BINTI NGUVA
EPISODE 10
Tunaendelea palepale tulipoishia baada ya sauti ya mwanamke iliposikika baada ya kelvin kusema “nimekumis Alice ” Sauti ya mwanamke ilisikika kwa nyuma kweli umenimis????kelvin aligeuka hakuweza kuamini yulr mwanamke alikuwa ni Alice
Kelvin aliita kwa sauti iliyojaa hisia na mahaba mazito “Alice ni wewe jamani “
aliacha mtumbwi wake pembeni wake na
kumkimbilia na kumkumbatia kwa nguvu.
Alice naye aliweka mikono kwa nyuma akiwa na maana amelipokea kumbatio hilo …..
Alice nimekutafuta kote lakini sijaweza kukuona ,ulienda wapi jaman ujue umenipa mawazo ??????
Kabla kelvin hajaendelea Alice alimziba mdomo na kutikisa kichwa akiwa na maana kelvin asiongee ,anaelewa
…..kuwa kelvin kammiss sanaaa..
Walikaa na kuzungumza maana walimisiana sana ……
Alice kwanza ulikuwa wapi na unaishi wapi
maana siku ile wewe na mdogo wako mlipoondoka ndo unarudi leo na hata mara ya kwanza mpaka nikahisi wewe ni jini
Alice alishtuka……… akihisi huenda kelvin ameshamjua yeye ni nani ….
Lakini kelvin alicheka na kusema “nakutania tu et usiwe na uoga kisha akamkumbatia na waka kaa kando ya bahati ……
Kelvin na Alice wako kando ya baharii, Kelvin akiwa amekaa kwenye mchanga na Alice kamlalalia miguuni uku Alice
Kelvin:
(Akiwa katabasamu, akimwangalia Alice
kwa macho ya utani)
Unajua Alice, wewe ni mtu wa ajabu sana. Si rahisi kukutana na mtu ambaye na ukampenda bila kujua tabia yake
,anakoishi hata historia ya maisha yake .
Alice:
(Akiangalia pembeni kwa aibu)
Ah, acha
kunitania.
Sijafanya lolote la
maana.
wacha
moyo
uzungumze
babaaaaaaaa..,……… Kelvin:
(Akiendelea kwa utulivu)
Hapana, nasema kweli. Wewe ni wa
kipekee. Tangu uingie kwenye maisha yangu tumeonana mara chache lakini nimekupenda duuuh , mapenzi ni moto , mpaka nahisi kama dunia imebadilika kuwa mahali pazuri zaidi.
Alice:
(Akimtazama Kelvin kwa macho ya kucheza)
Kelvin, nimekuja kugundua jambo. Nimekupenda bila hata wewe kunitongoza. Sasa nataka unipate haki yangu just seduce me kaka aliongea kwa sauti ya madaha ……
Kelvin:
(Akiinua macho kwa mshangao, kisha
akicheka kidogo)
Unataka nikutongoze, Alice? Mbona nahisi kama tayari tuko kwenye hatua nyingine ya maisha? mmmmmmmh una makusudi huku akimkodolea macho ….
Alice:
(Akitabasamu kwa mzaha)
Hapana, nataka ule ujanja wa vijana wa mjini. Hebu onesha ujuzi wako! usije ukawa ni domozege huku akimpiga piga mashavuni….kelvin akijifanya kama amenuna
Kelvin:
(Anainama kidogo, akimwangalia Alice
kwa macho ya dhati)
Sawa basi, kama ni lazima… (anakaa vizur zaidi huku akimshika mikono yote miwili na kumtazama machoni ) Alice, unajua nini? nikikutazama macho mwako nachokiona ni upendo. nqjuwa kwa uzuri wako kwa wanaume ni kama mwanga wakati wa giza hivyo lazima kila mwanaume akunganganie lakini unaponipa nafasi ya kunisikiliza unanifanya nijione mshindi…..
(Alice anacheka kidogo, lakini uso wake unabadilika kuwa wa hisia zaidi)
Kelvin:
(Akiendelea kwa sauti ya upole, lakini
yenye uzito wa kihisia)
Sauti yako ni kama muziki unaogusa moyo, na kila mara ninaposikia, nahisi kama maisha yamepata maana mpya. Macho yako… ni dirisha linaloonesha uzuri wa dunia. Na tabasamu lako… ndo linanipa wazimu ….
