Mwanaume Kwa Mara Ya Kwanza.
1. CHAGUA ENEO ULILOZOEA.
Kama umepata nafasi ya kuchagua,basi chagua eneo ambalo umelizoea.Kwenda sehemu
iliyozoea kunakuongezea utulivu na kujiamini.lakini hata ukialikwa sehemu flani
basi pendekeza eneo lenye hadhi sawa na hilo lakini ambalo umelizoea. zingatia
eneo hilo lisiwe nyumbani kwako ama kwake.
2. KULA /KUNYWA ULICHOZOEA.
Kama mtoko huo utajumuisha kula ama kunywa basi zingatia vile ambavyo
umevizoea.
3. KUWA NA PESA YA KUTOSHA MATUMIZI YAKO.
Zingatia sana hilo,uwe na hela ya kwenda na kukurudisha utokapo lakini pia
zingatia sana utachokula na kunywa kiendane na mfuko wako,habari za leo nina
ofa nitamkomesha achana nayo kabisa.
4. VAA MAVAZI YASIYOLETA MAANA TOFAUTI.
Kila jamii ina mila zake na mavazi yake ya kawaida na kuna aina ya mavazi ama
mikao ukikaa mbele ya mwanaume basi anaweza kutafsiri tofauti,epuka sana hiyo.
Wanasema kwamba nguo ya mwanamke inapaswa kuwa ndefu kiasi cha kufunika sehemu
zake muhimu lakini iweze kumvutia yule anayetazama. Hapa haijumuishi mavazi ya
kiimani.
5. MILIKI MUDA WAKO.
Jua muda gani unataka kutumia sio basi unakua kama mtu uliyekosa ratiba we upo
tu hadi unaambiwa tuondoke hapana na hata kama umenogewa na mazungumzo kiasi
gani basi anza kwanza kuaga wewe.
6. TAZAMA MAMBO GANI UNAPENDA KUYAJUA/KUYAONGELEA.
Si vibaya hata kufanya utafiti ukajua yeye ni nani na anapenda nini na mambo
gani ya msingi unataka kuyafahamu kutoka kwake
SIo unauliza kila swali ama huna hata cha kuuliza.Ndio muda wa kufahamiana.
7. MILIKI TABIA ZAKO KISHA CHUNGUZA TABIA ZAKE.
Miliki tabia zako tazama wakati gani ufanye nini,kipi useme kipi uachane nacho
lakini pia tazama mwenendo wake katika mtoko huo unaweza kupima ustaarabu wake
na kuona anafaa kutoka naye tena,anafaa kuwa rafiki wa kawaida,mfanyabiashara
mwenza,mpenzi ama umpotezee.
8. AMUA KAMA UNATAKA KUTOKA NAYE TENA.
Kama umeona mda ulotumia naye haujakugharimu basi unaweza mpa nafasi nyingine
akiomba tena mtoko lakini ukiona mtoko wenu umeenda ndivyosivyo mpige tu chini
usijichoshe na kujipotezea muda.
9. NOGESHA STORI USIWE TU MSIKILIZAJI UTABOA.
Usiwe kama mgeni tu mwalikwa changamka nawe leta stori.
10. AKITAKA KULIPIA BILI MUACHE ALIPIE.
Kama anataka kulipia mtoko basi muache alipie,hela yako iache itakufaa siku
nyingine
Lakini kama hujamsoma lipia tu msosi wako asije kukusema unapenda vya bure .
11. ZINGATIA USALAMA WAKO.
Muhimu sana hii,mahali pa kukutana pawe pa wazi na penye watu wengine.Baadhi ya
watu wajue unaenda wapi na kukutana na nani,epuka kunyanyuka nyanyuka na kuacha
chakula ama kinywaji.