamefika. Mikono yake iliinama, silaha yake ikaanguka chini kwa kishindo. Hakuwa na nguvu tena za kuendelea. Macho yake yakakutana na yangu – hakukuwa tena na tabasamu la ushindi usoni mwake – badala yake, alikuwa na woga wa mtu anayekaribia kifo.
Polisi waliokuwa wamejificha vizuri, walifyatuka kutoka kila upande wa nyumba hiyo . Walivaa mavazi meusi ya kombati, wengine walivaa sare rasmi, wote wakiwa na silaha nzito. Mlango mkubwa wa gereji ulivunjwa kwa mateke na mmoja wa askari akaingia .
“Mkanda! Mkanda!” alisikika akisema huku akimpeleka mbwa upande mwingine wa nyumba kuhakikisha hakuna mtu anayetoroka.
Mmoja wa askari alinikimbilia pale nilipokuwa nimefungwa kwenye kiti, huku akisema kwa sauti ya upole l
“Kijana utakuwa salama sasa. Tuko hapa kukuokoa.”
Alikata kamba zilizonifunga, na nilipoachiliwa nilidondoka kama mzoga – sikuwa na nguvu hata ya kusimama.
Nilikuwa nimeishiwa pumzi, macho
yakiwa mekundu, midomo mikavu.
Waliniinua na kunipeleka kwenye gari la wagonjwa lililokuwa tayari nje, huku mwingine akinipa maji.
Moses na wenzake wote walifungwa pingu, wakapigishwa magoti, na kuamriwa waweke mikomo vichwani. Hapo ndipo nilipomuona mmoja wa watu waliokuwa wakinitesa siku zote alikuwa analia kama mtoto mdogo.
“Nilikuwa nalazimishwa tu… sikutaka… nilikuwa natimiza amri!” Alilia lakini polisi hawakumskiliza – walimchukua kama mhalifu
Wakati hayo yote yanatokea, taarifa zilifika kijijini kwamba Goodluck ameokolewa akiwa hai. Maria alipoisikia taarifa hiyo, alipiga kelele kubwa na kuanguka kwa furaha. Mama yangu alilia kwa nguvu akisema:
“Ahsante Mungu wangu! Mwanangu amerudi… mtoto wangu amerudi!”
Baba naye alishindwa kujizuia, alisogea kwenye ukuta akapiga pigo moja kwa mkono wake kwa furaha.
“Nilijua mwanangu ni mpiganaji!” alisema kwa sauti ya kujivunia.
Na walipewa taarifa kuwa nimelazwa hospitali ya wilaya hakuna aliyesubiri mama , baba ,maria na
colince walifunga safarinkuelekea mjini kwa ajili ya kuja kunitazama safari ilikuwa ndefu lakini waliamini watafika .
Nkumbuka niliokolewa saa sita mchana
…..
Saa Mbili Usiku – Hospitali Kuu ya Wilaya
Nilifikishwa hospitalini. Daktari alinishughulikia haraka niliwekwa hewa ya oksijeni, wakasafisha majeraha yangu,
na kunipa dawa za maumivu. Nilihisi
amani ya aina yake japo mwili ulikuwa na maumivu, moyo ulikuwa na faraja.
Maria aliingia akiwa na mama yangu na baba. Alinisogelea taratibu, machozi yakimtoka usoni.
“Goodluck… pole sana. Nimesikitika mno. Samahan nimskuwa sababu ya yote haya na wewe kuteseka kweli mimi ni mwanamke mbaya sana i…”
Nilijaribu kutabasamu japo kwa uchungu, nikasema kwa sauti dhaifu,
“hapana usijali kuwa na amani wewe ni
wangu utabaki kuwa wangu nakupenda sana .”
Baba na mama walinitazama hawakuwa na la kusem zaidi ya kunitazama nikiyasema maneno yangu kwa maria.
Mroa hakuwa na cha kufanya zaidi ya kunikumbatia ” nakupenda sana Goodluck hata kisemwi nini nitabaki kuwa wako naamini utanipa furaha ambayo yule mwanaume katili Moses aliichukua …..
