DOCTA SIUMWI HUKOO
Sehemu Ya 11
ILIPOISHIA
“Je, nikigundua umetembea naye?”
“Nifanye lolote lile.”
“Sawa.”
ENDELEA
Mume wa Monica alifika nyumbani akiwa amechoka sana. Mkewe alipomwona alitoka mbio kumlaki…
“Pole na kazi mume wangu.”
“Asante sana.”
“Sasa ikawaje, mbona hujajibu meseji yangu wala hujapokea simu?”
“Niache Monica.”
Monica alishtuka sana kwani si kawaida mume wake kumwita kwa jina la Monica, alizoea darling au mke wangu,
wakati mwingine alimwita mama.
Akajua pana jambo zito limetokea…
“Kwani kuna nini?”
“Umenitumia meseji kwamba una limimba?”
“Ha! Baby, nina limimba au nina mimba?”
“Una limimba, mimba kwani kitu cha kufurahia wakati unajua kila kitu?”
“Kwani mume wangu kuna nini?”
“We! Mimi siyo mume wako.”
“He! Yamekuwa hayo jamani, kwa nini kwani?”
“Hilo limimba ni la nani?”
“Si yako.”
“Wewee, mimi sijakupa mimba wewe.”
“Kanipa nani sasa?”
“Unamjua, tena nitakupiga sasa hivi.”
Monica alimkwepa mumewe na kwenda kukaa sehemu nyingine lakini akiwa amejaa mawazo…
“Au kajua kuhusu mimi na Dokta Kisarawe?”
“Lakini kama kajua, kajuaje? Mbona hakuna mawasiliano kati yake na dokta?”
“Mh! Labda Sulee kamwambia hisia zake maana Sulee sijawahi kumwambia kwamba nimetembea na dokta, sasa?”
“Ha! Liwalo na liwe bwana, sasa nitafanyaje?”
“Monica,” aliitwa na mumewe Monica tena sauti iliyotumika ilikuwa kali sana.
“Abee.”
Monica aliinuka, akatembea kwa kasi mpaka kwa mumewe…
“Nataka tukapime DNA…”
“DNA ndiyo nini mume wangu?”
“DNA ni kipimo kitakachoweza kusema ukweli kama hilo litumbo lako ni la kwangu kweli au la!”
“He! Mume wangu jamani, umefikia huko?”
“Ndiyo.”
“Mh! sawa.”
“Kesho tutakwenda.”
“Sawa.”
Alipoondoka, Monica alimtumia meseji Dokta Kisarawe na kumuuliza kama amewasiliana na mwanaume yeyote anayeitwa David…
“Hapana.”
“Kwani vipi?”
“Nahisi mume wangu amejua natembea na wewe na ana wasiwasi na ujauzito wangu.”
“Unasema kweli?”
“Dokta kwa nini unauliza kama nasema kweli, ina maana hata wewe unajua huu ujauzito unaujua si wake?”
“Sijasema hivyo.”
“Sasa?”
“Nimeshtuka kusikia mtu ana wasiwasi na mimba yake.”
“Kasema kesho tunakwenda kwenye DNA sijui.”
“Mh! amefikia na huko?”
“We acha tu. Sina amani hapa nilipo.”
***
Usiku akiwa sebuleni, mume wa Monica alimpigia simu mume wa Sulee ambaye naye alikuwa amekaa sebuleni na mke wake…
“Haloo, kesho bwana nakwenda kwenye ile DNA, nakwenda na shemeji yako, nadhani imefika mahali ukweli ujulikane.”
“Sawasawa, naunga mkono.”
“Je, utakuwa tayari unisindikize?”
“Unataka niwepo kaka?”
“Muhimu sana.”
“Basi hakuna shida, nitakuwa na wewe.”
Baada ya kukata simu…
“Unaongea na nani umsindikize?” Sulee alimuuliza mume wake.
“David, kesho anampeleka mkewe wake kupima DNA ili ajue kama kweli ile mimba ni yake au la!”
“Mh!” aliguna Sulee.
“Unaguna nini, au unajua si yake kweli?”
“Hapana, nimeguna kuona amefikia huko.”
Palepale, Sulee alishika simu na kumtumia meseji Monica…
“Mwenzangu unalo, mpaka kwenye DNA?”
Monica aliposoma meseji ya shoga yake huyo alishtuka sana, lakini pia aliumia moyoni…
“Ina maana mume wangu amemwambia Sulee kuhusu hili?”
“Mbona siamini! Mume wangu na Sulee wapi kwa wapi mpaka amwambie mambo mazito kama haya?” aliwaza moyoni Monica huku akiseti namba za Sulee ili amtwangie…
“Ee…”
“Sulee, nani amekwambia?”
“Ni kweli si kweli?”
“Ni kweli ndiyo, lakini nani amekwambia?”
“Mume wangu.”
“Kaambiwa na nani?”
“Si kaambiwa na shemeji.”
“Kamwambia tu au?”
“Kamwambia amsindikize hospitali.”
“Mh!” aliguna Monica, mapigo ya moyo yalimwenda kwa kasi ya ajabu.
***
Usiku wa kuamkia siku ya kwenda hospitali, Monica alimwamsha mumewe…
“Baby…baby.”
“Mh!”
“Nataka kuzungumza kidogo.”
“Kuhusu nini?”
