Mwanamke Maisha Yake Yote
– Anakuwa hajiamini mbele ya Mwanamke,akiona mwanamke mwenye muonekano mzuri tu
anapagawa,anatetema sana,anahisi Mwanamke huyo ni malaika na mkamilifu,kisha
anajiona yeye yupo na dosari nyingi sana na mapungufu mengi sana ambayo
yatamkwaza Mwanamke huyo,hivyo ataanza kuonyesha kumnyenyekea sana,
kumbembeleza sana, kujitutumua sana, kujieleza sana, kumuahidi mambo mengi
sana,kutumia fedha nyingi sana ili kumfurahisha akiamini atapendwa sana kuliko
wanaume wote lakini huambulia kuchunwa fedha zako zote na kuachwa mifuko
mitupu,hujibiwa kwa maneno makali sana yenye
udhalilishaji,hufokewa,hutukanwahuambiwa wewe sio wa HADHI yangu kisha mwanaume
anaanza kulia, kuomba msamaha, kumpa ushauri,n.k
– Hana sauti ya mamlaka,akianza kuongea anatetemeka sana,anarudiarudia
maneno,anakosea kosea maneno,anaongea kwa upole sana au anaongea haraka haraka
sana,
– Anaogopa ugomvi na migogoro,hivyo mara kwa mara anaomba msamaha hata kama
hajafanya makosa
– Hana msimamo, anaweza kumtishia mwanamke kumuacha lakini hana ujasiri
huo,muda wote anataka kupendwa sana na kuonewa huruma
– Anaamini kwa sababu yeye ni mpole kupitiliza, mvumilivu sana,
mnyenyekevu,anajali sana,ni mstaarabu sana itakuwa sababu ya kupendwa sana na
wanawake kuliko wanaume wengine lakini uhalisia ni kwamba Mwanamke anahitaji
ULINZI sio tabia za kunyenyekea, kusamehe makosa haraka, uvumilivu
uliopitiliza, ustaarabu sana ndiyo maana anaweza kuvumilia kung’ang’ania kwa
mwanaume mbabe,jeuri,asiekuwa na huruma wala unyenyekevu kwa sababu anajua huko
anaweza kulindwa kwa urahisi.Hauwezi kumlinda mwanamke ambaye unatetemeka
ukimuona kwa sababu inaonekana haujazoea kuona wanawake wenye muonekano mzuri.
– Anakuwa anataka kumbadilisha Mwanamke wake tabia.Anaamini akiwa anajali
sana,anamsifia sana,anatoa fedha nyingi sana ataweza kumbadilisha Mwanamke wake
tabia ukweli ni kwamba Mwanamke akipenda huwa anabadilika tabia yeye mwenyewe
bila kuambiwa na mtu yeyote.
– Huwa anaishi kwenye mahusiano yenye kuendeshwa na upande mmoja.Yaani yeye
pekee ndiyo anapiga simu,kutuma sms mfululizo,kutuma zawadi za mara kwa mara
lakini anajibiwa kwa mkato,anagombezwa,anafokewa,anatolewa dosari za muonekano
lakini anakuwa mvumilivu sana.
– Huwa anamfuatilia Mwanamke ambaye amemkataa anamfuata
kimyakimya,anapokataliwa hakati tamaa,anakuwa king’ang’anizi,hata akifokewa
anajishusha,akijibiwa vibaya analia na kuomba msamaha hata kama hajafanya
makosa,huwa anatishia kujiua,huwa hawezi kustahamili kuachana na Mwanamke ,akiachana
na Mwanamke anashindwa kumtoa kichwani hivyo anaweza kuangukia kwenye ulevi
kupindukia,kuvuta bangi au dawa za kulevya baada ya mahusiano kuvunjika.
– Huwa anatumia fedha nyingi sana kubadilisha maisha ya mwenza wake akiamini
itakuwa kinga ya usaliti,kinga ya mahusiano kuvunjika lakini kilekile ambacho
alitaka kuzuia huwa chenye kumtokea baada ya kumsomesha, kumfungulia biashara,
kumtafutia kazi, kumnunulia zawadi za gharama,kulea watoto wa mwenza wake.
– Huwa yupo tayari kuongea kitu chochote,au kufanya kitu chochote ilimradi
athibitishe kwamba yupo na upendo wa dhati kwa Mwanamke mwenye kauli za mkato,
mwenye hasira kupitiliza,mwenye misimamo mikali sana na masharti magumu sana.
ZINGATIA HAYA MAMBO 4 UWE MWANAUME RIJALI
1.UHURU
Mwanaume Rijali anathamini uhuru wake kuliko kitu chochote,mwanaume Rijali
hawezi kuishi kwa kumtegemea Mwanamke wake kwenye fedha,salio,kula,kuvaa,
nyumba ya kuishi, gharama za matibabu, usafiri,zawadi n.k mwanaume Rijali
anajua ni wajibu wake kuhakikisha maisha ya mwenza wake yanakuwa salama.
mwanaume Rijali haishi kwa kutegemea sapoti ya Mwanamke bali Mwanamke akitoa
sapoti inakuwa bonus ili kuepuka kumlaumu Mwanamke pale ambapo haonyeshi
ushirikiano.
Mwanamke yeyote akiona unamhitaji sana ili mambo yako yaende huanza kuonyesha
dharau waziwazi,atakuwa na kiburi, majivuno,ataanza kuonyesha jeuri kwa sababu
anajua hauwezi kumuacha wala hauwezi kuishi bila yeye.Lakini kama unaishi bila
kumtegemea kwa chochote hauwezi kumlaumu kwa jambo lolote.
mwanaume Rijali anabeba majukumu yake yote kisha majukumu ya watu wengine
anawaachia wahusika.
