LOOH DADA MARTHA
Sehemu Ya 21
ILIPOISHIA
“Dogo hujambo?” alimsalimia muuzaji.
“Sijambo.”
“Eti, huyu kaka anayekaa hapa huwa anafika muda gani?”
SASA ENDELEA…
“Mh! We ni nani kwani?”
“Mgeni wake.”
“Kutoka wapi?”
“Tanga.”
Muuza duka huyo alimkodolea macho Martha akiwa anaonekana haamini kama alitokea Tanga.
Tanga bila hata kibegi cha nguo!!
“Kwani namba yake ya simu huna?” aliuliza muuza duka huyo.
“Nampigia hapokei.
Nikasema nije hadi hapa ili kama anakuja muda huu nimsubiri kama si muda wake nikatafute gesti ya kulala.
Muuza duka huyo alijua kuna kitu kilimfanya Roi asipokee simu.
Na kitu hicho si kingine ni jamaa huyo kuzama ndani na mwanamke mwingine aliyekuwa amekaa kwenye benchi nje ya duka lake.
Kwa hiyo uamuzi ulikuwa kwake.
Aseme ukweli au adanganye.
Moyoni mwake aliona Roi mwenyewe alitakiwa kuwa muwazi katika mipango yake kuhusu wanawake.
Si vizuri kugonganisha…
‘’Mimi nimemwona kaingia ndani muda si mrefu,’ alisema muuzaji huyo.
Martha akashangaa…
“Kwa miguu?” aliuliza.
“Na gari.”
Martha alitupia macho kwenye geti na kubaini kwamba, ni kweli gari linaweza kuwemo ndani halafu mtu aliye nje asilione…
“Aliingia na nani?”
“Mwanamke mmoja hivi.
Alimsubiri kwa muda mrefu hapohapo nje.”
“Mwanamke mmoja hivi! Kavaaje?”
“Huyo mwanamke kavaa haya magauni yenu ya siku hizi, marefu mpaka miguuni, amelaza nywele kwa nyuma, mweupe kiasi, ana figa namba nane.”
Kwa haraka sana, Martha alimuweka kichwani mama Anna kwani anakumbuka ndiye aliyevaa hivyo inavyosemwa.
“Huyo ni mama Anna tu.
Yaani kumbe…mh! Yaani mama Anna na Roi ni wapenzi? Mbona siamini. Wameanzaje kwanza?”
Martha aliinua simu yake akampigia mpangaji mmoja na kuzungumza naye…
“Hivi unaweza kuamini mama Anna alipotoka hapo kumbe amekuja nyumbani kwa yule mtu wangu?”
“Kweli?”
“Kabisa.
Nimepewa ushahidi wote.”
“Kwa hiyo?”
“Wamo ndani na geti limefungwa.”
“Mh! Mama Anna naye bwana.
Ana maana gani sasa kufanya hivyo kwa mtu wa karibu kama wewe?”
“Ndiyo hapo sasa.
Mimi leo sitoki hapa getini.
Nipo tayari hata kulala hapahapa,” alisema kwa uchungu Martha na kukata simu.
***
Roi na mama Anna walikuwa chumbani sasa, kitandani, wakigalagazana kwa mahaba mazito huku mwanamke huyo akilia kilio cha uongo ili kumkoleza zaidi mwanaume huyo pale kitandani.
Wote walikuwa wamelegea macho kwani kwa mama Anna yeye alishajua jinsi ya kumnasa Roi huku yeye Roi akiwa hoi bin taaban.
Simu ya mama Anna iliita mpaka ikakata, ikaita tena mpaka ikakata, ikaita tena…
“Mh! Hiyo simu itakuwa ya umuhimu kwangu,” alisema Roi na kumtaka mama Anna aipokee…
“Hakuna lolote, haina umuhimu wowote, ngoja niizime tu,” alisema mama Anna akiifuata.
Kabla hajaizima aliangalia missed calls akakuta mbili na zote ni za wapangaji wenzake, akahisi kitu.
Akampigia wa kwanza…
“Vipi mama nanihii…”
“Mwenzangu, Martha yupo getini.
Kasema ana ushahidi umo ndani kwa jamaa yake na hatoki mpaka kesho asubuhi.”
Palepale mama Anna alikata simu, akamwangalia Roi.
Naye Roi akamuuliza…
“Vipi kwani?”
“Martha yupo getini. L
akini ishu si hiyo bali amejua mimi nimo ndani, eti ana ushahidi.”
Roi alikumbuka kwamba, atakuwa ameambiwa na muuza duka ambaye alishuhudia kila kitu…
“Mmh! Atakuwa ameambiwa na muuza duka.
