LOOH DADA MARTHA..
Sehemu Ya 06
ILIPOISHIA:
Alikazana sana mpaka Liz akabadili mawazo…
“Bro…oooo…”
“Sist…aaa…”
“Una..unaonaje tukiachana na undugu? Mbona kama huku ni kuzuri zaidi…Broooo…oooo…”
JIACHIE MWENYEWE…
“Noo…tuendelee sista…lakini tusirudie tena baada ya leo, tena tujikanye kabisa na tukome kama tulivyokoma kwenye nido za mama zetu, si ndiyo… eee?”
alijibu Roi kwa sauti ya kubabaika…
“Bwana…aaa! Mimi sitaki undugu tena kuanzia leo na ufe, kwanza una faida gani kwetu?” alihoji Liz lakini kikubwa kilichoonekana ni tamaa ya mwili iliyombamba kwa wakati huo pale kwenye kitanda…
“Mimi nataka mbona,” aliendelea kusisitiza Roi.
“Ba.n..aaa…si tumalize kwanza…tu…t
ajadili.”
Wawili hao, waliendelea kuchekecha mpaka wakacheketuka!
Kwa Liz, moyoni aliamua kuwa, baada ya mechi hiyo, yeye na Roi waendelee kuwa kaka na dada kama walivyokubaliana…
“Si mbaya kama tumeanguka dhambini leo tu, lakini nakuhitaji tuendelee kuwa kaka na dada,” alisema Liz akiwa kwenye kasi ya kupiga mpira kwenye kona karibu na goli!
“Hata mimi ndivyo nitavyotaka.
Leo tukimaliza hapa tutubu dhambi zetu, tuanze upya kama kaka na dada, sawa dada angu?” alisema Roi…
“Si sawa…kwa…kwa muda huu tuendelee kuwa wapenzi si mpaka tumalize.”
“Haya.”
Liz alichekecha, akafika mwisho, akatangaza nia na kunyoosha miguu, akatulia tuli huku Roi akijitegemea mwenyewe mpaka naye alipotangaza nia yake.
***
Wote walilala wakiangalia juu huku mazungumzo yao yakiwa ya machalechale.
Yalikuwa mazungumzo ya kama ni wapenzi, wakati mwingine kama kaka na dada.
Katika kuonesha kwamba, Liz alijutia kitendo cha kuivunja amri ya sita ya Mungu, aliamua kukaa kitandani badala ya kulala…
“Kaka…”
“Dada…”
“Tutubu dhambi yetu sasa ili tuendelee kuwa kaka na dada kama mwanzoni.”
“Kweli bwana, hebu tubu wewe kwa niaba yangu,” alisema Roi baada ya kuhisi hakuna maneno rasmi ya kutubu…
“Tumwombe Mungu tusirudie tena kufanya dhambi hii, mimi na wewe kuanzia sasa ni kaka na dada tena.
Kwa kulitambua hilo naomba tukaoge, tuvae tuondoke,” alisema Liz huku akitoka kitandani.
Alikwenda bafuni, akaoga na kurejea, akavaa, akasimama akimsubiri Roi ili waondoke wote…
“Sasa dada wewe umeshavaa, kwa hiyo na mimi nivae mbele yako kama dada yangu?”
“Oo! Ngoja nitoke kaka, nisamehe sana.”
Liz alitoka, akasimama nje ya mlango.
Roi alikwenda kuoga, akarudi na kuvaa chapchap, akatoka, akaungana na Liz…
“Dada wewe unaondokea kwa njia gani?”
“Nitapanda Bajaj hapo nje kaka.”
“Oke, basi itabidi tuachane kwa nje au vipi sista?”
“Sawa kaka‘angu.”
Nje ya hoteli hiyo, Roi na Liz waligawana njia, kila mmoja akachukua usafiri wake, wakatawanyika kwa ahadi ya kuwasiliana kwa simu…
“Basi baadaye bro,” alisema Liz…
“Sawa, baadaye dada’angu,” alisema Roi.
Baadhi ya watu walipowaona wanatokea kwenye hoteli hiyo na kuitana dada, kaka walishangaa kwani dalili zote ziliashiria kwamba, wawili hao ni wapenzi.
