BINTI NGUVA
EPISODE 4
Tunaendelea pale pale tulipoishia sehemu ya tatu baada ya yule binti aliyepewa jukumu la kumfuatilia kelvin kuwapoteza kipindi anaongea na Goodluck ambaye ndiye aliyempa kazi ya kumfuatilia kelvin. Basi yule mzee alimuonyesha nyumba na alikuwa kamuandalia kila kitu ndani kuanzia Godoro na vitu vingine vidogo vidogo kama mahitaji hakika kelvin alifurahi sana na kuona kuanza kwake upya kumekuwa ni rahisi sana .Lakini shukrani nyingi ziende kwa mzee Ismaili kwa moyo wake wa upendo kwa kijana kelvin .
TURUDI TENA KWA KINA ALICE
(BAHARINI)
Bahari huko Alice alimwomba dada yake anaenda kwa binadamu kukutana na kelvin dada yake alimkataza sana lakini wapi Alice alimuomba sana dada yake naye alimpa ruhusa kuwa leo hata enda ila kesho ndo atamruhusu hivyo ajikaze tu .
Alichukia sana Alice lakini hiyo haikumfanya dada yake amruhusu aende kwa wanadamu basi siku hiyo ilipita kesho yake majira ya asubuhi kelvin kaandaa mtumbwi wake tayari kwenda kuvua samaki ili angalau afanye biashara aweze kuboresha nyumba yake na kununua vitu maana anaamini kwa jinsi alivyo na wateja hakuna linaloshindikana.
Basi lakini akiwa bize na mambo yake
mara ghafla nyuma yake alitokea Alice chapu …..
si unajua si kiumbe cha kawaida muda huo kelvin ana set set mambo yake . Ghafla akasikia sauti kwa nyuma yake “umefanya uamuzi sahihi sana ” huku Alice akipiga makofi …
Kelvin aligeuka na kuachia nyavu chini maana alikuwa amemshtuka na kusema “ooooooh kumbe ni Alice ,maana umenishtua sana “
“hahahaha kweli kelvin am sorry basi maana nilitaka nikufanyie suprise tu Sikujua kama nitakufanya ushtuke “
“hapana hata usijali mmmmmh siku ile
ulipotea potea tu nageuka mara vuuuh haupo??? ” aliuliza kelvin
” anhaaa ile siku niliona kama unachelewa chelewa nikaamua nikukimbie ila nilifika nyumbani salama tena mapema hivi we hukunyeshewa ???” alijibu na kuuliza Alice
kelvin alimjibu “siku nyeshewa sana ilikuwa kawaida tu yaani niliwahi mapema nikajificha kwa jirani yangu mmoja hivi mpaka mvua inaisha mambo mengine yakaendelea ita tabia mbaya
ulinikimbia …. hii inaonyesha jinsi gani
unaogopa mvua Alice …..”
Basi walizungumza kwa muda mrefu sana lakini ngoja nikuibie siri usiojua kuhusu NGUVA
NGUVA anapokuwa nchi kavu hatakiwi kabisa kunyeshewa na mvua wala kuguswa na maji yoyote yale maana kama ikitokea hali hiyo hapo hapo anabadilika na kuwa nguva .na kwa kipindi hicho ilikuwa ni vita kubwa kati ya jamii ya Nguva na binadamu . Ndo maana siku ile Alice alikimbia kama upepo kurudi katika jamii yao kabla hajanyeshewa na mvua maana hali hiyo itaweza kuhatarisha maisha yake
……
Basi tuendelee baada ya mazungumzo
marefu sana kelvin alimwambia Alice ni muda sasa wa kwenda kutafuta samaki Basi kabla hajaenda Alice alisogea na kugusa nyavu za kelvin huwezi amini mwanga wa bluu ulitokea kuanzia mikononi mwa Alice kutapakaa kwenye nyavu nzima lakini huwezi amini kelvin hakuweza kuona chochote kile maana tukio hilo ni nje ya upeo wa macho ya binadamu,mwishowe alimwambia unaweza kwenda kelvin …….