Alice:
(Akiwa amekaa kimya, akimtazama Kelvin kwa mshangao na hisia nyingi)
Kelvin…
Kelvin:
(Akinyanyuka kidogo, akishusha pumzi)
Alice, sihitaji maneno mengi kusema
kwamba… wewe ni kila kitu nilichokuwa natafuta bila kujua. Na sitaki siku ipite bila kukuambia kwamba wewe ni mtu wa pekee sana maishani mwangu.
Alice:
(Akiwa amezidiwa na hisia, anamkaribia Kelvin polepole)
Kelvin… hujui jinsi ulivyogusa moyo wangu sasa hivi.
(Alice anainama kidogo, macho yao yakikutana kwa muda wa sekunde kadhaa. Bila kusema neno, na kumpa romance nzito ….Mara ghafla wakiwa
wanapigana maromance kelvin
alishangaa mwili wa Alice wa baridi
Alimuuliza kwa mshangao”mbona mwili wako ni wa baridi sana !!!?
kabla Alice hajajibu mara ghafla ulitokea mwanga mwekundu kwa mbali Kelvin alimuuliza “kile ni nini l?????” lakini Alice hakumjibu lakini moyoni alisema
“Goodluck umrfanya nini ??? umeshaharibi kila kitu kwanini umeleta majini duniani kwa mkataba wa kijinga ..”
Ghafla anga likabadikika hadi kwenye bahari waishipo wa kina Alice cha ajabu geti lao lilijifunga na kwa sasa hakuna
anayeingia hakuna anayetoka wala
kuingia. Mfalme na watu wengine katika ulimwengu wa Bahari hawakujua kama aAlice yupo duniani mzee au mfalme baada ya kumtafuta sana aligundua mawanae hayupo katika kasri . mfalme alitetemeka sana
Aliita kwa sauti kubwa “Sabtina njooo huku mjinga wewe yaani hadi mdogo wako katoka wewe ulikuwa wapi na nilimkanya mara nyingi haelewi ona sasa
…….. yupo duniani na huku hawezi kurudi tena na sasa hakuna mtu anayeweza kutoka au kuingia ndani ya ulimwengu huu
Hivyo atabaki huko huko duniani akiguswa na maji yoyote atageuka kuwa nguva na
huo ndo uyakuwa mwisho wake daaah
mwanangu kafa kizembe sana….
Sabrina alisema “baba mi na uhakika Akice atarudi kwa sababu yule ni jasiri na jasiri hapotezi asili nakuambia mwisho Alice lazima arejeee nyumbani ……..
NDUGU MSOMSJI sasa nini hatima ya binti nguva Alice ??????????? ambaye yuko kwenye dunia za watu ….
Je ataishi wapi ikiwa dunia imeshavamiwa baada ya Goodluck kusaini mkataba wa kipumbavu na vipi kuhusu hatima ya wanadamu ????????
BINTI NGUVA
EPISODE 11
sehemu ya 11 inaanza ikiwa ni maeneo ya
porini kukiwa na hakuna kitu zaidi ya miti ikipulizwa na upepo na majani yakitisika kushoto kulia ,na miti pia ikipukutisha majani lakini pembeni kuna njia moja kubwa mara ghafla anatokea Goodluck .. huku macho yake yakiwa mekundu akiwa kavaa yale mavazi aliyopewa kule , alinyosha mkono wake mbele ghafla upepo ulianza kuvuma kwa kasi sana …….
na vijiti na miti midogo midogo ikaanza kuinuka alizidi kuiinua mpaka juu zaidi kisha akaviinua na kuvirusha mbali kwa mkono wake akazungusha mikono ikatengeneza kama kimbunga hivi . akawa anacheka na kusema “kwa sasa dunia ipo mikononi mwangu kila nafsi lazima ionje
mauti “. akapiga makofi mawili paaah!!!
paaah !!! na mavazi yalibadilika akawa kavalia mavazi ya binadamu wa kawaida cha ajabu alitokea maeneo yale yale aliyokuwa akiishi kelvin
sauti ya kutisha na nzito ilisikika ikisema “Tumekutuma dunia tunataka usiwe na huruma yoyote atakayekuzingua wewe muue tumekupa na watu takribani 15 tu muweze kuangamiza kila atakayejipitisha kwenye anga zenu nadhani unaelewa ?? kwa sasa nataka ukishikile hicho kijiji cha kina kelvin uhakikishe unamuua kelvin KIJIJI CHA KINA KELVIN KINAITWA KASONGO …..
