BINTI NGUVA
EPISODE 7
Alice hakuwa na namna bali kufuata wito wa baba yake. Mwisho wa siku, hakuwa tayari kusababisha vita kati ya dunia ya bahari na dunia ya binadamu. kwa sababu aliijuwa tabia ya baba yake hajawahi pindisha neno au kitu alichokisema
……..aliona mambo yasiwe mengi kabisa
bora arudi ili akomboe maisha ya wengi
sababu yeye pekee hawezi kufanya maisha ya watu yakaharibika ………
Akiwa ameingia ndani ya kasri la kifahari lililoko chini ya bahari, Alice macho yake yalikutana na ya baba yake , mzee mwenye uso wa hasira na nguvu zisizokuwa na kifani.
Baba Alice: (kwa hasira) “Wewe mtoto wa hovyo! Unawezaje kusaliti familia yako kwa kujipendekeza kwa binadamu, maadui wetu wa milele? Umeshindwa hata kuheshimu heshima ya kifalme unayopewa!”
“kingine ulivokuwa mjinga na hujitambuwi
,unajuwa kabisa hawa wanadamu ndo walimuua mama yako tena leo upo nao unakula nao …….
Alice aliinama kwa aibu , machozi yakimdondoka.
Alice: (kwa sauti ya chini) “Baba, sikusudia kuwasaliti. Niliona tu kuwa Kelvin hana ubaya. Hakuwa adui bali…”
Kabla hajamaliza, baba yake alimsogelea kwa kasi na kumzaba kofi kali usoni.
(Paaah!)
Alice alianguka chini, akitetemeka huku
akishikilia shavu lake lililokuwa linauma kwa uchungu. Baba yake aliendelea kumfokea kwa hasira.
Baba Alice: “Hautakiwi hata kuthubutu kujaribu kuwataja binadamu mbele yangu! Wewe ni mtoto mshenzi, na ukijaribu tena, nitaangamiza dunia yote ya binadamu kwa ajili ya upumbavu wako!”
Alice aliendelea kunyamaza, akijaribu kujizuia kulia zaidi. Hata Sabrina, ambaye alikuwepo pembeni, alionekana kushtushwa na hasira ya baba yao.
Baba Alice: (akigeukia walinzi)
“Mchukueni huyu mtoto, mfungieni kwenye chumba cha adhabu! Nilitahadharisha kila mtu kuwa yeyote anayesaliti bahari atapata adhabu kali, na yake hatakuwa tofauti na wengine “
Walinzi wawili wakubwa wenye miili yenye magamba ya samaki walimsogelea Alice, wakamshika kwa nguvu na kumburuza kuelekea kwenye chumba cha barafu. Alice hakupinga, akijua kuwa kupinga kutazidisha mateso yake.
Walipofika kwenye chumba hicho, mlango mkubwa wa chuma wenye kufunikwa na
alama za kifalme ulifunguliwa. Ndani,
kulikuwa na baridi kali iliyosababisha pumzi ya mtu yeyote kuganda mara moja. Ukuta wa chumba hicho ulikuwa umefunikwa na barafu, na sakafu yake ilikuwa kama kioo kilichogandishwa.
Walinzi walimtupa Alice kwenye chumba hicho na kufunga mlango kwa nguvu.
Walinzi: (kwa sauti ya kikatili) “Utakaa hapa kwa siku tatu. Hii ndiyo adhabu ya kusaliti familia yako.”
Alice alikaa chini, akikumbatia mwili wake kwa mikono yake, akitetemeka kwa baridi kali. Machozi yalichanganyika na baridi
kali, yakiganda kwenye mashavu yake.
Moyoni mwake, alijiuliza kama uamuzi wake wa kumlinda Kelvin ulikuwa sahihi au la.
Huku akiwa ameketi gizani na baridi, Alice alikumbuka maneno ya Kelvin na tabasamu lake la kweli. Hiyo pekee ilimpa matumaini kidogo, ingawa hali aliyokuwa nayo ilimfanya ajihisi kama maisha yake hayana thamani tena.
Je, Alice ataweza kuvumilia mateso haya? Na Kelvin atagundua kuwa Alice hayupo tena? Endelea kusoma ili ujue jinsi vitendo
vya Alice vitakavyoathiri maisha yao wote
wawili.