Loo! Sasa?”
“Hata sijui.
Kwani wewe hofu yako ipo kwa kiasi gani?” mama Anna alimuuliza Roi.
“Mimi sina wasiwasi wowote ule.
Nimeamua kuwa na wewe japo kibinadamu nitakuwa nimefanya makosa makubwa, kumuumiza mtu jambo ambalo silipendi katika maisha yangu,” alisema Roi kwa sauti ya upole.
Alitoka kitandani, akavaa.
Mama Anna naye akatoka kitandani, akamfuata kwa nyuma yeye akiwa amejizungusha upande wa kanga.
Walifika sebuleni, wakaangalia kwa nje kupitia nafasi ya matundu ya ukuta wa fensi.
Walimwona Martha amesimama dukani akizungumza na muuza duka.
Sura ya Martha ilitafsiri uchungu wa maumivu ya kutendwa.
Ikawa kama imejikunja, Roi akahisi huruma…
“Martha… Wajina wako anaumia sana. Sasa itabidi nikutoe kiaina.
Pita mlango wa nyuma, nenda mahali hapo nyuma kuna baa, kakae.”
“Mh!” Aliguna mama Anna, akatoa wazo…
“Sawa lakini turudi chumbani, nipe haki yangu kwanza ndiyo nitoke, siwezi kutoka hivihivi wakati uliishaanza kunipandisha mzuka wangu na mzuka wangu ukinipanda mimi akili zinachanganyikiwa kabisa.”
“Kuhusu hilo tu, twende sasa hivi.”
Walikwenda chumbani ambako Roi aliikuta simu yake ikiendelea kuita kwa namba ya Martha.
Mama Anna alikimbilia moja kwa moja kwenye kitanda huku akitupa kanga chini.
Alipokuwa juu ya kitanda akakaa mkao wa mechi tayari akijua anatakiwa kutoka ndani ya nyumba hiyo lakini moyoni alihakikisha anatoa mapigo ambayo, Roi anaweza kuamua asitoke tena na Martha kama kulala nje ya geti alale tu.
Roi, kuona mkao wa mama Anna alichanganyikiwa.
Kama paka aliyeona panya.
Akaenda kitandani kwa staili ya kuruka kama golikipa wa timu maarufu ya Ulaya…puu!!
Je unadhani kwa mshiko Huo aliyeshikwa ROI atafanikiwa kumtoa MAMA Anna kweli, na nini kitafata endela kufatilia CHOMBEZO HILI la aina yake ITAENDELEA
LOOH DADA MARTHA
Sehemu Ya 22
ILIPOISHIA:
Alipokuwa juu ya kitanda akakaa mkao wa mechi tayari akijua anatakiwa kutoka ndani ya nyumba hiyo lakini moyoni alihakikisha anatoa mapigo ambayo, Roi anaweza kuamua asitoke tena na Martha kama kulala nje ya geti alale tu.
Roi, kuona mkao wa mama Anna alichanganyikiwa.
Kama paka aliyeona panya.
Akaenda kitandani kwa staili ya kuruka kama golikipa wa timu maarufu ya Ulaya…puu!!
SHUKA NAYO HAPA…
Palepale alianza kuserebuka na mchezo huku mama Anna akimwangalia kwa hisia kali kama vile alikuwa akitumbuliwa jipu.
Mama Anna aliamua kujilegeza kabisa hivyo alitoa ushirikiano wa hali ya juu bila kuonesha dalili hata ya chembe kwamba kuna jambo hakubaliani na Roi…
“E…eti baby,” aliita Roi…
“Niambie baba…”
“Unaweza kuhama pale?”
“Kuhamia wapi baba angu?”
“Nitakaposema mimi?”
“Naweza ndiyo mume wangu.”
Roi kuitwa mume ndiyo kabisa, akajikuta anawewesekea uwanjani na kelele za mahaba kama vile yeye ndiye mama Anna.
***
Kule nje, Martha alitawala benchi la nje ya duka, mawazo yake yalikuwa usahihi wa mama Anna kuwepo au kutokuwepo ndani ya nyumba ya Roi…
“Ina maana kumbe niliposema nilimsikia mama Anna akimwita Roi baby nilikuwa sahihi? Lakini hawa walikutana wapi mpaka wakafahamiana?,
“Kwa pale nyumbani hapana,haiwezekani. Lini kwanza? Na ilikuaje? Siku zote, Roi anakuwepo wakati ambao na mimi nipo, akitoka kurudi usiku…
“Halafu pia mbona si muda mrefu, Roi kaja kwangu! Hawa huenda wanajuana kabla ya hapa. Itakuwa hivyo, wanajuana kabla ya hapa,” aliwaza moyoni Martha akijihisi unyonge f’lani hivi.