***
“Ila anajitahidi sana kitandani, hivi kweli tunaweza kuwa kaka na dada maisha yetu yote?” alihoji moyoni Roi…
“Mh! Kaka…kaka kweli! Kaka mzima uwanjani kama Pele…kakaaa…” alisema moyoni Liz akisifia.
***
Ilikuwa usiku wa siku hiyohiyo tu, Roi ndiye aliyeanza kumchokoza Liz…
“Dada Martha mambo?”
Martha aliachia tabasamu kwanza maana alishamwambia mara kadhaa Roi kwamba, asimwite Martha, amwite Liz…
“Kaka Roi,” aliitika kwa kulitaja jina Liz…
“Naam sista…”
“Unalipenda jina la Martha ee?”
Roi ndiyo akashtuka kwamba kumbe alitumia jina hilo…
“Da! Nisamehe sista, kusema ule ukweli nililizoea sana kuliko Lizie…”
“Ona sasa! Siyo Lizie kaka ni Liz…sasa sikia bro, nakuruhusu utumie jina la Martha kuanza leo.
Hilo la Liz lifute kabisa kwenye akili yako.”
“Daa! Sista nakushukuru sana mama.
Hakuna jina nalipenda kama la Martha kuliko Liz, nashukuru kwa kuniruhusu…”
“Oke usijali baby bro…uko wapi sweetheart kaka?”
“Nipo nyumbani darling sista…”
“Oke! Mtoto mzuri kumbe, wewe ndiye kaka wa kweli.”
“Hata wewe ni dada wa kweli.
Good sista…hujalala?”
“Ndiyo nataka kulala sasa.
nimechokaaaa!”
“Umechokeshwa na nini sista jamani?”
LOOH DADA MARTHA…
SEHEMU YA 07
ILIPOISHIA
“Daa! Sista nakushukuru sana mama. Hakuna jina nalipenda kama la Martha kuliko Liz, nashukuru kwa kuniruhusu…”
“Oke usijali baby bro…uko wapi sweetheart kaka?”
“Nipo nyumbani darling sista…”
“Oke! Mtoto mzuri kumbe, wewe ndiye kaka wa kweli.”
“Hata wewe ni dada wa kweli. Good sista…hujalala?”
“Ndiyo nataka kulala sasa.
Nimechokaaaa!”
“Umechokeshwa na nini sista jamani?”
SASA ENDELEA…
“Kwani hujui bro?”
“Sijui chochote.”
“Aaah! Si kule tulikokuwa,” alisema Martha lakini akilini mwa Roi alijua kilichomchokesha sista wake ni nini!
“Kule gesti?” aliuliza Roi…
“Ndiyo kulekule bro…daa!”
“Daa! Ila sista uko vizuri unajua?”
“Teh! Teh! Mh! Wewe je kaka? Mbona uko vizuri zaidi…”
“Mh! Kweli…?”
“Kweli bro…”
“Uliipenda chenga ipi pale uwanjani?”
“Mmh! Kaka bwana…chenga zote zilikuwa nzuri sana kaka, wewe ni kiboko.”
“Hamna! Lazima kuna chenga moja uliipenda sana…iseme tu sista jamani…”
“Ha! Ha! Ha! Niliipenda ile ulipokaribia golini ukawa unapiga chenga za zigzaga.
Halafu hata ile ya mimi kuchunga ng’ombe ilikuwa nzuri…”
“Nyingine, lazima kuna nyingine…”
“Nyingine ni ile uliponiambia una hamu ya kula mboga ya matembele, si ikabidi nikachume.”
“Mh! Sista…”
“Nini tena braza..?”
“Mwenzio hoi hapa…”
“Mimi je? We acha tu! Hivi hapa nataka kwenda kuoga.”
“Umechafuka na vumbi?”
“Kumbe je?”
“Kwa hiyo? Nije nini?”
“Ha! Ha! Mbali…halafu ukaka si unaendelea kama kawa au?”
“Laa! Aisee…huu ukaka na udada halafu tunapeana njaa si mzuri…nataka kuruka nije…”
“Njoo…”
“Kweli?”
“Kweli njoo.”
“Nikija?”
“Si utakula chakula kama mgeni.”
“Chakula gani?”