Kelvin aliingia majini na baada ya masaa mawili alirudi akiwa amechoka sana na watu wengi walikuwa wakimsubiri ata Alice naye alikuwa yupo hapo hapo ana
msubiri kelvin alionekana kuwa na furaha
sana , Samaki walikuwa ni wengi kuliko kawaida yaani kelvin alijisemea moyoni mwake “mbona siamini kweli mungu ni mkubwa leo nitauza sana samaki na nitakifanyia ukarabati kile chumba alifika mpaka ufukweni ambapo wapo watu na kuwambia wasogee ili wapate samaki …
watu walisogea cha ajabu alimuona Alice akamwambia “bado upo tu nikajua ushaondoka anyway utanisaidia kuuza
….”
waliuza kwa muda mrefu sana na baadaye walimaliza aisew walipata hela sana maana samaki waliopata walikuwa ni wakubwa hivyo bei nayo ilikuwa kubwa
Kama kawaida wavuvi wengine walizidi
kumchukia lakini yeye hakujali waliondoka na Alice wakiwa na hela nyingi sana nakuelekea kwenye nyumba aliyopanga . kelvin mpaka sasa hajuwi kuwa alice ni NGUVA na hata uwingi wa samaki chanzo ni yeye mwenyewe Alice
….. Basi walipokuwa wakitembea kelvin alimwambia nashangaa nimekuzoea ghafla tu
Alice alicheka na kusema “hakika ni kawaida tu kelvin sisi ni people sio milima “
lile tabasamu la Alice lilimfanya kelvin abaki tu akimtazama na mawazo yakienda mbali alijisemea kimoyomoyo “wewe ni
mzuri Alice jamani mungu anaumba
daaah”
Alice aliyasikia maneno hayo japo kelvin aliongea kimoyomoyo duuuuuh Alicheka na kusema “asante sana kelvin huku akicheka …
Asante ya nini Alice …….. ????? aliuliza kelvin maana hakumfanyia chochote wala kusema chochote
Alice alimjibu “kwa kila kitu tu et naenjoy tu kukutana na wewe hakika unanifanya nifurahi ” kelvin alicheka na kusema wewe pia unanifanya hivo ….
Mwisho wa siku walikuwa washafika nyumbani kwa mzee ismaili ambapi kelvin
aliamua kupelekea samaki wakubwa
watatu kama shukrani …….
Alifika na kumuita ” baba nimerudi baba njoo uchukue zawadi yako njoo haraka
zee Ismaili alitoka mbio mbio lakini alipotoka nje alimuona Alice yule mzee alishtuka je sababu ni nini usikose sehemu ya 5
BINTI NGUVA
EPISODE 5
Macho ya mzee Ismaili yalipomtazama Alice, alihisi miguu yake ikilegea. Picha za siku za nyuma zilianza kumiminika akilini mwake kama maji yanayotiririka mtoni. Alijikuta akitumbua macho kwa
mshangao, huku mapigo ya moyo wake
yakiongezeka kasi.
“Huyu msichana… mbona siwezi kusahau sura yake? ” mzee Ismaili alijiuliza kimoyomoyo, akijaribu kuunganisha matukio
siku mbili zilizopita, baada ya rafiki wa Kelvin, Emanuel, na familia yake kuuawa kikatili, maisha ya Kelvin yalikuwa yamevunjika vipande vipande. Kila mtu kijijini alimwona kijana huyo kama mwenye bahati mbaya, huku wengi wakimkimbia kana kwamba alikuwa laana. Ilikuwa ni mzee Ismaili pekee
aliyemchukua Kelvin na kumpa mahali pa
kuishi.
Lakini ukweli ulikuwa tofauti kabisa.
Kabla Kelvin hajaletwa nyumbani kwake Alice, alikuwa amemtembelea usiku wa manane. Alionekana kana kwamba alikuwa ametoka baharini moja kwa moja, akiwa na mavazi yale yale ambayo alivaa siku alipomtoa kelvim , sku ilipoungua nyumba yake na nguo hizo zilikywa na harufu sans chumvi ya bahari.Hivyo ilikuwa rahisi kwa yule mzee kugundua kuwa yule binti ametoka bahari na nikiumbe wa ajabu ……..
“Nataka Kelvin awe na mahali pa kuishi,
mbali na machungu yote ya yaliyompata,” Alice alimwambia kwa sauti ya upole lakini iliyojaa amri
Mzee Ismaili, akiwa na mshangao, aliuliza, “Kwa nini nisimwambie Kelvin wewe ndo umemsaidia ?”
