Mambo 5 Ambayo Utajifunza Baada Ya
Mahusiano Kuvunjika
Kila mtu huwa anajifunza kitu tofauti katika
mazingira tofauti.Ikitokea mahusiano kuvunjika wapo hujifunza kuacha kuamini
jinsia tofauti maisha yao yote , vilevile wapo huamua kujifunza kujichukia wao
wenyewe, vilevile wapo hujifunza kwenye makosa yao lakini vilevile wapo ambao
hawaamini kama wanakosea popote.
Kwa vyovyote itakavyokuwa mahusiano kuvunjika huacha athari hasi au chanya,
mahusiano kuvunjika yanaweza kukusaidia au kukuharibia.
tuangalie mambo 5 ambayo unaweza kujifunza baada ya mahusiano kuvunjika
MAMBO 5 AMBAYO UTAJIFUNZA BAADA YA MAHUSIANO KUVUNJIKA
Mambo hayo 5 kwanzia namba moja mpaka namba tano.
1. MAUMIVU YA MAPENZI NA AIBU YA MAHUSIANO KUVUNJIKA
Baada ya mahusiano kuvunjika kila mtu huwa na njia zake za kukabiliana na
maumivu ya mapenzi,wapo hujifunza kuboresha tabia zao ili waweze kufurahia
mapenzi siku za baadaye,wengine hujifunza kuwa na mioyo migumu sana na kuacha
kuruhusu mtu yeyote kuingia maishani mwao.
Aibu na fedheha ya kuachwa ghafla na mwenza husababisha tabia zifuatazo kwa
watu
a.Kumshambulia kwa maneno makali sana Ex wake ,pamoja na kumdhalilisha sana kwa
kauli kama “mtu mwenyewe alikuwa choka mbaya,alikuwa lofa masikini wa
kutupwa,mtu mwenyewe hana sura wala shape,mtu mwenyewe hakuwa na hadhi ya kuwa
na mimi basi tu nilimsitiri asidhalilike”
watu wenye tabia ya ubabe, ukali kupitiliza, kiburi, majivuno, jeuri na dharau
pale ambapo wameachwa huongea maneno hayo kwa sababu wao hujiona ndiyo
wanatakiwa kuacha wenzao na maumivu makali sana miaka yote,wao kuachwa huona
aibu na fedheha kupitiliza.
b.Kujishambulia na kujidhalilisha yeye mwenyewe kwa maneno makali sana baada ya
kuachana na mwenza,kauli kama vile “Mimi nipo na mkosi,mimi nipo na
laana,mimi nipo na nuksi,mimi sitakuja kupendwa ,hivi mimi ndiyo wa kupendwa na
yule alinionea huruma tu.”
c.Kujiapiza kutojihusisha na mapenzi maisha yao yote.atasema “sitakuja
kuamini mtu yeyote hapa ulimwenguni maisha yangu yote – wanaume/wanawake wote
ni mbwa”
d.Kujiepusha na mapenzi moja kwa moja kwa njia mbadala kama vile ulevi
kupindukia, uvutaji bangi, kutumia dawa za kulevya,kujichua
(masterbation),kufanya starehe sana,kutumia fedha nyingi sana ghafla,kufanya
kazi muda wote,kula sana,kulala sana,kucheza video game, kuangalia video za
ngono (pornography),wengine huamua kubadilisha wanawake au wanaume kila siku
ili kuzuia kuja kupenda mtu yeyote mpaka mwisho wa maisha yao.
2. KUJITOA MHANGA KWA MWENZA WAKO SIYO GUARANTEE YA KUPENDWA WALA KUDUMU NAYE
Baada ya mahusiano kuvunjika ghafla ndipo utagundua kwamba kuhatarisha maisha
yako,kujitesa,kujinyima chakula,kugombana na wazazi wako pamoja na ndugu zako,
kumsomesha mwenza wako, kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumnunulia
zawadi za gharama kubwa sana,kumuuguza,kuwasomesha watoto wa mwenza wako,
kuvumilia vipigo, matusi, unyanyasaji, udhalilishaji kutoka kwa mwenza wako,kuacha
kazi kwa ajili ya kumfurahisha mwenza wako siyo GUARANTEE ya kupendwa wala
kudumu naye.
Unaweza kujitoa mhanga kumfariji, kumlinda, kumliwaza, kumtetea, kubadilisha
maisha ya mwenza wako kutoka kudhalilika mtaani mpaka kuheshimiwa mtaani kisha
baada ya mwenza wako kufanikiwa anakuacha ghafla anakwenda kwa mtu mwingine
bila kujali jasho lako na maumivu ambayo umepitia ili kumtetea pale ambapo
alikuwa anapigwa vita na kila mtu.
Baada ya mahusiano kuvunjika ndiyo utagundua kwamba kujiwekea kauli kama
“Niliwafanyia 1,2,3 wao pia wanatakiwa kunifanyia 1,2,3 nikiwa katika hali
kama ya kwao” siyo utaratibu halisi katika maisha.
Siyo kila mtu anaweza kukupa kipaumbele katika maisha yake kama ambavyo wewe
unaweza kumpa kipaumbele maishani mwako.
