EPISDODE 10
Niliinua macho yangu polepole baada ya kuona hatua ya miguu ya mwanamke akiwa mbele yangu na sura niliyokutana nayo ilinifanya nishangae niliinuka na kumuacha mtoto pale chini.
” Maria”
Niliita kwa sauti ya upole na yenye msisimko sana . Nikamuuliza
” Umekuja kufanya nini mbona unanitazama?”
” Hapa mi nimekuja hapa kwa mangi na mwanangu lakini nashangaa mmefahamiani leo na Benson?
” Mmmh kumbe wewe ndo mama yake
Bensom ?
” Ndiyo ni mama yake “
” Mmmh yaani kumbe nilikuwa sahihi kukusaidia mi sikujuwa kama huyu ni mwanao “
” Hata mimi sikujua kuwa wewe ndo yule mjomba aliyekuwa ana msifia kila mtu hakika nimefurahi sana kumbe una moyo mzuri hivo”
” Ndo maisha Maria usimdharau mtu yoyote kumuheshimu mtu sio mpaka umjuwe sio mpaka mjuwane mheshimu mtu yoyote kuna leo kuna kesho Maria “
” Okay sawa sasa we unaenda wapi ?”
Aliuliza maria
” Naenda kucheki mechi kule chini kwenye banda la mpira “
” Anhaaa karibu ukakufahamu kwangu” alisema kwa furaha sana yaani kitendo cha mimi kumjali mtoto wake kwake ilikuwa ni kitu kikubwa na kilichofanya alainishe moyo wake .
Na hata hasira za jion muda ule mtoni ziliisha niliona hakuna maana ya kwenda kuangalia mpira nilimtumia meseji colince na kumjukisha kuwa sitaweza kufika nina dharula . Dharula yenyewe sasa ….
Alinunua mchele nusu kisha tukafunga safari mimi yeye na benson mpaka nyumbani kwake niliingia ndaninkwao kweli wana maisha ya kawaida lakini furaha imejaa tele …..
Alitoka nje na kuwasha moto kwenye jiko la kuni muda huo benson kanikalia kwenye miguu yaani mtoto ananiona mimi kama baba yake. Nilikuwa nikimtazama Maria akiwasha moto na machozi yakimtoka si unajua moshi..
Nilimuonea huruma nilimwambia benson
asogee pembeni,nikamsogelea na kumwambia
” Ngoja nikusaidie Mama.” Nikawa naupuliza taratibu
Macho ya maria yalikuwa yakinitazama navyoupuliza moto alijikuta akiweka mikono yake mashavuni nakunitazama ilionyesha tayari kidume nimeanza kupenyeza moyoni mwake …
Alikuwa akismile na tabasamu lake sasa ni kufuru nilikuwa naibia ibia si unajua.kipindi nataka kuchukua kiberiti kumbe kipo karibu na mkono wake nikaushika mkono wote tulishtuka wote
tulibaki tunatazamana. Benson naye
akaja” mama mbona unamshika mkono Uncle ?”
Tuliachiana wote kwa aibu mmmmh ila Benson kwa kuharubu mambo lakini moto ulikuwa ushawaka .Turirudi na Benson kukaa kwenye kiti na yeye kumuacha anapika . Kila alichofanya nilikiangalia kuja kumtazama Benson ameshapitiwa na usingizi ….
Nilimsogelea maria na kumuinua naye alitiii hakuwa na wasi wasi nikamfuta machozi yaliyosababishwa na ule moshi
kisha nikauchukua mkono wake na
kuubusu .Alibaki ametulia kaduwaaa
Nikawa namsogelea naye anarudi nyuma kwa wasiwasi mpaka akawa amefika ukutani. Kisha akahema huku macho yake yakinitazam nami namtazama yeye . Nilimsogelea na kumshika kiuno alishtuka nikamvuta karibu yangu …..
Nikawa nasogeza mdomo wangu karibu na wake alijua kifuatacho ni Romance hivyo ilimpasa ayafumbe macho na alifumnba bila hata kutarajia …..hata mimi yote nayafanya bila hata kuyatarajia
..