Alice alimtazama kwa macho makali, akasema, “Hapana. Usitaje jina langu kamwe. Mwambie tu umeamua kumsaidia kwa huruma zako. Ondoa wasiwasi, hii ni siri yangu na yako tu .”
Kwa muda mrefu, mzee Ismaili alihisi hatia
moyoni mwake kila alipomwona Kelvin, akijua kwamba msaada aliompa kijana huyo haukuwa wa huruma zake peke yake, bali ulikuwa mpango wa Alice. Na sasa, siku mbili baadaye , Alice alisimama mbele yake tena.
“Mbona amerudi? Na kwa nini sasa?” mzee Ismaili alijiuliza, akihisi hofu na msisimko wa ajabu.
Alice, akitabasamu kana kwamba hajuwi kitu , alimkaribia mzee huyo na kusema kwa sauti ya utulivu, “Babu, shikilia ile siri
yako na usiseme . Kila kitu bado hakijafika
mwisho.”
Maneno hayo yalimtikisa mzee Ismaili, akajua kwamba Alice ni zaidi ya kiumbe alichowahi kukiona na kitu kilichomchanganya zaidi ni kwamba Alice ana moango gani na kelvin ……
Alice alimtazama mzee Ismaili kwa macho makali yaliyojaa onyo na utulivu wa ajabu. “Nakusihi tena, jifanye hunijui. Kelvin hatakiwi kujua kuwa nilihusika. Wewe ni shujaa wake, si mimi.” nataha hii ibaki kichwani mwake hakuna haja ya kumwambia ata kidogo ……
Mzee Ismaili alijikuta akitikisa kichwa kwa
aibu na hofu. Kabla hajapata nafasi ya kuuliza chochote zaidi, mlango chumba cha kelvin ulifunguliwa taratibu, na Kelvin akaonekana akitoka nje.
Unajua wanaume wengi wale mabachelor wavivu sana kufanya usafi yaani mpaka waje wageni sasa ndo alichokifanya kelvin duuuuuh kazi ya kelvin kuvua samaki kufanya usafi aaaaaaaaaaaaah ………
Kelvin alimtazama Alice, alitabasamu, lakini macho yake yalipogeuka kwa mzee Ismaili, yalijaa shukrani kubwa.
Akamsogelea mzee huyo na kusema kwa
sauti iliyojawa na heshima:
“Babu, huyu ndiye yule msichana niliyekuambia. Lakini ningependa kwanza nikushukuru tena. Wewe ni zaidi ya malaika kwangu. Bila wewe, sijui ningekuwa wapi leo.”
Alice alibaki kimya, akijificha nyuma ya tabasamu la kawaida, huku akiona jinsi Kelvin alivyomsifia mzee Ismaili.
“Huyu mzee alinichukua wakati kila mtu alipoacha kunijali,” Kelvin aliendelea, huku sauti yake ikitetemeka kwa hisia. “Hakika Mungu anakupenda sana, babu.”
Mzee Ismaili alihisi shingo yake ikilowa
jasho. Alikuwa anataka kusema ukweli, kwamba msaada huo ulikuwa umetoka kwa Alice, lakini maneno ya msichana huyo bado yalirindima akilini mwake:
“Jifanye kama hunijuwi na huo msaada umetoa wewe na sio mimi sawa ??.” maneno haya yalumfanya mzee Ismaili ajichukulie ujiko kwa kelvin ningekuwa mimi ilikuwa nafasi ya kutamba huyu mzee ismail anataka kusema nini apunguze kimdomo domo …….
Alice aliingilia kati kwa upole, akisema kwa sauti ya upole, “Kelvin, ni kweli, babu yako ni mtu wa kipekee. Anapaswa kuwa
mfano wa jinsi wanadamu wanavyopaswa
kusaidiana.”
Kelvin alitikisa kichwa kwa kukubaliana, akitabasamu kwa furaha isiyo na kipimo. Hakujua kwamba kati ya Alice na mzee Ismaili kulikuwa na siri nzito ambayo bado yeye haitambuwi kuwa malaika mlinzi kwake ni Alice na sio Mzee Ismail …… yaaani bombooooclaaaaaaaaa mzeee ismail ni ujiko tu yaani bora alimchagua mzee angekuwa kijana tu na kwa binadamu navowajuwa ni kujichukulia sifa tu yaaani mtu yuko tayari akudhalilishe ili yeye asifiwe daaaah binadamu bhana ndo maana hata hamonize alisema ni bora ugali dagaa
kwenye amani ila kuliko wali nyama vitani.