“Hivi ni kweli kabisa umedhamiria kesho kwenda kupima DNA?”
“Hilo lilishapita na kama umeniamsha kwa ajili hiyo naomba aniache nilale vinginevyo niambie ukweli una mwanaume mwingine nje?”
Monica hakujibu swali hilo. Moyoni alijua anaye mwanaume hata kama si rasmi ambaye ni Dokta Kisarawe, lakini atawezaje kumwambia mumewe kuhusu hilo?
“Sina,” alijibu kwa mkato.
“Basi majibu tutayapata kesho kwenye DNA.”
“Mh!” Monica aliguna, akabaki kimya. Usingizi haukumpata, muda mwingi akili yake ilikuwa ikifikiria namna ya kufanya ili kuepukana na zoezi la kwenda kupima hiyo DNA…
“Au niamke mgonjwa?” aliwaza…
“Tena nataka kukwambia hivi Monica, kesho asubuhi hata ukiamka unaendesha tumboni, daktari na vipimo vyake atakuja hapahapa nyumbani,” alisema mume wake na kuuza mawazo kwamba aamke anaumwa japokuwa naye alitoa kauli ya kumchimba mkwara tu.
***
Asubuhi Monica ndiyo alikuwa wa kwanza kutoka kitandani, hakupata usingizi kwa usiku kucha huku akiendelea kuwaza kitanzi kilicho mbele yake…
“Za asubuhi?” alimsalimia mumewe.
“Nzuri, jiandae tuwahi.”
***
Saa mbili na nusu walifika hospitali yenye kutoa huduma ya DNA ambapo pia walimkuta mume wa Sulee…
“Za leo mkubwa?” mume wa Sulee alimsalimia mume wa Monica…
“Salama kaka, mzima?”
“Mzima sana. Naona tumewasili.”
“Sana tu.”
Sura ya Monicha ilionesha wazi kwamba haikutaka kusalimiwa na wala haikuwa tayari kupokea salamu kutoka kwa mtu mwingine.
“Shemeji vipi?” mume wa Sulee alijipa kichwa ngumu na kumsalimia hivyohivyo tu, aitikie, agome angejijua mwenyewe.
“Salama,”
Monica aliitikia kwa mkato, mumewe aligundua lakini hakuhusika naye kumuuliza kuna nini mpaka ameitikia salamu kwa staili hiyo.
Walipata huduma kwa kuchukuliwa vipimo muhimu ambapo Monica alichomwa sindano ya tumbo na kuchukuliwa sampo ya maji huku mumewe akichukuliwa vipimo vya kawaida.
“Majibu mje baada ya wiki mbili,” alisema dokta.
“Sawa dokta, hakuna neno.”
***
Mchana wa siku hiyo, Monica alikuwa kwenye chumba cha Dokta Kisarawe kwa mazungumzo muhimu…
“Kwa hiyo dokta kama nilivyokwambia, hapa sijalala. Mawazo yote ni kuhusu hicho kipimo je, kitasema mtoto wa nani wakati yeye kaenda kupima akaambiwa hana uwezo wa kuzaa?”
“Mimi ninavyojua, mtoto huyo tumboni ni kweli si wa mume wako.”
“Nini dokta?
Unamaanisha ni wa nani sasa? Maana mwanaume pekee niliyekutana naye kwa mwaka huu nje ya mume wangu ni wewe.”
“Inaweza kuwa ya kwangu.”
“Aaah! Dokta, lengo lako ni nini?”
“Ilitokea tuu!”
“Ili?”
“Unajua mazingira yalikuwa si ya kutafuta kinga Monica, sasa tungejikingaje? Halafu we shida yako si ilikuwa kupata mtoto kwa sababu mumeo hakuwahi kukupa ujauzito…”
“Sasa ndiyo we unipe kwa njia ya ukweli dokta?” alihoji Monica huku akianza kulia machozi.
“Ndiyo njia ninayoitumia Monica, hata rafiki yako Sulee pia ana ujauzito wangu.”
“Ha! Kweli dokta?”
Simulizi yetu ndo kwanza inaanza usisite kuisaport simulizi hii iendee kuruka hewani kwa muda muafaka
DOCTA SIUMWI HUKOO
Sehemu Ya 12
TULIPOISHIA
“Sasa ndiyo we unipe kwa njia ya ukweli dokta?” alihoji Monica huku akianza kulia machozi.
“Ndiyo njia ninayoitumia Monica, hata rafiki yako Sulee pia ana ujauzito wangu.”
“Ha! Kweli dokta?”
TUENDELEE
“Sana tu.”
Kidogo Monica alijiona kama amepoa kusikia Sulee naye ni mjamzito…
“Sasa utanisaidiaje mimi kuhusu maji ya DNA?”
“Rahisi sana, ila kama uko tayari kusaidiwa twende gesti sasa hivi.”
Mh! halafu?”
“Aah! Kwani Monica hujui tukienda gesti halafu ni kitu gani?”
“Ina maana dokta bado unataka?”
“Si sana, ila kwa ajili ya kuburudika mwili wangu.”
“Hivi dokta huoni kama sitajisikia vizuri kutokana na matatizo?”
“Ni akili tu Monica, unaweka pembeni mawazo yote. Kwani si nimekwambia nitakwenda kuongea na daktari wa DNA kwenye ile hospitali?”
“Utamwambiaje?”