“Lakini wewe Mangi utakuwa unamjua vizuri sana huyu kama anayeishi hapa.
Hivi, ni mwadilifu kiasi gani?” Martha alimuuliza muuza duka…
“Nani, Harson?” muuza duka aliuliza naye…
“Kwani huyu kaka mwenye nyumba hii anaitwa Harson?”
“Ndiyo.”
“Mh! Siyo Roi?”
“Mh! Mi silijui jina la Roi, namjua kama Harson.”
Martha alianza kuingiwa na wasiwasi zaidi.
Akahisi huenda Roi kujiita Roi alimwingiza mkenge, Na kama ni kweli halafu mpaka wameingia kwenye uhusiano hakusema ukweli wa jina lake, Martha alianza kuona kumbe alikutana na mwanaume tapeli…
“Labda ni jina la mtaani,” alisema Martha na kuomba Mungu iwe hivyo.
Mara mzee mmoja mteja aliwasili dukani hapo na kumwangalia sana usoni Martha…
“We binti kama nakufahamu,” alisema mzee huyo…
“Mimi sikufahamu.”
“We siye mdogo wake Benard?”
Ni kweli, Martha ana kaka yake anaitwa Benard.
Ni machepere ile mbaya…
“Kweli Benard ni kaka yangu,” alisema Martha…
“Sasa je? Sasa Benard ni rafiki wa mtoto wangu, Mawazo.
Akili zao kama sawasawa.
Mimi nilikuona siku moja tu pale Kituo cha Polisi Urafiki wakati kaka yako na Mawazo walipowekwa ndani…”
“Kweli, nimekumbuka,” alisema Martha akiwa amemkumbuka mzee huyo ambaye umri ulikwenda sana…
“Haya! Mimi naishi nyumba ile ya tatu kutoka hapa.
Hapa umefuata nini sasa?” aliuliza mzee huyo huku mkono wake mmoja ulioshika noti ya shilingi mia tano ukiwa umeshaingia kwenye dirisha la kuhudumiwa dukani hapo…
“Nina shida na kaka mmoja anaishi nyumba hiyo yenye geti jekundu,” alisema Martha huku macho yake yakielekea kwenye nyumba ya Roi…
“Nani, Ismaili?” aliuliza mzee huyo.
“Kwani anaitwa Ismaili?”
“Ee… ndiyo jina lake,” alisisitiza mzee huyo huku na yeye macho yake yakitua kwenye geti la nyumba hiyo.
Martha na muuza duka wote wakabaki wametumbua macho…
“Au wewe unamsema mwingine?” aliuliza Martha…
“Jamani! Kwani kwenye nyumba hiyo kunaishi watu wangapi? Si mmoja tu, kijana kijana hivi…mweusi, ana gari lina rangi ya kijiko cha chai ‘silva’.”
“Ee…” alikubali Martha…
“Ndiyo, anaitwa Ismaili.
We alikwambia anaitwaje?”
“Mimi namjua kwa jina la Roi…”
“Mh! Roi tangu lini? Yule anaitwa Ismail Twalib Mussa.”
“Mimi namjua kwa jina la Harson,” alidakia kijana muuza duka.
“Hakuna bwana, Anaitwa Ismail.”
Mara, gari jeusi lilifika na kupaki getini kwa Roi, wakashuka wanaume wawili, wakiwa wamevaa suti nyeusi.
Wakatembea kuelekea pale dukani.
Wakasalimia wote kisha mmoja wao akauliza…
“Jamani tuna shida na Edo…anaishi kwenye nyumba hii,” alisema akionesha kidole nyumba ya Roi…
“Sisi hatujamwona…kwenye simu vipi?” alidakia mzee huyo…
“Simu yake inaita tu hapokei,” alisema mmoja wa wanaume hao huku wakirudi ndani ya gari na kuondoka zao…
“Sasa hawa jamaa wanasema anaitwa Edo..mimi najua anaitwa Ismaili…wewe unasema unamjua kwa jina la Roi…huyu muuza duka anasema anaitwa Harson,. Huyu kijana si kawaida,” alisema mzee huyo akionekana kushangaa, akamwangalia Martha…
“Kwani wewe binti, unamfahamu kivipi?” mzee huyo alimuuliza Martha huku akimshika mkono na kwenda naye kando…
“Mimi ni jamaa yangu babu…”
“Jamaa yako?”
“Ndiyo babu, kwani vipi?”