Goodluck aliondoka kiuchawi hadi kijijini
daaah huuu ni zaidi ya uadui dhidi ya kelvin ambaye maskini ya mungu hajuwi kinachoendelea yeye anahesabu katika marafiki zake anawakubali na kuwaamini ni Goodluck lakini kwa Goodluck mmoja ya watu anaowachukia ni kelvin et kisa tu alikuwa na mafanikio zaidi yake ………
UPANDE WA KELVIN NA ALiCE .,………,
Alice na kelvin walirudi nyumbani na kelvin alishangaa Alice kuwa na mawazo sana akajiuliza kwa nini anawaza
kichwani kwa Alice alikuwa anawaza kwa sasa hawezi kurudi katika ufalme au ulimwengu wao sababu hakuna njia na
geti Pamoja na milango yote imefungwa
hivyo hawezi kujua kama waliopo ndani ni wazima au wamekufa hali hii ilimfanya awe na mawazo mengi sana……
Kelvin alimuita Alice kwa sauti”we Alice unawaza nini muda wote nakuita inaonekana haupo hapa nini shida …????
Alice alimwambia “hapana ni mawazo tu baba hata usijali mi niko sawa “
kelvin alikuwa na wasiwasi sana na Alice kwa sababu alijuwa huenda kuna kitu kina msumbua ………..
Muda huo huo Goodluck alifika kwenye hicho kijiji na akiwa njiani alipamiana na mtu na baada ya kumtazama mtu yule
alikuwa amelewa cha ajabu yule mtu
alianza kumtukana “we mjinga una dhani hii ni njia ya baba yako hii au ya mama yako unakatisha katisha tu wenye mji tunapita
……faraaaaaaa wewe!!!!!!!.Goodluck alimtazama na kucheka kwa sauti “asante bro tatizo umelewa na nitakusamehe sababu najua hizo ni pombe ila isingekuwa hivo ningekuua sio siri”
Jamaa yule alicheka sana na kusema “aiseee we ni chizi kweli we unadhani utanifanya nini mjinga wewe ” alichokosea zaidi alimsogelea Goodluck na kupiga kofi lilisikia
paaaaaaaaaaaaaaaaaaah
!!!!!!!!!Goodluck alicheka sana . na baada
ya sekunde mbili zaidi alichukia kwa
hasira
Ghafla macho yake yalibadilika na kuwa meusi mara yule jamaa akajikuta yupo juu sana na Goodluck akalivuta jiwe kubwa kichawi likasogea usawa wa yule mtu kisha akamuachia kutoka angani na yule jamaa alijipigiza kwenye lile jiwe paaaaaaaaaah!!!!!!
damu zilitapakaaa chini Goodluck akasema afadhali yaani mti yoyote akija kwenye anga zangu namuua alicheka kisha akasema ngoja nitafute nyumba ya kutulia ili kesho nianze kuwasumbua hawa wanakijiji cha kasongo ……
UPANDE WA KINA ALICE NA KELVIN
kimbembe muda wa kulala ndani kwa kelvin kuna chba kimoja na Alice hayupo tayari na anaogopa kulala na kelvin kelvin akamwambia “njooo tulale usiku ushafika “
Alice “aweeee kelvin sitaki kulala na wewe kijana mwenyewe damu imechangamka weee kwendraaaaaaaa!!!!!!
