PENZI LA KIKOMANDO
EPISODE 1
Mwanzo….
Ni katika vita kali vinavyopigana majira ya usiku kati ya wanajeshi na waasi .
Wanajeshi wengi wanapoteza maisha katika vita hiyo, James ambaye ni captain wa jeshi anawaambia wenzake sita walio salia wakimbie sababu tayari walikuwa wamezidiwa nguvu na waasi .
“ Kiongozi tukimbie wote, hatuwezi kukuacha hapa pekeyako ….” Wanajeshi walikuwa wakimwita James kwa sauti ya juu lakini james anaamua kubaki kupambana peke yake .
“Hii ni amri kutokakwa mimi captain wenu kimbieni , kumbukeni familia zenu zinawahitaji msihofu kuhusu mimi “ aliongea James kwa sauti ya juu akiwa anaendelea kufyatua risasi .
Wenzake sita waliobaki wanaanza kukimbia.
James anaendelea kupambana na waasi akiwa peke yake amejibana nyuma ya
Mti .
Taratibu waasi wanaanza kumshinda nguvu james na kuanza kusogea katika ule mti aliojibana .
Kuna kumbukumbu mbaya inamjia James akiwa yupo kwenye ule mti .
Baada ya kumbukumbu hizoJames akajitokeza kwa hasira akiwa na mitutu miwili kwenye mikono yake na kuanza kumimina risasi kama kichaa .
“Haaaaaaaaaaaaa……” James alipiga kelele kwa hasira akiwa anawashambilia waasi akisuri tu umauti umfike maana waasi walikuwa ni wengi zaidi na zaidi.
Mitutu ya James aliyokuwa ameishika katika mikono yake miwili inabaki kutoa sauti tu badala ya risasi.james anaharuki na kugundua risasi zilizokuwa ndani ya silaha zake zimeisha
Waasi wengi alikuwa tayari amewaangusha lakini waliobaki ni wengi zaidi ya waliokufa .
Hapohapo waasi wanamzunguka james wakiwa na siraha kubwa ambazo zote zilielekezwa katika kichwa cha james ikisubiriwa amri ya kiongozi wafyatue risasi.
James anamtazama kiongozi kwa macho ya hasira sana akiwa katikati ya waasi .
Kiongozi anatoa amri kwa sauti kali “ uwaaaaaaaa” ghafla sauti nyingine ya kike inasikika nyuma yao.
“Subirini …” Ilikuwa ni sauti nyororo sana iliyowafanya waasi wote wageuke kutazama ni nani?
Mambo ni moto
Je, james atapona mbele ya waasi ?
Mwanamke huyo ni nani?
Kumbukumbu gani mbaya zilizomjia james na kumpa hasira ?
PENZI LA KIKOMANDO
EPISODE 02
Twendelee……
Waasi wote wanageka na kumuona mwanamke mrembo aliye shika siraha kubwa mkononi .
“We binti ni nani?..na unafanya nini saa hizi za usiku? Au upo pamoja na jeshi we mrembo?….” Aliongea Aboku ambaye ni Kiongozi waasi taratibu akiwa anamsogelea karibu.
“Naitwa wonder nimekuja kufanya biashara na nyie, ila kama hamtoitaji mi naondoka..?
Aliongea binti kwa mapepe sana akiwa anamuangalia James.
“Biashara?!!, Biashara gani binti ?….” Aliuliza Aboku akionekana kushangazwa .
Wonder taratibu anaingiza mkono wake kwenye suruali yake na kutoa kitu ambacho kinamfanya Aboku ashituke na kushangazwa nacho.
“Gold key !! , Binti umepata wapi huu ufunguo …” Aliongea Aboku kwa furaha sana akiwa anamsogelea wonder ili apatiwe ufunguo.
“Mm, mmh ,mmh … Hapana nipatie huyo kijana na mimi nitakupa Gold key …” Aliongea wonder akiwa anauficha ufunguo nyuma .
Aboku anashikwa na hasira za ghafla baada ya kuambiwa amuachie James.
Msaidizi mmoja wa Aboku anamsogelea Aboku mpaka sikioni na kumnong’oneza.
“Mkuu hasira za nini sasa, tumuachie tu huyu jamaa tuchukue Gold key,Tukipeleka hii makao makuu bosi atafurahi sana…..” Aliongea kwa sauti ndogo.
“Wote shusheni silaha chini …”Aliongea Aboku kwa sauti kubwa akitoa amri James aachiwe .