TUNAENDELEA ………………………
Haya ni mandhari ya chumba ambacho Alice amewekwa ……
Chumba cha barafu kilikuwa na ukubwa wa wastani, lakini hali yake ilifanya kiwe cha kutisha. Ukuta wote wa chumba ulikuwa umefunikwa na safu nene za barafu iliyong’aa kama vioo, ikionyesha taswira ya Alice kila alipogeuka. Dari ya chumba hicho ilikuwa na matone ya maji yaliyoganda katikati.., yakionekana kama sindano zilizotundikwa angani. Sakafu ilikuwa imesawazishwa kwa barafu
tambarare na ilikuwa baridi kiasi cha
kuuma miguu, hata kupitia ngozi nene.
Mwanga uliingia kwa mwanya mdogo kwenye mlango wa chuma, mwanga huo ukitengeneza mwanga mdogo ndani ya giza kuu. Hakukuwa na joto hata kidogo; kila pumzi ya Alice ilitoka kama moshi mwembamba, na kelele pekee iliyosikika ilikuwa ni sauti ya upepo wa baridi uliozunguka chumbani humo, ukitoa milio ya kutisha.
Siku ya kwanza, Alice alijaribu kuvumilia kwa kujibana kwenye kona moja ya chumba, akijaribu kujisitiri kutokana na
baridi kali. Mikono yake ilikufa ganzi,
midomo yake ilibadilika kuwa ya rangi ya bluu, na mwili wake wote ulikuwa unatetemeka bila kukoma. Kila dakika ilikuwa ni kama saa nzima kwake lakini alivumilia .
Kila alipojaribu kusimama, miguu yake iliyoganda ilikataa kushikilia uzito wake. Akiwa hana nguvu, alirudi kuketi kwenye barafu baridi, akisikia maumivu makali kama sindano zikimchoma mgongoni. Hakukuwa na chakula wala maji, na kufikia mwisho wa siku, Alice alihisi kizunguzungu kutokana na njaa na kiu.
Siku ya pili, hali ilikuwa mbaya zaidi. Alice
alianza kuhisi kama ngozi yake inakauka kwa baridi, na kila alipohema, kifua chake kiliuma. Hakuna usingizi alioweza kupata, maana baridi ilimfanya ajihisi kama mifupa yake inavunjwa polepole. Mawazo ya kukata tamaa yalianza kumwingia, lakini kumbukumbu ya Kelvin na sababu za kumlinda zilimpa nguvu ya kuvumilia.
Siku ya tatu, Alice alikuwa karibu kuzimia. Macho yake yalikuwa mazito, na hakuweza kuhisi miguu wala mikono yake tena. Alijiona kama anakaribia kufa, akijiona mwenyewe kwenye kioo cha barafu, dhaifu na asiye na msaada.
Kila dakika ilizidi kuwa ngumu, lakini
alijikumbusha kuwa hatima yake ilikuwa mikononi mwa baba yake. Hali yake ilikuwa mbaya kiasi cha kwamba wakati walinzi walipokuja kumtoa chumbani humo, mwili wake ulirudiwa rudiwa mara mbili kutokana na baridi kali.
Adhabu hiyo ilikuwa ya kikatili, na ilimwacha Alice akijua kwamba ukaribu wake na unaweza kumgharimu kila kitu, hata maisha yake. Lakini moyoni mwake, hakujuta hata kidogo kwa kumlinda Kelvin na binadamu wengine , maana kwake, heshima ya moyo wake ilikuwa kila kitu.
UPANDE WA KELVIN………..
Baada ya Alice kuondoka ghafla, Kelvin alihisi kama sehemu ya moyo wake imeondolewa. Hakuwa na majibu ya maswali yake mengi: “Alice ameenda wapi? Kwanini alionekana kama mtu mwenye siri nyingi? Je, nitamuona tena?” Kila sekunde ilionekana ndefu zaidi, na mawazo ya Alice yalichukua kila wazo lake, yakimtesa kama kivuli cha huzuni.