Ila mim nataka hizo nyama na wali huko huko vitani . tuendelee
Baada ya muda mfupi wa mazungumzo ya kawaida, Kelvin alirudi ndani ya nyumba kumpatia mzee Ismaili kikombe cha chai alichokuwa amemwandalia. Alice alipobaki peke yake na mzee huyo, baada ya kelvin kuingia ndani , alisogea karibu na kumwambia kwa sauti ya chini:
“Hakikisha unaficha hadithi hii. Usiharibu imani yake kwako. Wakati ukifika, kila kitu kitakuwa wazi ,hivyo kuwa na amani kelvin
.”
Mzee Ismaili alimtazama Alice kwa macho
ya maswali, lakini msichana huyo alikuwa tayari ameanza kutembea kuelekea nyumbani kwa kelvin Alitembea pole pole huku mzee ismail akimsindikiza kwa macho tu.
MDA KAMA WA DAKIKA TANO BAADAYE….
Alice alikuwa ameketi kitandani, akionekana mwenye utulivu lakini akiwaza kwa undani. Kelvin alipokuwa akipika , alimuomba msaada.
“Alice, nisaidie kuwasha gesi. Nakwenda kuchukua nyanya haraka. sokoni sikujuwa kama ziliisha ….. narudi sasa hivi sawa
???????
Alice alitikisa kichwa kwa kukubaliana,
lakini ndani ya nafsi yake alihisi hofu. Yeye hakuwa binadamu wa kawaida; yeye ni binti nguva, kiumbe wa baharini, asiyejua shughuli za maisha ya kibinadamu.
Kelvin alipokuwa ametoka, Alice alisimama na kusogea karibu na jiko la gesi. Aliangalia kitufe cha gesi kwa udadisi, kisha akajaribu kukizungusha, lakini hakukuwa na mabadiliko. Alijaribu tena, lakini hakuna kitu kilichotokea. Akawa anajitahidi, akihisi huzuni na wasiwasi.
Kwa haraka, aliamua kumuita mzee Ismaili
aliyekuwa karibu nje ya nyumba. “Babu! Tafadhali njooni haraka!”
Mzee Ismaili alisikia sauti yake na kuingia ndani akiharakisha. “Kuna nini, binti?” aliuliza kwa sauti ya upole.
Alice akamwonyesha jiko la gesi. “Babu, siwezi kuwasha moto. Kelvin akirudi ataniona wa ajabu sana.” na hiki sijuwi ni kinini yaaani hata hakizunguki tatizo kwetu havipo ….
Mzee Ismaili alimtazama Alice kwa mshangao, lakini hakusema chochote.
Binti yangu gas unawasha hivi sawa?
Alichukua kiberiti na kuwasha gesi kwa urahis
Alice alicheka na kusema”kumbe rahisi yaani huu ushamba mimi jasho lilikuwa linatiririka kama napigana hivi “
Mzee Ismail alicheka na Alipomaliza, alitenga sufuria na kumwambia Alice:
“Sasa unachotakiwa kufanya ni kukoroga uji huu ili tutengeneze ugali.”
Alice alichukua mwiko kwa tahadhari, lakini mikono yake ilikuwa haina uzoefu kabisa. Alikoroga vibaya, na unga ulikuwa ukitapaka kila mahali. Mzee Ismaili
alicheka kidogo, lakini aligundua hofu
machoni mwa Alice.
“Binti, acha nikuonyeshe. Tunafanya hivi.” Alisema huku akichukua mwiko na kuanza kukoroga kwa ustadi wa ajabu, akipindua uji kwa haraka na kwa usahihi. Alice alimtazama kwa mshangao, akijaribu kujifunza lakini bado akihisi kutokuwa na msaada.
Baada ya kumaliza kusonga ugali, mzee Ismaili alimwambia kwa sauti ya pole:
“Usijali, Alice. Jifunze kidogo kidogo. Kelvin hatagundua lolote.”
Alice alimsifu kwa kumsaidia, na kabla
Kelvin hajarejea, mzee Ismaili alitoweka haraka, akiacha Alice akiendelea kujifanya kana kwamba alimaliza kila kitu peke yake. Kelvin aliporudi, alikuta ugali ukiwa tayari.
