PENZI LA KIKOMANDO
EPISODE 13
TULIISHIA
“Babaaaaaa”
“Mwanangu hawajakuumiza? . …”
ENDELEA….
“nipo salama baba …”alijibu wonder akiwa ameshikiliwa na Aboku.
“Haya naombeni mnipe binti yangu haraka lasivyo nitamchukua kinguvu…” General aliongea kwa kujiamini akiwa bado yupo chini ya ulinzi yeye na Askari wake .
“Rafiki yangu kipenzi, ukweli nilikuita huku ili ushuhudie kifo cha binti yako uone ni jinsi gani inauma kumpoteza mtu umpendaye …” Aliongea Ram akiwa anatoa bastora yake ndogo kiunoni .
“Acha ujinga gaidi wewe…” Aliongea Ramos kwa ukali alipoiona bastora lakini Ram taratibu alikuwa akisogea alipo wonder.
Ramos aliona ni wakati sahihi wa kuwaamuru wale Askari aliowaacha nje waanze kushambulia maana binti yake yupo hatarini. Lakini kabla hajatoa tamko lolote sauti za risasi zilianza kusikika nje alipowaacha Askari wake.
“Ram umefanya nini gaidi wewe? …” Aliuliza General kwa jazba baada ya kuanza kusikia kelele za risasi nje alipowaacha Askari wake .
“Hahaha Rafiki yangu tuliishi pamoja miaka ya nyuma kwa hiyo mimi nakujua vizuri sana ulidhani utaniweka mtegoni kwa kuwaambia askari wako wazunguke kambi yangu hahaha…” Ram aliongea akiwa anacheka na geti la kuingilia ndani ya kambi likiwa linafungwa
“We gaidi Umewafanyia nini Askari wangu wa nje..”
“Nilituma kikosi changu kiwazunguke Askari wako kwa nyuma, mda sio mrefu tutajua ni nani mshindi kati ya mimi na wewe..”
Ram aliongea kwa kujiamini akiwa anamgusagusa Wonder kwa bastora, milio ya risasi iliendelea kusikika kwa wingi nje askari wa General Ramos wakipigana na waasi wa Ram.
General Ramos anapatwa na hasira kali alipogundua mpango wake umeferi ndipo anatoa bastora yake haraka na kuanza kuwashambuliwa wale waasi waliokuwa wamemzunguka.
“Shambulieni kwa nguvu…” General Ramos aliwaambia wale Askari wachache aliokuwa nao wote wakaanza kufyatua risasi.
“Rafiki yangu punguza hasira unajua kama nipo na binti yako hapa?.. “ aliongea Ram akiwa amejibana kwenye pipa kubwa na wonder.
General Ramos aliendelea kuwafyatulia watu wa Ram risasi kwa hasira akiwa na askari.
Waasi hawakutaka kurudisha mashambulizi kwa general badara yake walikuwa wamejibana kwenye machuma makubwa wakisubiri amri ya kiongozi .
“ Aboku mnasubiri nini anzeni kushambulia sasa ..”
Ram alitoa amri akiwa pembeni ya pipa na wonder.
Waasi walianza kujibu mashambulizi kwa kasi baada ya kupata ruhusa kwa Ram haikuchukua mda mwingi utulivu unatawala eneo lote.
General Ramos anajikuta amebaki pekeyake askari wake wote wakiwa wamekufa wengine ni majeruhi wasioweza hata kusimama.
General anajaribu kufyatua risasi anastaajabu kuona Bastora yake ikiwa haina risasi hata moja.
“Haiwezekani waasi wajinga nyie lazima mtakufa na huyo kiongozi wenu….” Aliongea general Ramos kwa kutetemeka waasi wote wakiwa wanajitokeza sehemu walizokuwa wamejibanza .
“Hahahaha ulifikiria nini kuanza kutufyatulia sisi risasi, ulidhani ungeweza kutoka hapa!, Ona omebaki mwenyewe hahahaha.”.. aliongea Ram akiangua kicheko akiwa anajitokeza amemshika wonder.
Geti la kuingilia lilifunguliwa wote waligeuza macho kutazama ni nani aliyeshinda vita vya nje. Mala wanaonekana watu wa Ram wakiingia ndani wakiwa wamechafukwa damu za askari wa general Ramos .
“Hahaha, ona umeshindwa kote Rafiki, yani ndani umeferi na nje umeferi alafu unajiita general wa nchi.” Ram alicheka.
“Tafadhari Naomba uniache niondoke na binti yangu hiyo gold key baki nayo tu…” Aliongea general Ramos kwa huruma sana alipoona jeshi lote limeuliwa.
“Hapana Rafiki hii gold key uliichukua kutoka kwangu miaka kumi iliyopita kwa hiyo hii ni Mali yangu….” Aliongea ram akiwa amemuacha wonder kwa Aboku, yeye akimsogelea Ramos na gold key mkononi.
“Naomba tusahau kuhusu yote yaliyopita miaka ya nyuma…”aliongea Ramos alipoona Ram anasogea
“Wewe utasahau lakini Mimi siwezi sahau ile siku uliyotaka kuniuwa sababu ya tamaa zako na kunisambazia uchafu mjini mpaka leo watu wote mpaka watoto wadogo wanajua kuwa mimi nilikuwa ni msaliti wa nchi yangu…” Ram aliongea kwa uchungu sana .