“Najua mimi.”
“Nihakikishie kwanza ili kama nikiona kweli inawezekana tunaweza kwenda huko gesti.”
“Nitamwambia ayapindishe majibu. Yawe ni kweli mimba ni ya mumeo.”
“Lakini si amepimwa imeonekana hawezi kuzaa?”
“Bwana wewe Monica, kila kitu kinawezekana, ujue hilo kwanza ili mengine yaendelee.”
“Mh! Dokta huo ni mtihani mkubwa kwangu. Lakini poa twende.”
“Sasa sikia, wewe tangulia kufika kwenye ileile gesti ya siku ile.”
“Usichelewe.”
“Ndani ya dakika sifuri nitakuwa nimefika na mimi.”
Monica alikwenda gesti bila kupenda, lakini angefanyaje wakati aliitaka ndoa yake. Dada yake wa kwanza aliachika, wa pili pia, watatu hajaolewa, wa nne kaachika na uzee juu, sasa ilikuwa lazima yeye ajichunge.
Wakati anaingia gesti hiyo, mume wa Sulee akamwona akiwa ndani ya teksi…
“Haa! Yule si shemeji Monica?”
Alichofanya mwanaume huyo alimpigia simu mkewe, Sulee ili amsimulie lakini namba ikawa haipatikani hewani…
“Khaa! Huyu naye vipi? Mbona hayupo hewani!”
Alijaribu mara mbili tatu, mwishowe akaamua kumpigia simu mume wa Monica…
“Mshikaji wapi saa hizi?”
“Job, niambie…”
“Mh! Kuna ishu moja hivi lakini naona kama haijakaa sawasawa.”
“Ipi hiyo tena?”
“Nimepita kwenye gesti moja hivi, nimemuona shemeji akiingia. Mna mgeni yeyote ambaye amefikia gesti?”
“Hapana! Ni wapi?”
“Hapa Kinondoni Mkwajuni.”
“Nakuja, nisubiri hapohapo ulipo.”
“Poa.”
Mume wa Monica alikodi teksi akamuomba dereva aendeshe kwa kasi hadi Kinondoni Mkwajuni. Hakutaka kumpigia simu mke wake asije akapoteza ushahidi. Alikutana na mume wa Sulee ambaye alihama kwenye teksi akaiacha iende na kuingia kwenye teksi aliyofika nayo mume wa Monica.
“Vipi mshikaji, gesti gani?”
“Ile pale yenye maua. Lakini ni vyema umpigie umuulize aliko si ajabu si yeye, nilifananisha tu.”
“Hapana, nikimpigia nitapoteza ushahidi.”
“Huwezi, kwani akiwa yeye kweli na sisi tumesimama hapa nje atajiteteaje?”
“Lakini kweli.”
Mume wa Monica aliiseti simu yake akampigia mke wake, simu iliita kwa muda mrefu mpaka ikakatika…
“Hapokei,” alisema mume wa Monica kwa sauti iliyoambatana na mtetemesho wa ghadhabu kama siyo hasira za kupitiliza.
Mara Dokta Kisarawe akatokea, mume wa Sulee anamjua alishakutana naye siku moja…
“Ha! Mshikaji, huyo anayeshuka kwenye gari ndiye Dokta Kisarawe ambaye anawatibu wake zetu.”
“Mh! Au ndiyo jamaa mwenyewe?”
“Huenda.”
“Sasa?”
“Tusubiri hapahapa nje.”
Mara, simu ya Monica iliingia kwa mume wake…
“Huyo anapiga.”
“Pokea.”
“Haloo.”
“Ee my husband, nimeona missed call yako hapa.”
“Uko wapi kwani mpaka hukupokea simu?”
“Kwani we uko wapi?”
“Khaa! Mimi nakuuliza na wewe unaniuliza, una akili kweli wewe?”
“Mimi nipo jirani na nyumbani kwa mama Mariam.”
“Oke, sawa.”
Upande wa pili, yaani kwa Monica ikakata simu haraka.
“Sasa sikia, tukisema tukavamie vipi?” aliuliza mume wa Monica.
“Mawili. Kwanza niambie, kama kweli ni yeye utachukua hatua gani mzee?”
“Talaka tu.”
“Una uhakika?”
“Mungu vile ni talaka tu.”
“Okey, kama ni talaka basi tusivamie, tukae mpaka watoke sisi tushuke kwenye gari tukiwa wawili hivihivi.”
“Sawa, niko tayari.”
Mara, mume wa Sulee alimpigia
mke wake…
“Enheee, Sulee hebu njoo hapa Kinondoni Mkwajuni haraka sana, chukua Bajaj,” alisema mwanaume huyo.
“Kuna nini tena?”
“Nimesema njoo, utajua hapahapa.”
Sulee kwa sababu alikuwa amevaa gauni, alichofanya ni kubeba khanga moja tu, akatoka mbio na kuchukua Bajaj mpaka Mkwajuni. Alimpigia simu mumewe, akamwambia alipo. Ile anafika tu na kumwona mume wa shoga yake Monica akahisi kitu tayari kuhusu Monica mwenyewe…
“Hapana lazima Monica amefanya kitu,” alisema moyoni lakini alishindwa kumpigia kwa sababu tayari alikuwa mbele ya wanaume hao walioonesha sura za kuchukia…
“Kuna nini kwani? Eti shemu kuna nini?”