“Ha! Sasa mbona watu mtaani pote hapa wanajua ni kijana mwathirika.”
“Mwathirika?” aliuliza kwa sauti Martha, macho yakapoteza uwezo wa kuona, akaanguka chini.
***
Kule chumbani, sasa Roi alikuwa akikaribia ushindi wa pili na alishatangaza nia.
Mama Anna alikuwa amemkaribisha kwa shangwe huku akimuuliza anataka kumhamishia sehemu gani katika Jiji la Dar es Salaam…
“Si…sinza ku…na kufaa…”
“Sawa, tena Kwaremi…Kwaremi ndiyo kwenyewe,” alisema mama Anna huku mikono yake yote ikiwa mgongoni mwa Roi akimpa joto ambapo mlio wa geti kubwa la nje kugogwa ulisikika kwa nguvu…
“Mungu wangu, atakuwa nani amejitoa ufahamu mpaka kuamua kugonga geti langu?” alijihoji Roi akiwa anatafuta namna ya kutoka kwa mama Anna,.
Masikini MARTHA kazimia kwa taarifa mbaya za kijana ROI mwenye majina tofauti tofauti, huku akidhadikika kuwa ni mwadhrika wa gojwa hatari la UKIMWI Na upande wa pili kijana ROI anatafutwa kwa UDI NA UVUMBA huku geti lake lake likigogwa kwa KASI, je jina la ROI halisi anaitwa nani, na kwanini anatafutwa na hatima yake ni nini!??,
LOOH DADA MARTHA
Sehemu Ya 23
ILIPOISHIA:
“Mungu wangu, atakuwa nani amejitoa ufahamu mpaka kuamua kugonga geti langu?” alijihoji Roi akiwa anatafuta namna ya kutoka kwa mama Anna.
JIACHIE MWENYEWE SASA…
Roi alijitoa, akavaa bukta na kwenda sebuleni.
Lakini akili ikamwambia kwamba amalizane na mama Anna kwanza, atoke kisha yeye amfungulie Martha wayaongee na kuyamaliza…
“Atanielewa tu,” alisema moyoni Roi.
Alirudi chumbani, kweli alimalizana na mama Anna na akamtoa huku mwanamke huyo akiamini kwamba, Roi hatamudu kukutana kimwili tena na Martha labda mpaka waende kwake au kama watalala hapohapo, basi usiku sana.
Wakati Roi anamtoa mama Anna, alimuahidi kwamba, atampa pesa kwa ajili ya kupanga chumba Sinza kama walivyokubaliana.
“Poa baby,” alikubali mama Anna akiwa anatoka geti la uani ambalo lipo ubavuni mwa nyumba hiyo na kutokomea upande wa pili kwa nyuma.
Roi alirudi chumbani na kumpigia simu Martha.
Martha akiwa bado dukani baada ya kugonga sana geti, alishangaa kuona simu ya Roi, akaipokea haraka sana huku akisema moyoni…
“Utadhani alikufa sasa amefufuka.
Ngoja nimsikilize, Si ajabu anajua mimi nipo nyumbani, hajui kama nipo getini kwake…”
“Haloo…”alipokea Martha…
“Ee, nilikuwa sebuleni, simu ilikuwa kwenye chaja chumbani.
Si unajua sijabeba chaja kuja nayo huko…”
“Roi,” aliita Martha…
“Sema…”
“Una uhakika upo sebuleni?”
“Kha! Sasa nipo wapi kama si sebuleni? Au wewe upo sebuleni kwangu?”
“Mimi nipo nje kwako hapa.
Na nimeambiwa mengi sana kuhusu wewe.”
“Mengi kama?”
“Wewe unajijua, Unajua uko wapi na nani! Kama kweli upo sebuleni toka unifungulie geti.”
“Poa,” alijibu Roi na kukata simu huku moyoni akisema…
“Haya ndiyo mambo nisiyoyataka.
Anaanzaje kunikontroo wakati anajua mimi si mume wake?”
Martha, alikwenda getini na kupiga kambi hapo akisubiri kufunguliwa.
Yeye alijua Roi hawezi kufungua na kama atafungua kweli basi atakuwa ameongozana na mama Anna.
Alishangaa geti limefunguliwa, Roi akiwa ndani ya bukta tu, tena akionesha hana wasiwasi wowote ule…
“Unajua nikiwa hapa nyumbani sipendagi kuacha geti wazi.
Si unajua naishi mwenyewe?” alisema Roi akimbusu Martha ambaye alikuwa mbali sana kimawazo…
“Ina maana maneno ya muuza duka si ya kweli?” alijiuliza Martha akiwa hajui akubali au akatae.
