Haijalishi Atapata Mwanaume Wa Aina Gani Bado Migogoro Ipo Palepale
Kwa sababu baba ndiyo kichwa cha familia basi leo tuangalie namna ambavyo
mwanaume ambaye ni muadilifu, mwaminifu,anatenda haki,hataki migogoro ndani ya
familia,anataka kujenga familia imara namna ambavyo anaweza kuepukana na hawa
wanawake wasumbufu ambao haijalishi utakuwa muaminifu,unajali sana,unampa
kipaumbele muda wote lakini bado utaona kuna mfululizo wa matukio yenye kuibua
ugomvi na migogoro.
ujumbe huu umegawanyika sehemu zifuatazo
I.Sifa 8 za Mwanamke ambaye hapendeki
ii.Vyanzo vya Mwanamke kuwa hapendeki
iii.Njia za kukabiliana na Mwanamke ambaye hapendeki
SIFA 8 ZA MWANAMKE AMBAYE HAPENDEKI
Sifa ya kwanza mpaka ya nane
1. HUWA ANADAI HANA UHURU MUDA WOTE MWANAUME AKITAKA UKARIBU NAYE
Mwanamke ambaye hapendeki huwa siku zote anataka uhuru uliopitiliza,huwa hataki
ukaribu wa aina yoyote na mwanaume kwa sababu anakuwa na hofu ya kuachwa
mpweke,kuumizwa, kusalitiwa,kupigwa, kunyanyaswa hali hiyo husababisha anakuwa
anaibua ugomvi mara kwa mara akiona mahusiano yake na mwanaume wake yanazidi
kuwa serious sana.
Anakuwa busy kupitiliza kiasi kwamba simu hapokei,sms hajibu hali ambayo
husababisha mwanaume anapiga simu mfululizo na kutuma sms mfululizo lakini
hajibu chochote,au anajibu kwa mkato kuzuia mazungumzo kuendelea.
Mwanamke ambaye hapendeki hataki kuambiwa makosa yake, hataki kukosolewa,
hataki kuambiwa cha kufanya,hataki kukataliwa akiomba kitu chochote anataka
papohapo,hajui kuomba bali anatoa maagizo na vitisho vya kuvunja mahusiano.
Huwa anataka mwanaume ambaye ni mpole kupitiliza, mvumilivu sana, mnyenyekevu
kupitiliza, king’ang’anizi, mstaarabu sana ili iwe rahisi kumtawala,kumpangia
sheria, kumdhalilisha, kumgombeza, kumtangaza vibaya,kumpa vitisho mara kwa
mara.
2. HAJALI HISIA ZA MWANAUME WAKE
Mwanamke ambaye hapendeki huwa hajui kufariji,hajui kutoa pole,hajui kuomba
msamaha,hajui kusema ahsante, muonekano wa sura anakuwa na uso wa hasira
kupitiliza muda wote akiwa na mwanaume wake,anakuwa amekaza sura (pretty tough
exterior),hana hisia za mapenzi,hataki kuonekana dhaifu,anataka kuonekana ni
mkamilifu saa 24,kwa sababu anakuwa anaficha hisia zake muda wote unakuwa
haujui nini kinaendelea ndani ya akili yake ghafla tu anaweza kuanza
kufoka,kutukana,kutoa vitisho,kuvunjavunja vitu,kubamiza mlango,kuondoka eneo
ambalo ulipanga kuwa naye, anaweza kumgombeza na kumjibu vibaya mwanaume wake
hata mbele ya watoto au wageni hajali chochote,anakuwa hana huruma hata chembe,
anaweza kumdhuru mwanaume wake muda wowote akiwa na hasira.
3. MIPANGO YAKE ANAFANYA KWA SIRI
Hataki kueleza hatma ya mahusiano yake,mara kwa mara huonekana hajali chochote
kuhusu mahusiano yake,hata kama atakuwa na miaka 38 haonekani kujali chochote
kuhusu kuwa na familia au kulea watoto,au anaweza kumchukia mwanaume moja kwa
moja na kuamua kujali watoto tu huku anatangaza chuki dhidi ya wanaume wote
ulimwenguni akiwaita “mbwa”.
hawezi kumwambia mwanaume wake kama anampenda anahisi ni udhaifu,hawezi
kuonyesha hisia zozote za mapenzi anahisi ni udhaifu,akiona mwanaume anazidi
kumzoea sana anatafuta kisingizio cha kuibua ugomvi kuzuia ukaribu na mwanaume
wake.
anaweza kujenga kwa siri, kufungua biashara kwa siri,ataweka fedha nyingi sana
kwa siri,akiwa na kazi yenye kipato kikubwa kuliko mwanaume haijulikani fedha
zake anapeleka wapi.
hataki kuulizwa kuhusu tabia zake,akiulizwa tu anaibuka na hasira kupitiliza na
kuanzisha mabishano na mijadala,akifanya makosa makubwa anageuza kibao kwa
mwanaume,hakubali makosa wala hakubali kushindwa kwa jambo lolote.