Usiku wa Kwanza
Kelvin alijaribu kulala, lakini kila alipojitupa kitandani, picha ya tabasamu la Alice ilionekana kichwani mwake. Alikumbuka jinsi Alice alivyosimama
mbele ya moto wa jiko, akijaribu kuwasha
gesi bila mafanikio. Alikumbuka harufu ya samaki waliokaangwa, sauti nyororo ya kicheko chake, na namna macho yake yalivyoangaza, kama bahari isiyo na mwisho.
Aliamka katikati ya usiku mara kadhaa, akijikuta akimuita kwa sauti ya chini, “Alice… uko wapi?” lakini majibu yalikuwa ukimya wa chumba chake cha giza.
Kelvin alijaribu kupuuza hisia zake kwa kazi. Alijishughulisha sana kupika, kusafisha, na hata kwenda baharini kuvua samaki. Lakini kila samaki aliyemtoa
majini ulimkumbusha sura ya Alice.
Mawimbi ya bahari yalionekana kuimba jina lake.
Wakati mwingine, Kelvin alijikuta akitazama mbali kwenye upeo wa bahari, akihisi kama Alice alikuwa sehemu fulani, akimwita kimya kimya. Alijaribu kufuta picha yake kwa kujishughulisha na marafiki, lakini hata mazungumzo yalihisi kama mzigo, maana akili yake ilikuwa mbali, ikimtafuta mwanamke aliyemvutia kwa njia isiyoelezeka.
Kelvin aliwaza: “Labda ni mawazo tu. Labda sina budi kuendelea na maisha
yangu.” Alijaribu kusoma vitabu, lakini kila
hadithi aliyoisoma ilihusiana kwa njia fulani na Alice. Alijaribu kuongea na wanawake wengine, lakini hakukuwa na hata mmoja aliyeweza kulingananishwa naye. Alice hakuwa tu mrembo; alikuwa wa kipekee, mwenye mvuto wa ndani ambao Kelvin alihisi mara moja.
Kufikia siku ya tatu, Kelvin hakuwa na hamu ya kula wala kufanya kazi. Alikaa tu kando ya dirisha lake, akiangalia jinsi jua linavyotua baharini, akiota kuwa Alice angejitokeza, akigonga mlango wake na kusema, “Nimerudi.” Hata hivyo, kilichokuwepo kilikuwa ukimya tu.
Mara kadhaa, Kelvin alijilaumu: “Labda
nilifanya makosa. Labda sikumwonyesha jinsi alivyokuwa wa muhimu kwangu. Je, nitamuona tena?” Mawazo haya yalizidi kumtesa, hadi hata marafiki zake waliona mabadiliko.
Kelvin alikumbuka maneno ya mzee Ismaili: “Mapenzi ya kweli hayajifichi; hujitokeza bila hofu.” Aliahidi moyoni mwake kuwa, ikiwa kuna nafasi yoyote ya kumuona Alice tena, hataacha kumwambia jinsi anavyomhitaji. Lakini kwa sasa, alibaki na kumbukumbu pekee, kumbukumbu zilizojaa maumivu na matumaini yasiyokufa.
UPANDE WA GOOODLUCK ………………..
Alikuwa akitembea usiku akijisemea “kila nikijaribu kumuua inashindikana
,nimfanyaje huyu mweu ????? alizidi kutembea lakini kuna mtu mmoja alikuwa kavaa mavazi meusi kaziba sura na prova kubwa jeusi alimwita kwa sauti nzito….
“Goodluck kama unataka kumuua kelvin ungana na sisi .sisi ni majini tunaweza kumuua kirahisi lakini kama wewe pekee hutaweza yule analindwa na BINTI NGUVA jina lake ni ALICE “
Goodluck akauliza “kwa hiyo nikiungana na nyinyi mtamuua ??????
Yule jamaa alimjibu “ndiyo”
Goodluck alicheka na kusema kelvin
umeisha ……….