“Baba ni kweli haya anayoyasema?. , ulifanya huo ukatili ili uwe general wa nchi, haya sio ya kweli baba si ndio? ….” Alionga wonder kwa mshangao akiwa ameshikwa na Aboku aliposika yale maneno ya Ram .
General Ramos hakujibu chochote kwa binti yake badala yake alitazama chini kwa aibu.
“Binti nimeishi huku milimani miaka mingi kwa sababu ya baba yako lakini leo ni mwisho wa yote nitakamilisha kisasi changu hapa, wewe na baba yako mtakufa.”..
“Mimi ndo ninahiyo zambi na wala sio huyo binti, muache aende, jaribu kuwa na huruma hata kidogo..” General Ramos aliongea kwa upole akiwa ananyoosha mikono juu.
“Ngoja nikuonyeshe kama sina huruma … “ Aliongea Ram haraka na kugeuka nyuma alipo kuwa Wonder Kisha akamnyoshea bastora akitaka kufyatua risasi.
Mala ghafla kuna mtu anaingia langoni akiwaa amevalia maski nyeusi mwili wake ukiwa umevaa magwanda ya vita mgongoni akiwa na siraha nzito mkononi akiwa na mashine bomba kubwa lililotoa risasi kama maji zilizoenda moja kwa moja kuwachakaza waasi .
Ram akiwa anageuka kushangaa mala ni nani mala anapigwa risasi ya mkono na kujikuta anaangusha bastora aliyokuwa ameshika mkononi.
Kila Muasi anatafuta chocho yake ya kujificha kulinda uhai wake , Aboku anajikuta anamuachia wonder bila kujua na kuangaika kulinda maisha ya bosi wake Ram. Wonder anakimbia kwa kuinama mpaka sehemu aliyojibanza baba yake.
General Ramos taratibu anaanza kutabasam akijua tayari wameshapata msaada wakati huo mvua ya risasi ikiendelea kunyesha eneo hilo waasi wakiangushwa chini kama vifaranga .
INAENDELEA……..
Ni nani huyo ???????
🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
General Ramos atasalimika pale na binti yake?
🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
PENZI LA KIKOMANDO
EPISODE 14
TULIISHIA….
Mtu aliyevalia maski anajitikeza pale na kutoa msaada kwa General Ramos na binti yake. General Ramos anajibana kwenye kona na kutabasam baada ya kuona amepata msaada,
Wonder anaachiwa na Aboku moja kwa moja anaenda sehemu aliyojibana baba yake .
Mvua ya risasi ikiendelea kunyesha eneo hilo kati ya mtu aliyevaa maski na waasi.
ENDELEA…..
“Mwanangu usihofu tutatoka hapa salama..” Aliongea general Ramos akiwa amejibanza kwenye kwenye kona na wonder.
“Nakuchukia sana baba, ivi uliwezaje kumfanyia ukatili yule Rafiki yako ?..” Aliongea wonder kwa hasira milio ya Risasi ikiendelea kusikika kwa wingi eneo hilo.
“Sahau kuhusu maneno aliyo ongea yule gaidi, nia yake ilikuwa ni kutugombanisha tu …”
General Ramos akiwa bado anaendelea kuongea na binti yake kwenye ile kona mala yule mtu aliyekuwa akipambana na waasi anawaita kwa mbali.
“ General mchukue binti yako tuondoke hapa haraka…” Aliita kwa sauti akiwa anaendelea kuwafyatulia risasi waasi.
“Kijana tukitoka hapa tunaweza tukashambuliwa kirahisi …” Aliongea general kwa sauti ya juu akiwa bado amejibana kwenye kona na wonder.
“Tokeni haraka mi nitawalinda …” Aliongea yule mtu mwenye maski kwa sauti kali akiwa mbali kidogo na ile sehemu aliyojibana general.
General Ramos alimshika wonder mkono na kuanza kukimbia nae kuelekea alipo yule mtu aliyevaa maski nyeusi. Mtu yule aliwalinda mpaka wanafika eneo alilosimama yeye
“Haya tokeni nje ya geti haraka mkimbie ..”
“Vipi kuhusu wewe lakini? Tukimbie wote?…” aliuliza wonder kwa hofu.
“Acha ujinga amesema tuondoke yeye atabaki kupambana nao…” General anaamvuta wonder na kutoka nae nje ya geti kuu.
Mtu aliyevaa maski anaendela kupambana vikali na waasi, taratibu akaanza kurudi nyuma ili akimbie.
“Hakikisheni hamumuachi huyo ameuwa wenzetu wengi…” Aliongea Ram kwa hasiraalipoona yule mtu anatoka nje ya geti akiwa chini anauguza mkono wake aliopigwa risasi na mvaa maski.
Waasi waliosalia wanatoka sehemu walizokuwa wamejificha na kuanza kumfukuzia yule mvaa maski
“Bosi we rudi ndani hali yako sio nzuri, tuachie sisi hii kazi tutaikamilisha …” Aboku aliongea kwa heshima alipoona Ram anaongozana na waasi wengine kumkimbiza mvaa maski pamoja na general Ramos.
“Usinipangie nini cha kufanya wewe..”Aliongea kwa hasira akiwa anakimbia mkono wake ukiwa unavuja damu.
