PENZI LA SINGLE MAMA
UTANGULIZI
Kwa majina naiwa Goodluck “Katika maisha yangu, sikuwahi kuwaza kuwa siku moja ningependa mwanamke mwenye mtoto. Nilidhani mapenzi ni kati ya vijana wawili waliopitia chuo au waliokutana mjini au kijijini, na
siyo mwanamke mwenye mtoto niliamini kuoa mwanamke mwenye mtoto ni
sawasawa kuanza mechi matokeo yakiwa
1 bila on the score board . Sio mimi hata kijiji chetu cha kiberege kilipinga suala hilo ….
kijiji chetu kilichozungukwa na milima ya Uluguru, ndipo moyo wangu ulipoandika hadithi yake mpya hadithi ya upendo isiyo na mipaka. Kati yangu na mwanamke mmoja kwa jina la Maria
…….ambaye alikuwa na mtoto mmoja wa miaka minne jina lake ni benson karibu uungane na hiki kisa ….
SEHEMU YA KWANZA
Nilikuwa nimerejea kijijini kutoka chuo
kikuu baada ya kuhitimu kozi ya ualimu katika chuo cha Udom. baada ya miaka i mitatu ya masomo . Siku hiyo
jioni, nilifika nikapokelewa vizuri na wazazi hata majirani, ilikuwa kama kuna sherehe yaani kijiji chetu ww acha
tu wana upendo sana ….
“karibu sana mwanangu ,tulikukumbuka sana yaani baba yako haipiti siku hajakutaja ujuwe”alisema mama
” mmmmh ! Hata mimi niliwakumbuka wazazi wangu kwa kazi ngumu mlizofanya kama vibarua usiku na mchana ili nisome na sasa nimemaliza’
Wazazi wangu walinikumbatia,wakiendea kushangilia ushindi wa kijana wao waliousubiri kwa muda mrefu sana . Basi siku hiyo walijichangachanga wakanunua nyama . Yaani ujuwe
wazazi wanatupenda sana wapo tayari wajinyime wateseke ili tu kutupa furaha …
Na hii ndo sababu nawapenda sana wazazi wangu yaani wao ni maisha yangu niambie vyote ila sio kibaya kuhusu wazazi wangu kuna muda nilikuwa mpaka nalia nikikumbuka wanavyopambana kwenye vibarua ili nisome ….
Baba yangu alikuwa hanunuwi hata
suruali ilimradi mimi nisome mara ashone iliyotoboka yenye kiraka anaongeza kiraka yaani afu nimdharau hata dunia itanihukumu sana . Mama naye hivo hivo kila siku kitenge hicho hicho ili tu mi nisome . Kila siku wanakula ugali na maharage na majani ya kunde .
Walikuwa wakisema nyama watakula siku nikimaliza masomo yangu . Hivyo nilijiona nina deni kubwa sana kwao . Kuanzia shule ya msingi nilikuwa nsoma kama mtumwa mpaka nimemaliza chuo .
Nmshukuru sana mungu.
Tuendelee ……
Basi siku hiyo siku jua walifanya kibarua kwa muda mrefu .wakapata hela na siku hiyo walinichinjia mbuzi yaani tulikula na kusaza lakini nilijuwa ugumu walioutumia kunifanyia ili mradi tu niwe na furaha
Nilikuwa natokwa mpaka machozi jamani nikimtazama baba nikimtazama mama na marafiki zao wanacheka lakini najua wanachopitia moyoni mwao…
Mmoja wa marafiki zangu kwa jina
la maiko .alliwambia wazazi na watu wengine kuwa leo nina jambo la kusema japo sikuwa nalo …
Nilisimama mbele na kusema ,” nashukuru wote mliokuja kwenye hafla fupi . Hii imeonyesha jinsi gani mnaupendo na ni majirani wema kwangu na hata kwa familia yangu….