BINTI NGUVA
EPISODE 8
Baada ya Goodluck kukubali la yule mtu aliyevaa mavazi meusi, upepo mkali ulivuma ghafla, ukizunguka mwili wake kwa nguvu kiasi cha kumvuta kutoka ardhini. Mtu aliyevaa nguo nyeusi na glovu nyekundu alimkazia macho kisha akamgusa begani. Mara moja walipotea kwenye mwanga wa dunia na kujikuta katika giza la kutisha, ulimwengu wa ajabu uliojaa sauti za kutisha zilisikika sauti za
bundi, nyoka na viumbe vingine ambavyo
vinaashiria kuwa wapo katika mazingira tofauti na ya dunia
Goodluck alihisi kama roho yake ilikuwa ikitenganishwa na mwili wake. Walipotokea kwenye giza, ardhi chini yao haikuwa ngumu; ilikuwa kama kuota mizizi ya viumbe vilivyokuwa hai, ikitetemeka na kutoa milio ya ajabu. hali iliyomfanya Goodluck aogope sana na kutamani hata kurudi lakini yule mtu alimwambia njia hii umechagua wewe mwenyewe
…………………………..
Goodluck alihisi baridi ikipenya moja kwa
moja kwenye mifupa yake, huku sauti za kelele za kupiga mayowe zikisikika kutoka mbali. Zilionekana kama sauti za watu waliokuwa wakiteswa, na sauti hizo zilisikika wazi zaidi kadri walivyoendelea mbele.
Wakiwa katikati ya njia, ghafla ardhi ilianza kupasuka, na kutoka ndani ya nyufa, fuvu la mkono yailitokea, ikijaribu kumkamata. Mikono hiyo ilionekana kana kwamba ilikuwa ikiyataka maisha yake, ikijinyonga na kutafuta kila njia ya kumkamata Goodluck. Kwa hofu, Goodluck aliruka nyuma, lakini mtu yule hakuwa na wasiwasi na hakujali. Alitembea mbele
kana kwamba mikono hiyo haikuwepo, na
kila mkono uliogusa mwili wake uliteketea na kupotea.
Goodluck alijikaza na kumfuata, akiepuka mikono hiyo kwa juhudi kubwa, huku akihisi jasho baridi likitiririka mgongoni mwake.
moyoni mwake alijisemea “hakika sijuwi kama nitafika salama kule tunakoenda
…….
Walipofika mbele kidogo, walikuta mti mkubwa na mweusi , . Majani yake yalikuwa kama nyoka, yakijiviringa huku na kule. Shina lake lilionekana kuwa na nyuso
za watu waliolia kwa maumivu makali,
huku wakilia na kuomba msaada.
(Tusaidie tusaidie kijana huku mti ukitirisha damu ).Damu hizo zilitapakaa chini kqma kisima cha maji Goodluck alipokuwa amesogea juu ya mti ghafla matone ya damu yalimwangukia …………..
Alishtuka na kutazama juu ya mti alitahamaki na kujaa woga baada ya kuona ni miili ya watu ikiwa ndo inayotiririsha damu wengine hawana macho wengine miguuu yaani ilikuwa inatisha sana ………
Mti huo ulitoa harufu mbaya ya kuoza, na kila alipokaribia, Goodluck alihisi
kizunguzungu. Mtu wa giza alinyanyua
mkono wake na kusema kwa sauti nzito, “Njoo, lakini usiangalie nyuma.”
Goodluck, akiwa na hofu kali, alijaribu kuzingatia maneno hayo, lakini macho yake hayakuweza kuacha kutazama mti ule wa kutisha. Kila mara alipoangalia, alihisi kana kwamba alikuwa anavutwa ndani ya mti, kama nguvu isiyoonekana iliyokuwa ikimvuta.
Hatimaye walifika mahali palipo na daraja lililotengenezwa kwa mifupa ya binadamu. Daraja hilo lilining’inia juu ya lambo kubwa la maji meusi yaliyochemka, yakitoa
mvuke wenye harufu ya damu na uchafu.
Walipovuka daraja hilo, sauti za kelele za mateso ziliongezeka, na Goodluck alihisi kana kwamba alikuwa akisikia majina ya watu aliowajua yakitamkwa kwa maumivu.