“Samahani kiongozi kama nimekukosea…”aliongea Aboku
“Acha ujinga wako ebu ongezeni kasi wasije wakatupotea…”
Waasi wote wakiongozwa na Ram waliingia kwenye msitu mkubwa uliokuwa ndani ya mlima wakimsaka general na mvaa maski.
General Ramos na wonder walikimbia umbali mrefu kidogo lakini wonder alionekana kuchoka sana.
“Baba tunaweza tukapumzika sasa…” Aliongea wonder akiwa anapunguza kasi akipumua kwa nguvu sana.
“Sawa binti twende tukakae pale kwenye mti…”
“Mrembo hawajakuumiza …” Ilikuwa ni sauti iliyotekea nyuma yao, wote waligeuka na kumuona yule mtu aliyevaa maski akiwa ameshika mitutu mkononi.
Yule mtu alisogea mpaka pale kwenye mti alipokuwa general na wonder..
“Asante sana kijana yani umefanya jambo kubwa sana kunisaidia Mimi na binti yangu. Unaweza ukatoa hicho kinyago chako nikuone shujaa…” Aliongea general akiwa amekaa.
“Hapana siwezi …” Alijibu akiwa amesimama.
“Lakini sauti yako sio ngeni kwenye masikio yangu …”
“ Hata mimi baba hii sauti Ni kama nimewai kuisikia….”Wonder aliongea baada ya baba yake kumaliza kuongea.
Mvaa maski hakuona haja ya kuendelea kuficha sura yake, alishika maski usoni kwa mkono wake wa kulia na kuitoa.
“Woow!, Afande kijana kumbe hujafa !..” aliongea Wonder kwa furaha alipogundua mvaa maski ni James.
“Nimekuja kukusaidia mala ya pili mrembo sababu mwanzo nilishindwa kufanya hivyo….”
Aliongea James akiwa anamtazama Wonder kwa tabasam
“Aaaa kaptain James ndio maana nilikuchagua uongoze kikosi kwa sababu wewe ni Askari shupavu sana hahaha, tukifanikiwa kurudi salama nitakukupandisha cheo Askari wangu.. “
Aliongea general Ramos akiwa anatabasamu lakini James alimtazama general kwa hasira sana.
“Inukeni tuondoke huku milimani maana tut……”
Aliongea James kabla hata ajamaliza kuongea kundi la waasi lilitokea nyuma yao na kuanza kufyatua Risasi kama mvua.
“Kimbieniiiiiii, chukueni na hii pisto itawasaidia mbele…”
Aliongea James akimpa General pisto kisha yeye anavuta mtutu kutoka mgongoni na kuanza kushambulia.
General anaanza kukimbia na wonder wakiwa wamemuacha James nyuma.
James anatoa mtutu mwingine mgongoni baada ya kuona waasi wanaanza kumzidi na kufanya idadi ya mitutu mkononi mwake kuwa miwili yenye uzito mkubwa na kuendelea kushambulia kwa kasi.
Umaridadi na uzoefu wa kupambana wa james unamsaidia kuwaangusha waasi wengi.
Ram na Aboku wanafika pale wanakuta vita bado ni kali waasi wengi wakiwa wameuwawa wamesalia waasi watano tu ndo waliosalia wakiwa wanaendelea kupambana na James.
“Bosi huyu jamaa anatuzidi nguvu…” Aliongea muasi mmoja baada ya kumuona Ram akiendelea kushambulia.
“Wajinga nyie mnashindwa na mtu mmoja ….” Aliongea Ram kwa hasira na kuchukua silaha ya Aboku Kisha anaweka target kwa James aliyekuwa amejibana kwenye mti.
James anatoka kwenye ule mti na kuendelea kushambulia kwa kasi bila kujua yupo kwenye target ya Ram. Haikuchukua mda mrefu Ram alimshuti James kifuani eneo lile ambalo alipigwa risasi awali na Aboku.
Taratibu James alikosa nguvu na kuanguka chini damu nyingi zikimtoka.
“Haya twendeni tumkamate general kabla hajafika mbali…” Aliongea Ram na kuanza kukimbia baada ya kumuangushaJames.
Ram, Aboku pamoja na waasi watano wa waliendelea kukimbia kuelekea mbele alipo general na wonder.
Baada ya mda mchache Ram anafanikiwa kumuona general mbali kidogo na alipokuwa.
“Baba ona wanatukaribia! ….”aliongea wonder kwa pressure akiwa anatazama nyuma.
“Bora yule kijana kanipunguzia idadi, Hawa waliosalia naweza nikawamudu we endelea kukimbia, mi….” General aliongea kabla hajamaliza hapohapo Wonder alipigwa risasi ya mguu na kuanguka chini.
General Ramos alitoa pisto aliyopewa na James, anageuka nyuma kwa hasira na kuanza kuwashambulia waasi akipiga kelele.
“Haaaaaaaa kufeni mbwa nyie…” zilisikika risasi tu mda huo.
Kwa umahiri wa general Ramos anafanikiwa kuwaangusha waasi watano na pisto yake inaisha risasi . Ram na Aboku walisalia pekeyao baada ya kuona ukimya wanasogea mpaka alipo general Ramos.
