MAUDHI, MAJARIBU NA VITIMBI VYA MWANAMKE KATIKA MAHUSIANO
Tafiti za kisaikolojia zinaeleza kwamba wanawake
hawajui wanataka nini kutoka kwa mwanaume hivyo basi ikiwa wewe ni mwanaume
acha kupoteza muda wa kutaka kujua mwanamke anataka nini bali weka sheria na
muongozo wako mwenyewe kisha mwanamke wako ataufuata.
ZIFUATAZO NI NJIA 7 AMBAZO MWANAUME RIJALI ANAWEZA KUYASHINDA MAUDHI, MAJARIBU
NA VITIMBI VYA MWANAMKE KATIKA MAHUSIANO
Njia hizi 7 zipo kama ifuatavyo
1. KUPIMA UANAUME WA MWANAUME (DOMINANCE TEST)
Mwanamke yeyote ambaye nyumbani kwao mkuu wa familia ni mama,au amekuwa bila
baba ndani ya familia,au baba yake mzazi alikuwa dikteta,au baba yake mzazi ni
mpole kupitiliza kiasi kwamba hana kauli wala mamlaka yoyote ndani ya familia
huwa anapenda kumfanyia mwanaume jaribio hili.
Mwanamke hapa anataka kuwa kichwa cha familia hivyo ataonyesha tabia zifuatazo
-atampangia mwanaume sheria,atampa mwanaume maagizo,atamfokea, kumtukana,
kumkashifu, kumkaripia, kumgombeza, kumtangaza vibaya,kumtishia kumuacha mara
kwa mara,atamwabia mwanaume chagua mimi au mama yako mzazi,
atampiga marufuku mwanaume wake mara kwa mara kwa kumchagulia
marafiki,kumpangia matumizi ya fedha, kumpangia muda wa kurudi nyumbani,
kumuamrisha mwanaume atoe fedha nyingi sana ikiwemo kukabidhi mshahara wake
wote kisha Mwanamke anapanga matumizi.
Atamkosoa mwanaume mara kwa mara kwanzia muonekano, uvaaji, utembeaji,
lafudhi,harufu ya mwili, usafi wa mwili,atakuwa anamrekebisha mwanaume wake
tabia kila siku,atamnyima unyumba mwanaume wake kwa makusudi kama adhabu,
Atamwabia mwanaume siwezi kupangiwa cha kufanya,atakuwa haambiwi makosa,atakuwa
hashauriki, haambiliki, anakuwa mjuaji sana, anakuwa na hasira kupitiliza,
anakuwa na misimamo mikali sana ( rigid),akiamua jambo lolote ni hivyo hivyo hawezi
kubadili mawazo,anakuwa anataka kuwa juu saa 24,hataki kukosolewa, hataki
kuambiwa makosa yake, hataki,kupewa maagizo.
UFUMBUZI WAKE
Huyu mwanamke ni maalumu kwa ajili ya kuzaa kila mtoto na baba yake kisha huwa
anatelekezwa bila huduma zozote, vilevile mwanamke huyu huwa maalumu kwa ajili
ya kuzaa na waume za watu.
Hawezi kukubali kuongozwa ndani ya familia kwa sababu tangu utotoni anaamini ni
UTUMWA kuwa chini ya mamlaka ya mwanaume.
ufumbuzi wake ni kumrudisha nyumbani kwao akae mpaka akili ikimkaa
sawa,atakubali kuwa mwanamke.Hili ni zao la feminist.
2. KUPIMA UWEZO WA MWANAUME KUJIAMINI (CONFIDENCE TEST)
Ili mwanamke aruhusu mwanaume kumuongoza lazima mwanaume aonyeshe uwezo wa
kujiamini mbele ya mwanamke husika.
Ikiwa mwanaume hajiamini vilevile mwanamke atampuuza,mwanaume hawezi kumuongoza
mwanamke ikiwa yeye mwenyewe hawezi kujiongoza.
Mwanamke akiona mwanaume ananyenyekea sana,anaomba msamaha mara kwa
mara,anapiga magoti,anatuma sms ndefu sana,anajishusha sana huanza kumfokea,
kumtukana, kumkashifu, kumkaripia, kumgombeza,kumjibu vibaya,kusema wewe sio wa
HADHI yangu .