“Utakacho…kuna ndizi za kuiva na maandazi ya donati.”
“Mh! Unanitamanisha sista…mimi nitakula donati…”
“Haya mimi nitakula ndizi za kuiva,” alisema Martha.
“Lakini sista…”
“Nini tena jamani kaka..?”
“Kwani umelala sista?”
“Nipo kitandani bro…”
“Umelalaje hapo kitandani?”
“Nahesabu paa…wewe bro?”
“Mimi nasoma kitabu.”
“Kumbe tupo sawa basi!”
“Basi acha kuhesabu paa.”
“Na wewe utaacha kusoma kitabu?”
“Nimeshakiweka pembeni.”
“Oke, mimi nimeshaacha kuhesabu paa.”
“Miguu ikoje?”
“Mashariki na Magharibi mwa nchi.”
“Basi mimi niko kanda ya kati nakuja kwako.”
“Njoo broo.”
“Ndiyo nakuja sasa…”
“Njoo tu.
Na mimi nimeanza kukuona unavyokuja.”
“Kwa hiyo utanipokea..?”
“Ukifika nakupokea bro tena kwa mikono miwili kaka…njoo!”
“Nakaribia, nimeanza kukuona umesimama mlangoni unanisubiri…”
“Karibu broo…njoo…”
Roi alitumia meseji nyingine lakini hakujibiwa, akatuma nyingine, hakujibiwa, akapiga, Martha hakupokea…
“Jamani dada…nini tena?”
Baada ya dakika kumi na tano, meseji ikaingia, Roi akaisoma kwa haraka sana…
“Brooooo…”
“Sistaaa…”
“Nipo vibaya, please kama unaweza njoo kweli sasa hivi…chukua usafiri wowote ule nitakuelekeza kwangu please bro njoo tucheze…”
“Sista Martha…”
“Yes brooo…ooo!”
“Ukaka na udada je? Ufe?”
“Aaaah! Potelea mbali bwana…kwani lazima wakati mi nateseka?”
“Hapana dada…undugu ni bora kuliko mapenzi…tutagombana kila siku tukiwa wapenzi dada…”
“Hapana kaka…basi leo tu…”
“Baada ya leo?”
“Tusirudie tena bro…”
“Haya nakuja…kaa tayari…”
“Njoo kaka mpaka Kimara Mwisho, kuna barabara inaingia kulia, fuata hiyohiyo mpaka sehemu kuna pub, kuna muziki nje…nipigie…”
“Kwani saa hizi unafanyaje dada?”
“Natandika kitanda kaka, si unakuja kweli?”
“Nakuja dada…”
“Njoo kaka…”
***
Baada ya dakika kumi, Roi alimpigia simu Martha akiwa kwenye pub aliyomwelekeza…
“Nakuja kaka…”
“Poa dada.”
Usiku huo, Martha alivaa gauni la kulalia kwa hiyo lilimwonesha umbo lake kwa usahihi wote kiasi cha kumfanya Roi kuanza kufikiria upya kuhusu kuendelea na ukaka na udada baada ya tukio la muda huo…
Martha alikuwa akiishi na wapangaji wengine, wanawake wenzake ambapo kwa usiku huo walikuwa wamekaa nje jirani na dirisha la chumba cha Martha wakiongea…
“Karibu sana kaka…! Jamani huyu kaka ‘angu, anaitwa Roi…”
LOOH DADA MARTHA…
Sehemu Ya 08
ILIPOISHIA
Martha alikuwa akiishi na wapangaji wengine, wanawake wenzake ambapo kwa usiku huo walikuwa wamekaa nje jirani na dirisha la chumba cha Martha wakiongea…
“Karibu sana kaka…! Jamani huyu kaka‘angu, anaitwa Roi…”
JIACHIE MWENYEWE SASA…
Martha alimtambulisha Roi kwa wapangaji wenzake, nao walimtupia macho Roi kwani vaa ya Martha ya gauni la kulalia halafu aseme eti mgeni huyo ni kaka yake, kwao haikuingia akilini hata kidogo..!
“Oo! Karibu sana kaka yake Martha,” alisema mpangaji mmoja kwa akili za kujiongeza, wakacheka, Roi pia akacheka…
“Asante sana. Za hapa?” alisalimia Roi…
“Njema tu.”