Kelvin alisema kwa tabasamu:
“Alice, umefanya kazi nzuri sana. Nashukuru kwa msaada wako.”
Alice alijibu kwa tabasamu la aibu, lakini ndani yake alihisi hatia kwa kutojua hata kazi rahisi kama hiyo. Alijua kwamba hawezi kuficha ukweli wake milele, na kwamba siku moja Kelvin angelazimika kugundua siri yake kubwa.
UPANDE WA BAHARINI NYUMBANI KWA
KINA ALICE
baba aliangalia kwenye darubini yake ya kichawi na akamkuta Alice yupo anakula ugali samaki na kelvin mzeealishtuka sana na kusema sabrina…….. kwa hasira
……..
Sabrina aliitika “abee baba “……
kwa hasira ” hiki nini sabrina mdogo wako anacheza na maadui zetu tena yupo ndani kwa mwanaume wanakula ugali samaki , vipi akikutana na kijana wa hovyo si atawekwa kwenye menu pia aje huku na mimi ya binadamu ……” mzee alikuwa kakasirika sana lakini hiyo
Sabrina alisema lakini baba…… mzee
alimstopisha kwa bonge la kofi ((paaàaaaaaaaaaaaaaaaaaah ) lakini nini
……
BINTI NGUVA
EPISODE 6
Baba wa kina Alice alisimama kwa hasira, akitikisa kichwa huku macho yake yakiwa mekundu kama miali ya moto. Alirudi kukaa kwenye kiti chake kikubwa cha kifalme ndani ya kasiri lenye kuta za dhahabu , akiendelea kutazama kupitia darubini ya kichawi inayomwonyesha
Alice na Kelvin wakicheka na kula ugali na
samaki.
“Hili halikubaliki!” mzee alinguruma kwa sauti nzito, akitisha viumbe wengine wa baharini waliokuwa karibu naye. “Sabrina! Siku zote nimewaambia binadamu ni maadui zetu yaani umesahau hata mama yako aliuawa na hao hao . Lakini mdogo wako amekiuka sheria zetu. Hili halina mjadala!”
Yaaani lazima adhabu ,imhusu hatuwezi kulea mjinga mjinga nmekasirishwa sana leo na ujinga yaani muangalie ana cheka cheka tu kama hana akili vizuri ………”
Sabrina, akiwa bado ameshika shavu lake
baada ya kofi zito kutoka kwa baba yao , aliinama kwa unyenyekevu lakini hakukubali kushindwa. aliendelea kumtetea mdogo wake ……….
“Baba, tafadhali sikiliza,” alisema kwa sauti ya kusihi. “Alice anajua alichokuwa anakifanya. Pengine kuna sababu ya yeye kuwa karibu na binadamu huyo. Labda anataka kutafuta siri za maadui wetu.” na pia huenda ana mtafuta aliyewahi husika na kifo cha mama yetu ……
Mzee alimstopisha kwa sauti yenye hasira kali.
“Hakuna sababu ya kuingia kwa adui zetu
kama rafiki! Wanafiki hao hawaaminiki. Kwa nini hakunijulisha kuhusu mpango huo kama kweli ni mkakati wa vita?”
a wewe endele tu kumtetea naweza kuwaunganisha kwenye adhabu jikute mama huruma.utauponza we endeleee tu
………..
Alisimama kwa nguvu, akizidisha hofu kwa Sabrina na wengine waliokuwa karibu.
“Nipe sababu moja ya kutomrudisha Alice mara moja na kumfungia kwenye mji wa baharini ili asitoke tena. na akirudi mwekeni kwenye chumba chenye maji ya baridi sana kama adhabu akae humo siku
tati bila kutolewa pumbavu kabisa huyu
binti”
Sabrina alijaribu tena kumtetea Alice.
“Baba, pengine binadamu huyo si kama wengine. Na kama ni mpango wake wa kupendwa ili aingie kwa maadui, basi tumpe nafasi ya kufanikisha hilo. Alice ni mwerevu, hatatuangusha.”
Mzee alimtazama Sabrina kwa macho makali na kusema kwa sauti nzito:
“Kama kweli unamwamini Alice, basi itabidi uthibitishe. Utakwenda duniani kumrudisha mwenyewe. Hakikisha anajua adhabu ya kuvunja amri zetu. Na
ukishindwa, utawajibika kwa matokeo
yake!”
