Kufa – Chukua Hatua Mapema
1:
MIGOGORO Ya Mara kwa Mara.
Ni Jambo la kawaida Kupishana Mwanaume na Mwanamke wakiwa kwenye MAHUSIANO.
Kwa sababu Ya “Gender Difference”……!
Lakini Kuna Kiwango Cha Migogoro ikianza unajua kabisa hapa Hamuendi MBALI.
Migogoro isiyoisha ( Endless Conflict)…!
Migogoro inayokuja kwa kujirudia rudia ( Repeating Conflict).
Kuna kitu kinaitwa “CONFLICT SPINNING”
“Ni Hali ya kuwa kwenye Mzunguko wa Migogoro”.
MGOGORO huu ukiisha unaibuka Mwingine.
Hii ni Kusema……..!
“Mnatumia Muda Mwingi katika KUTATUA Migogoro Zaidi Ya Muda wa Kufurahia
PENZI lenu”.
2: MANENO Mnayotamkiana Mkiwa kwenye MGOGORO.
Umewahi kusikia USEMI unaosema…..!
“Sikiliza Sana MANENO anayosema mtu wakati akiwa kwenye HASIRA”.
Kwanini usikilize…?
Kwa sababu ili Mtu aongee lazima pawepo na JAMBO linalomsukuma Kusema.
Mara nyingi maneno anayosema Yanakuwa Ya kweli KABISA.
Maneno KAMA……..!
( Kama Vipi TUACHANE, Najuta kuwa na WEWE).
Ukisikia Maneno haya kutoka kwa MPENZI wako, ujue Hamuendi MBALI.
Yaani anaona kuwa na wewe…… Amepata Hasara kubwa Sana….!
03: MAHUSIANO KUEGEMEA UPANDE MMOJA.
Mahusiano ili Yastawi Yanahitaji (MUINGILIANO (Intersection) Ya watu wawili.
Ila ukiona wewe TU ndio umeanza KUYAPAMBANIA ili yabakie HAI.
HALAFU…..!
Mwenzako hata Hajigusi Wala kutaka kuyaimarisha.
Wewe TU ndio wa KUMPIGIA simu KUMJULIA Hali.
Wewe TU ndio wa Kumtafuta bila hivyo mnakaa KIMYA.
MAWASILIANO ndio MAHUSIANO.
Mawasiliano ndio kuni za mahusiano,
Bila mawasiliano PENZI linakufa.
Wewe TU ndio wa Kuomba MSAMAHA hata kwenye makosa Yake
Huu ni UTHIBITISHO tosha kwamba na wewe Kuna SIKU Utachoka tu ( exhausted).
Na wewe Ukichoka utashangaa penzi linapoa na Kufa kabisa ( fatigue).
Kuna kinachotakiwa KUFA, Kuna kinachotakiwa KUPONA.
Usiue kinachotakiwa kupona, na ukaacha kinachotakiwa KUFA.
Kuna ishara Ukiziona ni taarifa kwamba unatakiwa uchukue hatua za haraka Sana
otherwise UTAJUTA BADAE.