Analolipanga ndiyo hilo hilo anataka lifanyike.Hakubali mawazo mbadala hata
siku moja.Anataka kumtawala na kumpangia sheria mwanaume wake ndani ya
nyumba,anakuwa na sauti ya ukali kupitiliza na ubabe ndani yake.
Kwenye mahusiano hawezi kumtambulisha mwanaume wake kwa ndugu zake au marafiki.
4. PAKITOKEA UGOMVI HAKUBALI KUSHINDWA
Akifanya makosa endapo ataulizwa kuhusu makosa yake anaibuka kwa jazba na
kuanza kumshambulia mwanaume wake kwa matusi, vitisho, kumdhalilisha,
kumgombeza, kumtangaza vibaya, kumlaumu sana muda wote,anakuwa haambiliki,
hashauriki, anakuwa na hasira kupitiliza na misimamo mikali sana kwa jambo
lolote ambalo amepanga.
anataka kila mtu na kila kitu kifanyike vile ambavyo yeye mwenyewe
amepanga,hawezi kukubali kuwa chini ya mamlaka ya mwanaume hata siku moja,bora
mahusiano kuvunjika kuliko kukubali kupangiwa cha kufanya na mwanaume wake.
Akiomba fedha anataka kiasi hichohicho bila kujali hali ya kiuchumi ya mwanaume
,kwake kukubali kiti tofauti na matarajio yake anaona ni UDHAIFU mkubwa
sana,hataki kuonekana dhaifu mbele ya Mwanaume hata siku moja.
5. HAWEZI KUMUAMINI MWANAUME HATA SIKU MOJA
Siku zote anasisitiza kwamba “usije kumuamini kiumbe anaitwa
mwanaume” ,anakuwa na msisitizo huo kwa sababu baba yake huenda alikuwa
anampiga sana na kumtesa mama yake mzazi,huenda alitelekezwa akiwa mdogo,huenda
alitelekezwa na ujauzito au watoto,huenda alipitia vipigo kwa muda mrefu
alipokuwa anampenda sana mwanaume siku za nyuma.
Hivyo anakuwa na chuki, kinyongo moyoni na uchungu mkali sana dhidi ya wanaume.
Muda wote anahisi mwanaume anataka kumdhuru hivyo anaweza kumdhuru mwanaume
kabla ya mwanaume hajafanya hivyo.
6. HUWA NA MATARAJIO AMBAYO SIYO HALISI
Anatarajia kupata mwenza ambaye hana dosari zozote,jambo ambalo husababisha
anakaa mpaka miaka 35 bila mume au mtoto kwa sababu anakuwa anabagua sana
wanaume,kila mwanaume kwake anamuona siyo wa HADHI yake.
Anakuwa bingwa wa kubadilisha maamuzi ghafla tena dakika chache kabla ya
makubaliano.
kwa mfano umepanga naye kuonana sehemu XYZ ,muda ABC nusu saa kabla ya kuonana
anapiga simu akidai amepata dharura,au anazima simu haipatikani kabisa anafanya
kwa makusudi ili kukomoa.,
Huwa hafanyi juhudi za kudumisha mahusiano hivyo mara nyingi anakuwa na mpango
wa kuachana na mwanaume wake kimyakimya kabla mwanaume wake hajamuacha ghafla.
Akikwazana mara moja na mwanaume wake hapohapo mahusiano yamevunjika.Kuishi
naye inatakiwa kuepuka kumkasirisha saa 24 jambo ambalo wanaume wengi hawawezi
hivyo husababisha mahusiano kuvunjika mara kwa mara kwa sababu ndogondogo.
7. ANAJISIFIA SANA NA KUSHUSHA THAMANI MAFANIKIO YA MWANAUME WAKE
Mara kwa mara anajisifia sana kuhusu muonekano wake, fedha, ukoo, elimu,
umaarufu,kujuana na watu mbalimbali n.k lengo kumfanya mwanaume wake apoteze
uwezo wa kujiamini.
Huwa anataka mwanaume ambaye ananyenyekea sana ili amgeuze mtumwa.
anapenda kutengeneza mazingira ya kumfanya mwanaume ajione kituko,ajione kitu
cha aibu,ajione mwenye bahati sana kupendwa naye.,yeye huwa anajiona mkamilifu
kisha huwa anawaona wanaume ni wakosaji tu saa 24.
8. ANATUMIA MUDA MWINGI SANA AKIWA PEKEAKE
Anaweza kuwa na marafiki wengi sana,anakuwa mcheshi, mkarimu, mwenye kujali
sana mbele ya jamii lengo kuficha tabia zake halisi au anaweza kuonekana
anaringa sana muda wote anataka kusujudiwa.
kauli zake “mwanaume hawezi kunibabaisha,”,anapenda mashindano na
wanaume kwa kila kitu.