“aliendelea sitakuwa na huruma kwa mabinti zangu au hata mtu yoyote atakayevunja amri yangu yoyote kati ya nilizoziweka hata kama ni mwanangu nitqmpimia kipimo ambacho hata wengine tunawapimia yaani hapa no haki sawa “
Sabrina alishtuka, lakini alijua kwamba kubishana zaidi kungeleta matatizo.
“Ndiyo baba, nitaenda mara moja,” alisema kwa sauti ya heshima, lakini ndani yake alihisi hofu na shaka.
Mzee aligeuka na kutoa amri kwa walinzi
wa baharini:
“Andaa farasi wa maji kwa Sabrina. Anapaswa kuondoka mara moja. Na ikiwa Alice atakataa kurudi, mwambieni kwamba hatutamkaribisha tena ! na atakuwa adui yetu mara mbili ya wanadamu ….”
Wakati Sabrina akijiandaa kwa safari yake ya hatari kwenda kwa binadamu, Alice, akiwa na Kelvin, hakujua kinachotokea upande wa baharini. Kelvin aliendelea kumpongeza Alice kwa ugali wake wa
“kawaida,” bila kujua kabisa kwamba ugali
huo ulikuwa ni kazi ya mzee Ismaili.
ndani ya mchana tulivu , na Kelvin alikuwa amekaa mezani akimalizia sahani yake ya ugali na samaki, huku Alice akiwa pembeni, akitazama jinsi binadamu wanavyokula na kuzungumza kwa furaha. Ghafla, mlango ulibishwa kwa sauti ya upole kama ya mtoto. Kelvin alisimama, akakuna kichwa chake kwa mshangao.
Kelvin: (kwa sauti ya kawaida) “Hii lazima itakuwa jirani mmoja wa watoto hapa. Ngoja nifungue.”
Kelvin alifungua mlango, na mbele yake
alisimama msichana mdogo wa umri wa miaka saba hivi, akiwa na uso wa upole na macho makubwa ya kuvutia. Alivaa gauni jeupe
Kelvin: (akiwa na tabasamu) “Hujambo, mtoto? Unahitaji msaada gani?”
Msichana huyo alijifanya kutabasamu kwa aibu na kusema kwa sauti ya upole:
“Samahani, kaka, naitwa Sabrina. Naishi jirani, mama yangu aliniambia nimuite dada Alice aje.”
Kelvin aligeuka kumtazama Alice, ambaye
alikuwa amesimama mlangoni. Macho ya Alice yalikutana na ya msichana huyo na aliweza kutambua baada ya kumtazama kiini cha jicho la yule mtoto hivyo aligundua sio kiumbe cha kawaida , na mara moja alitambua ni nani aliyekuwa mbele yake.
Alice: (kwa mshangao mkubwa) ” dada Sabrina!” maneno hayo alisema kimoyomoyo
Sabrina alitabasamu kwa hila, lakini kabla Alice hajazungumza zaidi, Sabrina alikata
kwa sauti ya upole lakini yenye maana
nzito:
“Mama anataka kuzungumza na wewe. Tafadhali, njoo kwa haraka.”
Kelvin alihisi kutatanishwa na mazungumzo hayo lakini hakusema lolote.
Kelvin: “Nadhani bora uende ukamsikilize mama . Labda ni jambo la muhimu.”
Alice alitoka nje, akimfuata Sabrina, lakini mara baada ya kufika mbali kidogo na ile nyumba, Sabrina aligeuka na kurudisha sura yake halisi kama mrembo wa baharini mwenye uso wa kuvutia sana …….
Alice: (kwa hasira na hofu) “Sabrina! Kwa
nini umenifuata hapa? Unajua hili ni kinyume cha sheria yaaani baba akijuwa na wewe upo hulu huoni kama itakuwa shida sana !”Asijuwe kuwa baba yake ndo kamtuma katika dunia hiyo ……..kumfuata
Sabrina: (kwa sauti ya kujiamini) “Sheria? Alice, unavunja sheria zaidi kwa kuishi na binadamu huyu. Baba ametuma ujumbe wa wazi: unatakiwa kurudi baharini mara moja, au kama hutaki akutoe na usiwe miongoni mwa familia yetu
Alice alitetemeka, akijaribu kuficha woga
wake.