“Hahaha hatimaye wewe na maski mmefanikiwa kuniulia watu wangu wengi lakini tayari mwenzako ameshakufa..” Ram aliongea kwa kucheka akiwa anamkaribia Ramos pembeni kidogo akiwa wonder amelala chini mguu wake ukitiririka damu.
Ram alimuangalia General kwa hasira kali Kisha anamuangalia wonder akiwa yupo chini anamkaribia na kuelekeza bunduki pale chini akitaka kumuuwa wonder bila huruma
Kabla ajashuti
“Achaaaaaaaa …….” Maria alitokea vichakani akiwa anahema kwa nguvu wote wote walitaharuki baada ya kumuona.
INAENDELEA……
Maria huyo katokea msituni sasa Mambo sijui yatakuwaje?!!!!! …ndo hivyo maria kakutana na Ram baada ya miaka mingi akiamini Ram alikufa kibaya/kizuri Wonder ni mtoto wa Ram itakuwaje hapo ukweli ukifahamika?…. 🔥🔥
R.I.P super soldier / Afande kijana
PENZI LA KIKOMANDO
EPISODE 15
TULIISHIA…..
Ram anamuweka target wonder akitaka kumshuti ghafla sauti ya mwanamke isikika
“Achaaaaa ….” Alikuwa ni Maria aliongea kwa sauti ya kubwa akiwa anapumua kwa nguvu
ENDELEA…….
“unataka kumuuwa binti yako unaakili vizuri wewe …” Aliongea Maria kwa hasira wote walibaki wameduaha wakimtazama Maria.
“Binti yangu?, Huyu sio binti yangu ni binti yenu nyie wasaliti wawili…” Aliongea Ram akipuuza maneno ya Maria na kuendelea kumnyooshea Wonder siraha.
“Hapana huyo binti ni wako Ram, mala ya mwisho kabla hujaenda kwenye vita ya SK tulilala pamoja umesahau na hilo?…” Maria aliongea kwa hasira sana akisogea alipokuwa Ram General Ramos akabaki ameduaha kama aamini kitu alichosikia.
Ram alirudisha kumbukumbu zake nyuma miaka ishirini iliyopita na kugundua ni kweli alilala mala ya mwisho na Maria.
Ram alikosa nguvu gafla na kujikuta akiangusha siraha yake chini.
“Huyu ni binti yangu si ndiyo Maria?…”aliuliza Ram akiwa anatabasam, wonder akiwa yupo chini ameshikwa jazba.
“Hapana huyo sio binti yako ni binti yangu Mimi…” Aliingilia general Ramos kwa hasira.
“Mtoto huyu ni wa Ram General Ramos samahani kwa kukuongopea miaka yote, na mwanangu wonder naomba unisamehe kwa kutokueleza ukweli kuhusu baba yako…” Aliongea Maria kwa upole.
Ram machozi ya furaha yalianza kumtoka baada ya kugundua Wonder ni binti yake taratibu alimkalibia wonder pale chini .
“Mwanangu kwa miaka mingi nimekuwa nikiishi milimani nikifanya ugaidi nikiamini sina familia, ndugu wala mtoto lakini kumbe damu yangu ipo kwenye hii dunia wewe ni binti yangu ety Mimi ni baba yako, naomba tu uniite baba hakika utanipunguzia maumivu na mateso niliyopitia miaka yote..” aliongea Ram kwa uchungu akiwa amemshika wonder begani.,
“Baba yangu, pole sana.. “ wonder aliongea akiwa analia Kisha akamkumbatia Ram.
Maria alikuwa pembeni kidogo akitabasam alipoona baba na binti yake wamekutana tena.
Mda huo Ram akiwa na amemkumbatia binti yake Ramos anapata nafasi ya kukimbia ile sehemu.
“ Aboku hakikisha unamkamata.”
Alitoa amri Ram baada ya kuona general anakimbia, aboku kwa kasi akaanza kumkimbiza general.
Mda mfupi badae Aboku anarudi akiwa amembeba juujuu general Ramos.
“Ram naomba umuache Ramos aende mi nilikuja hapa kuzuia usimuuwe binti yako basi, lakini siwezi kuona unaendeleza uwo ukatili wako…” Maria alimwambia Ramos kwa msisitizo.
“Maria unajua vitu alivyonifanyia huyu mmewako miaka ishirini iliyopita?..” Aliongea Ram akiwa anasimama pale alipokuwa na wonder na kuelekea alipo Maria.
“Alifanya vitu gani kama sio wewe mwenyewe uliamua kuwasaliti wenzio vitani na kushirikiana na SK…”Aliongea Maria haraka haraka akionekana kumchukia Ram.
“Mama general Ramos ndiye mwenye hatia na wala sio baba yangu…” Aliingilia Wonder.
“Kivipi mwanangu?…” Aliuliza Maria
“Nimesikia kwa masikio yangu leo general alikiri kuwa zamani alitaka kumuuwa baba sababu ya madaraka pia yeye ndiye aliyewageuka Askari wenzake na kuwauwa…” Wonder alimwambia mama yake kila kitu.
Baada ya Maria kuambiwa hivyo na wonder alimuangalia general Ramos kwa macho makali na kumuuliza.
“Ni kweli Ramos ulifanya yote hayo ….” Aliuliza Maria.