Kazi ikawa moja kwa wapangaji hao, kuhakikisha wanaujua ukweli wa uhusiano wa Martha na mgeni wake…
“We Enjo, kama kweli huyu ni kaka yake Martha angempokea na gauni la kulalia?”
“Aaa! Siyo kweli hata kidogo, hapa ametudanganya,” walisemezana wapangaji hao pale nje tena jirani kabisa na dirisha la chumba cha Martha.
“Karibu baby,” Martha alikaribisha kwa sauti ya chini sana. aliogopa akisikika nje akiita baby wakati alishasema ni bro wake…
“Asante nashukuru,” alikaribia Roi na kutaka kukaa kwenye sofa sebuleni, lakini Martha akamdaka akiwa hajakaa, akamsimamisha, akamwomba denda palepale sebuleni…
“Mmm….mmmm…”
“Mm…mmmm…waaaa…”
Walichukua kama dakika tatu nzima wapo ndani ya denda motomoto huku wakisikika kwa sauti za kuhemka.
Miguu yao chini ilitembea sawasawa na kila mmoja na uwezo wake wa kuhimili sakafu.
Ilitembea kama iliyokuwa ikiamrishwa na sauti moja.
Ilikuwa kulia…kulia yote, kushoto…kushoto yote! Wakati mwingine mbele…mbele yote pia…
“Baby,” aliita Martha baada ya kujichomoa kwenye denda na Roi…
“Yes darling…”
“Chumbani ni noma, wale wapangaji wenzangu wamekaa nje ya dirisha langu la chumbani…”
“Kwa hiyo itakuaje sista..?”
“Bwana! Kwanza mi sitaki uniite sista…mimi ni baby wako…”
“Sawa sweet…sasa itakuaje?”
“Si hata hapa sebuleni panatosha au?”
“Wewe tu! Unaona panatosha kweli?”
“Panatosha darling,” alisema Martha kwa sauti iliyokwishazidiwa nguvu na joto la mahaba.
Tayari Martha alishalishika lile gauni lake la kulalia ambalo lilimchora umbo lake lote na akalichojoa kwa juu kichwani, akalitupia kule mbali…
“Mmh!” aliguna moyoni Roi kwani kwa mara ya kwanza alimwona vizuri mrembo huyo alivyoumbwa tofauti na siku ya kwanza.
Martha kwa kuwa hakuwa na vazi jingine ndani ya gauni hilo kwa hiyo hakuwa na kibarua kingine cha kuchojoa, akamshika Roi, akamfungua vifungo viwili vya t-shirt aliyovaa, akamnyoosha mikono, akamchojoa nguo hiyo, akammalizia na singlendi!
Akiwa amebakiza vazi la chini tu, Roi alijitegemea mwenyewe kujichojoa, akamaliza na kubaki saresare maua na mwenyeji wake, Martha.
Martha alikimbilia mlangoni kwanza ili kujiridhisha kwamba, umefungwa.
Sasa wakati anakwenda, macho ya Roi ambayo yalikuwa kwake, yalikuwa cherekochereko kwa namna wowowo lilivyokuwa likivaibreti kwa papara kama siyo pupa!
“Mbengenyu…mbengenyu…mbeng
enyu…duu!” alisema moyoni Roi akifuatilia wowowo hilo lilivyokuwa likisumbuliwa na mmiliki wake.
Martha alirudi na kufikia kwenye mwili wa Roi, wakaenda wote hadi chini kwenye sofa kubwa! Puuu!
Kazi ilianza palepale, kila mmoja alikuwa moto kimahaba akimtaka mwenzake.
Ni Martha ndiye aliyeonesha kumtaka zaidi Roi kwani alikuwa moto zaidi ya ule wa kifuu!
Kwa vile kila mmoja alijua wanatakiwa kutosikika nje kwa hiyo walicheza kwa ububububu ili sauti isitoke kwenda nje…
“Mm…mmmm…”
“Mm…mmmm…”
Ilikuwa ni miguno tu! Lakini yenye kutoa kielelezo tosha kwamba wapo uwanjani wanajiandaa kwa mechi ya kikubwa!
