MREMBO MAWENGE
“hahahahahah Makubwa shoga madogo yana nafuu huhuhuhuhuhuhuhuhuhuhu huyo nae ni bwana kati ya mabwana ‘’
lilikua ni cheko la nguvu kutoka kwa bi husna alikua akimcheka rafiki yake mpendwa shoga ake wa dhati Anifa,,,,
sasa shoga mbona sikuelewi jamani Hassan anashida gani shoga angu na kama anatatizo mbona toka mwanzo huku niambia shoga ,wewe siunanipenda shoga toka uchumba urafiki ulikua unatuangalia tu kwanini huku sema leo hii unaishia kunicheka mimi daaah sawa shoga angu unayumba sana ngoja niondoke zangu,……
Anifa aliondoka kwa hasira kuelekea nyumbani kwake huku akiwa na mawazo chungu nzima ,
Anifa ni msichana mrembo sana urembo wake ulikua hauelezeki alikua ni mweupe kidogo mrefu na mwenye mwili uliyojazia vizuri ,hipsi zake zilijitengeneza vyema na makalio yake yalikua yamejijenga vyema kiasi cha kuwavutia sana wanaume ,anifa kabla hajaolewa na Hassan alikua akijiamini sana alikua anaamini kwa uzuri wake huo anauwezo wa kuolewa na mwanaume yoyote hata mtoto wa raisi ,,,anifa alidondoka mikononi mwa penzi la kijana Hassan Hussein mapenzi yao yalinoga sana.
Hassan alikua ni kijana mtanashati na mpole sana ,aliku ni mtaratibu alijushughulisha na shughuli za utabibu katika hospitali kubwa ya mkoa,mkoani mwanza ,mapenzi kati ya anifa na Hassan yalianza pale anifa alipompeleka mama yake mzazi hospitalini ,pale Hassan alimuhudumia kwa huruma zote na hatimaye mama mzazi wa Hassan alipata auhueni (nafuu) na toka hapo anifa alichukua mawasiliano ya dokta Hassan ,Hassan alikua akimjulia mama yake mzazi hali ,alikuja kumtibu nyumbani kwao na hii ilifungua njia ya wazi kwa Hassan kupata tunda lake la roho kujikwanyulia binti mrembo kupindukia aitwaye anifa
Hatimaye anifa aliolewa na Hassan maisha yao yalikwenda vyema japo anifa alikua akimfayia vitimbi Hassan ila Hassan alikua mnyenyekevu sana hivyo alimvumilia anifa kipenzi chake ,,siku moja Hassan aliporejea kutoka kazini alishangazwa na ukimya uliokuwa umetawala nyumbani pale alipitiliza moja kwa moja chumbani alishaanga mkewe hayupo alipoelekea sebuleni alimuona anifa akiwa ameketi kwenye sofa rimoti ikiwa mikononi akitizama televisheni “hellow my lovely wife nikupendae natumaini u mzima’’ “ yap niko poa honey ‘’
ohooooo sawa my wife Hassan alijibu na kukaa pembeni yake
Hellow honey nasikiaa njaa naomba chakula nile mpenzi “mhhhh chakula sijapika bado ‘’
Hujapikaa ????? mpaka sasa sawa bwana Hassan alijibu na kuondoka “ nyooooo muone huna haya mwanaume wewe umenioa niwe mtumwa wako ishia hapohapo mjinga sana wewe ‘’ Hassan hakuamini alichokisema anifa ilikua ni mwezi tu toka waoane aling’ata meno kwa hasira ila aliona haina haja ya kubishana na mkewe
Siku iliyofuata anifa akiwa na shoga zake ,shoga zake walikua na wivu sana walikua wakimsuta sana na kumwambia mwanaume gani huyo ,,,,,bi zuhura aliaanza “` hahah shoga Hassan naye ni mtu mtu mwanaume anakufuga kama kuku achana nae nakwambia kimshahara chake milioni kwa mwezi wewe mwanamke unalipa mtoto mbichi wewe yaan unaweza olewa na mtu atakayekupa milioni kwa siku mwangalie fatuma mwenzako anamiliki magari kwa sasa sasa nakwambia shoga kazi unayo’’
Anifa alihisi kama msumari unamchoma aliondoka palepale na kuelekea nyumbani alifungua mikabati ya nguo alichukua pochi zake na kila kitu tayari kuondoka hakuwa na muda wa kuendelea kuwepo pale akiwa ameshapaki kila kitu Hassan huyo nae alitia mguu .
Hassan hakuamini alichokiona mbele yake kwa mshangao alimuuliza anifa wewe mwanamke nini shida anifa alijibu `
“mpumbavu wewe huna akili dume suruali ,umekua bize na kazi zako unanitupa mimi ,hela unipi unaanzaje kunipa laki tano kwa mwezi hainitoshi kabisa mapenzi hujui wewe upo tu kama dume jike sasa kwa taarifa yako usinijue kuanzia sasa bye’’ ohoooo maneno haya yalimpenya sana Hassan yalivyoingia kwa moyo wake alishindwa kustahimili alidondoka chini na kuzimia pale aliwaza aibu ataipeleka wapi juzi tu madaktari wenzake aliwakaribisha kwa harusi yake walimpa zawadi kedekede masofa ,friji leo hii hata miezi miwili haijapita amemwacha hakika ni kosa kubwa kuoa mwanamke kigeugeu ili basi Hassan amekosea
Anifa akiwa anatokeza njiani alishangaa kuwaona mashoga zake wanamcheka alivyowatizama ghafla waliaacha kumcheka kumbe walikua ni wanafiki na wachonganishi ,anifa alidhania watampongeza kumbe hata hawakuwaza hivyo walikua wakisubiri anifa aharibu mambo ndo ilikua furaha yao ,bi zuhura aliropoka “ anifa wewe ni mama la mama utakaaje na mwanaume suruali ,mwanaume kibamia Yule ana kitu safari njema mama ukatafute mwanaume mwingine siyo huyo ‘’ alipo maliza kusema hivyo wote walicheka ,,….
Anifa alianza kuwaza alitamani arudi kwa Hassan ila alishindwa alianza kuvuka barabara ili akakae na shoga ake fatuma anayeishi mbezi ,alikua ana mawazo sana hivyo alipofika katikati ya barabara teksi iliyokuwa inakuja kwa kasi ilimsagasaga pale pale na kuwa kama chapatti dereva wa teksi alijitahidi kupiga honi ila hakusikiwa kutokana na wingi wa mawazo aliyokuwa nayo anifa ,,,,na huo ndo ukawa mwisho wa anifa
Hassan baada ya kuachwa na anifa alidhania marafiki zake wangemcheka ila haikuwa hivyo walikua nae karibu kupita maelezo baada ya muda Hassan alipata mwanamke mwingine aitwaye ashura waliishi pamoja maisha ya raha mustarehe walibarikiwa watoto wawili juma na anifa Hassan alimpa mtoto wake jina la anifa kama kumbuumbu la yaliyomkuta.