KUUMIA KIMAPENZI
Wanaume
huwahitaji wanawake kwa sababu kuu mbili, tendo na upendo wa kweli, lakini mara
nyingi wanaume huwa hawatambui wanawahitaji wanawake kwaajili ya tendo au kwa
ajili ya upendo, hali hii hupelekea wanaume kuoa mtu asiye sahihi kwenye maisha
yake.
Mwanaume anaweza kukupenda kwa kiasi kikubwa na asikuoe.
Mwanaume anaweza kufanya mapenzi na wewe kwa miaka mingi bila kukuoa. Lakini
kama atapata mtu ambaye ataleta utulivu katika maisha yake, basi atamuoa.
Wanaume ni watu wenye maono ya ajabu sana hasa wanapofikiria kuhusu ndoa, huwa
hawafikirii kuhusu wao wanafikiria kuishi tu na mtu yeyote atakae wafaa hata
bila harusi wanaweza kuishi na mtu
Wanaume Wanafikiri kwamba mwanamke huyu anaweza kuniletea furaha ndani ya
nyumba. Wanawake ni kama zabuni, wana uwezo wa kukupokea na kukuzalia
anakuandalia chakula pale unapompa pesa kwa wakati anakupa amani, wewe unampa
manii na anakupa watoto.
Kama Utampa usumbufu, inakuwa kama unajitengenezea ndoto mbaya ya maisha yakona
wanaume wengi wanaijua hilo. Ndiyo maana mwanaume anaweza kukaa na mwanamke kwa
miaka mingi na kukutana na mwanamke mwingine ndani ya mwezi mmoja, kisha
akamuoa.
wanaume wengi kinachowaroga Ni utulivu tu wanaotaka.
Mapenzi ni raha kama kuna utulivu na muwe mnapendana, mapenzi ni mapenzi tu,
lakini HESHIMA ni utulivu.