“sasa mimi nitalala wapi jamani ” alisema kelvin lakini Alice alimkazia na kumwambia utajua wewe mimi hainihusu mara ghafla sauti za vilio zilisikika nje ya kile kijiji
“njoooooni njooni amekufa yule kijana
mlezi njooni “”
kelvin na Alice walitoka nje ya lile jengo na kukuta umati wa watu ukikimbia kuelekea sehemu moja ya lile pori sio siri walipofika pale hawakuweza kuamini walimkuta yule chapombe kichwa kimepasuka na damu zimetapakaaa na katika kijiji cha kasongo halijawahi kutokea ……
Alice alisogea kidogo mbele macho yake yalikuwa ya blue aliweza kugundua kuwa Goodluck ndiye kahusika katika yale matukio hajakaa sawa alihisi kama kuna mti umerushwa alisema kwa sauti kuu
“wote inameniiiiiiiiiiiii fanyeni haraka
aaaaaa!!!! watu walipoinama tu ghafla mti mkubwa ulipita na kukita kwenye mbuyu uliokuwa karibu na eneo hilo .
Alice kuja kushangaa aligundua kuwa Goodluck ndiye alituma ule mti akasema asiinuke mtu muda huo na kelvin kainama pale chini alisogea hadi eneo la uwazi ambapo Goodluck akiwa na macho mekundu alikuwa akimsubiri ……..
na kelvin muda huo anajiuliza Alice kaenda wapi???????
Goodluck, akiwa amesimama eneo la uwazi lililojawa na giza na upepo mkali,
alionekana mwenye kiburi huku macho
yake mekundu yaking’aa mithili ya taa za moto. Alitabasamu kwa dharau, huku akiizungusha mikono yake hewani na kutengeneza upepo wa ajabu i na sauti zilizosikika kote ………
Goodluck:
(Kwa sauti nzito na ya kutisha)
“Leo ni usiku wa kufungua milango ya maangamizi. Dunia sasa ipo mikononi mwangu, na kijiji hiki hakitakuwa salama tena!”
Akaipiga ardhi kwa nguvu, na mara miti
mikubwa ilianza kujikunja huku vijiti vidogo vikiruka hewani kama vumbi.
Muda huo Alice anamtazama tu anaamini anauwezo mkubwa lakini hataki kelvin ajuwe kuwa yeye ni nguvu ……..
UPANDE WA ALICE NA KELVIN
Kelvin bado alikuwa amekaa pale chini, akihisi hofu isiyoelezeka. Mawazo yalizunguka kichwani mwake.
Kelvin:
(Kwa sauti ya chini, akijisemea)
“Alice yuko wapi? Ameenda wapi huyu?”
Muda huo huo, Alice, akiwa na macho yakiwa yamebadilika kuwa rangi ya blue , alikuwa amesimama mbele ya Goodluck kwa umbali wa mita chache tu. tayari kwa ajili ya pambano zito ….
Alice:
(Kwa sauti thabiti lakini yenye hofu kidogo)
“Goodluck, siwezi kuamini kuwa wewe ni yule rafiki wa Kelvin ambaye halipiti neno akakutaja kumbe wewe ni msaliti . Nini kimetokea kwako? Kwa nini umeamua kuwa tishio kwa kijiji hiki?”
Goodluck:
(Akiangua kicheko kwa dharau)
“Rafiki? Rafiki wa Kelvin? Hicho kiumbe dhaifu hakistahili hata kuwa jirani yangu! Leo hii nimekuja kuonesha nguvu zangu, na hakuna mtu atakayenizuia!”
Alice alijaribu kuchukua hatua moja mbele, lakini upepo mkali ulizuia mwendo wake.
Alice:
(Kwa sauti ya hasira)
“Hutashinda, Goodluck! Kelvin hana hatia, na kijiji hiki hakijakukosea. Mimi niko hapa kumlinda Kelvin na watu wake.
Utapambana na mimi kabla ya kuleta
uharibifu zaidi.”
Goodluck akacheka tena, akionyesha meno yake mithili ya simba aliye tayari kwa mawindo.
Goodluck:
(Kwa sauti nzito)
“Kwa nini unahangaika, Alice? Hili sio jambo linalokuhusu. Mimi nimepewa nguvu za kutawala, na nitafanya hivyo kwa gharama yoyote!”
UWANJA WA MAPAMBANO
Alice alikaza moyo, akijua kuwa mapambano haya hayakuwa rahisi. Kelvin, aliyekuwa akitazama kutoka mbali, alijaribu kusogea ili kumsaidia Alice, lakini alihisi hofu ikimzidi.