Sijuwi huu usharkan umeingia vipi leo najikuta ni mwepesi niko romantic sio siri kazi nimeiweza nilikuwa nataka nimpe denda saa ngapi harufu ya wali kuungua isisikike alinisukuma pembeni
‘ ona tunataka kuunguza ubwabwa “
Niliposukumwa pembeni, nilicheka kwa aibu na kuchungulia sufuria. Harufu ya wali uliokuwa karibu kuungua ilianza kusambaa taratibu hewani.
Maria alikimbilia haraka, akichanganya wali kwa mwiko huku akisema kwa sauti ya kuficha aibu:
“Mbona hufikiri? Tumekuwa karibu kuunguza chakula!”
Nikaitikia huku nikijikuna kisogoni:
“Si unajua tena… wakati mwingine moyo unatangulia kuliko akili.”
Alinitazama kwa jicho la upole lakini lenye ujumbe mzito.
“Goodluck, naomba uniambie ukweli… hivi unamaanisha haya yote
unayoyafanya? Au ni huruma tu kwa
sababu ya mtoto wangu?”
Nilikaa kimya kwa sekunde kadhaa, nikamkaribia pale jikoni, nikiwa makini asije tena kunisukuma. Nikasema:
“Maria, siwezi kukudanganya. Kile kilichotokea sasa hivi hakikuwa mipango. Kimekuja tu – kutoka moyoni. Benson ni mtoto mzuri, lakini vile vile, mama yake ni mwanamke mwenye moyo wa kipekee.
Ule upendo unaotoka kwako kwake, huo upendo… umenivuta.”
Maria alichanganya wali polepole, halafu
akaniuliza kwa sauti ya chini:
“Unajua mimi ni nani? Mimi ni mama wa mtoto, si msichana wa kuchezewa.”
“Ndiyo, na hilo ndilo linanivutia zaidi,” nilijibu kwa sauti ya uthabiti.
“Wewe ni mwanamke ambaye amejifunza maisha kwa tabu, ambaye hana muda wa maigizo, na huyo ndiye ninayemtafuta.”
Maria alinitazama tena, halafu akaachia tabasamu dogo.
“Hivi unajua umebadili hali ya nyumba hii leo?”
Nikamuuliza kwa mshangao, “Nimebadili vipi?”
“Nyumba hii ilikuwa kimya. Nilikuwa nimezoea kufanya kila kitu mwenyewe. Leo, kuna sauti ya kicheko, kuna mtu wa kunisaidia kuni, na kuna macho yanayonitazama kwa heshima. Sijui kama ni ndoto au ni kweli.”
Nilimshika bega lake kwa upole, nikamwambia:
“Maria, usiogope. Wewe si ndoto wewe ni mwanamke ambaye maisha yameamua
kuandika ukurasa mpya. Na kama utanipa
nafasi… nitataka kuwa sehemu ya ukurasa huo.”
Tulitulia kwa muda kidogo. Benson alikuwa bado amelala usingizi mzito. Harufu ya wali sasa ilikuwa tamu, chakula kilikuwa tayari.Lakini Maria ilibidi amuamshe Benson ili tiweze kuka chakula
Nilijisikia amani sana kuwa na Familiaa hii hakila ilinivutoa namna inavyoishi kwa upendo kila nikimuangalia maria nazidi kuchanganyikiwa yaani nampenda sio siri
….
Tulikaa mezani, tukala kimya kimya, lakini mioyo yetu ilizungumza kwa lugha ya macho. Na hili suala hata Benson alikuwa kama kalishtukia
” baada ya kula mnatazamana ,kuleni uko” alisema benson kwa sauti ya utani na ukali.
Baada ya chakula, nilimsaidia kuosha vyombo. Kila mara mikono yetu ilipogusana, tulicheka kwa aibu. Ukimya kati yetu ulikuwa wa amani, si wa mashaka.
Ilipofika saa tatu usiku, niliwaaga ma
kuondoka. Maria alinitazama kwa macho ya kutamani nisiondoke.
Nilimwangalia pia, kisha nikamwambia: “Nikienda sasa hivi, sitalala usingizi.
Lakini najua nikibaki, siwezi kujizuia…”
Maria alishusha pumzi, halafu akasema kwa sauti ya chini sana:
“Nenda… lakini usisahau kurudi.”