Walizama mpaka sebuleni, Roi akakaa hapo kisha akamwambia Martha kama amefika kufanya usafi, aanze na chumbani.
Martha alisimama, akaenda chumbani.
Lakini akashika mlango wa chumba cha kwanza, akaufungua, hakuona mtu, akashika mlango wa chumba cha pili, hakuona mtu, akaenda jikoni, hola. Akaenda stoo, hakuna kitu, akaenda chooni na bafuni hakukuwa na dalili ya kuwepo mtu…
“Mh! Basi yule kijana ni mwongo mkubwa. Afadhali hata ningemwona mwanamke, hata kama si mama Anna kuliko kutokuwa na mtu yeyote yule,” alisema moyoni Martha akiingia chumbani.
Sebuleni, Roi alikuwa kwenye kompyuta mpakato akibofyabofya huku akijivunia ushindi wake kwa mama Anna.
Martha alifanya usafi sehemu mbalimbali za nyumba hiyo hadi akafika sebuleni, kisha uani.
Alipofika uani, kwa mara ya kwanza alibaini kuwepo kwa mlango mdogo ambao mtu anaweza kutoka nje.
Lakini ulikuwa umetiwa kufuli…
“Aa…aaaaa! mama Anna alikuwepo, ametokea mlango huu.
Sasa nimejua,” alisema moyoni Martha huku hasira za wivu zikimpanda kama mwanamke.
Ili aujue ukweli alimfuata Roi sebuleni na kumwambia ampe funguo za mlango huo ili akatupe taka nje…
Kwa kujikaza sana, Martha alisema…
“Baby, naomba funguo za mlango wa uani.
Nataka kutupa takataka.”
Roi naye alijua kimenuka au kitanuka, kwamba Martha atajua nini kiliendelea…
“Ooh! Baby, ule mlango tangu nimehamia nyumba hii haujawahi kufunguliwa na wala sijawahi kuona funguo yake.
Pia kwa sababu ni uchochoroni sijawahi kutaka kuufungua,” alisema Roi kwa macho makavu kabisa.
Martha alikubaliana na utetezi wa Roi, moyo wake ukarejea katika hali yake ya kawaida.
***
Mama Anna alipotoka hapo, moja kwa moja alikwenda nyumbani na kuwasimulia wale mashoga zake, wapangaji wenzake kilichojiri nyumbani kwa Roi.
Walicheka sana na kumshauri…
“Wewe usiwe mjinga.
Pesa za kupanga za nini? Usipokee. Unachotakiwa kufanya wewe ni kung’ang’ania kuishi kule kwake.
Mwambie wewe utakuwa unaishi kule yeye na Martha waishi hapa.
Kwa hiyo akitoka kazini anakufuata kule. Mnajirusha halafu midamida anakuja huku,” alisema mmoja wa wanawake hao.
Mama Anna alikubaliana na ushauri huo kwani kwake aliuona kama ni wa kuweza kumfikuisha kwenye ndoa kabisa na kumpiku Martha.
***
Martha na Roi waliwasili nyumbani hapo, usiku wa saa tatu.
Waliwakuta wapangaji wapo nje bado wakipiga domo licha ya kibaridi cha mbali.
Macho ya Martha yalitua kwenye sura ya mama Anna, akakasirika kwa mbali.
Kilichomshtua zaidi Martha na gauni alilovaa mama Anna muda huo ndiyo lilelile ambalo aliambiwa na muuza duka kwamba, mwanamke aliyeingia na Roi ndani alikuwa amevaa…
“Inawezekana kweli mama Anna alikuwa amekwenda kula kwa Roi lakini labda hakukaa sana akatoka ila yule kijana wa dukani hakumwona ndiyo maana alijua bado yupo,” alisema moyoni Martha…
“Jamani za leo?” alisalimia Roi akiwa nyuma ya Martha wakiingia ndani…
“Nzuri tu za kwako shemeji?”
“Salama za kazi shemeji?”
“Salama za kazi honey,” alijibu mama Anna kwa sauti ya chini…
Dohh kumechimbika, Unadhani marthaa hajasikii neno hilo tamu lenye mvuto kweli ,bs tukutane hapa hapa
LOOH DADA MARTHA
Sehemu Ya 24
ILIPOISHIA:
“Wewe usiwe mjinga.
Pesa za kupanga za nini?
Usipokee.
Unachotakiwa kufanya wewe ni kung’ang’ania kuishi kule kwake.
Mwambie wewe utakuwa unaishi kule yeye na Martha waishi hapa.