“Nisamehe mke wangu…”
“Usiniite mi mkeo tena shetani wewe umemsababishia mwenzio maisha magumu sababu ya pesa …” Maria aliongea kwa hasira sana general Ramos akiwa amekabwa na Aboku.
Ram alisogea mpaka alipo Ramos .
“Aboku muachie …”
“Sawa bosi ..” alijibu Aboku akiwa anamuachia General Ramos.
“Rafiki yangu kipenzi nakupa nafasi ya mwisho baada ya hapo sitakuwa tena na kisasi na wewe ….” Aliongea Ram akimuangalia Ramos usoni.
“Usiniuwe tafadhali niambie chochote nitafanya…” Aliongea general Ramos kwa woga.
“Leo leo nenda mjini ukawaambia watu wote dhambi zako ulisofanya miaka ishirini iliyopita pia nataka kila mtu ajue mimi sikuwahi kuisaliti nchi yangu, nadhani tumeelewana…”
“Hakuna shida nitafanya hivyo..”
Alijibu general Ramos kwa woga akiwa yupo chini.
“ sawa lakini nawaza nawezaje kukuamini tena we msaliti? Vipi kama utarudi na kuanza kukusanya nguvu tena badala ya kusema ukweli…”
“Siwezi kufanya hivyo niamini mimi Rafiki yangu, sitaki tena kuishi kwenye hii dhambi…” Aliongea General akionekana kujutia mambo yote aliyoyafanya.
“ Astahili hata kuishi huyo shetani…” Aliongea Maria alipoona Ram anataka kumuachia General.
“Tumpe nafasi ya pili kipenzi changu …” Aliongea Ram akiwa anamuangalia Maria usoni.
Maria alitabasam baada ya kusikia ameitwa kipenzi changu na Ram hisia zake zinampeleka mbali sana kipindi kile Ram anamtongoza akiwa anafanya kazi kwenye kile kituo cha watoto yatima.
“Maria mbona unatabasam..” aliuliza Ram akiwa na yeye anatabasam alipoona Maria kama Kuna kitu anawaza
“Nilikumbuka tu ile siku uliyokuwa unaogopa kusema kama unanipenda mpaka nikakusaidia Mimi hahaha”
Aliongea Maria akiwa anacheka taratibu mda huo General Ramos akiwa pembeni anaumia kuona penzi la Maria na Ramos kama linarudi tena hivi.
“Hahaha baba kumbe mwanzo ulikuwa unaona aibu kumtongoza mama ebu nipe story ilikuwaje?..” aliingilia Wonder mazungumzo ya Maria na Ram .
“Hahaha nitakusimulia vizuri siku tutakayo tulia ndani pamoja, ngoja saizi tumalize hili swala…” Aliongea Ram Kisha akamfuta General Ramos na kumuinua kutoka chini.
“Asante sana naweza sasa kwenda mjini kuweka kila kiti sawa Rafiki yangu? ..”
“Hapana …” Alijibu Ram akiwa anatoa karatasi mfukoni.
“Nini hiyo?..”aliuliza General Ramos .
“Ni karatasi, najua umetembea na muhuli wa kigavana hapo, sasa utaandika barua humu itakayoeleza mabaya yako yote Kisha utatia saini yako baada ya hapo itapelekwa makao makuu kila mtu akijua dhambi zako zote ndipo nitakusamehe na tutarudi pamoja mjini, kinyume na hapo nitakuuwa..” Aliongea Ram akiwaamenyoosha karatasi ili general Ramos aanze kuandika barua.
General alikaa sekunde chache akitafakari bila kuchukua karatasi, mwisho anafanya maamuzi anachukua karatasi
“Siwezi kuandika bila peni…” Aliongea general Ramos akiwa ameshika karatasi.
“Peni hii hapa …” Aliongea Maria akiwa anatoa peni na kurusha kwa Ramos
“Inaonekana Ni kama wote mliambizana mfanye hiki mnachokifanya kwangu..” Ramos aliongea akiwa kama hataki hivi kuandika barua
“Acha maneno mengi andika barua haraka…”aliongea Ram kwa hasira akiwa amemkaba roba Ramos na kumuachia aanze kuandika.
General Ramos alipiga goti moja chini Kisha akaweka karatasi juu ya goti la juu na kuanza kuandika barua.
Mda huo Ram alimtazama Maria na kumkonyeza, Maria alitabasam tu kwa sababu alijua Ram amemkonyeza sababu alimmiss tu.
Ramos akiwa anaendelea kuandika barua anataza pembeni yake anamuona Ram akiwa bize anaangaliana na Maria kwa mahaba, anatazama nyuma yake Kuna Aboku amesimama kama mlingoti anaangalia barua jinsi inavyoandikwa.
“Acha kunishangaa endelea kuandika barua..” aliongea Aboku mkononi akiwa ameshika Bunduki.
General Ramos akili yake yote ilikuwa ni kupokonya ile Bunduki aliyoshika Aboku ajaribu kujitetea.
“Wewe si nimekwambia uache kuni……….” Aliongea Aboku akiwa anampigapiga Ramos na kitako cha Bunduki lakini ni kama alifanya kosa kubwa kumpigia kile kitako chs Bunduki.