Kila hatua aliyopiga kwenye daraja hilo, mifupa ilionekana kutikisika kana kwamba ingetokea. Mtu wa giza alitembea kwa kujiamini, lakini Goodluck alihisi miguu yake ikitetemeka. “Hii ni sehemu ya jaribio lako,” mtu wa giza alisema kwa sauti yenye ukali, “ukishindwa hapa, utakuwa chakula cha maji haya.”
hapo ndo kulifanya goodluck
achanganyikiwe zaidi na zaidi lakini alijipa moyoni lazima ashinde tena kelvin yeye na kiumbe kinachomlinda ni lazima wateketeee …….Alizidi kufuata masharti japo moyoni aliogopa sana na kuhisi huenda ni mwisho wa safari ya maisha yake hatimaye alifanikisha lile zoezi duuuuuh huyu Goodluck walllai anataka kuwa shetani ………
Walipokaribia mwisho wa safari yao, viumbe waliotisha zaidi walitokea. Walikuwa viumbe weusi , wakiwa na macho mekundu yanayong’aa na meno makali yaliyokuwa yakitoa sauti ya kugugumia. Walizunguka njia yao,
wakicheka kwa sauti ya kutisha, na kila
mmoja alionekana kuwa na nia ya kumshambulia Goodluck tu mmmmmmh naogopa nahisi kufa sauti ya Goodluck ilisikika ………..
“Usiogope,” mtu wa giza alisema kwa sauti nzito, huku akiweka mkono wake mbele na kuwafukuza viumbe hao. “Wanajua wewe ni mgeni hapa, na wanataka kukuonyesha udhaifu wako. Lakini usisahau, unahitaji kuwa jasiri ili kumaliza kazi yako.”
Goodluck aliitikia “sawa nimekuelewa nitajikaza” akajishika kifuani na kusema mimi ni jasiri na jasiri haachi asiri .
Kwa kila hatua aliyopiga, Goodluck alihisi
mapigo yake ya moyo ylipiga kwa kasi isiyo ya kawaida. Hofu ilimkumba, lakini pia kulikuwa na sehemu ndogo ya nafsi yake iliyokuwa na shauku ya kuona mwisho wa safari hiyo. Picha ya Kelvin ilimjia akilini mwake, na hasira na chuki zilimpa nguvu ya kuendelea. huwezi amini mpaka macho yake yakawaka mwanga mweusi ikiwa na ishara huyu anaweza kuja kuwa shetani ………..
Mwisho wa safari ulionekana mbali, na Goodluck alijua kwamba bado alikuwa na changamoto nyingi za kutisha mbele yake. Lakini aliahidi moyoni mwake kuwa, kwa
gharama yoyote ile, angemfikia Kelvin na
kumuangamiza kama alivyoahidi.
lakini maskini kelvin muda huo alikuwa hata haelewi chochote kwenye maombi yake anamuombea mtu ambaye anatamani hata saizi kusikia amekufa ila maisha daaaaah linalomkuta kelvin wamekumbana nalo watu wengi sana katika hii dunia unamuombea mtu mazuri kumbe yeye anakuombea mabaya daaah ila binadamu …. mungu atusamehe sana
…
Mwisho wa safari iliyojaaa vitimbwi na visa vingi hatimaye Goodluck na yule mtu
wa giza walifika nje ya lango kubwa
lililokuwa limefungwa kwa minyororo mikubwa ya dhahabu iliyoonekana kung’aa gizani. Lango hilo lilionekana kana kwamba lilitengenezwa kwa mifupa ya viumbe wa ajabu na lilikuwa likitoa sauti ya kuunguruma polepole kama likuwa hai. Kulikuwa na mwanga kidogo uliotokea juu ya pango hilo, ikimulika maeneo mawili ambapo mavazi mawili tofauti yalikuwa yametandikwa kwa uangalifu – sare nyekundu na sare nyeusi.
Mtu wa giza alimgeukia Goodluck na kusema kwa sauti nzito, “Hii ni hatua ya mwisho kabla ya kuingia. Chagua sare
itakayokufaa, kwa sababu utaishi nayo
maisha yako yote katika ulimwengu huu.”
Goodluck alisimama mbele ya sare hizo, akitafakari. Sare nyekundu ilikuwa na nembo ya moto ikiwaka, ikionekana kuwakilisha nguvu na vurugu, huku sare nyeusi ikiwa na alama ya nyoka, ikiashiria ujanja na usiri. Baada ya muda wa kutafakari kwa wasiwasi, alichagua sare nyeusi, akihisi kwamba ingempa uwezo wa kufanikisha lengo lake bila kupoteza kila kitu.