Ufumbuzi wake ikiwa wewe ni mwanaume epuka tabia za upole, huruma kupitiliza,
kujali sana, kunyenyekea sana, kusamehe makosa haraka badala yake simama kama
kiongozi shupavu, mwambie ninakuheshimu sana fulani, sihitaji tuvunjiane
heshima,akiwa na heshima mwanamke huyo ongea naye kwa utulivu,tazama
usoni,zungumza kwa pause,usiongee haraka haraka sana au polepole sana,epuka
kuonyesha hasira pale ambapo mwanamke anapoonyesha dharau mbele yako.
3. KUPIMA WIVU WA MWANAUME (JEALOUS TEST)
Mwanamke anaweza kupima wivu wa mwanaume kwa kupuuza sms,kupuuza simu,kupost
picha za wanaume wengine, kuzungumza habari za Ex wake,anaweza kusema kuna
mwanaume anamtongoza, anaweza kuzungumza na mwanaume mwenzako mbele yako kwa
kujilegeza legeza, anaweza kuchat mpaka usiku wa manane lengo uone wivu,au
anaweza kukaa na simu muda wote.
Hapa epuka kupaniki,epuka kuonyesha hasira,epuka kuonyesha kwamba hauwezi
kuishi bila yeye.
Ongea kwa utulivu kwamba ûnampenda sana na unamuheshimu lakini ikiwa atashindwa
kukuheshimu na kukuacha uwe mwanaume kamili katika maisha yake utamuacha uende
sehemu ambayo unapewa heshima..
Hapa nguzo ni mwanaume kuonyesha UONGOZI wake mahiri.
4. KUPIMA KAMA MWANAUME ANAWEZA KUMPA CHANGAMOTO (CHALLENGE TEST)
Wanawake ambao ni “wife material” hawavutiwi kimapenzi na wanaume
wenye tabia za huruma kupitiliza, kujali sana, kunyenyekea sana, kusamehe
makosa haraka, uvumilivu uliopitiliza, wastaarabu sana,bwana ndiyo,mwanaume
mpenda amani,mwanaume ambaye anajishusha sana.
Ukiwa na sifa hizo unapata mwenza mwenye tabia ya ubabe, ukali kupitiliza,
kiburi, majivuno, jeuri, ujuaji, misimamo mikali,anakuwa anataka kumtawala
mwanaume,anataka kila mtu na kila kitu kiwe chini yake, mwanamke ambaye anataka
uhuru uliopitiliza huwa anavutiwa kimapenzi na mwanaume mpole kupitiliza kwa
sababu anakuwa anataka kumtawala, kumpangia sheria,kum-control, kumgombeza,
kumbambikia ujauzito n.k
Mwanamke ambaye ni wife material akiona mwanaume anatabirika,mwanaume ni
mstaarabu sana anaanza kumchukia kwa sababu anahisi anaishi na mwanamke
mwenzake.
Kuwa mwanaume ambaye hautabiriki,zipo nyakati unakuwa mpole kiasi vilevile zipo
nyakati unakuwa mkali kiasi.Lengo mwanamke asijenge kiburi cha kuamini kwamba
hauwezi kuishi bila yeye,hauwezi kumuacha hata afanye kosa kubwa namna gani.
Zingatia kwamba mwanamke yeyote akiwa na uhakika kwamba ûnampenda sana kuliko
kitu chochote hapo ndipo anakuwa na kiburi, majivuno, jeuri, ujuaji, misimamo
mikali,anakuwa na masharti magumu sana, anaweza kufanya makosa makubwa sana kwa
makusudi kabisa kisha anageuza kibao kwako.
Hot & cold response
5. KUTAFUTA KISINGIZIO CHA KUACHANA (NUCLEAR TEST)
Mwanamke anapotaka muachane huonyesha tabia zifuatazo
atakaa kimya muda mrefu sana,simu hapokei, ukituma sms hajibu, au ukitumia
namba mpya anapokea kisha anatafuta kisingizio cha kukata simu.
ataomba fedha nyingi sana kuliko uwezo wako lengo ukishindwa tu
anakuacha,atakuwa na kiburi, majivuno, jeuri na dharau katika kuzungumza na
wewe.