General Ramos kwa haraka sana aliivuta Bunduki na kumshuti Aboku tumboni, Ram aligeuka kwa haraka sana kutazama tukio baada ya kugeuka anajikuta amewekewa siraha kichwani na Ramos.
“Hahaha, hahaha Pole sana mshikaji ulizani kuanzia leo utaanza maisha mapya hahaha utaenda kuanza hayo maisha ukiwa kuzimu…”
INAENDELEA……..
Leo Mimi siongei mtaongea wenyewe.
PENZI LA KIKOMANDO
FINAL WAR 🔥
FINAL EPISODE (16)
TULIISHIA
General Ramos kwa haraka sana aliivuta Bunduki na kumshuti Aboku tumboni, Ram aligeuka kwa haraka sana kutazama tukio baada ya kugeuka anajikuta amewekewa siraha kichwani na Ramos.
“Hahaha, hahaha Pole sana mshikaji ulizani kuanzia leo utaanza maisha mapya na familia yako hahaha utaenda kuanza hayo maisha ukiwa kuzimu…” . aliongea Ramos akiwa ameelekeza siraha kwa Ram
ENDELEA…..
“ Naomba ushushe siraha yako we mjinga …” Aliongea Ram akiwa amenyoshewa siraha kwenye paji la uso.
“Hahaha Pole sana rafiki yangu kipenzi, lakini leo ndio mwisho wako nakuuwa na hii familia yako ya kipuuzi ..”
Aliongea Ramos akiwa anarudi nyuma.
“We mshenzi ukiona umemshuti baba yangu nakuhakikishia nitakukuuwa kwa mikono yangu mwenyewe…” Wonder aliingilia kwa sauti ya juu akiwa nyuma kidogo ya baba yake Ram.
“Hahaha binti leo unanipwayukia mimi ngoja nianze na wewe…” Ramos aligeuza siraha yake kutoka kwa Ram mpaka kwa Wonder na kufyatua risasi.
Kabla risasi haijafika Ram alijitupa na kwenda kusimama mbele ya binti yake, risasi iliingia kwenye mwili wa Ram.
“Baba …” Aliongea wonder kwa woga Ram akiwa mbele yake amesimama.
Taratibu ram alianza kukosa nguvu na kumuegamia binti yake aliyekuwa nyuma.
“Baba haukutakiwa kufanya hivi…” Aliongea wonder machozi yakimtoka akiwa ameshika Ram.
“Mwanangu unatakiwa kuishi, wewe ni binti mdogo na ni mrembo sana..” aliongea Ram kwa kutabasam akiwa mikononi mwa wonder.
“Hahaha naona unampenda sana binti yako mpaka unaamua kufa badala yake, sio mbaya ngoja nikumalizie tu…” Ramos aliongea akiwa anainua tena siraha yake na kumpiga Ram risasi zingine mbili kifuani.
Hali ya Ram inakuwa mbaya zaidi taratibu anaanza kwenda chini akiwa mikononi mwa binti yake.
Maria kawa kasi alitoka eneo alilokuwa amesimama na kwenda pale chini alipokuwa wonder na Ram.
“Ram Hapana usituache wenyewe tafadhali mtazame binti yako na mimi unawezaje kutuacha usifumbe macho kipenzi tafadhali….” Maria aliongea kwa uchungu wonder akiwa pembeni analia.
Ram alianza kufumba macho yake taratibu akiwa anatabasam kwa furaha ya kuiona familia yake kwa mara ya mwisho Kisha mapigo yake moyo yanaacha kudunda.
Mwisho umauti unamfika shujaa huyu aliyelipigania taifa lake kwa uzalendo mkubwa.
“Babaaaaaaaaaaa ….” Wonder alipiga kelele kubwa iliyobeba hasira na uchungu ikijirudia kwa mwangwi ndani ya ule msitu.
Kelele ya wonder inafika mbali mpaka ile sehemu aliyokuwa James amelala mahututi akiwa na matobo ya risasi mwilini akisubiri tu umauti umfike.
Ile sauti inapenya mpaka kwene ngoma za masikio ya James na kurudisha matumaini…
Kwa umbali jicho moja la James linafumbuka na kutazama juu akiwa bado amelala pale chini.
Upande wa pili Maria yupo kwenye majonzi makubwa ya kumpoteza Ram
“Ram kipenzi amka tafadhali, hujafa Ram, najua hujafa umelala tu si ndio haya amka shujaa wangu….” Aliongea Maria akiwa anautikisa tikisa mwili wa Ram, uso wake ukiwa ametapakaa machozi na wonder akiwa pembeni analia.
“Haya nilikuwa nasubiri mmalize kulia lakini naona kama ndo kwanza mnaanza ngoja niwapeleke alipoenda huyo marehemu….” Aliongea Ramos mbali kidogo akiwa anainua Bunduki na kuweka target pale chini alipokuwa Maria na wonder.
Maria alishakata tamaa ya kuendelea kuishi, alimkumbatia binti yake na kuendelea kulia wakisubiri tu Ramos afyatue risasi wafe kwa pamoja.
Ramos ali target vizuri
Bila huruma Ramos ali…..
Kabla Ramos hajafanya chochote mala sauti nzito inasikika nyuma yake.
“ Acha ujinga general…” Alikuwa ni James amechafuka damu mwili mzima na mkono wake mmoja ukiwa umeziba tobo la risasi lililokuwa tumboni.