“Binti siwezi kukupa huyu mtu kirahisi rahisi hivi kwa sababu ameuwa watu wengi lazima alipie.. “ Aliongea Aboku akiwa ananyanyua siraha yake na kumpiga James risasi kwenye paja la mguu wa kulia .
“Ahaaaaaaaaa……….” James alipiga kelele za maumivu.
“Haya binti mtu wako huyu hapa naomba sasa hiyo Gold key… “
Aliongea Aboku akiwa anamsukumia James kwa Wonder.
Wonder bila kujiuliza mala mbilimbili anampatia Aboku Gold key kisha anashika mkono wa kushoto wa James na kuuweka kwenye bega la mkono wake wa kulia ili amsaidie James kutembea sababu tayari James alikuwa ana risasi mguuni.
“Kwa herini jamani……..”aliongea
Wonder kwa sauti ya juu akiwa anaondoka na James .
Wonder alipofika mbali kidogo na waasi akaanza kumkokota James kwa haraka.
“Ayaaaaaaaaaa!…..unaniumiza we binti si twende taratibu tu ! …”
Aliongea James kwa sauti yenye iliyobeba maumivu .
“We mpumbavu inatakiwa tukimbie ndani ya huu msitu maana Hawa jamaa nimewachezea mchezo tu …” Aliongea Wonder akiwa anaendelea kumkimbiza James.
KWA WAASI
“ Hahahaha, hahahaha leo nimekupata Gold key, mmmmmwa “ Aboku alikuwa akicheka sana na kuibusu Gold key wenzake wakiwa wamekaa pembeni wanamtazama tu kiongozi wao alivyo pagawa.
Kadri Aboku alivyozidi kuishika shika Gold key ndivyo ilivyozidi kutoka rangi ya juu. Aboku anashituka baada ya kuona rangi ya gold inatoka katika funguo , anachukua tochi na kuangalia kwa umakini ndipo anagundua amepewa kitu fake.
“ Nyie washenzi chukueni silaha zenu haraka watafutwe na wauliwe …..” Alitoa amri Aboku kwa hasira sana akianza kukimbia yeye kuelekea kule Alikoelekea Wonder na James.
PENZI LA KIKOMANDO
EPISODE 3
ILIPOISHIA
“Nyie washenzi chukueni silaha zenu haraka…” Aliongea Aboku akiwa anaanza kukimbia kuelekea msituni alipo James na wonder.
YA LEO …….
“ Wewe ni nani ?, Kwanini umenisaidia mimi.?.na ile gold key uliyowapatia wale waasi umeipata wapi? …” James alikuwa akimuuliza wander maswali lakini wonder hakujibu hata moja aliendelea kumvuta James haraka haraka.
Ghafla sauti za waasi zinasikika nyuma yao zioiongozana na milio ya risasi.
“We binti hawa wanatutafuta sisi wakati umesha wapa gold key! , Kwa nini sasa ? kimbia mimi niache hapa hapa nitajua la kufanya…”. Aliongea James aliposikia sauti za waasi nyuma yao.
“Ndio wanatutafuta sisi, niliwapatia gold key fake sasa itabidi tuongeze mwendo hata kama kimguu chako kibuvu tutaenda ivoivo ….” Aliongea wonder akiwa anamuweka vizuri James .
Waasi walitawanyika msituni ili wampate James na wonder lakini ilikuwa ni kama kazi bure sababu James na wonder walipita njia tofauti iliyowafanya watoke nje ya ule msitu wa vita. Sehemu wanayoingia ni tulivu na yenye kiza kinene kana kwamba hakuna mtu yeyote anayeweza kumuona mwenzake ndani ya poli hilo.
“James inatakiwa tuitoe risasi kwenye paja lako….” Aliongea wander akiwa anamsaidia James kukaa chini .
“Hotoweza kunitoa risasi na hili giza, we acha nitajaribu mwenyewe…..” Aliongea James akionekana kupatwa na maumivu sana.
“ Subiri na uone…” Aliongea wonder akiwa anapapasa papasa pembeni kutafuta kimti
Anachukua kimti na kumuwekea James mdomoni.
“Jikaze….” Wonder taratibu anapeleka mkono wake sehemu ilikopita risasi kwa hisia bila kutumia macho. Vidole vinazama ndani ya jeraha kutafuta risasi huku meno ya James yaking’ang’ania kwa nguvu kijiti kilichokuwa mdomoni.
“Haaaaaaaaaaaaa…” James alipiga kelele baada risasi kuvutwa kwa nguvu kutoka kwenye mguu wake.
“Hahahaha tayari imetoka umeona sasa …..” Aliongea wonder akiwa anacheka na risasi akiwa ameishika mkononi.