Nilitabasamu, nikamshika mkono kwa
upole na kuubusu tena.
Kisha nikamwangalia usoni na kusema:
“Asante kwa leo. Umekuwa tiba ya moyo wangu uliokuwa na majeraha yasiyoonekana.”
Nilipotoka nje, upepo wa usiku ulikuwa mtulivu. Lakini ndani ya moyo wangu, kulikuwa na upepo wa upendo uliopuliza matumaini mapya.
Nikitembea kurudi kwangu, moyo wangu ulikuwa umejaa furaha mpya, na macho yangu yalikuwa na picha moja tu – uso wa
Maria, tabasamu lake, na uzuri wa macho
yake ..
Lkini kumbe Benson alikuwa akituchora hata hakulala alimuuliza mama yake
” mama unampenda Uncle ” Maria alishtuka sana …..
EPISODE 11
“Mama, unampenda Uncle?”
Swali la Benson lilimchoma Maria kama
sindano ya mshipa. Alikuwa bado amesimama mlangoni, akimtazama Goodluck akitoweka gizani, huku moyo wake ukiwa umevurugwa kwa hisia mpya, zisizoeleweka kirahisi. Lakini swali hilo la mtoto wake lilimrudisha ghafla kwenye uhalisia – na uhalisia huo ulikuwa mtoto mdogo mwenye akili ya haraka sana.
Maria aligeuza uso wake na kumtazama Benson kwa mshangao.
“Benson! Umekuwa hujalala bado?”
aliuliza kwa sauti ya kustaajabu, akijaribu kuficha mshituko wake.
Benson alicheka kimtoto, kisha akajibu, “Nilikuwa nimefungua kidogo macho… nilikuwa nasikia sauti zenu. Mama ulikuwa unacheka sana na uncle, halafu ulitabasamu ile ya shuleni ile ile.”
Maria alipigwa na butwaa, akabaki anamwangalia mwanae bila kujua aanze wapi. Alitamani amwambie Benson kuwa hayo yote ni mambo ya watu wazima, lakini hakuwa na moyo wa kumdanganya. Huyu alikuwa mwanawe wa damu, na pia rafiki yake wa karibu zaidi.
“Benson,” alisema kwa sauti ya upole,
“Uncle ni mtu mzuri sana, si unakubaliana na mimi?”
“Ndiyo, ni mzuri sana. Alininunulia pipi na
akanibeba kwenye mgongo! Akaniambia kuwa mimi ni jasiri.”
Maria alicheka, kisha akamchukua mtoto wake na kumlaza kitandani. “Sasa twende kulala, kesho tuna kazi nyingi.”
“Lakini mama hujanijibu… unampenda?” Benson alisisitiza kwa sauti ya kupoza.
Maria alishusha pumzi ndefu,
akamtazama mwanawe aliyekuwa akimkodolea macho kwa matumaini.
“Siwezi kusema bado, Benson… lakini
kuna kitu kizuri kinachokua moyoni mwa mama yako. Nikihakikisha ni kweli, nitakuambia.”
“Nitafurahi sana kama mtaoana, maana
Uncle ni shujaa!” alisema Benson kwa furaha kisha akageuka na kupitiwa na usingizi haraka.
Basi na mimi nilirejea nyumbani na
nilimpigia rafiki yangu Colince ili nimuelekeze maana alinambia na kunishauri bora nimwambia ukweli Maria
Simu iliita haikupita muda naye akaipokea
” Oya kaka vipi”
” Mzima wewe ?’
” Niko powa Goodluck , vipi mtoto kakurlewa”
” Yeah kanielewa sema kuna shida ” ” Mmmh shida gani rafiki yangu?”
” Kumbe Maria ana mtoto?” ” Ana mtoto tena ?”
“Ndyo anaye mtoto tena nilikuwa namjua
ila sikujuwa kama alikuwa ni mtoto wa Maria “
” Mmmmmh pagumu hapo “
” Kwelu pagumu sana hususani na hii sheria kali ya kijiji .kwamba mwanamke ambaye ana mtoto haolewi na hutakiwi kuwa naye kwenye mahusiano adhabu yake ni kunyongwa “
” Kama adhabu unaijuwa si uachane naye tafuta pisi nyingine hata kale kanessi VERONICA.