“Ingia kwanza ndani ya gari,” mume wake alimwambia akiwa ameshamfungulia mlango…
“Rafiki yako ameingia gesti ile…”alisema mume wa Monica.
“Na nani? Ameingia na mwanaume gani?”
“Hatujajua, lakini tumemwona yule Dokta Kisarawe naye akiingia,” alisema mume wa Sulee…
“Mungu wangu, ina maana Dokta Kisarawe ndiyo wa kwake siku hizi siyo?”
“Hatujathibitisha.”
“Sasa kwa nini msiende?”
“Tumeona hakuna haja ya kwenda shemu, ila tukae hapa mpaka watoke ndipo na sisi tujitokeze,” alisisitiza mume wa Monica.
“Mh! Makubwa,” alichoka kabisa Sulee. Moyoni alikuwa na mambo mawili, kwanza shoga yake kuingia kwenye mkenge huo, pili ni wivu wa dokta kutembea na Monica jambo ambalo aliwahi kulihisi lakini akakosa ushahidi wa moja kwa moja.
“Lakini mkuu je kama shemeji atatoka peke yake na Dokta Kisarawe naye peke yake itakuwaje?” alihoji mume wa Sulee hoja ambayo ni ya kweli kwani kama angeanza kutoka mmoja wao, mfano dokta wangemuingizaje kwenye tuhuma za kumfumania?
“We sikiliza, hata kama itakuwa hivyo bado ni tatizo, ishu hapa ni yeye kuja gesti, iwe na dokta iwe na mwanaume mwingine lakini hoja ni moja tu, sijapenda. Halafu ananidanganya kwamba yuko nyumbani,” alilalamika mume wa Monica.
Nusu saa ilikatika, hakukuwa na mtu yeyote aliyetoka ndani achilia mbali Dokta Kisarawe na Monica. Sulee akashauri…
“Mimi shemeji nashauri kwamba, kama inawezekana mimi niende kuingia, nikaulizie…”
“Hapana,” alikataa mume wa Sulee, akataka uendelee utaratibu uleule kwani ufafanuzi ulikuwa tayari kwamba, awe amenaswa laivu au la, ishu ni yeye kuingia katika gesti hiyo.
Dakika sitini zilionesha kwenye saa zao za kwenye simu na mkononi, walitoka watu wawili, mwanamke na mwanaume lakini wakiwa wamepishana kwa dakika kama tatu hivi. Aliyeanza ni mwanaume.
“Loo! Shemeji naona shoga yako kaamua kumkinaisha Dokta Kisarawe, lisaa limoja sasa,” alisema mume wa Monica…
“We acha tu, mi mwenyewe nashangaa, muda wote huu?”
“Ungekuwa wewe ungetumia dakika ngapi?” Sulee aliulizwa na mume wake lakini kicheko cha mume wa Monica kukalifanya swali hilo kuwa jepesi zaidi.
“Mimi sina mpango huo kwanza, sijui yeye ametolea wapi haya mawazo,” alijibu Sulee.
Mume wake akaendelea…
“Nimekuuliza kwa sababu umesema unamshangaa yeye kutumia muda mrefu hivi, ndiyo maana nikataka kujua ungekuwa wewe ungetumia muda gani?”
Kabla jibu halijapatikana, ndani ya gesti hiyo alitokea mwanaume mmoja, si Dokta Kisarawe. Alikuwa akifunga vifungo vya shati vizuri huku uso ukionekana kuwa na jasho kwa kazi ya chumbani.
“Jamani, inawezekana yule mwanaume ndiyo alikuwa na Monica chumbani?” alisema kwa mshtuko mume wa Sulee…
“Haa! Halafu namfahamu, ni jirani yangu bwana. Anaitwa baba Anode, atakuwa yeye,” alisema mume wa Monica huku akianza kufungua mlango ili atoke, tayari alikuwa amekasirika kuona kumbe anayemwibia ni jirani yake.
Kabla hajatoka, msichana mmoja naye wa nyumba ya jirani na mume wa Monica alitoka kwenye gesti hiyo hivyo kutoa picha kwamba, alikuwa na baba Anode.
“Yule msichana anaitwa Mwasiti, ina maana anatembea na baba Anode?” alihoji mume wa Monica akionekana kushangaa sana.
Tena ili kudhihirisha kwamba kweli walikuwa wote gesti, Mwasiti alikazana na kumfikia baba Anode ambapo walishikana mikono na kutembea kwa maringo kama wapo fungate.
Baada yakuona kimya hawatoki Mume wa Monica na mume wa sulee waliamuwa kuingia ndani nakuwakuta Monica na dokta wakiwa chumbani
Monica kumwona mumewe akadondoka chini
nakupoteza fahamu kwa presha aliyo kuwa nayo.
Wanasema anayefumaniwa hupoteza nguvu hata kama ni baunsa uwa mdhembe, mume wa Sulee licha ya wembamba wake lakini aliweza kumkwida Dokta Kisarawe na kumtembeza hadi lipokuwa Sulee,
Monica alikuwa hajazinduka
Kumekucha je itakuwa je!?