MAPAMBANO MAKALI
Mapambano kati ya Alice na Goodluck yalizidi kuwa ya kutisha. Upepo, moto, na sauti za vilio vilitawala. Wakazi wa kijiji cha Kasongo walikuwa wamejificha nyuma ya miti,wengine wameinama wakiwa hawajuwi nini kinaendelea na kumbuka
mambo yanayotokea majira ya usiku
………
Alice:
(Kwa sauti ya ujasiri)
“Hutashinda, Goodluck! Hii dunia haiwezi kumilikiwa na nguvu za giza.”
Goodluck, akiwa amechoka kidogo, alitabasamu kwa dharau.
Goodluck:
“Hatutaki amani, Alice. Kila mtu lazima aonje mauti!”na nguvu ninazo fikilia siku kelvin akijuwa wewe ni nguva unadhani
utapendwa tena ???? kazi kushobokea
yasiyokuhusu unadhani utapewa nini Alice
Maneno hayo yalimnyong’onyesha na kujisahau kuwa yupo kwenye vita na Goodluck alitumia hiyo kama fursa aliinua mwanga kabla hajarusha akasikia sauti ikiita Alice ! Alice ! Alice !. Alikuwa ni kelvin
EPISODE 12
Basi karibu sana katika sehemu ya 12 ya simulizi yetu ya BINTI NGUVA
…………tunarendelea palepale tulipoishia baada ya kelvin kuita Alice ! Alice ilimbidi Goodluck asitishe lile shambulio huku
akisema “aiseee daaah huyu fara anakuja
kufanya nini huku “
Goodluck akamwambia Alice “mimi na wewe hatujamalizana nitarufi kwa ajili yako “
kisha ile kelvin anatokea na Goodluck akakimbia lakini kelvin hakuweza kufanikisha kumuona hata sura na Alice kuzuga kutoulizwa maswali mengi, alijifanya kama anataka kuanguka chini na kuzimia .
Ndipo kelvin alipomuwahi haraka na kumdaka huku akimuita mara tatu “we Alice ,! we alice , Alice amka huku
akimtikisa tikisa .. lakini Alice hakuinuka
badala yake Alice kimoyo moyo alijisemea
“kumbe unanipenda kelvin lakini nahofia siku ukijua mimi sio binadamu nahisi itakuwa mwisho wa furaha hiii” .
muda huo kelvin kambeba juu juu mpaka nyumbani kwake .Alifika na kumlaza kitandani kisha alipotaka kutoka nje kwenda kumuita daktari Alice alimshika mkono na kumwambia
“usiende siwezi kuwa pekee yangu hapa nahitaji ukaribu wako “
kelvin aliongea kwa hasira na uchungu “unadhani tukiwa wote tumekaa wote
hapa unadhani nini kitatokea ndo utapona
au ????
Hapana we nilete maji kwanza nahisi nitakuea sawa kelvin alichota maji na kumpa Alice alikunywa na baadaye alikuwa yupo sawa na mzima kabisa mpaka kelvin alishangaa asijuwe kuwa yote haya yalikuwa ni maigizo ili maswali yasiwe mengi .
“hivi unajua nilikuwa na wasiwasi na wewe kwa kiasi gana Alice yaani wewe unaondoka tu yaani unaondoka unacyojisikia bila kujua huku wamiliki moyo ukiondoka utaniacha na nani ,plz usinipe wasiwasi mama ” alisema kelvin kwa sauti ya upole na upebdo mkubwa
Alice hakuwa na jivu zaidi ya kumkumbatia
kelvin kwa nguvu na hisia kubwa huku machozi yakimtoka na kujisemea moyoni
“najua unanipenda sio siri hata mimi nakupenda sema tatzo ni kwamba mimi sio binadamu na endapo kama ukijua daaah itakuwa mbaya sana nachofanya nikukupa furaha coz wewe ni moyo wangu lakini kuwa na wewe milele najua haitowezekana ………..”