“Mh hapana nitashikilia hapa hapa tuone mwishowe itakuwaje”
Haya usiku mwema rafiki yangu mwana kulitafuta mwana kulipata
Nilicheka kisha nikakata simu . Kweli nilikuwa nikiwaza nifanyaje . Nampenda maria lakini mila potofu ndo zinazofuatwa kijijini kwetu . Nilijipa moyo vita hii nitashinda sio kwa faida yangu na hata faida ya wengine …..
Kumbe sio kwangu hata Maria anawaza hicho hicho atawezaje kulinda penzi jipya ilihali sheria ngumu ndo imeshikiliwa na sio kwamba hatujuwi tunajua.
Nachowaza mimi ndo anachowaza yeye
Mwisho kila mtu alipitiwa na usingizi
.Japo tupo mbali lakini hisia zetu zinafanana sana .
SIKU ILIYOFUATA
kama kawaida nilijiandaa na kuelekea kazini ambako huku shughuli zangu ziliendelea kama kawaida na sasa
naanza kuizoe kazi yangu hii.Nilifika kazini japo nilikuwa na mawazo niliyaweka pembeni na kupiga kazi majira ya jioni niliondoka nakuelekea nyumbani.
Nilipitia nyumbani kwa Maria sikuweza kumuona nilijaribu kumuuliza moja ya majirani akanambia atakuwa
sokoni.nilichoka sana lakini kwa kuwa
nimependa sina namna inanibidi nimfuate huko huko.NAMPENDA MARIA
Nilitembea haraka nikiwa nahema hadi sokoni nikamkuta anasinzia ….
Nilikuwa namcheka maana alionekana amechoka sana ….
Nilimsogelea na kukaa pembeni yake yeye bado anasinzia tu . Alipotaka kuanguka kwa kuwa nilikuwa karibu aliangukia begani kwangu na hapa ndipo akashtuka …” Mmmh Goodluck umefika muda eeeh?
Nilimjibu ” hapana nimefika sasa hivi tu”
” Pole na kazi baba “
” Asante mzima wewe nakuona umejichokea “
“Ni kweli siku nzima wateja hakuna “
” Ndo maisha leo sio jana na kesho sio lei cha msingi ni kupambana mama yangu “
” Asante kwa maneno yako ya faraja hakika yananitia sana moyo nitapambana bila kuchoka ” Alisema Maria
Basi watu wakaanza kunong’onezana
,niligundua dhahili wanatuzungumzia sisi. Maana walikuwa wakitunyoshea vidole na wote wanajua kuwa yule Maria ana mtoto
Mzee Onesmo ni moja ya wazee wenye busara sana alisogea pale na kutuambia
” Mnaweza mkawa mko kwenye
mahusiano nachowashauri myasitishe au mnaweza msiwe nayo kabisa hiyo ndo itapendeza .”
Tulitulia kama maji kwenye mtungi safi.Na ndipo hapo hapo ikaingia gari moja zuri sana pale kijijini.Nilishtuka maana kijiji chetu hakuna hata mwenye uwezo wa kumiliki Gari hilo. Vioo vilishushwa akashuka jamaa mmoja kavaa sio kavaa tu kavaa na kapendeza .
Maria alishtuka na kusema ” MOSES” . moses alivua miwani na kusogea karibu yetu . Na nakumbuka Maria alinambia
kuhusu Moses kuwa ndo baba wa Benson
. JE UJIO WAKE NI WA NINI WAKATI ALISHAWAHI KUMKATAA MARIA NA MIMBA YENYEWE …..
EPISODE 12
Tunaendelea pale pale tulipoishia ambapo Moses mwanaume aliyemtelekeza Maria karudi tena anaonekana ana pesa wakati alikuwa kapuku na mtu wa kutupwa miaka miwili sahizi kawa tajiri….