Kwa hiyo akitoka kazini anakufuata kule. Mnajirusha halafu midamida anakuja huku,” alisema mmoja wa wanawake hao.
SASA ENDELEA MWENYEWE…
Mama Anna alikubaliana na ushauri huo kwani kwake aliuona kama ni wa kuweza kumfikisha kwenye ndoa kabisa na kumpiku Martha.
***
Martha na Roi waliwasili nyumbani hapo, usiku wa saa tatu.
Waliwakuta wapangaji wapo nje bado wakipiga domo licha ya kibaridi cha mbali.
Macho ya Martha yalitua kwenye sura ya mama Anna, akakasirika kwa mbali.
Kilichomshtua zaidi Martha ni gauni alilovaa mama Anna muda huo ndiyo lilelile ambalo aliambiwa na muuza duka kwamba, mwanamke aliyeingia na Roi ndani alikuwa amevaa…
“Inawezekana kweli mama Anna alikuwa amekwenda kule kwa Roi lakini labda hakukaa sana akatoka ila yule kijana wa dukani hakumwona ndiyo maana alijua bado yupo,” alisema moyoni Martha…
“Jamani za leo?” alisalimia Roi akiwa nyuma ya Martha wakiingia ndani…
“Nzuri tu za kwako shemeji?”
“Salama za kazi shemeji?”
“Salama za kazi honey?” alijibu mama Anna kwa sauti ya chini kiasi kwamba, Martha alijua amezungumza kitu kwa sauti ya chini ambayo hakuisikia hali iliyompa dukuduku kubwa sana…
“Baby,” Martha alimuita Roi wakiwa wameshazama ndani kwao…
“Yes! Niambie…”
“Mimi nahisi huyu mwanamke huyu…mama Anna ana jambo na wewe lakini sijalijua, Ila nalifanyia kazi.”
“Jambo kama lipi?”
“Kuna jambo, Mfano, hapo wakati tunaingia wenzake wamekusalimia.
Hata yeye amekusalimia, lakini kuna maneno f’lani ameyasema naamini siyo salamu na ameyasema kwa sauti ya chini sana.”
“Mh! Mimi sijui kwa kweli, Labda ana mambo yake mwenyewe,” alijibu Roi huku moyoni akiujua ukweli.
***
Ilikuwa saa nne usiku, Martha akiwa anapiga pasi sebuleni, Roi yuko chumbani.
Nje, usawa wa dirisha la sebuleni kwa Martha, alikaa mama Anna peke yake.
Alikuwa akichati na Roi kule chumbani.
Alichokishangaa Martha, simu ya Roi ilipotoa mlio wa meseji, baada ya dakika kadhaa, simu ya mama Anna kule nje nayo ilitoa mlio wa meseji.
Martha alishtuka, hasa baada ya kubaini kuwa, milio hiyo ya meseji ilikuwa ikipokezana kusikika.
Kwamba, unapolia wa simu ya Roi, baada ya muda unadakia wa simu ya mama Anna…
“Mh!” aliguna Martha, akaacha kupiga pasi, akasimama kusikilizia kwa umakini zaidi…
“Titiri…titiri…” huo ulikuwa mlio wa simu ya Roi…
“Titiiiti…” huo ulikuwa mlio wa simu ya mama Anna.
Martha aliingia chumbani, akampiga jicho moja Roi, akamwona akiweka simu juu ya dressing table…
“Baby, nataka kumpigia simu bro, lakini kumbe simu yangu sijaweka salio, niazime ya kwako nimpigie,” alisema Martha…
“Mh! Hata yangu haina salio, chukua elfu mbili hii ukanunue vocha,” aliwahi kusema Roi, Martha akaanza kushtuka.
Aliamini Roi alikuwa akichati na mama Anna nje.
Alikwenda dukani kununua vocha, wakati anarudi alisimama chini ya mti wenye giza na kumwangalia mama Anna anavyoongea na simu huku akicheka…
“Teh! Teh! Mimi ni mashine baby…tena nakwambiaje?
Siku akijua naamini patachimbika.
Lakini mimi wala simuogopi,” alisema mama Anna huku akicheka.
Akaendelea…
“Duu! Baby, mfano pale kwako.
Mimi miguu yote ilinyong’onyea, nikajua tumekwisha! Loo!”
Martha alipojitokeza, mama Anna alishtuka, akapunguza sauti huku akisema…
“Basi tufanye kesho baby wangu, usiku mwema.”
Martha alipita bila kusema kitu kwa mama Anna, akazama ndani na kumpa Roi vocha ya buku, akabaki na ya buku kuingiza kwenye simu yake.
