4 YA KUZINGATIA UKITAKA KUWA MWANAUME IMARA AU RIJALI
1. UHURU
Mwanaume Rijali anathamini uhuru wake kuliko kitu chochote,mwanaume Rijali
hawezi kuishi kwa kumtegemea Mwanamke wake kwenye fedha,salio,kula,kuvaa,
nyumba ya kuishi, gharama za matibabu, usafiri,zawadi n.k mwanaume Rijali
anajua ni wajibu wake kuhakikisha maisha ya mwenza wake yanakuwa salama.
mwanaume Rijali haishi kwa kutegemea sapoti ya Mwanamke bali Mwanamke akitoa
sapoti inakuwa bonus ili kuepuka kumlaumu Mwanamke pale ambapo haonyeshi
ushirikiano.
Mwanamke yeyote akiona unamhitaji sana ili mambo yako yaende huanza kuonyesha
dharau waziwazi,atakuwa na kiburi, majivuno,ataanza kuonyesha jeuri kwa sababu
anajua hauwezi kumuacha wala hauwezi kuishi bila yeye.Lakini kama unaishi bila
kumtegemea kwa chochote hauwezi kumlaumu kwa jambo lolote.
mwanaume Rijali anabeba majukumu yake yote kisha majukumu ya watu wengine
anawaachia wahusika.
Ukibeba majukumu yako ipasavyo hauwezi kumlaumu mtu yeyote.
2. KUJIHESHIMU
Mwanaume Rijali anajiheshimu sana kuliko anavyoweza kumheshimu mtu yeyote. Binadamu
yeyote ukionyesha kumheshimu kupitiliza anakupanda kichwani.
mwanaume Rijali hana muda wa kutaka kumbadilisha tabia mwenza wake isipokuwa
anaweka sheria na taratibu za kuongoza mahusiano kisha anatimiza wajibu wake na
kumuacha mwenza wake atimize majukumu yake.
mwanaume Rijali hawezi kushobokea muonekano wa Mwanamke bali anaona ni kitu cha
kawaida hivyo hawezi kubabaika kwa uzuri wa Mwanamke,Bali anathamini sana
heshima ambayo anapewa na Mwanamke .
mwanaume ambaye anashobokea muonekano wa Mwanamke huwa ja wakati mgumu sana
kuachana na Mwanamke pale ambapo Mwanamke anapofanya usaliti, kumdhalilisha
mwanaume, kumnyima unyumba kwa muda mrefu.
Mwanamke akijua hauna ujanja juu ya muonekano wake anakuwa hana muda wa kujali
tabia zake kwa sababu anajua unasamehe makosa yote na utakuwa mvumilivu miaka
yote kwa sababu yeye ni mzuri sana.
3. KUSTAHIMILI HISIA
Mwanaume Rijali anaishi kwa kujitegemea yeye,akiwa mpweke haitaji
simu,faraja,sms ,zawadi kutoka kwa Mwanamke ili apate kujisikia vizuri.
mwanaume Rijali anakuwa kama komandoo kwenye uwanja wa vita kwa maana anabeba
furaha yake yeye mwenyewe vilevile anabeba maumivu yake yeye mwenyewe.
Mwanaume Rijali akiwa na huzuni,upweke, majonzi anajua ni wajibu wake kubeba
maumivu hayo siyo jukumu la Mwanamke .
Kama hauna furaha kwa sababu Mwanamke hajapiga simu,hajatuma sms,hajakufariji,hajakupa
pole kwa kazi utakuwa na malalamiko, manung’uniko,utanuna, kususa,kuishi ukiwa
na chuki, kinyongo moyoni kwa sababu unampa Mwanamke wako jukumu la
kukufurahisha jambo ambalo husababisha migogoro ya kimapenzi mara kwa mara.
Mwanamke yeyote akiona haulalamiki juu ya ukimya wake,au tabia zake ataanza
kutilia shaka kama ûnampenda.Kwa sababu Mwanamke anaweza kukupuuza kwa makusudi
lengo aone kama utaanza kulalamika ili ajue kama ûnampenda sana,akijua
anapendwa sana huanza kuonyesha dharau waziwazi kwa sababu anajua hauwezi
kumuacha wala hauwezi kuishi bila yeye.
Lakini kama upo na furaha yako wewe mwenyewe akiwepo au akiondoka haiwezi
kukusumbua wala kwake hauwezi kuonekana msumbufu.
4. KUJIWEKEA MIPAKA
Mwanaume Rijali anajua tabia gani za kuvumilia na tabia gani siyo za kuvumilia.
mwanaume Rijali anajua makosa ya kusamehe na makosa ambayo siyo ya kusamehe.
mwanaume Rijali anamuongoza Mwanamke , mwanaume Rijali
hampigi,hamdhalilishi,hamtukani Mwanamke bali anaishi naye kwa misingi ya kuheshimiana
na uadilifu.
mwanaume Rijali anajua Mwanamke akiwa mgonjwa anahitaji faraja,anajua Mwanamke
akiwa na huzuni anahitaji faraja, anajua Mwanamke akiwa amefanya kazi nyingi
anahitaji kupewa pongezi, vilevile mwanaume Rijali anajua hawezi kumnyenyekea
Mwanamke kama njia ya kuzuia mahusiano kuvunjika.
mwanaume Rijali anampa onyo Mwanamke pale ambapo anaonyesha utovu wa
nidhamu,anampa onyo siyo kwa kumfokea, kumtukana, kumkashifu, kumkaripia,
kumgombeza, kumtangaza vibaya n.k bali anamweleza wapi amefanya makosa na
vilevile anamuonyesha wapi pa kujirekebisha.
Mwanaume Rijali hana gubu, kisirani,chuki, kinyongo,wivu wa mapenzi
uliopindukia.
Mwanaume Rijali anaishi kwa kujiongoza.
mwanaume Rijali anajua kumlinda na kumtetea mwenza wake dhidi ya kukosolewa,
kusemwa vibaya, kutukanwa, kujibiwa vibaya kutoka kwa mama yake mzazi pamoja na
dada zake.
mwanaume Rijali anasimama katikati hayupo upande wa mama yake mzazi,au dada
zake vilevile hayupo upande wa mwenza wake.
mwanaume Rijali anafanya uadilifu,mwanaume Rijali anakuwa mtenda haki,mwanaume
Rijali hafanyi upendeleo,mwanaume Rijali anaongozwa na akili siyo hisia za
mapenzi.
mwanaume Rijali hana uwezo wa kumpenda Mwanamke kwa hisia kali bali anampenda
Mwanamke kwa kuongozwa na akili sio hisia.