******
siku hiyo ilipita na maisha mengine yaliendelea na kesho yake asubuhi kelvin alipoamka aliamua kumpigia rafiki yake Goodluck na kumwambia
“haloo Goodluck daaah rafiki yangu wa
thamani vipi hali yako ” alisema kelvin
“‘sama kabisa kelvin umepotea ndugu yangu ni mwezi sasa hatujawasiliana kuliko ndugu yangu maana sio kawaida yako akamtania “au simu ulitumia kama chambo ya kuvulua samaki”alisema Goodluck
Myda huo Alice anatazama na kusema “usiolijuwa sawasawa na usiku wa giza na kikulacho ki nguo mwako pole sana mpenzi wangu nitakulinda na hakuna atakaye kudhulu wewe ikiwa mimi niko hai
,am ready to die for you kelvin (nipo tayari kufa kwa ajili yako kelvin )kisha akafuta machozi yake yote ……
kelvin aliendelea kuongea na Goodluck
“hahahahaha hapana rafiki yangu sio hivo nilipitia msoto (akamsimulia yaliyomkuta mwanzo mwisho asijuwe kuwa kwa sasa kuwa kelvin yupo kijijini hapo hapo KASONGO na yote aliyofanyiwa aliyesababisha ni huyo huyo Goodluck aliyemuamini sana …….daaah natamani tumwambie kelvin lakini hawezi kutusikia na hata tukimtumia Alice aliyekuwa karibu yake swali kubwa umejuaje ………………..
Basi majira ya asubuhi upande wa msituni kuna mtu alikuwa anakata kuni ghafla nyuma yake kikapita kitu kama upepo tena kwa kasi sana lakini alijua ni mawenge
aliendelea kukata kuni taaaaaaah
taaaaaaah taaaaah mara akapitiwa vuuuuuuuuuuh lililoanguka ni panga na kichwa chake tu ………
sasa mkewe aliyekuwa akikusanya kuni alisogea upande wa mumewe baada ya kuhisi kimya kizito …..
“Amani uko salama wewe !!!!?????aliuliza mwanamke lakini alizidi kuhisi sauti za ukimya zikilindima ikabidi asogeee alipofika pale alianza kuona damu . hali ya uoga ikaanza kumuingia alizidi kusogea mmmmh mara akajikwaaa na kuanguka chini .
Akahisi kama kagusa kichwa cha mtu ile kugeuka hivi anakiona kichwa cha mme
wake tena kimekodoa macho alipiga
kelele nzito
“oooooiiiioiiioiiiiih ms aaaada uuuuuuuuh nakufa mimi aliacha kila kitu hapo hapo mbio mbio kijijini akiwa anahema sana
…..
*****”
Alipofika kijijini alikutana na watu akawa anawambia jamani mume wangu !!!!!huku akionyesha mkono porini watu wakawa wanamuuliza kuna nini lakini kigugumizi kimembana hawezi kuzungumza lakini anachoweza ni kusema “mume wangu ” huku akiunyosha mkono wake poriji …
na muda huo huo kelvin na Alice walikuwa wanapita mitaa hiyo hiyo ya kijiji kuelekea
kununua vifungua kimya baada ya kuona
kundi la watu limekusanyika nao waliwafuta na yule mama baada ya kupewa maji alisema kila kilichotokea
……………..
“”******
na walipoenda eneo la tukio walikua kila kitu kama alivyoeleza tule mama na basi walirudi na mke wa kijiji akaitisha kikao na huwezi amini katika kikao hicho Goodluck naye alikuwepo lakini kwa sura ya bibi kizee mmoja hivi ambaye bibi mwenyewe wa kweli Goodluck ashamuua lakini macho ya yule bibi yalipogogangana na Alice Alice aligundua kuwa huyu ni kelvin na kadri anavyokunywa damu za watu ndo roho ta ubinadamu bye bye ………..
Basi walitazamana wakaongea nafsi kwa
nafsi huku wakitazamana
“leo nataka uone ukatili wangu namuua mwenyekiti mbele yako na haunambii na hatuwezi kupatana mpaka utoke upande wa kina kelvin uje kwangu “
Akaendelea angalia kwa makini hii leo na Alice akawa anaitazama Lesso . kila nitakapoikunja huyu mwenyekiti weny ndivyo nitakavyomyonga alianza kukiciringisha kitambaaa kila kule kila mtu akawa mwenyekiti amepatwa na nini
Usikose Episode 13