***
Kule nje, wale wapangaji walikuwa wakizungumza kwa sauti ya chini ili kutoa nafasi kwa sauti za chumbani kwa Martha kuwafikia kama wangekuwa wameingia na kuanza kulisakata kabumbu!
“Itakuwa kaka yake kweli si unaona wako sebuleni…”
“Itakuwa kweli.
Lakini wakiingia chumbani tu, ujue ni geresha, hakuna cha ukaka pale,” walizungumza wale wapangaji.
Penzi ni kikohozi kulificha huliwezi, ni kweli kabisa! Licha ya mechi kuihamishia kwenye uwanja wa sebuleni lakini ile wanapuliza kipyenga tu, Martha alianza vuvuzela la mahaba.
“Nyie…nyie kumbe wapo sebuleni kweli lakini si mtu na kaka yake, hebu sikieni,” waliambiana pale nje.
Sauti ya Martha ilisema na kutafsiri kila jambo lililokuwa likiendelea…
“Ooo…”
LOOH DADA MARTHA…
Sehemu Ya 09
ILIPOISHIA:
Penzi ni kikohozi kulificha huwezi, ni kweli kabisa! Licha ya mechi kuihamishia kwenye uwanja wa sebuleni lakini ile wanapuliza kipyenga tu, Martha alianza vuvuzela la mahaba.
“Nyie…nyie kumbe wapo sebuleni kweli lakini si mtu na kaka yake, hebu sikieni,” waliambiana pale nje.
Sauti ya Martha ilisema na kutafsiri kila jambo lililokuwa likiendelea…
“Ooo…”
JIRUSHE NAYO SASA…
“Mmm,” aliguna Roi.
Hamasa ya mapenzi kwake ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba, kila nukta ilikuwa ya furaha kwake.
Kilio cha Martha kilifika nje vizuri sana, wapangaji wenzake wakajisogeza hadi kwenye dirisha la sebuleni na kukaa hapo huku wakijikemea kuwa kimya!
“Ndiyo kaka yake huyu?” mpangaji mmoja aliwaambia wenzake kwa sauti ya chini.
Ilifika mahali, wapangaji hao walitamani kuangalia mechi laivu hivyo wakaanza kuinua vichwa na kusogelea dirishani kabisa lakini pazia lilikuwa madhubuti kutotoa nafasi kuangalia ndani.
Mpangaji mmoja, anaitwa mama Mbega, yeye aliangaza huku na kule na kuona kipande cha mti, akakiokota na kuanza kukipitisha kwenye nyavu, sehemu iliyotoboka.
Lengo lake lilikuwa ni kuweka pazia pembeni ili apate nafasi ya kuona mechi inavyoendelea ndani.
“Mh! Jamani tutaonaje sasa ndani?” alisema mama Mbega kwani alishindwa kupenyeza mti kwa kukosa sehemu iliyotoboka.Kelele za Martha ziliwapagawisha wote pale nje.
Sasa walikuwa wakihema mihemo kama vile wao ndiyo wako ndani kwenye tukio.
Walishindwa kujizuia mpaka wakaanza kujinyonganyonga huku na kule kwa sababu ya kukumbwa na joto la mahaba ya sauti ya Martha.
Martha alisikika kabisa akitangaza nia na kuwafanya wale wa nje kuzidi kuwa moto zaidi…
“Jamani Martha…kwa nini anatufanyia hivi lakini?” wapangaji waliulizana wao kwa wao tena kwa sauti, sema tu Martha na Roi hawakuisikia kwa sababu walikuwa kwenye eneo la mpira wa piga nikupige.
Walipomaliza, wale wapangaji nao wakakimbia. Kila mmoja aliingia ndani kwake na kujilaza kitandani huku wakiugulia maumivu ya joto la mahaba.
“Sweet,” Martha alimwita Roi…
“Niambie.”
“Daa! Afadhali sasa, maana loo…ilikuwa hatari sana,” alisema Martha huku akichekacheka…
“Kwa hiyo sasa umeridhika?”
“Sana tu.”
Wakati Martha anamsindikiza Roi, wale wapangaji walijua, wakatoka kwa mkupuo nje mpaka Martha mwenyewe akashangaa sana…
“Kuna nini kwani? Mbona kama wameibuka kwa mpigo?” alijiuliza Martha lakini hakutoa sauti yake kuwauliza.