Mtu wa giza alitabasamu kidogo, ishara ya
kuridhika. “Chaguo sahihi,” alisema, kisha akanyosha mkono kwenye lango
Uliwaka mwanga mweusi na mwekundu na yakatokea maneno haya ” ULIMWENGU WA MAJINI “
Lango lilianza kufunguka taratibu, na harufu ya ajabu ya damu, moto, na uchafu ikaingia puani mwa Goodluck.
Mandhari ya Ndani ya Ulimwengu wa Majini
Goodluck alipoingia, aligundua kuwa ulimwengu huo ulikuwa tofauti kabisa na kile alichowahi kufikiria. Ardhi ilikuwa ya mawe meusi yenye miiba, ikitoa moshi kila
ulipokanyaga. Anga lilikuwa na kivuli cha
kijivu chenye miale ya rangi nyekundu . ikiwaka na kuzima kama mapigo ya moyo.
Watu waliokuwa ndani ya ulimwengu huo walikuwa wa kutisha sana. Walikuwa na nyuso za kibinadamu, lakini macho yao yalikuwa kama mashimo yasiyo na mwisho, huku miili yao ikiwa imefunikwa na nyoka wakubwa, nge, na tai. Nyoka hao walizunguka miili yao kana kwamba walikuwa mavazi , huku nge wakiwa wamekaa mabegani kama walinzi wa karibu. Tai wenye macho mekundu waliruka juu yao, wakitoa milio ya kutisha ambayo ilifanya Goodluck ahisi mwili wake ukitetemeka.
Watu wa kule walikuwa wamevaa sare
mbili za kutisha – nyekundu na nyeusi. Wale waliovaa nyekundu walionekana kama wapiganaji wa vurugu, wakiwa na mapanga makubwa yenye damu iliyoonekana kuwa bado hai. Wale waliovaa sare nyeusi walionekana kimya na wenye sura za kikatili, kana kwamba walikuwa wakitekeleza maagizo ya siri na ya hatari zaidi.
Goodluck, akiwa amevalia sare yake nyeusi, alitembea katikati yao, akihisi macho yao ya kutisha yakimtazama kwa karibu. Walionekana wakimchunguza kama mnyama mpya aliyeingia kwenye
msitu wa mawindo. na kuna mmoja
alimrukikia akitoa ulimi wake mrefu sana mithili ya kamba za katanI yule mtu wa giza alimnyoshea mkono ti kile kiumbe kilisambaratika kama jiwe la udongo ukilipigiza ukutani ………………
Goodluck alihisi hofu ikimkaba koo, lakini alijikaza kutotazama nyuma. Kila hatua aliyopiga ilionekana kuwa ngumu zaidi, na mawazo ya Kelvin yakawa kama kisu kinachomchoma moyoni. “Lazima niendelee,” alijiambia mwenyewe, “ni lazima nimlipizie haya yote.
Mtu wa giza alimgeukia Goodluck mara
walipofika mbele ya kasri kubwa lililokuwa kama ngome. Kuta zake zilikuwa zimejaa picha za mateso, na milango yake ilikuwa imepakwa damu hai na nyingine ikitiririka
…..
Goodluck alishika ile damu na kusema “mbona hii ni damu ya mwanadamu kabisa ????
Yule mtu wa giza alicheka na kusema kwa majini naitwa ROY ,Mimi ndiye ninayepandikiza chuku ndani ya miili ya wanadamu yaani mimi ndo hasira yenyewe kwa sasa tunaingia ukaonane na mfalme wa ulimwengu wetu. usishangae kuiona hii damu itakupasa uzimwage damu nyingi ili ukamilishe adhma yako “
macho yake yaligeuka na kuwa meusi na
hata sauti ilikuwa nzito zaidi mikono ilikuwa mikubw na miguuu pia mmmmmmh au huku ni kuzimu …..kisha ROY akasema ………
“Hapa ndipo utakapofanyia kazi zako. Utapewa majaribio na kazi za kuthibitisha thamani yako. Usishindwe, kwa sababu kushindwa hapa ni sawa na kufa mara mia,” mtu wa giza alisema kwa ukali.