Lakini shukrani ziende kwa mama na baba sio kwa jili ya sherehe hii tu pia kwa ajili ya upendo wao na jitihada zao mpkaa mimi kumaliza chuo na kuhitimu masomo yangu . Nilielezea kila kitu kuhusu wao hakuna mtu ambaye hakutokwa na machozi hata baba mwenyewe na hata mama pia …….
Basi mwishowe nilipomaliza walinipigia
makofi wakunipa zawadi walinipa na wakunipongeza walinipongeza nilihisi furaha na amani na siku hiyo ilipita na maisha yakaendelea
Mwezi mmoja baadaye …………..
Niliamka asubuhi na mapema na kuanza kufagia uwanja, nikaenda mtoni kuchota maji njiani nilikuwa nasalimiana na watu kama iliyodesturi ya kijiji chetu
cha kiberege ……
Nilitembea kuelekea mtono huku nikisikiliza nyimbo za wasanii mbalimbali na ndo kitu nachokipenda .Nilipofika
mtoni nilitoa kibakuri changu na kuanza
kujaza maji huku napiga winjaaaaaaa.. Mluziiiiiiiiiiiiiiiiiii………….
Mara nikasikia sauti nyuma yangu ” habari za asubuhi kaka “
Nilijibu huku nageuka ” salama za kwako dada?”
” mmmh namshukuru mungu niko salama “
‘ sura ngeni kama sijawahi kukuona hivi”
” mbona mi nipo tu kakanguh wewe sura yako ndo ngeni”
“nilikuwa chuo nimemaliza sio muda ” ” hongera zako kwa kusoma “
” hongera tumpe mungu maana si kwa
uwezo wangu”
” mmmmh jaman hongera “
Nilisogeza ndoo yangu pembeni na kumchotea yeye pia …..
Aliniomba nimtishwe nami sikuwa na hiyana ile namuwekea kichwani alipepesuka kidogo nikajua anataka kuanguka nikamshika kiuno sura zetu zimesogeleana karibu tunatazamani hafu maji kidogo yakanimwagikia usoni
Tulibaki tumeganda kama sanamu
Mkono wangu kiunoni kwake macho yetu
yanatazamana.
UNADHANI NINI KITATOKEA, ENDELEA NA SEHEMU YA PILI
SEHEMU YA PILI
TULIPOISHIA ….
Aliniomba nimtishwe nami sikuwa na hiyana ile namuwekea kichwani alipepesuka kidogo nikajua anataka kuanguka nikamshika kiuno sura zetu zimesogeleana karibu tunatazamani hafu maji kidogo yakanimwagikia usoni
Tulibaki tumeganda kama sanamu
Mkono wangu kiunoni kwake macho yetu
yanatazamana
************
Endelea na sehemu ya pili ……
Tulibaki tukiangaliana, mapigo ya moyo yakiwa yanakwenda mbio. Ilikuwa kama muda umesimama, upepo , sauti za ndege zilikiwa zinasikika , yaani kam.a wanatushuhudia Mikono yangu bado ilikuwa kiunoni kwake, maji yakinimwagika usoni na nguo zangu na hata zake zilikuwa zinalowa tu kwa matone madogo dogo yaliyodondoka kutoka kwenye ndoo. hakuna aliyekuwa na haraka ya kuondoka.
Nilipomtazama Machoni mwake kulikuwa na kitu cha kipekee. Si uzuri tu, bali hata namna alivyonitazama ilikuwa ya kuvutia japo iliambatana na uoga. Nilitazama kwenye koromeo lake alionekana kumeza mate kwa shida sana. Licha ya hivyo hakuacha kunitazam wala kupepesa machoni ukimtazama macho, lipsi daah kweli ni mrembo ….
Mwisho akili zilirudi, kama umeme baada ya giza la muda mrefu. Mara zote tukajikuta Ghafla wote tuliinamisha vichwa kwa aibu kana mtoto mdogo akikamatwa na pipi mfukoni. Akasema
kwa sauti ya taratibu na macho ya ajabu,
“Mimi naenda.”