DOCTA SIUMWI HUKOO
Sehemu Ya 13
TULIPO ISHIA
Wanasema anayefumaniwa hupoteza nguvu hata kama ni baunsa uwa mdhembe, mume wa Sulee licha ya wembamba wake lakini aliweza kumkwida Dokta Kisarawe na kumtembeza hadi lipokuwa Sulee,
Monica alikuwa hajazinduka
SONGA NAYO…
Dokta Kisarawe akawekwa chini akae pembeni ya Monica huku kazi ya kumpepea Monica ikiendelea ili azinduke… “Katika hali kama hii shemeji halafu mwanamke aje kuniambia eti mimba ni yangu inawezekana kweli?” Mume wa Monica alimwambia Sulee…
“Kweli lakini shemeji.
Inauma sana!” Dokta Kisarawe aliinua uso na kumwangalia Sulee kwa sura inayosema…
“Hata wewe unaongea maneno kama hayo wakati mimba yako pia ni yangu?”“Unaniangalia nini, kwenda huko?” Sulee alimkandia daktari huyo kwani alijua kwa pale hakuwa na ujanja wa kumfanya chochote wala kutoboa siri.
Atoboe siri ale mkong’oto! Katika hali isiyotarajiwa, mume wa Monica alimvaa Dokta Kisarawe kwa kumpiga teke la tumbo na mangumi ya kichwani hadi naye akaanguka na kupoteza fahamu…
“Siwezi kumlegezea mtu kama huyu, ameharibu ndoa yangu,” alisema mume wa Monica huku akitaka kumwongezea kipigo lakini mume wa Sulee akazuia. Watu walianza kujaa eneo la tukio.
“Jamani kuna nini kwani?” Walihoji watu huku wengine wakiwa tayari wameokota mawe kutaka kumpiga Dokta Kisarawe.
“Ha! Jamani huyu si Dokta Kisarawe?” Mwanamke mmoja aliuliza kwa mshangao mkubwa.
“Ni yeye bwana,” mwenzake alijibu halafu akaendelea kusema…
“Halafu mi nilijua tu jamani kwamba iko siku moja dokta atafumaniwa.
Kutibu gani wagonjwa kila siku uko na wake za watu?” “Mimi mwenyewe siyo siri niliacha kwenda kwake baada ya kunitongoza kila nikifika. Wengine dokta hatujaumbwa hivyo.
Wewe kila mwanamke unadhani anaweza kukukubali?”
Mazungumzo ya wanawake hao wawili yalitoa mwanga mpya kabisa kwa akina Sulee, mume wa Monica akasema anataka kummaliza dokta kwa kumpiga risasi… “Noo…nooo, usifanye hivyo,” mume wa Sulee akamzuia.
Alipoona amezuiwa kwa tendo hilo, mume wa Monica akaomba watu watawanyike ili abaki yeye, Sulee na mume wake.
Watu walitii, wakaondoka lakini wengi walionekana kumkandia daktari huyo.
Wapo waliodai wamewahi kusikia kwamba kuna daktari anapenda ngono na wake za watu.
Wakati huo Monica alishaamka. Sasa walibaki sita tu, wakamuomba dereva wa teksi aondoke akakae mahali ili wao waingie ndani ya gari. Walimbeba Monica hadi ndani ya gari, wakamwingiza na Dokta Kisarawe.
Walikaa wote wakaenea… “Dokta,” alianza kwa kuita mume wa Monica…
“Naam.” “Ni kwa nini unatembea na mke wangu tena mpaka umempa mimba?”
Dokta Kisarawe aliangalia chini tu.
Alijua ukweli wa madai ya mwanaume huyo…
“Monica,” mumewe alimwita…
“Bee.” “Ni kwa nini uliamua kunisaliti kwa kutembea nje ya ndoa hadi kupata mimba?”
“Nisamehe mume wangu ni shetani tu.”
“Sawa, labda nikuulize kitu kingine.
Ni kwa nini uliamua kusema mimi ndiye mwenye mimba?”
Monica alibaki kimya, akaulizwa tena pia akabaki kimya.
Kidogo mume wake amchape makofi…
“Si nakuuliza wewe mbwa.” “Monica si useme tu ukweli, kama kusamehewa usamehewe, unakatakata maneno ya nini?” Alisema Sulee, Monica akakasirika sana na kusema…
“Jamani, haya yote sababu kubwa ni Sulee.” “Ha! We Monica mwogope Mungu, sababu kubwa ni mimi kivipi?
“We si ndiyo ulinipeleka!”
“Halafu nikakutongozea kwa dokta?”
“Unajua mwenyewe.” “Sikia Monica, sidhani kama mimi ni mjinga kiasi hicho.
Wewe mzigo wote huu ni wako, hakuna ubishi.
Unapotaka kumsukumia mwenzako ni kutapatapa tu.”
“Mwambie shemeji, nahisi kama anataka tufe wote.” “Siyo nataka tufe wote, kwani na wewe si una mimba ya Dokta Kisarawe.”
Mambo yaliharibika! Monica alisema kauli nzito na mbaya, ni kama alichochea kuni kwenye moto wa kuni ulioanza kuzimika. “Unaona Sulee…unaona? Sikukwambia mimi kwamba nahisi hata wewe hiyo mimba ni ya Dokta Kisarawe?” Mume wake alikuja juu.
“Jamani maneno ya Monica si ya kuyaunga mkono, amechanganyakiwa huyu mume wangu,” alijitetea Sulee, msala ulishamwangukia.