UPANDE WA BAHARINI
Adhabu ya Alice iliisha na wale walinzi walimtoa akiwa na yuko hoi sana na kwa muda huo alikuwa sijuwi kafa sijuwi
kazimia alisogezwa hadi karibu ya
mfalme na ghafla mfalme ambaye ni baba yake alionyosha mkono kwenye kabati lake ghafla unyoya wa tai ukatoka akausogeza kwa nguvu za giza mpaka karibu na binti yake mwanga wa blue uliwaka kumzunguka Alice na baadaye
Alice alifungua macho yake …………… Itaendelea
BINTI NGUVA
EPISODE 9
Basi baada ya Alice kufumbua macho yake huwezi amini alipona kabisa alipiga magoti na kusema “nisamehe sana baba nakuahidi sitorudia tena haya makosa “
Baba Alice au unaweza kumuita mfalme
aliinuka na kusema “simama mwanangu wewe ni shujaa wangu lakini ukikosea lazima nikuadhibu ……”
Basi lakini moyoni mwake alijisemea “i miss you kelvin natumai leo usiku nije kukuona kwa namna yoyote siwezi kuzizuia hisia zangu kwangu , sijuwi kwanini lakini NAKUPENDA ….tokea siku ya kwanza nilipokuona japo ulimwengu wetu ni tofauti lakini mioyo yetu lazima ionane “
UPANDE WA KELVIN
kumbe si kwa Alice tu hata kwa kelvin mambo ni yale yale naye anampenda sana
Alice yaani mapenzi ni ya ajabu na hii ni
ajabu ya mapenzi watu wanapendana mmmmmmmh na wanaogopana kila mtu anakumbuka tabasamu la mwenzake na kusema siku nikikuona nitakwambia
…..cha ajabu wote walisema hivo hivo ndo maana wahenga walisema kama kama mapenzi ni ya kweli basi hisia hufanana
……..je wewe
na
huyo my
wako
mnapendana
???au
tumuulize
yeye
???????
TURUDI UPANDE WA ULIMWENGU WA MAJINI
Baada ya Goodluck kukaribishwa ndani ya kasri ya ulimwengu wa majini tunamwona yupo mbele ya kiti cha enzi cha mfalme wa
majini, Liti. Kiti hicho kilikuwa cha ajabu,
kikiwa kimeundwa kwa mifupa ya viumbe kiboko na nyati na mapambo ya dhahabu iliyochanganyika na damu iliyoonekana kuwa bado inaonekana ni mbichi
Nakinywaji pekee ndani ya dunia hiyo ni damu ya watu na chakula pekee ni nyam za watu yaani huku ni nyama na damu lakini licha hali hiyo ,Goodluck hakukata tamaa zaidi zaidi alitaka atimize lengo la kumuua Kelvin…..
Mfalme Liti, mwenye sura ya kutisha yenye mchanganyiko wa kibinadamu na kiumbe kisichojulikana, alimuangalia Goodluck kwa macho mekundu yaliyokuwa kama miali ya moto.
Mazungumzo Yalianza
Mfalme Liti alizungumza kwa sauti nzito na yenye kugonga moyo:
“Binadamu, umefika hapa kwa lengo. Unahitaji msaada wangu, lakini msaada wa aina hii hauji bure. Nataka kitu kikubwa kutoka kwako—ruhusu majini wangu waingie duniani kwenu.”
Kwa sababu hadi kufika hapa inaonyesha jindi gani ulivyo na nguvu maana wengi walifia njiani kupita kwenye lile daraja chini kule kuna watu waliokufa zaidi ya laki 5 pale kwenye ule mti wa ajabu wamekufa wengi pale kwenye kuchagua vazi Wamekufa wengi.
Lakini wewe kuvuka inaonyesha una
nguvu kubwa na ukitufanyia kazi tutakupa dunia uitawale wewe hapo.
Walimgundua kelvin ni mtu mwenye tamaa sana hivyo walitaka wamulaghai mwisho wa siku wamuue na wakamilishe malengo . Lakini Goodluck hakuligundua hilo zaidi zaidi yeye kwake aliona ni sawa kuitawala dunia na mawazo yake yalienda mbali sana..
MAWAZO YA GOODLUCK
kama nikitawala dunia magali nitayabadilisha nitafanya vitu ambavyo nilitamani kufanya yaani nitakula kila
nilichotaman na nilichoshindwa kula na
sio hivyo tu mke wangu nitamuacha na nitamiliki pisi kali na nitakuwa nachagua wa kulala naye kama wale wafalme wa zamani wa kikorea yaani unaweza ukaniita KELVIN MFALME NITAKAYETAWALA DUNIA …………….