“Jamani kaka yangu anaondoka sasa.”
“Oo! Karibu sana kaka.”
“Asanteni sana, siku nyingine.”
“Haya, wasalimie huko, siku nyingine uje hata kama dada yako Martha atakuwa hayupo,” alisema mama Mbega huku akicheka kicheko cha kejeli kama vile moyoni alikuwa akisema…
”Kaka gani wewe Martha, tumesikia kila kitu sisi.”
***
Ulikuwa usiku wa mawazo kwa Martha. Licha ya kwamba alikata kiu yake lakini Martha alijikuta akiumizwa na dhamira mbaya kuhusu Roi…
“Hivi tungebaki kuwa kaka na dada nini kingetokea? Kwanza undugu ungedumu zaidi.
Kwa hii hatua tuliyofikia uhusiano wetu utakatika ghafla siku si nyingi,” alisema moyoni Martha akiwa amelala kuangalia juu.
“Ni lazima nichukue uamuzi mgumu.
Nimwambie ukweli kwamba tusitishe uhusiano wetu ili ukaka na udada uendelee.”
Alichukua simu, akamtumia meseji Roi…
“Upo?”
Baada ya dakika kumi, Roi alijibu…
“Nipo darling, niambie.”
“Nina jambo linanisumbua, naweza kuchati na wewe kama hutajali?”
“Unaweza baby…”
“Oke.
Nimekaa, nimewaza sana. Licha ya kwamba umenikata kiu yangu lakini muda mwingi dhamira inaniambia kwamba tunatakiwa kuendelea kuwa kaka na dada kama makubaliano yetu ya siku ya kwanza kabisa.”
“Mh!” aliguna Roi na ndiyo ikawa jibu lake kwa Martha…
“Usigune Roi, nasema kutoka moyoni mwangu.”
“Mmmh!” Roi alizidisha kuguna, Martha akakasirika na kukaa kimya.
Roi alipoona Martha ametulia, akajua amekasirika, akamtumia meseji…
“Naweza kukupigia?”
“Yes! Unaweza.”
Roi alipiga simu, Martha akapokea haraka sana…
“Halooo…”
“Sista…”
“Yes braza.”
“Umewaza nini tena jamani?”
“Mh! Bro, nimewaza mengi.
Mimi nimefikia uamuzi huohuo.
Lazima tuendelee kuwa kaka na dada ili uhusiano wetu uendelee kudumu zaidi na zaidi,” alisema Martha…
“Mh! Nikwambie kitu Martha..?”
“Niambie bro…”
LOOH DADA MARTHA
Sehemu Ya 10
ILIPOISHIA:
“Mh! Bro, nimewaza mengi.
Mimi nimefikia uamuzi huohuo.
Lazima tuendelee kuwa kaka na dada ili uhusiano wetu uendelee kudumu zaidi na zaidi,” alisema Martha…
“Mh! Nikwambie kitu Martha..?”
“Niambie bro…”
SASA ENDELEA…
“Hata mimi sasa nimeamua kuwa kuanzia sasa hivi tuwe ndugu, tena wa damu moja! Mimi ni kaka yako, wewe ni dada yangu.”
“Loo! Jamani napiga vigelegele, umenifurahisha sana kaka yangu,” alisema Martha.
“Hata mimi dada nimefurahi sana.
Unajua tulikuwa tunafanya makosa makubwa sana. Watu tumekubaliana kuwa kaka na dada sasa hizi tamaa nyingine za kutoka wapi?” aliuliza Roi…
“Ndiyo hapo sasa bro,” alishadadia Martha.
Baadaye waliagana wakakubaliana kuwasiliana asubuhi inayofuata ili kujuliana hali.
***
Martha alilala kwa amani na furaha. Alihisi ameutua mzigo mkubwa sana.
Ilipofika saa kumi na moja alfajiri, Martha alipigiwa simu na shangazi yake kuwa, mumewe huyo shangazi amefariki dunia.
“Ha! Shangazi kweli? Mbona sijajua kama alikuwa anaumwa?” aliuliza Martha akianza kulia.
“Kafa ghafla Martha.”