Mume wake alimvaa mume wa Monica na kumnyang’anya bastola, akamwelekezea mke wake, lakini mume wa Monica akamuwahi na kumpiga mkono, ikaanguka chini.
Kuona hivyo, mume wa Sulee alitoka ndani ya gari, akaenda kuokota jiwe kubwa akawa anakwenda nalo kwenye gari ili ampige nalo mke wake.
Yeye hakuonekana kuwa na haja na Dokta Kisarawe…
“Naua mimi, naua nasema,” alilirusha jiwe hilo likatua kwenye mlango jambo ambalo mle ndani hakuna aliyetegemea… “Mume wangu jamani siyo kweli,” alisema Sulee akianza kulia.
Tayari gari sehemu ya mlango ilikuwa nyang’anyang’a kwa lile jiwe na mwenye gari alikwenda mbali kidogo kwa vile..
Itakuwa aje endelea Kuwa na
DOCTA SIUMWI HUKOO
Sehemu Ya 14
TULIPO ISHIA
Tayari gari sehemu ya mlango ilikuwa nyang’anyang’a kwa lile jiwe na mwenye gari alikwenda mbali kidogo kwa vile..
SONGA NAYO
kwa vile mahali aliposimamisha gari hakukuwa na njia nyingine ya kutokea zaidi ya ile aliyoelekea yeye kwa miguu… “Mtasha mbona umekuwa mstari wa mbele sana kunizuia mimi nisifafanye uhalifu, inakuwaje wewe unashindwa kujizuia?”
Mume wa Monica alisema akimwita mwenzake huyo kwa jina lake la utani.
Mara, mwenye gari alitokea
Alishtuka kuona gari lake limeharibika sehemu ya mlango huku timbwili likiendelea…
“Jamani vipi tena?” aliuliza kwa mshangao mkubwa.
Majibu aliyoyapata yalimfanya ajutie lakini akaahidiwa kulipwa fedha ili kwenda kutengeneza gari hilo japokuwa alikubali lakini kwa shingo upande.
Baada ya utulivu kurejea lakini huku wanaume wote wakiwa na hasira ya wivu, waliamua kwenda kituo cha polisi ambapo Dokta Kisarawe aliwekwa ndani ili kupisha uchunguzi wa madai ya wanaume hao kwamba ametembea na wake zao na kuwapa ujauzito.
***
Baada ya kuandikisha maelezo, walirudi nyumbani.
Wote walifikia nyumbani kwa Mtasha, mume wa Sulee ambapo kikao kilikaa na misimamo ilitolewa…
“Mimi bwana kwa upande wangu nasema wazi kwamba sina haja ya kuwa na mke kama huyu,” alisema mume wa Monica huku akimwangalia mkewe kwa macho yaliyojaa uchungu…
“Hata mimi, Sulee nakuandikia talaka zako tatu sasa hivi,” alikuja juu Mtasha na kutaka kumpiga tena mke wake kwa hasira…
“Sasa Mtasha si umeshasema unamwandikia talaka si ufanye hivyo, achana na kumpiga bwana,” alisema mume wa Monica.
Wanawake hao wawili waliangua kilio huku kila mmoja akimlaumu mwenzake kwamba alimsababishia lakini lawama za Monica kwa Sulee zilikuwa za kweli kwani yeye alipelekwa na shoga yake huyo ambaye alikuwa akiijua tabia chafu ya Dokta Kisarawe…
“Bila wewe Sulee mimi yasingenikuta haya.
Ulijua Dokta Kisarawe ni mwingi wa habari ni kwa nini hukuniambia maana hata wewe ulishapitiwa…
“Halafu nilimwambia dokta. Alikuwa akipenda kunishikashika sehemu zisizohusika na matatatizo yangu, nikamwambia dokta mimi siumwi huko yeye hakusikia,” alilalama sana Monica…
“Monica ni shetani, hata mimi nilimwambia dokta mimi siumwi huko wakati akipeleka mikono yake kwenye matiti yangu lakini hakutaka kunisikia. Tusameheni jamani.”
“Hakuna msamaha hapa… Ala!” wanaume wote walijikuta wakijibu kwa pamoja bila kutaarifiana…
“Kwanza ni muhimu kwenda kupima afya zetu maana kama mna mimba ina maana mlikuwa hamtumii kinga,” alisema mume wa Monica…
“Huko kuchepuka kwenu ndiyo faida yake mnaiona sasa,” alisema mume wa Sulee huku akikohoa.
Hapo alikuwa akisaka karatasi ya kuandikia talaka mara moja.
***
Siku ya pili, Mtasha, yaani mume wa Sulee na mume wa Monica walikwenda kupima virusi vya Ukimwi.
Walikutana na wake zao huko wakiwa na shangazi wa Sulee ambaye aliomba kuzungumza na Mtasha kabla ya kuingia kwa dokta.
Kwa heshima Mtasha alikubali na akatoka pembeni…
“Baba najua unaniheshimu sana…”
“Kweli shangazi…”
“Mwenzio kanijia na talaka analia.
Lakini aliponisimulia kisa hata mimi nilikuunga mkono mwanangu…”
“Nashukuru sana kusikia hivyo shangazi…”
“Enhee, lakini sasa nina ombi moja tu kwako…”
“Lipi hilo shangazi?”
“Msamehe Sulee.”