Anaweza kukudhalilisha mara kwa mara,anakulinganisha na wanaume wengine kisha
anasema wewe sio wa HADHI yake,mara kwa mara anakuwa na hasira kupitiliza
akiona sura yako.
Utajikuta unafanya kazi kubwa sana kumfurahisha lakini anakuwa hana huruma wala
hana shukurani kwako.
Mara kwa mara atakuwa anakukosoa kwa vitu vidogo vidogo sana ili muachane kwa
ugomvi.
Akionyesha tabia hizo haitaji ushauri,haitaji kubembelezwa,hataki risala,hataki
kuambiwa makosa yake, hataki umlazimishe aseme hatma ya mahusiano yenu,hataki
umkumbushe wema wako kwake,hataki kusikia maisha yake yatakuwa magumu bila
wewe.Hapo anataka muachane tu.
6. KUKAA KIMYA BILA MAWASILIANO KWA MAKUSUDI (UNEXPLAINED DISTANCE)
Wanawake wenye tabia za ubabe, ukali kupitiliza, kiburi, majivuno, jeuri na
dharau hupenda sana tabia hii (ghosting).Yaani leo mnaongea kwa furaha sana
kisha kesho simu hapokei, ukituma sms hajibu.
Ukipiga simu kwa namba mpya anapokea kisha akisikia sauti yako anakata.
Hapa anataka kukuvuruga akili uanze kujiuliza wapi umefanya makosa lakini
haupati jibu.
Endapo utapiga simu mfululizo, kutuma sms mfululizo, kulalamika kwamba hauna
furaha kwa ukimya wake anapata kiburi cha kuamini kwamba hauwezi kuishi bila
yeye, hauwezi kumuacha hata afanye kosa kubwa sana namna gani.
Tabia hii anakuwa anataka kujua kama umeshampenda sana akiona unaonyesha
kubabaika kwa ukimya wake dharau, majivuno,na kukutesa huwa ndiyo tabia zake.
Ufumbuzi wake -Akikaa kimya sana bila mawasiliano yoyote,acha kupiga simu,acha
kutuma sms, ilimradi umepiga simu hajapokea na umetuma sms hajajibu.
Kaa kimya muonyeshe kwamba yeye ni binadamu kama walivyo binadamu wengine wala
hauwezi kuteseka kwa ukimya wake vilevile kama ataamua muachane pengo lake
unaziba na unamtoa kichwani haraka.
7. KUVUNJA MAKUBALIANO GHAFLA (FLAKE TEST)
Njia nyingine mwanamke anatumia ni kuvunja makubaliano ghafla.
Hapa inatokea umekubaliana na mwenza wako tunakwenda sehemu XYZ,muda ABC kisha
baada ya makubaliano anasubiri nusu saa kabla ya muda wa tuko lenyewe anatuma
sms kwamba amepata dharura au anakaa kimya tu bila sababu zozote za msingi
(ghosting).
nini cha kufanya zingatia sababu za hali hiyo
a.Hana hisia zozote kwako lakini anashindwa kukataa
b.Anakujaribu ili kupima tabia yako ikoje
c.Ipo sababu ya msingi ambayo ni DHARURA kwa muda huo.
ufumbuzi wake acha kupiga simu mfululizo,acha kutuma sms mfululizo.
kaa kimya muonyeshe kwamba yeye kukaa kimya haijaleta athari zozote katika
ratiba yako.
Endapo utapiga simu mfululizo na kutuma sms mfululizo itamfanya aweze kuwa na
kiburi, majivuno, jeuri,dharau na vilevile anakuona haujielewi kwa maana anaona
hauwezi kuishi bila yeye, hauwezi kumuacha na vilevile furaha yako anaicontrol
yeye.
Kaa kimya,muache apange ratiba nyingine yeye mwenyewe,kama alikuwa anakupima
atakuja na visingizio kibao,kama alikuwa anataka muachane utakuwa umeokoa fedha
zako na muda wako ambao ungepotea kwa mtu huyo.