***
Ilikuwa saa saba usiku, Martha alichelewa kupata usingizi kwa mawazo kuhusu kutaka uhakika wa kuwepo kwa mawasiliano kati ya mama Anna na jamaa yake, Roi…
“Hivi kama ni kweli nichukue hatua gani?” alijiuliza moyoni Martha…
“Na yale mazungumzo ya kwenye simu ya mama Anna muda ule mbona ni kama alikuwa akiwasiliana na Roi?”
Ghafla alipata wazo, alitoka kitandani huku macho yake yakitua kwa Roi.
Alipobaini anauchapa usingizi mzito, aliifuata simu yake, akaichukua na kwenda nayo sebuleni.
Aliikuta simu hiyo haina ‘password’ kwa hiyo akaingia ndani moja kwa moja kwenye kiboksi cha meseji…
“Baby, unajua wakati tunaongea ghafla akatokea demu wako, ndiyo maana nikakuaga.”
Meseji hiyo ilitoka kwa mama Anna kwenda kwa Roi.
Martha aliishiwa nguvu, nusura aanguke. Akaendelea kusoma nyingine…
“Basi usiku mwema baby.
Nimekumisije jamani!”
Roi naye akajibu…
“Mimi je? Natamani kesho ifike haraka tukutane unikate kiu yangu.
Lala salama mpenzi wangu nikupendaye.”
Martha alisimama, akamwomba Mungu kwanza kisha akajipa moyo na ujasiri wa hali ya juu.
Akatuma meseji kwa mama Anna…
“Baby…”
Ingawa ilikuwa usiku sana, Martha akaamini atajibiwa, lakini hakujibiwa, akatuma nyingine…
“Jamani baby, naomba nije kwako basi, nimekumisi kweli mwenzio.”
Dakika zilikatika, hakupata jibu.
Akazifuta meseji zake hizo mbili na kuamua kurudi chumbani kulala.
Alitamani sana kumwamsha Roi ili ambane kuhusu meseji hizo lakini akajivumilia.
Aliirudisha simu mahali alipoichukua na kulala.
***
Kulikucha, Martha aliamka na kuanza kufanya kazi za ndani lakini siku hiyo hakumwamsha Roi mpaka alipoamka mwenyewe.
Roi, kabla hajatoka kitandani, aliichukua simu na kuangalia meseji, akakutana na meseji ya mama Anna ikiomba radhi…
“Baby samahani, ulipotuma meseji usiku nilikuwa nimelala fofofo mwenzako.
Halafu uliposema umenimisi unataka kuja ulikuwa unamaanisha au utani tu? Bibiye ungemwachaje kitandani peke yake?”
**”
Je ROI atamjibu nini Anna ama ndho siri ya ROI itaenda kufichuka, vipi kwa upande wa Martha atafunguka kwa ROI ???
LOOH DADA MARTHA
Sehemu Ya 25
ILIPOISHIA:
“Baby samahani, ulipotuma meseji usiku nilikuwa nimelala fofofo mwenzako.
Halafu uliposema umenimisi unataka kuja ulikuwa unamaanisha au utani tu? Bibiye ungemwachaje kitandani peke yake?”
SASA JIACHIE MWENYEWE…
Roi alishtuka sana.
Akaangalia kama alituma meseji amesahau, hakuona meseji yoyote.
Akahisi huenda meseji hiyo ya mama Anna ilimfikia yeye kwa bahati mbaya tu, akamuuliza…
“Sweet, meseji hii ya nani?”
Akajibiwa…
“Ya nani kwani darling.
We unadhani inaweza kuwa ya nani zaidi yako jamani? Au unanituhumu kwamba nina mchepuko?”
“Mh!” Roi aliguna kwanza.
Akakaa kitandani na kufikicha macho. Bado aliamini mama Anna anajitetea tu…
“Mimi nilikutumia meseji wewe ya kukutaka nije kwako?”
“Ndiyo. Kwani si imekuja kwa namba yako baby! Acha hizo bwana.”
Roi alitoka kitandani, akasimama na kujishika kichwa.
Mapigo ya moyo yakamwenda kwa kasi ya ajabu.
Aliizima simu, akaenda kuoga.
Aliporudi alivaa kisha akamuaga Martha kwamba anaondoka…
“Baadaye baby.”
“Poa sweetheart,” Martha alimjibu kama hakuna lolote jambo ambalo lilizidi kumchanganya Roi.
Hatua kumi hazikufika baada ya kutoka na gari, Roi alimtumia meseji mama Anna akimtaka akae sehemu nzuri anataka kumpigia simu…
“Piga tu baby, niko chumbani bado nimelala, Kwani we umeshatoka kwenda kazini?”