Goodluck alihisi jasho likimtoka, lakini kwa hasira na kiu ya kulipiza kisasi dhidi ya Kelvin, alikubali. “Nitakubali, lakini nataka uhakikisho kwamba utanipa nguvu za kutosha kumwangamiza Kelvin na mtu yeyote anayenizuia. na utanifanya niitawale dunia na kuwaua wote wanaonizingua …..”
Mfalme Liti alitabasamu kwa ujanja, meno
yake makubwa yakionekana kama visu vilivyopangwa vizuri. “Kwa mara ya kwanza, binadamu unakubali bila shaka yoyote. Wengi wameshindwa kufungua lango hili, lakini wewe ni tofauti. Na sasa, kwa kukubali kwako, mlango unaotenganisha ulimwengu wetu na wenu utafunguliwa.”
Kuna maneno yaliandikwa kwenye kitabu aliambiwa asome naye aliyasoma kama ifuatavyo
“MIMI GOODLUCK NIKIWA NI MMOJA YA BINADAMU NAKUBALI KUSAINI MKATABA NA ULIMWENGU WA MAJINI NA KUWARUHUSU WATUTAWALE NA
NITAKAPOMALIZA MANENO NA KUKATA
DAMU YANGU NA KUWEKA KWENYE HIKI KIKOMBE LANGO HILO LIFUNGUKE “
baada ya kumaloza kusema hayo maneno aliomba kisu na kwa ujasiria alijikata na kuweka damu yake kwenye kile kikombe na kumwambia yule mfalme kuwa
“nimekubali kuruhusu mlango unaotutenganisha ufunguke mfalme liti alicheka sana na kusema hakika umefanya vyema……….
Mara Goodluck alipotoa kauli yake ya mwisho, ardhi nzima ya ulimwengu wa majini ilianza kutikisika. Miale ya mwanga wa kijani na bluu ilianza kutoka ardhini,
ikiangaza lango kubwa lililokuwa katikati
ya kasri. Lango hilo, lililotengenezwa kwa mawe meusi yenye alama za kale, lilianza kufunguka polepole kwa mlio wa kupasua masikio.
Katika sekunde chache, mlango ulifunguka kikamilifu, ukitoa mwanga wa kutisha uliowaka kama kioo kikubwa kilichowezesha kuangalia dunia ya binadamu. Majini waliokuwa wamekusanyika walishangilia kwa sauti za ajabu, wengine wakigeuka kuwa wingu jeusi lililokuwa likijikusanya tayari kupita kwenye lango.
Goodluck alisimama pembeni, akishuhudia tukio hilo kwa hofu na
msisimko. Viumbe wa kutisha walipita
lango moja baada ya mwingine, wakiwa na miili mikubwa iliyopambwa na magamba, wengine wakionekana kama wanyama waliounganishwa na binadamu. Harufu ya damu na kifo ilizidi kuenea hewani, lakini Goodluck hakutetereka.
Mfalme Liti Atangaza Maagizo
Mfalme Liti alisimama na kutangaza kwa sauti kubwa:
“Sasa, ulimwengu wa binadamu hautakuwa salama tena! Kwa makubaliano haya, tuna mamlaka ya kuingia na kutawala. Na wewe, Goodluck, utakuwa mshirika wetu wa karibu, lakini
usisahau—ukiukwaji wa makubaliano
haya utakulipuka mwenyewe!”
Goodluck aliinama kichwa chake, lakini ndani ya moyo wake alihisi uzito wa kile alichokubaliana nacho. Hata hivyo, hasira yake dhidi ya Kelvin ilizidi kumfanya apuuze hofu zote na kuendelea na mpango wake wa kulipiza kisasi.
UPANDE WA KELVIN
Kelvin mida ya jioni baada ya kutoka kutegesha nyavu zake ili usiku aingie kufanya kazi alikuwa amechoka sana akasema ‘kinachofanya nichoke sio kazi najiuliza ni lini nitakuona Alice jamani daaah nimekumis sio.siri “
Ghafla nyuma yake akasikia sauti ikisema
“kweli umenimisi??????” kumbe alice alikuwa nyuma yake usikose sehemu ya kumi