“We, we e ee kumbe bado hujafa ! …”
General aliongea kwa hofu akimtazama James kwa kushangaa sana.
“ siwezi nikafa kabla yako. General, umefanya kosa kubwa kutaka kumuuwa huyo mwanamke mbele yako…”
Aliongea James na macho yake mekundu yenye hasira kali.
“Hahaha kijana mdogo, huna siraha yoyote alafu unanitisha mimi ngoja nikuonyehe….” Ramos aligeuza siraha haraka na kushuti kwa james.
Kabla risasi haijatoka James alisogea haraka mbele alipo Ramos na kuweka mkono wake mmoja kwenye bomba la Bunduki.
Ramos alifyatua risasi iliyopiga kiganja cha James kilichoziba tobo la Bunduki.
Risasi inazama kwenye kiganja cha mkono wa james lakini James hakupiga kelele yoyote ya maumivu zaidi ya kudondosha machozi ya damu sura yake ikiwa inazidi kuwa nyekundu kwa hasira kali.
General Ramos anaataka kufyatua risasi nyingine , James anavuta Bunduki kwa mkono uleule alioweka kwenye tundu la bunduki.
General anabaki akitaharuki baada ya bunduki kuchukuliwa hapohapo anapigwa kichwa kizito sana na kudondoka chini.
James akiwa amesimama ananyoosha ile Bunduki aliyopokonya mpaka kichwani kwa general Ramos .
“Kijana usiniuwe tafadhali mi ni general wa nchi pia Mimi niliwai kukusaidia wewe…” Aliongea Ramos kwa woga akiwa amelala chini.
“Amemuuwa baba yangu hastairi hata kuishi mpuuzi huyo muuwe…” Aliongea Wonder kwa hasira akiwa yupo chini na mama yake.
James kwa hasira alifyatua risasi tatu pale chini haraka haraka.
Risasi zilizokuwa ndani ya ile Bunduki zilikwisha zote
General alipumua kwa amani baada ya kuoana risasi zote zimepiwa pembeni kidogo ya kichwa chake.
James alizuia hasira zake.
Alimuacha general pale chini na kuondoka kwa kujikokota akionekana kuzidiwa akiwa anaelekea alipo kuwa wonder na maria.
“Kwanini umemuacha mjinga huyo ameniulia baba yangu bila huruma..” aliongea wonder akiwa analia anasimama pale chini ulipokuwa mwili wa Ram na kumfuata James ambaye alionekana kuzidiwa sana.
“ Zamani sana nikiwa mdogo wazazi wangu walifariki general alinichuka na kunipa makazi jeshini, nimeshindwa kumuuwa kabisa alikuwa Ni kama baba kwangu kipindi hicho…” Aliongea james akiwa amezidiwa na majeraha ya risasi taratibu alikosa nguvu na kwenda chini.
Mda huohuo Kuna kundi la Askari watano wa general Ramos wanaingia eneo hilo.
General Ramos alipata nguvu baada ya kuwaona wale Askari wake.
“Afadhari vijana wangu mmekuja naombeni siraha tuwamalize wajinga hawa…” Aliongea general Ramos kwa mukari akiwa anasimama kwenda kwa Askari wake.
Aliposogea mpaka kwa wale askari waliongia pale, aliona mabadiliko kidogi kwa Askari wake.
“Vipi jamani mbona mnaniangalia hivyo nimesema naombeni siraha niwauwe hawa watu..”Aliongea general akiwa anataka kuvuta siraha kwa askari mmoja
Yule Askari alimpiga ngumi nzito general akaanguka chini.
“wajinga nyie mmenigeuka na mimi kiongozi wenu!…” Aliongea akiwa chini.
Wale Askari walikuwa ndio wale ambao walikuwa wakipigana vita ya kwanza msituni wakiwa na James na James aliwaambia warudi kambini yeye atabaki kupambana mwenyewe na waasi maana jeshi lilizidiwa sana. Walirudi kambini wakiwa wamejeruhiwa sana na kutoa taarifa kwa General Ramos kama wameshindwa vita.
Hao Askari Ni marafiki wakubwa wa james na wanamuheshimu james kama kaptain wao
Baada ya kumgeuka general wao Askari mmoja mzee anasogea mpaka alipokuwa James
“ Kaptain upo sawa ? …” Aliongea Askari mmoja aliye umia kwenye mbavu akiwa anasogea
James alikuwa amezidiwa sana jambo lililo pelekea anashindwa hata kuongea
“Kuna Siri nilikuficha kwa miaka mingi kaptain …” Aliongea yule Askari kwa huzuni ambaye alikuwa ni mzee kidogo .
“Siri gani?…..” James aliuliza kwa shida sana.
“ Kipindi kile wazazi wako wanafariki kijijini General Ramos ndiye aliye wauwa ili akuchukue wewe uende jeshi maana ulikuwa Ni mtoto shupavu sana…” aliongea yule mzee kwa uchungu hapohapo James anasimama akiwa anahasira nyingi na kuanza kuelekea pale chini alipokuwa general.
“ Nisamee kijana nilifanya hivyo ili uwe shupavu zaidi…”aliongea akiwa anarudi nyuma
James alivuta Bunduki kutoka kwa Askari mmoja na kumuwekea General Ramos mdomoni.