Alijigeuza na kuanza kuondoka, miguu yake ikikanyaga maji na nyasi za pale kisimani pembeni vipepeo na wadudu waliokuwa karibu na alipopita nao wariluka. Niliangalia mgongo wake, gauni lake jeupe likishuka kwenye nyonga taratibu . Kabla hajafika mbali, nikajikuta namuita bila kupenda, “Dada… naweza nikalijua jina lako?”
Akasimama, akaangalia nyuma polepole. Macho yake yakakutana na yangu kwa mara nyingine, safari hii yakiwa ya
kawaida zaidi. “Naitwa Maria,” akasema
kwa sauti laini . “Wewe je, unaitwa nani?”
Nikajibu huku nikijikaza kutotetemeka, “Naitwa Goodluck.”
Akatabasamu, tabasamu la mtu aliyefurahishwa lakini hakutaka kuonyesha zaidi. Kisha akageuka na kuondoka kwa hatua za upole. Macho yangu yalimbeba hadi alipopotelea kwenye matawi ya migomba.
Nikabaki nimesimama pale mtoni, nikijisemea kwa sauti ya ndani, “Mambo gani haya asubuhi asubuhi? Na huyu
?”huku najitwisha ndooo nakuelekea
nyumbani
Nilirudi nyumbani nikiwa bado nimechanganyikiwa, akili ikiwa haiko sawa. Kila hatua niliyopiga kuelekea nyumbani ilikuwa kama najivuta kutoka kwenye ndoto niliyotamani isishe.
Nilipofika, nikaweka ndoo ya maji pembeni na kuingia jikoni. Nikaanza kuosha vyombo lakini mikono haikutii, ilikuwani kama mtu aliyepotelea kwenye giza zito .
Niliendelea na kazi lakini kumbukumbu za pale mtoni hazikuniacha. Nilipomshika
kiuno, macho yetu yalipotazamana,
majibu aliyonipa, tabasamu lake, hata jina lake Maria kila kitu kilirudi kichwani mara kwa mara. Nilikuwa naosha vyombo lakini akili iko mbali , mpaka mama aliniona kama nimechanganyikiwa.
“Mwanangu! Goodluck! Una nini?” Sikuitika.
“Goodluck!”
Bado nilikuwa kimya.
Mara ya tatu, sauti ya mama ikawa ya juu
zaidi, “GOODLUCK!!”
Nikastuka kana kwamba nimetolewa ndotoni. “Naam mama!”
“Hebu chukua hii hela nenda kwa Mangi kamlipe deni lake ”
“Sawa mama.”
Nilichukua pesa nikaelekea dukani kwa haraka, lakini hata barabarani, mawazo hayakuwa kwa Mangi wala deni. Akili yangu.ilikuwa ikilikumbuka hasa lile tukio la ukaribu wetu ….
Nilitembea mpaka nilipofika dukani kwa mangi palikuwa na foleni ikanibidi nisubiri kidogo angalau wapunguwe
Dakika chache baadaye walipungua na ikawa ni zamu yangu
‘ mangi habati za asubuhi?” “salama sijuwi hali yako wewe”
” niko salama mama kasema nije kulipa deni”
” okay vizuri,kijana umemaliza chuo ” ” ndiyo nimemaliza nina mwezi sasa ” ” hongera pia karibu”
“asante mangi “
Mara ghafla tukiwa tunaendelea kuongea
mara ghafla akaja mtoto mdogo
” Mangi shikamoo, anko shikamoo “
” marahaba , tulimjibu na mangi akawa anamsikiliza
” kanituma mama kasema anaomba sukari viwili na viberiti robo “
Nilicheka maana mtoto kayachanganya maagizo badala ya sukari robo na viberiti viwili kayakoroga mambo.Niliinama na kumshika mashavu na kumvuta vuta kiutani
” sukari robo na viberiti viwili sio vibeeiti robo na sukari viwili”
Katoto kalicheka kakasema ” asante sana
uncle “
” nimekwambiya siku nyingine usemaje?” nilimuuliza
” niseme sukari robo na viberiti viwili”
Nilipigia makofi na kumwambia mangi ” mpe pipi na biscut” kisha nikatoa elfu moja na kumkabidhi mangi
” Asante sana Uncle ,mi naenda “
Aliondoka na kutuacha mimi na mangi dukani yeye akaenda zake huku akikenua si unajua watoto mambo yao .Basi nami nilimuaga mangi na kuondoka pale dukani.