James akaichana nguo yake ya jeshi na kujifungia sehemu ilipotolewa risasi.
“ Wewe kweli ni malkia wa nguvu hahaha …” Aliongea James akiwa anakaza kitambaa alichojifunga.
“Hahahaha..nilikwambia … “
Usiku huo wa saa tisa James na Wonder wanapitiwa na usingizi wakiwa katika eneo eneo hilo lenye kiza kinene.
MAJIRA YA ASUBUHI
Asubuhi tulivu yenye milio tofauti tofauti ya ndege ndani ya kapori kadogo kalikozungukwa ns mauwa ya kupendeza .
Wonder anafumbua macho yake akiwa bado amelala chini, anaanza kusikia harufu ya moshi kama kuna kitu kinachomwa hiyo inamfanya anaamka kwa haraka kutazama kitu ambacho.
“Hooooooow , kumbe ni wewe ! Umeamka saa ngapi?….” Wonder alimuuliza james akiwa anapiga mihayo baada ya kumuona James mbele yake akiwa anachoma nyama.
“Nimeamka mapema kutafuta chochote kitu maana tumbo langu lilikuwa na njaa …” Aliongea James akiwa anageuza nyama nyama yake juu ya moto ili ikauke vizuri.
“Iyo nyama ya nini sasa?..” aliuliza wonder akiwa bado amekaa chini .
“Panya buku , niliwakamata kwenye majani kule…” James aliongea akielekezea kidole chake mbele kulipo kuwa na nyasi nyingi zenye ukijani.
“Mmh !, Huyo mdudu wako mimi siwezi kula pekeyako ni bora nibaki na njaa hivihivi!…” aliongea wonder akiwa anasimama eneo alilo kuwa amekaa.
“Sawa, hata hivyo nilikuwa siandai kwa ajiri yako . Nikimaliza kula naanza safari kuelekea kwenye Kijiji ambacho kuna kambi yetu ya jeshi , nashukuru kwa msaada wako ila baada ya hapa kila mtu apite njia yake…..”Aliongea James akiwa anaanza kumla panya buku aliye mchoma.
“Hapana mimi nitaenda na wewe kwenye hiyo kambi yenu ….” Aliongea wonder kwa mukari.
NDANI YA KAMBI
Wanajeshi sita ambao walikuwa vitani na James wanawasiri kambini wakiwa wamechoka na baadhi yao wakiwa na majeraha ya risasi.
Askari aliyesimama juu ya geti kuu la kuingilia kambini anawaana wale Askari sita kwa mbali .
“Jamaniiiiiiiiiiiii , special ajents wamerudi……..” aliongea yule Askari wagetini kwa sauti kubwa akiwaita wenzake wa ndani .
Kwa haraka sana Askari wote wanatoka na kwenda kuwasaidia wenzao . Special ajents wanachukuliwa na kupelekwa kwenye vyumba vya matibabu.
General Ramos ambaye ndiye mkuu wa jeshi lote akiwa ofisini kwake anapatiwa taarifa kama special ajents wamerudi. Haraka sana Ramos anainuka kwenye kiti chake na kuanza kuelekea kwenye vyumba vya wagonja akitembea haraka haraka .
“Doctor toka nje …..” Aliongea General Ramos macho yake yakionyesha kuwa hasira . Doctor kwa haraka sana anatoka nje .
“Mmeshindwa tena kupambana na waasi? Simngekufa tu, mnamaana gani kuwakimbia adui zenu nyie wajinga, mafunzo yote mliopewa ni yakupigwa kila vita, haya sasa Kaptain na wengine wapo wapi ?” Aliongea general Ramos kwa hasira sana baada ya kugundua wameshindwa kuwateketeza waasi na mwisho anaulizia wanajeshi wengine walipo.
“ Mkuu tumewapoteza wote ……”
Alijibu Askari mmoja kwa machungu sana akiwa amelala kitandani analia.
General Ramos akiwa kwenye chumba hicho cha wagonjwa analetewa taarifa kuma mkewe yupo nje anamsubiri. General Ramos anatoka nje haraka na kumkuta mkewe akiwa analia .
“Maria unalia nini ? “ Aliongea general Ramos kwa mshangao akiwa anamkaribia mkewe.
“Mwanetu atakuwa amefariki…” Aliongea Maria akiwa analia na mkononi mwake akiwa ameshika barua.
INAENDELEA
*Mambo ni 🔥 moto Siri ya wonder yafichuka je , Ni siri gani hiyo twende sambamba .
*Hii ni hatari na nusu usikose mwendelezo sehemu ya 04.
*