“Sawa Lakini hukupaswa kumuuwa mama yangu mimi bila ya ridhaa yanguuuu…” Aliongea kwa hasira na kufyatua risasi nyingi mdomoni mwa general.
General Ramos anapoteza maisha palepale
Mda huohuo na James anadondoka chini na kufumba macho yake.
“Afande kijana umepatwa na nini?..” aliongea Wonder kwa hofu akielekea alipoanguka James.
“Kaptain shida nini…” Walikuwa ni wale askari nao Wanakimbia kuelekea alipoanguka james
WIKI MOJA BAADAE………
“ Doctor John, vipi hali ya mgongwa?..” Alikuwa ni Wonder ameenda kumuangalia mgonjwa.
“Kwa kweli binti mgonjwa bado hajapata fahamu mpaka sasa, na hutujui ni lini atahamka..”
Alijibu dactari,
Mazungumzo kati ya doctor john na wonder yalikuwa yanaendelea kwenye chumba alicholazwa mgonjwa.
“ Jamani doctor kwani hali yake ni mbaya sana?! …”
“Ndiyo cha msingi tumuombee Dua tu…” Aliongea doctor mala Kuna sauti inasikika kitandani iliyowafanya wageuke
“Mumuombee Dua nani wakati tayari nimepona ….” Alikuwa Ni james anajifunua shuka jeupe
“James jamani …” Wonder alimkimbilia kwa furaha na kumkumbatia.
Dactari alitoka nje kwenda kutoa taarifa.
“Usinikumbatie sana bwana unaniumiza vidonda mrembo…”
“ Hata ukiumia sawa ila sikuachii…” Aliongea wonder akiwa bado amemkumbatia James.
Mda huohuo anaingia Maria na kumuona James akiwa mzima. Maria anapiga kelele za furaha sana na kumpa James zawadi ya mkufu kisha anamwambia habari ambazo zilimfanya james akose furaha.
“Mwanangu leo mimi na wonder tunaondoka huu mji tunaenda kuishi mbali kabisa na hapa…”
“Kwa nini muondoke sasa wakati mimi ndo nimepona saivi?..” tabasam la james lilipotea ghafla baada ya hizo taarifa
“Tulisha panga mda mrefu ukweli tunataka tukae mbali na huu mji tusahau Mambo yote mabaya, saizi Kuna usafiri unatusubiri hapo nje twende wote nje maana Kuna surprise yako utaipenda…”
Aliongea Maria Kisha akamsaidia James kusimama kitandani wote wakatoka nje wakiwa wememshika James mikono.
Baada ya kufika nje….
“Wooow, watu wote na wanajeshi wanafanya nini hapa nje?…”
Aliuliza James akiwa anatabasam baada ya kuona kundi kubwa la watu pale nje.
“wamepata taarifa General wao mpya amepata fahamu wote wamekuja kumuona…”
“Hooooooow nimekuwa general wa nchi?…..”
“Ndio afande kijana…”
James alifurahi sana baada ya kugundua ameshika nafasi ya ya kuwa general,
Watu wote pale hadi madaktari walianza kumpa baraka James
“Uishi maisha marefu general James…..” Hizo ni kelele zilizo sikika kwa wingi sana kila kona
Baada ya kufurahi kwa mda mrefu hatimaye
Mda wa kuondoka Wonder na Maria
Ulifika. General James alikuwa amekaa kwenye kiti cha wagonjwa akiwa na wale askari marafiki zake wakiwatizama wonder na Maria wakiwa wanaingia kwenye usafiri.
“Mshikaji kweli unamuacha aondeke hivihivi …” Aliongea kidogo yule askari mzee sikioni kwa James.
“Tulia mzee usiingilie…” Aliongea james akiwa anatazamana na wonder kwa mbali.
Wonder kabla hajaingia kwenye usafiri alitabasam na kurudi nyuma alipo James
“Mwanangu mbona unarudi tuondoke?..”
“Nakuja sasa hivi mama ngoja nimpe kitu james…” Aliongea wonder akiwa akimbia kuelekea alipokaa James.
Anafika pale na kumpa kikaratasi chenye ujumbe .
“Kwa heri afande kijana…”
Wonder alianza kurudi kwenye usafiri akiwa anatabasam
James mda huohuo anafungua kile kikaratasi na kusoma, baada ya kumaliza kusoma
Anatabasamu na kutazama mbele anaona usafiri unaondoka na wonder
“Fanya kama nilivyo kuandikia kwenye hiyo karatasi afande kijana…”
Aliongea wonder kwa sauti ya juu akiwa kwenye usafiri anaondoka .
James anatabasam na kuangalia juu anamuona ndege mzuri aliyekuwa akipaa kufuata usafiri wa Wonder na mama yake.
“General James hiyo karatasi imeandikwaje…”
Aliuliza yule mzee wakiwa wanaondoka pale
“Acha umbeya utajua badae kilicho andikwa,
Saizi nenda ukawaambie wachonga masanamu wachonge sanamu la shujaa Ram kisha liwekwe katikati ya jiji….”
Aliongea James akiwa anakunja ile karatasi aliyopewa na Wonder kisha anaiweka mfukoni taratibu akiwa anasukumwa kwenye kiti cha wagonjwa na kuondoka
*************MWISHO********************