PIA
Kanuni
ya kwanza ya maisha: Ili kuheshimiwa kama mwanaume, ni lazima watu wamheshimu
mwanamke wako! Najua inaweza kuonekana kama jambo dogo, lakini ndiyo ukweli.
Kama watu hawamheshimu mwanamke wako, basi jua hata wewe wanakudharau. Iwe ni
mama yako mzazi, dada yako, au marafiki zako, ni lazima wamheshimu mwanamke
wako. Hapo ndipo utajua kwamba wanakuheshimu wewe.
Labda nikupatie mfano: Umeoa, kama mama yako anamtukana mke wako, kama
dada yako anamtukana mke wako, au kama jirani au rafiki wanamzungumzia vibaya
mke wako mbele yako, si kwamba hawamheshimu mke wako tu, bali wanakudharau
wewe. Wanakuona kama mwanaume ambaye huna uwezo wa kuwa na mke anayestahili.
Mfano: Wanasema, “Mke wako hana akili,” usichekelee, kwani ni
kama wanakuambia, “Huna akili ya kuoa mwanamke mwenye akili!” Mfano
mwingine, mama yako anamtukana mke wako na kusema, “Mjinga umekuja kula tu
hapa, unajaza tu choo na kutumia pesa za mwanangu!” Hapo hawamtukani mke
wako tu, bali ni kama mama yako anakuambia wewe ni fala huna uwezo wa kumchagua
mwanamke mwenye akili.
Ndiyo maana mimi, hata kama mke wangu amekosea, hata kama mke wangu
humpendi, nilazima ujue kwamba unapaswa kuongea na mimi kwanza! Huwezi
kumtukana mke wangu na mimi nikacheka. Hata kama ni mama yangu mzazi au ndugu,
ukianza kumtukana mke wangu na kisha unakuja kwangu kunichekea, nitakuona kama
mnafiki.
Kama kuna kitu, njoo uniambie! Shida inakuja pale ambapo wewe mwanaume
unamtukana mke wako mbele za watu, unamdhalilisha na kusema hana akili. Hapo,
wale watu wanakudharau kwa kuona huna akili ya kuchagua na kumiliki mke mwenye
akili. Kwa hiyo, mheshimu mke wako na watu watakuheshimu pia!