Maria alitetemeka. Uso wake ukabadilika. Mdomo wake ukafunguka kidogo kisha
akatamka kwa sauti ya mshangao
uliogubikwa na hofu: “Moses…”
Mwanaume huyo alimtazama Maria juu chini kisha akacheka kwa dharau
“Kumbe bado upo, Maria? Hivi wewe huoni hali yako? Mbona umekuwa mbona imepauka sana ? Tofauti na nilivyokuacha
? , Hivi ndivyo unavyoishi? Hii sura imezeeka kuliko nilivyotarajia.”
Nikamtazama Moses kwa macho ya hasira, lakini nikajizuia.
Maria hakusema kitu zaidi ya kumuangalia tu.
Moses alikuwa akifikicha mikono yake na kusema
“Sijaja hapa kujipendekeza, Maria . Niko kwa ajili ya mtoto wetu…”
“Mtoto wetu?” Maria alirudia kwa kicheko cha dharau.
“Huyo Benson? Huyo sio mtoto wako si ulisema mwenyewe ile siku nikaamua kumlea,
Leo kimekuwasha nini hebu toka hapa ! Alisema maria kwa ukali
Lakini Moses alikuwa anacheka sana “
hahah eti nilimuacha na kumkataa mwanangu lazima nitakuwa nilikuwa nimelewa ! Yaani mimi nikatae damu yangu hivi Maria una akili kweli
Maria alimtazama Moses kwa hasira sana na kusema ” nimekwambia toka hapa kabla sijakuaibisha mbele za watu mbw* wewe”. Mpaka hapa ndipo nilipogundua kuwa Maria ana hasira sana
” Unataka uonekane shujaa mbele ya hiki kibwana chako ambacho kinaonekana hakina malengo . Hivi hamuoni wote mnanuka shida sasa mtaishije maskini
olewa na tajiri . Masikini + maskini si
utapia mlo “
Nilizidi kupandwa na hasira niliona kama moyo unawaka moto kwa hasira ya maneno ya dharau na kiburi cha Moses kwa sababu tu kapata hela .
Maria alimsogelea na kumwambia ” hapa huwezi kupata chochote kama una maisha mazuri kayaishi niache mimi na mwanangu”
Mara ghafla wenyewe wakiendelea kuzozana . Mlango wa lile gari ulifunguliwa na alishuka msichana
mmoja kavaa vizuri yaani kitajili san gauni
la thamani la rangi ya njano na kiatu cha bei sana . Hivyo vyote vilionyesha ni mtu wa hadhi ya juu na hawezi kuishi kijiji kama chetu.
Alikuwa anatembea kwa maringo kuja kwetu.Moses alipogeuka alisema kwa kujidai ” oooh Natasha i mpenzi wangu njoo karibu sekunde chache tu nishakumis”
” Mmmh kweli mpenzi ?” Alisema Natasha
” Yeah k” kisha akamsogelea na kumkumbatia mbele ya maria na kumwambia maneno haya
” Maria umeona wasichana wa hadhi yangu ni wale wenye maisha kama yangu. Ujuwe ndege wanaofanana huruka pamoja na mimi naruka na Natasha lakini wewe si unaruka na hii taka taka.
Nilikasirika na kumsogelea nikiwa nahema kwa nguvu nilimsukuma natasha pembeni na kumkwida nilisema kwa hasira ” sema tena uone nitakachokufanya hapa sokoni siku ya leo
….
Macho ya watu sokoni yakaanza kutugeukia. Macho ya kejeli kwa baadhi, macho ya huruma kwa wengine. watu walianza kukusanyika na muda huo alikuwa ameshavuka mstali wangu wa ustaarabu sasa nimegeuka mbogo
Lakini cha ajabu alicheka na kusema
” nimesema wewe ni takataka ambacho hujasikia ni nini we takataka ?
PAAAAAA!!!!!!!
ngumi ya hasira ilitua taya la kushoto la Moses.
Akaanguka. Miwani yake ikarushwa
pembeni. Damu ikamtoka mdomoni
.akajifuta damu na kusimama
Watu wakazidi kukusanyika. Wakabaki kimya. Kijiji chetu hakijazoea kuona mtu tajiri akipigwa hadharani. Nilimkaribia akijaribu kuinuka.
“Hiki sio kipindi cha maigizo, Moses,” nilimwambia kwa ukali.