Mtasha palepale alijishika kichwa na kujikuna huku akitumbua macho, akakumbuka mema aliyowahi kuyafanya na shangazi huyo kwake maana ana uwezo si wa kitoto.
***
Kuna mwaka Mtasha alipata kesi mbaya sana, uchumi wake ukayumba sana akajikuta hana hata pesa ya kula.
Shangazi huyo wa mkewe akawa ndiye mfadhili wake kwani alikuwa akimpa pesa ya kula na pia alimsimamia kwenye kesi hiyo kwa kumuwekea wakili na akashinda.
Baada ya kushinda alimpatia mtaji akaendelea na miradi yake iliyosimama…
Wakati wa maongezi hayo, shangazi mtu hakumkumbusha kitu chochote Mtasha. Alimwacha ajipime mwenyewe tu…
“Da!
Shangazi kusema ukweli umenipa wakati mgumu sana,” alisema mume wa Sulee…
“Kwa nini mwanangu? Kusameheana kumewekwa na Mungu na ukimsamehe mwenzako hata Mungu atapenda na kukubariki.”
“Ni kweli, lakini shangazi unalionaje hili la ujauzito?”
“Hilo unaweza kuliacha mikononi mwangu nikashughulika nalo.”
“Utafanyaje shangazi? Maana mimi kusema kweli siwezi kuishi na mke mwenye ujauzito wa mwanaume mwingine.”
“Ndiyo maana nimesema niachie mimi kuhusu hilo.”
“Shangazi maamuzi yako ni mema na nakuheshimu wewe sana, je vipi kuhusu kupima Virusi vya Ukimwi?”
Muda wote huo, mume wa Monica alipokuwa amekaa alikuwa akimtumbulia macho mume wa Sulee kama anayemwambia asithubutu kukubali hata siku moja maneno ya shangazi wa Sulee…
“Ndiyo maana tupo hapa! Wewe unadhani Sulee ana virusi?” alisema shangazi mtu huyo…
“Siwezi kusema anavyo au hana, ila kupima ni muhimu shangazi.”
“Kwa hiyo kama atakuwa salama utakuwa umepokea ombi langu siyo?
“Naamini hivyo.”
“Basi turejee kusubiri zoezi likamilike.”
Walirudi kwenye fomu.
Mume wa Monica akamuuliza mume wa Sulee mazungumzo yao yalihusu nini…
“Shangazi anataka nimsamehe Sulee.”
“Uko tayari kwa hilo?”
Je sulle atasamehewa na vipi kuhusu kupima virusi vya ukimwi kutatokea nini,, Usisite kufuatilia SIMULIZI HII hapa hapa….
DOCTA SIUMWI HUKOO
Sehemu Ya 15
TULIPOISHIA
Mume wa Monica akamuuliza mume wa Sulee mazungumzo yao yalihusu nini…
“Shangazi anataka nimsamehe Sulee.”
“Uko tayari kwa hilo?”
ENDELEA
“Mh! Nimemwambia kama atakuwa hajaathirika naweza.”
“We unataka kumrudia Sulee?”
“Unajua nini mshkaji? Huyu shangazi amenisaidia sana katika maisha yangu kuliko mtu mwingine yeyote…”
“Kwa hiyo?”
“Kwa hiyo naweza kuangalia upya cha kufanya.”
“Mh! Nadhani sijakuelewa.”
“Kivipi?”
“Yaani pamoja na mambo yoote waliyotufanyia hawa Malaya wewe unakubali tuwasamehe, Mungu aniepushie hilo mawazoni mwangu,” alisema mume wa Monica na kumfanya mume wa Sulee kuwa na mawazo nusunusu tofauti na alivyoongea na shangazi mtu.
***
Majibu ya vipimo yalitoka, waliitwa mtu mmoja mmoja lakini huku wakiruhusiwa kwenda na watu wao kama wapo walioongozana nao.
Sulee alikwenda na shangazi yake huku akidondosha machozi kwa kuwa muda wa zamu yake ulifika. Alikuwa akitetemeka sana.
Monica, mumewe na mume wa Sulee walibaki nje lakini mume wa Sulee aliuliza kama itakuwa busara na yeye aende kwa vile yanaweza kutoka majibu ambayo yamechakachuliwa na shangazi huyo kwa vile alitaka ndoa ya Sulee iendelee kudumu.
“Noo, achana nao bwana. Wewe mbona hueleweki? Kwanza kama wao walitaka uwazi na ukweli kwa nini wasikwambie muingie wote?” alihoji mume wa Monica mpaka mwenyewe akaona ni kweli, akabaki kwenye fomu.
Baada ya dakika kama kumi, kilio kikubwa kikasikika kutokea chumba cha daktari…
“Uuuwi, Mungu wee nisaidie. Nitakwenda wapi mimi?” ilikuwa sauti ya Sulee…
“Ngoma tayari hiyo mwanangu, hakuna kurudiana wala kwenda mbele,” alisema mume wa Monica huku akichekelea. Alijua mpango wa shangazi mtu kuirejesha ndoa hiyo haupo tena.
Kwa upande wake, Monica alionekana kuwa mtu mwenye mchecheto zaidi kwani kila wakati alikuwa akisimama na kukaa. Aliamini kama Sulee ‘aliungua’ hata yeye yumo ndani ya ‘moto’ huo.
