Siri ya 1:
Kila unayemuoa ana udhaifu. Hakuna mtu aliye mkamilifu, anayekuja katika vivuli
vyote vya ukamilifu ndiye aliye hai ndani ya mwenzi wako, na huyo ni Mungu tu.
Kwa hiyo ukizingatia udhaifu wa mwenzi wako huwezi kupata kilicho bora kutokana
na nguvu zake. Tazama, wanandoa wanaodumu ni wale wanaokuza nguvu za kila
mmoja, badala ya udhaifu wao.
Siri ya 2:
Kila mtu ana historia mbaya kwenye mzunguko wa maisha yake. Hakuna mwenye
umalaika. Unapooa au kuolewa acha kuchumbia zama za mtu. Cha muhimu kwenye
maisha ya ndoa ni kujari maisha ya sasa ya mpenzi wako. Mambo ya zamani
yameshapita. kama kakukosea Samehe na sahau yaliyopita. Zingatia ya sasa na
yajayo mnayojenga pamoja.
Siri ya 3:
Kila ndoa ina changamoto zake. Ndoa sio kitanda cha waridi. Kila ndoa unayoiona
nzuri imepitia tambua kuwa imepitia mtihani mgumu. Upendo wa kweli
huthibitishwa wakati wa changamoto za kimaisha. Pigania ndoa yako. Pambana,
Pambana hadi adui atoke nje ya ndoa yaki. Fanya maamuzi ya kubaki na mwenzi
wako kwenye heka heka zenu.
Siri ya 4:
Kila ndoa ina viwango tofauti vya mafanikio. Usilinganishe ndoa yako na ya mtu
mwingine yeyote. Ndoa mbili zinaweza kuonekana kuwa Kithibitisho, lakini kamwe
haziwezi kufanana. Natumai unanisikia nachokwambia Kamwe usilinganishe kiwango
cha upendo kutoka kwenye ndoa nyingine na yako. Jifunze kuwa na subira,
Siri ya 5:
Kuoa ni kutangaza vita. Unapooa lazima utangaze vita dhidi ya maadui wa ndoa
yako. Baadhi ya maadui wa ndoa yako ni:
Ujinga
Kumsahau mungu
Kutosamehe
Kuomba ushauri mtu wa tatu
Ubahili
Ukaidi
Kutokuwa na upendo
ufedhuli
Uvivu
usaliti
.
Ili kuweka ndoa yako kuwa sawa inabidi uwe tayari kupigana na chochote kwa
maombi na bidii. Ndoa yenye furaha si ya wanandoa wanaotaka kuwa wasafi.
Siri ya 6:
Hakuna ndoa iliyokamilika. Hakuna ndoa utakayoikuta ipo sawa. Ndoa ina kazi
ngumu. Jitolee kufanya kazi kila siku juu ya ndoa yako. Ndoa ni kama gari
linalohitaji matengenezo na huduma inayofaa. Hili lisipofanyika itavunjika
mahali fulani na kumuweka mmiliki kwenye hatari au hali fulani zisizofaa.
Tusiwe wazembe kuhusu ndoa zetu.
Siri ya 7:
Mungu hawezi kukupa mtu aliyekamilika. Anakupa mtu katika mfumo wa malighafi
ili umtengeneze wewe mtu hasa mtu unayetamani. Je, unakumbuka kwamba Mungu ni
Muumbaji? Hii ina maana kwamba wewe pia ni uliumbw kama Yeye, na Mungu
amekuumbia uwezo wako wa kuyashinda baadhi ya mambo. Jitahidini kila mmoja wenu
kwa sala, upendo na Subira.
Siri ya 8:
Ndoa haina mkataba. Ni jambo la kudumu. linanahitaji kujitolea. Upendo ni kama
gundi inayowaunganisha wanandoa. Talaka huanzia kwenye akili na kumchanganya
shetani kucheza na akili yako. Kamwe usije kutoa taraka mapema kwenye maisha
yako. Usijaribu kumtishia mkeo kwa neno talaka. Kadiri unavyohangaika basi,
chagua msaada wa Mungu ili kubaki katika ndoa.
Siri ya 9:
Kila ndoa ina gharama ya kulipa. Ndoa ni kama akaunti ya benki. Ni pesa
unazoweka ambazo unazitoa. Usipoweka upendo, amani na matunzo katika ndoa yako,