VYANZO VYA KUPATA MWANAMKE
AMBAYE HAPENDEKI
Mwanamke ambaye hapendeki huwa hivyo kwa sababu zifuatazo
1. KULELEWA NA BABA LEGELEGE (PASSIVE FATHER)
Sifa za baba yake ni upole kupitiliza, kunyenyekea sana, kusamehe makosa
haraka, uvumilivu uliopitiliza, mstaarabu sana hivyo tangu utotoni mwake
amekuwa amezoea kunyenyekewa,haambiwi makosa, chochote ambacho anataka anapewa
,baba alikuwa hana kauli wala mamlaka juu yake,hivyo alizoea kujiona
malaika.Baba akiwa mpole kupitiliza mama huwa anakuwa mkali kupitiliza,hivyo
mara kwa mara alikuwa na ugomvi na mama yake mzazi kwa muda mrefu kwa sababu
mama alikuwa anaona anapendwa sana na kudekezwa sana akiwa na baba yake.
2. KULELEWA BILA BABA
Sababu nyingine yenye kusababisha Mwanamke ambaye hapendeki ni kulelewa bila
baba ndani ya familia.
Hapa unakuta familia ya single mother analea watoto yeye mwenyewe hivyo binti
anakuwa hajui kuheshimu mamlaka ya mwanaume tangu akiwa mdogo sana,hivyo akiwa
mkubwa hawezi kukubali kuongozwa na mwanaume kwa sababu anaona kama anapitia
manyanyaso kwa kukosa uhuru .
Sababu ya kumkosa baba utotoni ni kifo cha baba,talaka,mama kutekelezwa na
ujauzito au watoto,baba kukataa ujauzito,
Kukua bila baba husababisha binti anaanza kujipambania yeye mwenyewe kama
mwanaume tangu utotoni mpaka ukubwani.
3. KULELEWA NA BABA DIKTETA
Hapa ni familia ambayo baba anakuwa mkali kupitiliza mpaka kila mtu
anamuogopa.Kutokana na ukali kupitiliza mtoto wa kike hauna kupambana na baba
yake tangu utotoni kwa kujibizana, kufokeana,kugomea maagizo, kutoroka nyumbani
kwao kwenda kulala mtaani n.k hivyo akiwa mkubwa hataki kugombezwa wala
kuambiwa makosa yake.
4. KUANZA MAJUKUMU AKIWA BADO MDOGO SANA
Mwanamke mbabe sana anakuwa hivyo kwa sababu ya kumlea mzazi au wadogo zake
tangu akiwa mdogo sana,kuishi na baba au mama mlevi kupindukia, mcheza kamari,
mhalifu, mwizi kuona mama anapigwa na kudhalilishwa mara kwa mara hivyo
anajifunza kumtetea mama dhidi ya kipigo cha baba.
5. KUPITIA MANYANYASO NA MATESO
Matukio ni kama vile kubakwa, kulawitiwa, kunyang’anywa mali, kufukuzwa
nyumbani usiku wa manane,kupiga mpaka ujauzito unatoka, kudhalilishwa
hadharani,.
UFUMBUZI WAKE
1. JALI HISIA ZAKO
Mwanaume Rijali epuka kumtegemea mwenza wako kwa ajili ya faraja,epuka kusubiri
sms,simu kutoka kwa mwenza wako,
kama unaishi kwa kutegemea sms,simu kutoka kwa mwenza wako atakuwa na kiburi
cha kuona kwamba hauwezi kuishi bila yeye hivyo atakuwa mara kwa mara
anakupuuza,simu haupokei,sms hajibu,ananuna,atasusa,atakaa kimya mara mara kwa
mara,atatoroka kwenda nyumbani kwao mara kwa mara ili kupima kama hauwezi
kuishi bila yeye akiona hauna furaha atatumia njia hiyo kama udhaifu wako mara
kwa mara.
2. JENGA UWEZO WA KUJIAMINI
ona
kawaida kuzungumza na wanawake wenye muonekano mzuri sana ili asije kutishia
muachane mara kwa mara kwa sababu anajua hauwezi kupata mwenza mzuri zaidi yake
.Acha kujiona upo na bahati kwa sababu upo na Mwanamke mwenye muonekano mzuri kwa
sababu ataona huo udhaifu,badala yake jenga mazoea ya kuzungumza na wanawake
wenye muonekano mzuri sana ili uondoe hofu.Ukiwa unajiamini utaweza kuishi na
Mwanamke mzuri bila hofu ya kuachwa.
Zingatia zaidi heshima ambayo anakupa siyo uzuri wa muonekano wake.Kemea tabia
mbaya ,muelekeze kama anaweza kukubali akiwa jeuri muachane.
Mwanamke ambaye hapendeki huwa maalumu kwa ajili ya player boys wale
wanaume ambao hawana malengo yoyote ya kujenga familia,kisha wanawake
wasiopendeka wakiachwa ndio huwa wanataka mwanaume mstaarabu sana ili kulea na
kukuza watoto wa wanaume wajeuri.
usimpe ushauri, kumbembeleza, kumkumbusha wema umefanya zamani,akitaka muachane
ruhusu aondoke.