Mtoto alikula kona mwishowe akatokea
kwenye nyumba ya kupanga ambapo mama yake alikuwa yupo ndani anaweka mkaa kwenye jiko la mkaa. Mtoto akaanza kusema
” mama leo nimekutana na uncle mpya “
Mama akiwa ndani hata sura hakuonekana
” Uncle gani tena mwanangu ” ” hata mimi simjuwi “
” kuwa makini wengine wanachinja watoto”
” mmmh mama yule ni uncle mzuri” ” kaninunulia biscut na pipi kijiti”
” mmmmh uache kuomba omba “
“hapana mimi sikumuomba alinipa mwenyewe kwa sababu nilipatia kitu alichonifundisha “
” alikufundiaha nini mwanangu?”
” kusema sukari robo na viberiti viwili” ” khii sasa si ndo nilivyokuagiza ?”
” nilichanganya mama “
” uliasemaje?” aliuliza mama yake kisha akatoka nje
HUWEZI AMINI MWANAMKE YULE NI MARIA NA NDO MAMA WA YULE MTOTO
SEHEMU YA TATU
TULIPOISHIA…
“Ulisemaje?” aliuliza mama yake kisha akatoka nje.
HUWEZI AMINI, MWANAMKE YULE NI MARIA NA NDO MAMA WA YULE MTOTO.
************” ENDELEA SASA….
” mama nilisema viberiti robo na unga viwili”
Maria alicheka sana na kusema ” ama kweli mwanangu we bado ni mdogo”
Kakanuna” mama mi mbona mkubwa “
” haya sawa mwanangu wewe ni mkubwa haya sogea unawe uso ( mama
akamuosha mwanae uso kisha akaingia
ndani na kuchukua taulo. Kisha akamfuta)
” mwanangu sasa umependeza “. Mara ghafla tumbo likaunguruma wote wakacheka ….
Maria alipomtazama mwanaye, alitabasamu kwa mbali, kisha akamwambia, “Sawa mwanangu, ingia ndani ukakae sebuleni, mama anakutengenezea chai.”
Mtoto akasema kwa furaha, “Asante mama!” kisha akakimbia ndani kwa mikogo ya kitoto, huku akiwa ameshika pipi yake kijiti na biscuit yake kwa furaha.
Wakati hayo yakitokea kwa Maria, upande wangu nilirudi nyumbani na kukuta
wazazi wangu tayari walishatoka kuelekea shambani. Waliniachia chai mezani, nikanywa harakaharaka huku mawazo yangu ni kuwahi kwenda shamba.
Sikufichi msomaji najihisi nina deni kubwa kwa baba na mama . Hasa walivyopambana kunisomesha mpaka leo ndo maana kila kazi nipo.Angalau nipunguze deni kijana mwenzangu tusiwadharau wazazi wetu hao ndio
sababu ya leo kufika hapo. Huwezi jua
wamejinyima vingapi kwa ajili yako ? Waamefanya mangapi mpaka leo una furaha ??
Tuendelee……..
Baada ya kumaliza, nilifunga safari kuelekea shambani tulikokuwa tunapalilia migomba ya ndizi. Kazi haikuwa nyepesi, jua lilikuwa linachoma na ardhi ilikuwa ngumu. Tulifanya kazi kwa bidii hadi majira ya jioni, ambapo wazazi walitangulia kurudi nyumbani.
Mimi nilichelewa kidogo kwa sababu nilikuwa bado naongea na baadhi ya vijana pale kijijini, tukijadili maisha, kazi, na ndoto.