” usijali Darling nitafanya kila kitu kwa ajili
yako si unajua ninavyokupenda Maria .
Sio wewe tu na hata Benson ninyi kwangu ni familia na mtabaki hivyo ….nawapenda pia wazazi wangu naomba mheshimu mawazo yangu …..
Kisha Maria akaniachia baada ya kunikumbatia kwa muda mrefu .Alikuwa anatoka machozi ya furaha
Mama alinikumbatia pia , huku baba akiwa pembeni akiwa na macho yaliyolowa kwa machozi ya furaha.
“Mwanangu… Nashukuru kwa sababu uumzima nina furaha sana mwanangu”
Wote walijawa na furaha na baadaye ya siku nne niliruhusiwa na kurudi nyumbani
Tukiwa nyumbani sasa angalau naweza hata kusimama na kutembea sauti ilisikika Redioni ……
“MTUHUMIWA HATARI WAALIYESUMBUA
JESHI LA POLISI KWA MATUKIO MBALI MBALI IKIWA NI PAMOJA NA UUZAJI
WA MADAWA YA KULEVYA , UTEKAJI NA PAMOJA NA MAUAJI YA WATU KADHAAA
AMEKAMATWA NA JESHI LA POLISI
KATIKA OPARESHENI KALI ILIYOFANYIKA USIKU KATIKA KIJIJI CHA
KIBEREGE KIJANA GOODLUCK ALIYEKUWA AMETEKWA ALIOKOLEWA AKIWA HAI I.”
Watu wengi walishangaa na wengine walifika nyumbani kuniona – hata watu niliowahi kuwasaidia zamani walikuja kuniombea na kunitia moyo.
Siku chache baadaye, Moses na genge lake walihukumiwa kifungo cha maisha jela. Familia yangu, Maria, Colince, na hata mwenyekiti walikuja kuniomba
msamaha kwa kutochukua hatua
mapema. Nilijua sasa maisha yamebadilika. Nilikuwa nimepita kwenye bonde la mauti, lakini bado niliishi – na sasa, nilitaka kuishi kwa maana.
Nilimshika Maria mkono nikamwambia:
“Baada ya yote haya, nakuhitaji milele. Je, utakuwa wangu?”
Maria alitabasamu na kusema, “Nilikuwa wako tangu siku ya kwanza
uliponambia una unanipenda Goodluck.”
Wanakijiji wakikuwa bado wanapinga
suala la mimi kuwa na mahusiano wakiamini ni laana lakini niliapa kwrnye kikao nitafundisha najuwa watapinga lakini lazima niondoe mila hiyo na nyingine zote…..
……WiKI MOJA BAADAYE SANA ……..
SIKU YA MKUTANO ILIFIKA NA HAPO ILIKUWA MWISHO WA MWEZI..
Wakazi walikusanyika chini ya mti mkubwa wa mkangazi hapo ndipo mikutano yote ya kijiji ilifanyikia tangu enzi. Nilikaa mbele, pembeni ya wazee wa
kijiji, akiwa upande mwingine alikuwa
baba yangu, Colince na Maria. Watu walinitazama kwa huruma, wengine kwa mshangao, lakini zaidi kwa hamu ya kusikia nitakachosema. Baada ya agenda za muhimu kujadiliwa …..
Mwenyekiti alisimama na kusema:
“Leo tumekusanyika hapa si tu kujadili usalama wa kijiji tu , bali pia kusikiliza ujumbe wa kijana wetu Goodluck ambaye alikuwa mhanga wa tukio baya. Lakini pia ana jambo muhimu la kutushirikisha.”
Watu walipiga makofi na kunisubiri
niongee .. Nilihema kwa nguvu sikuwahi kuwa na ujasiri wa kuongea mbele za watu
Nilisimama, nikisikia mapigo ya moyo wangu yakidunda kwa nguvu.
Nilimwangalia Maria kwa upole, kisha nikaanza…
“Ndugu zangu,” nilianza, “maisha yamenifundisha kuwa si kila anayesema anakupenda ni mpenzi wa kweli, na si kila anayekupuuza ni adui. Maria, mwanamke huyu mliyemhukumu kwa kuwa na mtoto, ndiye aliyekuwa mstari wa mbele
kuhakikisha naokolewa. Wengi
walimnyoshea vidole, wakamuita mzigo, hawajui kuwa yeye ndiye furaha ya maisha yangu leo.”