Martha alikata simu, akatoka kitandani na kutungua nguo za kuvaa ili kwenda kwa shangazi yake.
Lakini wakati anatoka akampigia simu Roi…
“Kaka, mume wa shangazi yangu kafa ghafla jamani…eeee..ooo,” alilia.
“Wapi?”
“Nyumbani kwake Magomeni.”
“We uko wapi sasa sista?”
“Mimi ndiyo nakwenda huko.”
“Uko wapi?”
“Nipo hapa kituoni Kimara.”
“Nakuja hapohapo kituoni sista.”
Roi alikurupuka, akatoka mbio hadi kwenye gari, akaendesha hadi kituoni Kimara.
Akamchukua Martha kwenye gari hadi Magomeni msibani.
Nyumba yote ililipuka kwa vilio, majirani walijaa nao wakilia sambamba na familia ya marehemu.
Martha alifikia kulia akiwa ameishiwa nguvu.
Ilibidi Roi ajumuike na wanaume wengine waliokaa nje ili kuona hali inakwendaje.
Kulipokucha, Martha ndiyo akamkumbuka Roi kwamba hawakuagana baada ya kuachana…
“Ooo! My God! Bro atakuwa ameondoka bila kujua nini kinaendelea!” alisema moyoni Martha, akampigia simu huku akiwaza…
“Sikumfanyia fea hata kidogo. Mtu akupe lifti hadi msibani halafu unamwacha bila kumshukuru.”
Simu ilipokelewa, Martha akashtuka kusikia kelele…
“Bro, upo wapi?”
“Nipo hapa nje sista.”
“Haa! Nakuja.”
Martha alitoka mbio hata waombolezaji wengine wakamshangaa.
Alimkuta Roi amekaa kwa kujikunyata akitetemeka baridi.
“Ooh! Pole baby,” Martha alijikuta akisema hivyo.
Alimsimamisha Roi, akamvutia pembeni…
“Nisamehe sana sweet, nilichanganyikiwa. Sikujua kama upo nje, mawazo yangu umeshaondoka,” alisema Martha.
“Nilishindwa kuondoka sista,” alisema Roi kwa sauti ya upole huku akimpa pole Martha kwa msiba…
“Asante sana baby.
Sijajua mazishi itakuaje? Lakini kikao kitakaa baadaye kwenye saa nne asubuhi,” alisema Martha.
Roi aliaga, akaondoka huku Martha akimsindikiza kwa macho yaliyojaa huruma…
“Maskini.
Yaani amekubali kuacha usingizi wake kwa sababu ya msiba wangu.
Huenda Roi si kaka yangu,” alisema moyoni Martha.
***
Baada tu ya kikao cha familia cha kujadili namna ya mazishi ya mume wa shangazi yake Martha, Roi akapiga simu kama alijua vile…
“Kaka…”
“Ee dada! Vipi kuhusu utaratibu?”
“Tunazika kesho saa kumi jioni,
Kinondoni.”
“Ooh! Nakutumia shilingi laki moja na nusu kama mchango wangu.”
“Da! Nitashukuru sana kaka yangu.”
“Poa…poa! halafu kesho nitakuja kwenye mazishi.”
“Sawa kaka, sawa.”
***
Ulikuwa mchana wenye mawazo kwa Martha…akiwa ametulia tuli huku wachache wakiendelea kulia, aliwaza…
“Hivi kweli yule ni kaka yangu au mume wangu? Ina maana anaweza kunijali kiasi hiki kweli?” alijiuliza Martha huku akiiangalia meseji ya pesa aliyotumiwa na Roi.
***
Wiki moja ilikatika tangu mazishi ya mume wa shangazi yake Martha, siku hiyo Martha alikaa kwenye mgahawa mmoja akimshukuru Roi kwa ushirikiano wake katika msiba…
“Wala usijali dada yangu.
Tuko pamoja.”
“Yaani bro kusema ukweli umenipa kampani kubwa sana.”
“Usijali dada yangu.”
“Asante sana,” alisema Martha huku akimwangalia Roi, wakakutana macho, wote wakajikuta wakisisimka…
“Brooo,” aliita Martha kwa sauti iliyojaa mahaba.
Je, unajua nini kiliendelea?