Alice: “Sabrina naogopa kurudii. Huyu binadamu si adui wetu. Yeye ni tofauti. Na siwezi kumuacha.”
Sabrina alitazama kwa macho yake yaking’ara.
Sabrina: “Baba hatakuwa na huruma, Alice. Ukikataa kurudi, atakutangaza kuwa msaliti wa bahari.”
Alice alinyamaza, macho yake yakijaa machozi. Sabrina, akitambua huzuni ya dada yake, alibadilisha sauti yake na kuwa ya upole.
Sabrina: “Dada, tafadhali sikiliza. Narudi
baharini sasa hivi. Kama hutaki kurudi na mimi, basi jiandae kwa hasira ya baba. Uamuzi ni wako.”
Sabrina aligeuka na kuanza kuondoka, lakini kabla hajaenda mbali, Alice alimuita Dada !!,
nmekubali kupewa adhabu na narudi kwenye dunia yetu ya baharani ….
sabrina alimwambia ‘”usijali mdogo wangu , jitahidi ukifanya kosa hutakiwi kukimbia nyumbani tafuta nafasi ya kusuluhisha ….
Nawasihi ndugu zangu,
Katika maisha yetu ya kila siku, hakuna
binadamu aliye mkamilifu. Sote tunaweza kukosea, iwe kwa makusudi au kwa bahati mbaya. Lakini jambo la msingi si kosa lenyewe, bali ni jinsi tunavyolichukulia na kulitatua. Leo nataka niwazungumzie juu ya dhana muhimu ya uwajibikaji na suluhisho badala ya kukimbia matatizo, hususan nyumbani.
Wakati mwingine, tunapofanya kosa, tunashawishika kuficha au hata kukimbia nyumbani kwa hofu ya kuadhibiwa, kuhukumiwa, au kudharauliwa. Tunajisemea, “Nikionekana nyumbani, mambo yatakuwa mabaya zaidi.” Lakini
ukweli ni kwamba, kukimbia hakutoi
suluhisho; kunazidisha tatizo na mara nyingi kunasababisha maumivu makubwa kwa wewe mwenyewe na kwa familia yako.
Nyumbani ni msingi wa maisha yetu. Hapo ndipo tunapaswa kujifunza misingi ya upendo, kusamehe, na uvumilivu. Wazazi, ndugu, na familia kwa ujumla wanatakiwa kuwa kimbilio letu tunapopitia changamoto. Lakini ili hilo litimie, lazima pia sisi tujenge uaminifu kwa kukubali makosa yetu na kuwa tayari kuyasuluhisha badala ya kuyakimbia.
Kukubali kosa ni hatua ya kwanza ya
ujasiri. Inapokuwa vigumu, kumbuka kuwa kila mtu ana mapungufu, na kila mmoja anapaswa kupokea nafasi ya pili. Kuomba msamaha ni njia ya kuonyesha unyenyekevu na kujitahidi kuboresha. Pia, kutafuta suluhisho badala ya kulalamika kunaonyesha ukomavu na nia ya kujifunza kutokana na kosa lako.
Ndugu zangu, kumbukeni kuwa familia haitakukataa kwa sababu ya kosa. Inawezekana wakakasirika au kuhisi maumivu kwa muda, lakini mwisho wa siku, upendo wa kweli unashinda hasira yoyote. Lakini ukikimbia, unajiondolea nafasi ya kuelezea upande wako wa
hadithi, na mara nyingi huacha maumivu
makubwa kwa wale wanaokupenda.
Kwa hiyo, ninawasihi, unapokosea, usikimbie nyumbani. Badala yake, tafuta njia ya kusuluhisha. Zungumza na wazazi wako, ndugu zako, au mtu mwingine anayeheshimika katika familia. Eleza kilichotokea, omba msamaha, na toa mpango wa kulitatua tatizo. Hii itakuweka huru na kukuonyesha thamani ya uwajibikaji.
Mwisho wa yote, kumbukeni kuwa maisha ni safari ya kujifunza. Makosa ni sehemu ya safari hiyo, lakini jinsi tunavyokabiliana
nayo ndicho kinachotufanya kuwa bora
zaidi. Nyumbani ni mahali pa kujifunza na kukua, si mahali pa kukimbia.
Nawapenda sana, USIKOSE SEHEMU YA SABA