Roi hakujibu meseji ya kuulizwa kama ameshatoka kwenda kazini, Alichofanya yeye alimvutia uzi moja kwa moja…
“Yes baby, niambie,” alipokea mama Anna kwa sauti iliyojaa kudeka kimahaba…
“Hivi ulichosema ni kweli au utani?” aliuliza Roi…
“Kwamba?”
“Kwamba nilikutumia meseji ya kutaka nije kwako?”
“Khaa! Jamani! Sasa …kwanza nikuulize baby, kwani jana ulilewa?”
“Sikulewa, Hata wewe unajua sikulewa.”
“Sasa kwa nini usijue kama ulinitumia meseji mimi mke wako?”
“Sijatuma meseji ya hivyo kwako, Imeingia saa ngapi?”
“Mh! Hujatuma? Ilikuwa usiku kama saa saba hivi.”
“Kweli?”
“Kweli baby.”
“Meseji ngapi?”
“Mbili.”
“Zilisemaje?”
“Ya kwanza uliita baby…ya pili ukasema jamani baby, naomba nije kwako basi, nimekumisi kweli mwenzio.”
Roi alikosa nguvu, kidogo aiingize gari kwenye mtaro, Ni Mungu tu alimsaidia…
“Mimi siamini mpaka nizione hizo meseji kama kweli zimetoka kwenye namba yangu ya simu.”
“Ina maana huamini?”
“Siamini.”
“Nije ofisini kwako muda huu?”
“Itakuwa vizuri aisee, Njoo,” alisema Roi.
Roi alimwelekeza mama Anna ofisini kwake akimsisitizia kwamba aende na Bajaj, yeye atalipa.
***
Mama Anna naye alianza kuingiwa na wasiwasi.
Alijua kama Roi hakutuma meseji zile basi aliyetuma ni Martha.
Alitungua taulo, akavaa, akatoka kwenda uani kwa sababu mbili.
Kwanza akamwone Martha anafananaje! Sura yake inasema kwamba kuna donge moyoni au kawaida.
Pia, akaoge tayari kwa kwenda mjini kazini kwa Roi.
Hakumwona Martha zaidi ya wale wapangaji wenzake wawili…
“Jamani kimenuka,” alisema Martha.
“Ki nini?”
“Martha alichukua simu ya jamaa yake usiku akanitumia meseji mimi.”
Wale walishtuka sana…
“Kwa hiyo wewe ukajibu nini?”
“Sikujibu, nilikuwa nimelala.”
“Loo! Sasa?”
“Hata sijui, naoga nakwenda kazini kwake muda huuhuu.”
Mama Anna mpaka anaondoka,
hakuonana na Martha.
Alifuata maelekezo mpaka akafika ofisini kwa Roi.
Kitu cha kwanza, Roi aliomba simu ya mama Anna na kuangalia meseji.
Kweli zilitoka kwenye simu yake…
“Daa! Hatari.
Hizi alituma Martha kweli.
Na kama alituma yeye ina maana kwamba aliziona meseji zote za awali ambazo mimi nilikutumia,” alisema Roi akiwa tayari na macho mekundu.
“Sasa itakuaje?” alihoji mama Anna…
“Hamna jinsi.”
“Jinsi ipo.”
“Ipi?”
“Akikuuliza mwambie mimi ni dada yako.”
“Ah! Kwa zile meseji halafu niseme wewe ni dada yangu, inakuja kweli?”
“Inakuja.
Huna utetezi mwingine kwa siku ya leo.
Lakini pia si ulisema unataka kumwacha Martha uwe na mimi tu, yameishia wapi mpaka unakuwa mwoga?” aliuliza mama Anna kwa sauti iliyojaa ujasiri wa hali ya juu.
“Ni kweli, lakini si katika mtindo wa kukuta meseji zako kwenye simu yangu.
Nilitaka iwe amani tu.”
“Ameshakuta sasa, itakuaje?”
“Hata sijui.”
“Ndiyo ujue sasa.
Mimi nakushauri jambo moja mpenzi wangu.”
“Lipi hilo baby?”
“Mimi na Martha wajina wangu, nani unampenda zaidi?”
“Martha wewe.”
“Basi mtumie meseji kwamba umeamua kuwa na mimi, hivyo jioni utakwenda kuchukua nguo zako tu.”
“Mh! Atakuibulia ugomvi wewe.”
“Mimi nipo tayari.”
Wakati wakizungumza hayo, mara Martha akaingia…
Je unadhani kutatokea nini dahh Martha ndani ya NYUMBANI kuna usalama kweli!!?