” mwangu wewe ndo
unaonyesha uhalisia wa mwanaume” ” kwanini jamaa yangu” muda huo
naliweka vizuri mgongoni na kumsikiliza
“vijana wachache waliosoma wanafanya kazi hizi .wengi wanalingia Elimu yao hata kuongea nao ni kazi tofauti na wewe ni mcheshi na unazungumza na kila mtu”
” Elimu ni ujuzi na kuna tofauti kati ya elimu ya darasani na elimu ya maisha ya darasani ninayo sasa najifunza na ya maisha naamini nitafanikiwa “
” daah we ni watofauti rafiki yangu.Ndo maana watu wengi wanakupenda hapa kijini”
Basi tulionge a mengi lakini lengo langu ni kumtolea ile dhana kuwa mtu kuwa msomi ndo kamaliza kila kitu.safari bado inaendelea tuliagana kisha kila mtu akaondoka zake …
Wakati narudi nyumbani kupitia mitaa ya sokoni, macho yangu yakakutana na sura nisiyoisahau kirahisi Maria. Alikuwa kando ya barabara, amejipanga vizuri, akiuza mboga za majani. Kando yake kulikuwa na gunia la mboga, na meza ndogo iliyojaa nyanya, hoho, na vitunguu.
Sikujizuia, nilijikuta nimesimama na
kutazama. Alikuwa amejifunga kanga ya rangi ya zambarau iliyojaa maua meupe, alijiremba kwa kawaida tu, lakini bado alionekana mrembo mno.
Alipokuwa akiwahudumia wateja, mara kwa mara alijifuta jasho kwa kitambaa kidogo, na kila alipotabasamu, moyo wangu ulijawa na furaha isiyoelezeka.
Nilifurahi kumuona akiwa na bidii, akiwa mwanamke mwenye juhudi, aliyekuwa tofauti na picha niliyokuwa nayo awali ya mwanamke wa kisimani.
Nilijikuta nikimtazama sana, nikifurahia
kila tendo lake. Hata nilipogundua kuwa tayari giza linaingia, sikuona muda ukisogea. Nilishtuka sana, nilipopiga jicho juu na kuona anga limeanza kuwa rangi nyeusi yaani giza hilo apo
Huku sauti za chura zikisikika kroooh kroooh !!! Kroooh ! Kroooh…
Nilianza kukimbia kuelekea nyumbani.Nilisahau hata kwenda kumsalimia mbio mbio kiguu na njia mpaka nyumbani..
Niliofika nyumbani nilimkuta mama anataka alushe nguruwe nilimwambia “
mama acha mimi si nipo nenda kakae
huku hizi ni kazi zangu”
” sawa mwanangu”. Alinipisha na kukaa nyuma yangu akinipigisha stori kidogo..
Muda huo baba kaenda kijiweni kucheza bao na kubishana simba na yanga yaani baba yangu na yanga utamwambia nini na kweli hata mtaa wanamjuwa Mzee mlowe kwa ubishi hasa lwa atakayeisema vibaya Yanga .
Basi mimi na mama tuliendelea na kazi nilimsaidia kupika na kuosha vyombo na ndio kazi yangu nina deni kubwa yaani kila
nachokifanya najiona ndo kwanza
mambo bado…..
Basi mzee alirudi amechoka akala kisha akaenda zake kulala na mimi muda huo niko zangu bize. Nikaingia chumbani na kumwomba mola anilinde wakati wa usiku kisha nikakakaa kitandani.
Mawazo yakahamia kwa Maria nikikumbuka toka tulipokutana hadi nilipomuona sokoni. Mawazi yalinipeleka mbali sana nikajikuta
natabasamu mwenyewe .nakuangukia mgongo mikono ya nimeiweks kichwani mwangu.
Nikasema ” inakuaje namuwaza mtu ambaye anaweza akawa haniwazi .lakini kumbe upande wa pili kwa maria alijisemea ” yule kaka kunishika kiuno maana yake nini kama sio ukorofi ???
1 Comment
Pingback: Penzi la Single Mama – Full Story - Raha Special