“Mmh! Sasa kama Sulee analia amegundulika kuwa na virusi je mimi? Maana mwanaume aliyemwambukiza yeye ndiyo huyohuyo ametembea na mimi,” alisema moyoni Monica huku akimtupia macho ya wizi mumewe.
“Monicaaa…” aliita jina muuguzi kabla hajamalizia, Monica mwenyewe alisimama haraka sana. Mara Sulee na shangazi yake wakatokea huku Sulee akichuruzika machozi.
“Pole Sulee,” alisema Monica lakini hakuitikiwa hata shangazi yake hakusema kitu.
“Baba tunaondoka, uamuzi wako ubaki kuwa palepale,” alisema shangazi mtu akimwambia mume wa Sulee. Alipita kwenye korido kwa aibu kubwa akiwa amejiinamia mpaka kwenye gari lake akifuatwa na Sulee kwa nyuma.
****
“Eee, thanks God. Asante Mungu, wewe ndiye muweza wa yote. Oooh! Si kwa nguvu zangu bwana bali kwa neema tu. Mimi Monica mimi kwamba sina virusi?” sauti ya Monica ilisikika kutokea kwenye chumba cha daktari.
Ilifika mahali akapiga na vigeregere kufurahia majibu ya vipimo vyake.
Mumewe alianza kuhisi ganzi akiwaza kwamba endapo mkewe yuko fiti halafu yeye akakutwa na ngoma itakuwaje?
“Itakuwa poa tu kwani maisha bado yataendelea,” alisema moyoni mume wa Monica huku akiangalia chini kwa mawazo.
“Mkubwa unasikia huko ndani? Shemeji yuko ngangari,” mume wa Sulee alisema.
“Eee, ndiyo sherehe inaendelea ndani.”
Mara Monica alitokea…
“My dear niko fiti, sina virusi wala vijidudu,” alisema Monica huku akirukaruka kwenye miguu ya mumewe…
“Kwa hiyo?” mumewe alimuuliza…
“Heee! Hujapenda?”
“Hata nikipenda, kwani kuna nini? Si umekutwa upo fiti tu.”
“Hunisamehi?”
“Haitatokea Monica.”
Monica aliangua kilio mbele ya watu huku mumewe naye akiitwa kuchukua majibu yake. Kumbe Sulee na shangazi yake hawakwenda mbali, walikuwa kwenye gari wakisubiri matokeo ya mume wa Sulee, mume wa Monica na Monica mwenyewe.
“Mshkaji mimi nataka twende wote,” alisema mume wa Monica baada ya kuitwa jina lake na muuguzi mmoja.
Walizama wote mpaka kwa dokta na wakasema wote wamefika kwa kupima…
“Kwa hiyo majibu mnasikiliziana?” alihoji dokta.
“Ndiyo.”
Alianza kwa kuwashauri huku akiweka majibu ya wote sambamba, karatasi ya mume wa Monica ikianza juu.
“Sasa kwa kuwa mpo wote na wote mmepima na majibu yote yapo hapa baada ya ushauri niliowapa, wote mpo vizuri hakuna mwenye virusi vya Ukimwi,” alisema dokta. Walisimama, wakakumbatiana. Wakampa mkono dokta na kutoka nje huku wakicheka kwa furaha…
“Mungu anajua cha kufanya mshkaji, wale wanawake siyo kabisa,” alisema mume wa Monica…
“Lakini kama wewe huna na shemeji hana si mnaweza kurudiana?” alihoji mume wa Sulee.
“Na ile mimba?”
“Si utailea tu.”
“Mimi nilee mimba ya Dokta Kisarawe?”
“Kwani mshkaji kuna nini?”
“Haitatokea. Mara kumi angenibambika nisijue kuliko kujua.”
***
Sulee na Monica walikumbatiana kwenye gari huku wote wakilia. Kilio kikubwa kilikuwa kwa Sulee kwani alikutwa ameungua wakati mwenzake yupo fiti.
“Mwanangu nyie naona mambo mazuri maana naona vicheko,” shangazi wa Sulee alimuuliza mumewe…
“Mungu hamtupi mja wake shangazi. Mungu mkubwa bwana,” alisema mume wa Monica huku wakiondoka zao kwa mbwembwe wakicheka na kupigiana mikono na wakitembea kwa ujasiri wa hali ya juu.
Wake zao walikuwa wakiwatazama kwa macho yanayoendelea kujaa machozi wasijue la kufanya.
Ghafla waliangua vilio mpaka watu wakajaa lakini hakukuwa na jinsi, waume zao walishaamua. Walijuta na kujuta kwa usaliti wakati waume zao walikuwa wakihangaika kusaka maisha
na siyo uhuni kama walio
kuwa wakifanya wakezao.
“shangazi mimi sijuwi kwa nini
jamani Yani nimetembea na Monica kwa mwanaume mmoja
lakini mwenza hana shangazi”
“pole Sulee Nimipango ya Mungu
wala usijari”
“Monica ladhima nijari
Moyo wangu una umia sana najuta na juta”
lakini shangazi yake sulee
hakuwa na wasiwasi kabisa
kuhusu suara hilo
“Sawa Sulee mimi narudi
kijijini nikaanze maisha mapya”
alisema Monica huku
akitokwa na Machozi sana”
“sikiliza Monica baki nasi hapa hapa mjini sawa utakaa na sisi”
“kweli shangazi oooh Asante Mungu wangu”
****