Ukibeba majukumu yako ipasavyo hauwezi kumlaumu mtu yeyote.
2.KUJIHESHIMU
Mwanaume Rijali anajiheshimu sana kuliko anavyoweza kumheshimu mtu
yeyote.Binadamu yeyote ukionyesha kumheshimu kupitiliza anakupanda kichwani.
mwanaume Rijali hana muda wa kutaka kumbadilisha tabia mwenza wake isipokuwa
anaweka sheria na taratibu za kuongoza mahusiano kisha anatimiza wajibu wake na
kumuacha mwenza wake atimize majukumu yake.
mwanaume Rijali hawezi kushobokea muonekano wa Mwanamke bali anaona ni kitu cha
kawaida hivyo hawezi kubabaika kwa uzuri wa Mwanamke,Bali anathamini sana
heshima ambayo anapewa na Mwanamke .
mwanaume ambaye anashobokea muonekano wa Mwanamke huwa ja wakati mgumu sana
kuachana na Mwanamke pale ambapo Mwanamke anapofanya usaliti, kumdhalilisha
mwanaume, kumnyima unyumba kwa muda mrefu.
Mwanamke akijua hauna ujanja juu ya muonekano wake anakuwa hana muda wa kujali
tabia zake kwa sababu anajua unasamehe makosa yote na utakuwa mvumilivu miaka
yote kwa sababu yeye ni mzuri sana.
3.KUSTAHIMILI HISIA
Mwanaume Rijali anaishi kwa kujitegemea yeye,akiwa mpweke haitaji
simu,faraja,sms ,zawadi kutoka kwa Mwanamke ili apate kujisikia vizuri.
mwanaume Rijali anakuwa kama komandoo kwenye uwanja wa vita kwa maana anabeba
furaha yake yeye mwenyewe vilevile anabeba maumivu yake yeye mwenyewe.
Mwanaume Rijali akiwa na huzuni,upweke, majonzi anajua ni wajibu wake kubeba
maumivu hayo siyo jukumu la Mwanamke .
Kama hauna furaha kwa sababu Mwanamke hajapiga simu,hajatuma sms,hajakufariji,hajakupa
pole kwa kazi utakuwa na malalamiko, manung’uniko,utanuna, kususa,kuishi ukiwa
na chuki, kinyongo moyoni kwa sababu unampa Mwanamke wako jukumu la
kukufurahisha jambo ambalo husababisha migogoro ya kimapenzi mara kwa mara.
Mwanamke yeyote akiona haulalamiki juu ya ukimya wake,au tabia zake ataanza
kutilia shaka kama ûnampenda.Kwa sababu Mwanamke anaweza kukupuuza kwa makusudi
lengo aone kama utaanza kulalamika ili ajue kama ûnampenda sana,akijua
anapendwa sana huanza kuonyesha dharau waziwazi kwa sababu anajua hauwezi
kumuacha wala hauwezi kuishi bila yeye.
Lakini kama upo na furaha yako wewe mwenyewe akiwepo au akiondoka haiwezi
kukusumbua wala kwake hauwezi kuonekana msumbufu.
4.KUJIWEKEA MIPAKA
Mwanaume Rijali anajua tabia gani za kuvumilia na tabia gani siyo za kuvumilia.
mwanaume Rijali anajua makosa ya kusamehe na makosa ambayo siyo ya kusamehe.
mwanaume Rijali anamuongoza Mwanamke , mwanaume Rijali
hampigi,hamdhalilishi,hamtukani Mwanamke bali anaishi naye kwa misingi ya kuheshimiana
na uadilifu.
mwanaume Rijali anajua Mwanamke akiwa mgonjwa anahitaji faraja,anajua Mwanamke
akiwa na huzuni anahitaji faraja, anajua Mwanamke akiwa amefanya kazi nyingi
anahitaji kupewa pongezi, vilevile mwanaume Rijali anajua hawezi kumnyenyekea
Mwanamke kama njia ya kuzuia mahusiano kuvunjika.
mwanaume Rijali anampa onyo Mwanamke pale ambapo anaonyesha utovu wa
nidhamu,anampa onyo siyo kwa kumfokea, kumtukana, kumkashifu, kumkaripia,
kumgombeza, kumtangaza vibaya n.k bali anamweleza wapi amefanya makosa na
vilevile anamuonyesha wapi pa kujirekebisha.
Mwanaume Rijali hana gubu, kisirani,chuki, kinyongo,wivu wa mapenzi
uliopindukia.
Mwanaume Rijali anaishi kwa kujiongoza.
mwanaume Rijali anajua kumlinda na kumtetea mwenza wake dhidi ya kukosolewa,
kusemwa vibaya, kutukanwa, kujibiwa vibaya kutoka kwa mama yake mzazi pamoja na
dada zake.
mwanaume Rijali anasimama katikati hayupo upande wa mama yake mzazi,au dada
zake vilevile hayupo upande wa mwenza wake.
mwanaume Rijali anafanya uadilifu,mwanaume Rijali anakuwa mtenda haki,mwanaume
Rijali hafanyi upendeleo,mwanaume Rijali anaongozwa na akili siyo hisia za
mapenzi.
mwanaume Rijali hana uwezo wa kumpenda Mwanamke kwa hisia kali bali anampenda
Mwanamke kwa kuongozwa na akili sio hisia.