Watu walikuwa kimya, wakinisikiliza kwa makini.
“Kuna mila potofu ambazo tumekuwa tukizikumbatia—moja wapo ni ile ya kutokuoa mwanamke mwenye mtoto. Hii mila si haki! Tunawakatisha tamaa wanawake waliojeruhiwa na mapenzi, tunawanyima nafasi ya pili katika maisha kwa kosa ambalo si lao. Kuna watoto wengi yatima, kuna wanawake
waliotelekezwa—je, wote hawa
hawastahili kupendwa?”
Nilipoanza kutoa mifano hai, akiwemo mama yangu mdogo aliyelelewa na mama wa kambo na akafanikiwa maishani, machozi yaliwatoka baadhi ya akina mama.
“Leo naomba tuseme ukweli mtoto wa Maria si tatizo. Tatizo ni sisi tunaowahukumu. Mimi mwenyewe nimepita katika maumivu, lakini huyu hapa (nikimwelekeza Maria) ndiye aliyeshikilia mkono wangu wakati
nimevunjika, wakati hata familia yangu
haikujua niliko.”
Kisha nikageukia wazee wa kijiji:
“Naomba leo, mbele yenu, niseme wazi: siioni sababu ya kuendelea kuishi kwa mila zinazobagua. Leo nataka nitangaze kuwa nitamuoa Maria, awe na mtoto au la. Sitaki mtoto wake aitwe ‘mtoto wa Maria’ tena—yule ni mwanangu kuanzia sasa.”
Walikuwapo waliopinga:
“Lakini mila zinasema mwanamke mwenye mtoto ni mzigo!”
Lakini kabla hawajaendelea, mzee mmoja mwenye busara alisimama na kusema:
“Mila hutengenezwa na binadamu. Kama tunaona hazileti haki, basi tunao uwezo wa kuzibadilisha. Leo Goodluck ametufumbua macho. Tuache unafiki, tuishi kwa upendo, si hukumu.”
Baada ya kikao hicho, kulikuwa na mjadala mrefu. Wengine walionekana bado kushikilia mila hizo, lakini wengi walishawishika. Niliona mabadiliko
yakianza pale pale — watu walianza
kumpokea Maria kama sehemu ya jamii, na hata mwanamke mmoja aliyelelewa na mama yake pekee alikuja mbele na kumkumbatia Maria akisema:
“Umenipa tumaini jipya, dada yangu.”
MIWISHO WA MWEZI Baada ya siku chache, nilipata taarifa kuwa nilikubaliwa kujiunga na shule moja mjini . Nilihama kijijini, nikiwa nimebeba matumaini mapya. Maria, akiwa na mtoto wake, alikuja kunitembelea mjini, na hapo ndipo tulipoamua kuhalalisha mahusiano yetu.
Niliamua kumuoa Maria. Harusi yetu
ilifanyika kijijini, mbele ya watu waliokuwa wamebadilika, waliokuwa sasa wanaamini kuwa mapenzi siyo kuhusu hadhi, wala historia ya mtu, bali moyo na nia njema.
Na hivyo, mila potofu moja ilizikwa rasmi siku hiyo. Lakini baada ya hapo nilianza kupambana na maisha mjini miezi ilienda mara miaka mapambano yaliendelea
MIAKA SITA BAADAYE NILIKUWA NISHAWAJENGEA WAZAZI WANGU NYUMBA NZURI NA YA KISASA . Kijiji
kwetu walinipenda kwa kuwa nimebadili
vitu vingi …
Walikuwa wakiniagizia vitu kama mchele viazi na vitu kadha wa kadha kijiji chetu kilikuwa na hawakuweza kunisahau …..
Maria alipata ujauzito na kujifungua kipindi hicho Benson tayari shule imekorea kweli maisha yetu yalikuwa ni bora sana na najivunia kuwa na yeye
She is my everything NAMPENDA SANA …
*********””MWISHO”””””””””””””””””””””’