“Huyu mwanamke uliyemwacha akiumia, ndio huyo huyo umekuja kumdhalilisha leo mbele za watu ? Huna haya?”
Maria alikuwa amerudi nyuma
akitetemeka, machozi yakimtiririka. Nilimgeukia na kumwambia:
“Usiogope. Leo, hakuna mtu atakayekuvunjia heshima nikiwepo.”
Maria alionekana bado akiogopa na kunionea huruma kwa kuwa nimenunua ugomvi ambao sio wangu. Ujuwe kijiji watu wananiona mstaarabu na mtu mwenye heshima kutokana na namna wazazi wangu wanavyonilea na sikuwahi ata kupigizana kelele na mtu .
Moses alijifuta damu, akasema kwa hasira tena kwa sauti :
“Sheria ya kijiji chetu ni marufuku
mwanaume kuoa au kuwa na mahusiano na mwanamke mwenye mtoto tunahesabia kama laana kama mnakumbuka mwaka 2018.hakukuwa na mvua mwaka mzima njaa ilikuwa kali tulipoenda kwenye mizimu chanzo ikaonekana yule kijana Eliasi alikuwa na mahusiano na mwanamke mwenye mtoto ikiwa mume wake bado yuko hai”
Wanakijiji waliendelea kunon’gona kana kwamba anachokisema Moses ni cha kweli . Moses aliendelea
” Leo tena huyu kijana wenu anataka awarudishe kule kule zama za 2018 mpo tayari?
” Hatupo tayari na tutamudhibu mtu yoypte ambae anakiuka miiko na tamaduni zetu” alisema mwanakijiji mmoja kwa hasira kali na wengine wakaunga mkono .
Hapo hapo kelele zilikuwa nyingi .Moses alicheka na kusema ” we taka taka muda wowote wanaweza wakakuuwa huwezi shindana na mimi nakuangalia tu. Lakini kwa kuwa umenunua ugomvi nitakuonyesha na utanijuwa vizuri na utajuwa kwanini watu husema ” mtu asiyenapesa sio mwenzako “
Kisha akapanda gari na kuondoka
wanakijiji walikuwa wanalalamika na kupiga kelele kuhusu Penzi langu na maria single mama . Wengi wakiogopa laani na mikosi kwenye kijiji
Mwenyekiti alisema ” leo tukekusamehe tukija kuwaona mkiwa pamoja tena katika mahusiano ambayo hatuyataki sio siri tutakuchoma moto sio utani na hatutanii”
Na wanakijiji wengine waliunga mkono suala hili na wakatawanyika kwa kuwa onyo washanipa. Nilimshika mkono Maria maana alikuwa anaonekana na hofu
mpaka nyumbani kwake . Tulimkita
benson kalala anakoroma tu nahisi sababu ni upweke tu….
“Maria samahani sana “
” Samahani ya nini tena ?
” Huenda nimekuharibia mood”
” Ulikuwa sahihi mtu hatakiwi kuvunja heshima sababu ya mali alizonazo lakini…’
” Lakini nini Maria au hujapenda “
“Nimependa sana na umeonyesha unanijali na kunipenda tatizo ni wanakijiji “
” Wanakijiji wakina nani Maria “
” Nachoangalia ni maisha yetu watakuua “
” Hapana hawawezi nataka nitoe dhana
ya kuwa ukiwa single mother kuwa s na mpenzi ni laana”
” Mi naona tuachane tu ili uwe mzima niwe mzima “
” Pumzika nadhani umechoka lakini shikilia hili mimi kuacha na wewe haitowezekana ” niliongea kwa hasira kosha nikatoka kwake
Njiani nilikuwa nawaza sana …….
Lakini Moses akiwa kwenye gari na Natasha
” Natasha unataka nimfanyaje yule maskini jeuri”
” Mpenzi huyo kwa kukudhalilisha
anachohitaji ni nini? Zaidi ya kifo ? We muue tu hafu tumtupilie mbali ” kisha Natasha akacheka ..
Moses akamwambia dereva niandalie Vijana wanne wenye nguvu nataka wamteke huyu kijana maskini jeuri …
” Sawa bossi” Aliitikia dereva