Maisha hayaendeshwi kwa tit for tat kwa kusema “Nimefanya 1,2,3 na wewe
fanya 1,2,3 kama nilivyofanya kwako.
Kwenye Maisha halisi kila mtu yupo na utaratibu wake ambao kwake anaona ni
sahihi.
Baada ya mahusiano kuvunjika ndipo utagundua kwamba kila mtu yupo hapa ulimwenguni
kuandika historia yake na kila mtu atafanya makosa yake kivyake vyake na kila
mtu atakuwa na njia zake za kukabiliana na matatizo yake.
Kila mtu atakuwa na njia zake za kuishi au kujifunza namna ya kuishi,kila mtu
anawajibika kwa vitendo vyake na maamuzi yake.
Kila mtu yupo na uhuru wa kuchagua nini aamini na nini asiamini.
Unaweza kuwa na nia njema kwa mwenza wako lakini kwa sababu mwenza wako yupo na
kumbukumbu mbaya juu ya njia ambayo unataka kuitumia lazima ataipinga hata kama
kwako utaona ni njia sahihi.
3. KUACHA KUMTEGEMEA MWENZA WAKO KAMA CHANZO CHA FURAHA YAKO
Baada ya mahusiano kuvunjika ndipo utagundua kwamba mwenza wako hatakiwi kuwa
chanzo cha furaha yako na endapo mwenza wako atakuwa chanzo pekee cha furaha
yako utakuwa unalia kila siku.
Ukiwa hauna furaha utatamani kampani ya mwenza wako lakini yeye atakuona kero,atakuona
mzigo,atakuona hauna pa kwenda.
Mwenza wako hawezi kukuthamini kama anakuona hauna furaha muda wote,ili mwenza
wako awe na hofu ya kukupoteza anatakiwa akuone upo na furaha sana bila uwepo
wake hapo atagundua kwamba endapo ataondoka hakuna pengo lolote ataliacha
kwako.
Mtu yeyote unakuwa na hofu ya kumpoteza huwa ni yule ambaye unajua ukiondoka tu
pengo lako linazibwa haraka na kumbukumbu zako zote anazisahau papohapo.
Kama mwenza wako anajua hauwezi kuwa na furaha maishani mwako endapo atakuacha
utafanya mwenza wako awe na kiburi, majivuno, jeuri na dharau kwako kwa sababu
atakuwa anajua hauwezi kumuacha wala hauwezi kuishi bila yeye.
Lakini akiona upo na furaha sana pale ambapo anaondoka hofu ya kukuacha inazidi
kuongezeka kwake siyo kwako.
4. HAUWEZI KUBADILISHA TABIA YA MWENZA WAKO IKIWA YEYE HAYUPO TAYARI KUBADILIKA
Haijalishi utakuwa ûnampenda sana mwenza wako lakini kitendo cha kutaka
kumbadilisha tabia huwa ni kumkosea heshima.
je wewe unaweza kuruhusu mtu yeyote aje kukupangia namna ya kuendesha maisha
yako?
utagundua kwamba mtu ambaye anataka kukubadilisha tabia huwa anageuka kero.
Binadamu kwa asili ni mbinafsi hivyo unapotaka abadilishe tabia anahisi ni kwa
faida yako siyo yake.
Hakuna mtu ambaye anaweza kukubali akufurahishe wewe wakati yeye hana furaha
labda kama atakuwa na tatizo.
Badala ya kutaka kumbadilisha tabia mwenza wako jiulize nini kimekuvutia kwake
?
mwanaume anavutiwa na Mwanamke mwenye tabia nzuri je wewe mwanaume unawezaje
kuvutiwa kimapenzi na Mwanamke ambaye hana tabia njema ? ukiona unavutiwa
kimapenzi na Mwanamke ambaye hana tabia njema ujue hauna sifa za mwanaume
Rijali.
mwanaume Rijali huwa ni kiongozi mkuu wa familia kwa maana anatoa maagizo na
sheria kisha Mwanamke anatii na endapo atagomea maagizo anaondoka.
Kwa upande wa Mwanamke sifa ya mwanaume ni uongozi hivyo kama mwanaume hawezi
kukuongoza je umevutiwa na nini kwake ? ukiona unavutiwa kimapenzi na mwanaume
ambaye hakutaki ujue hauna sifa za Mwanamke bali upo na hulka ya kiume.
Mwanamke mwenye hulka ya kiume huwa anataka kumpangia sheria mwanaume,huwa
anataka kumtawala mwanaume,huwa anataka kubeba majukumu ya mwanaume.Ukiona
unataka kumbadilisha tabia mwanaume ujue hauna role model mzuri kwanzia baba
yako na kaka zako hakuna mwenye sifa za kiume bali huenda baba au kaka zako
walikuwa na tabia za ubabe, ukatili, udikteta, udhalilishaji,hasira kupitiliza
au walikuwa ni wanaume legelege ambao hawana uwezo wa kujiongoza.
Ukiona unamrekebisha mwanaume wako tabia ujue huyo mwanaume wako hajielewi wala
hajui wajibu wake na vilevile wewe kama Mwanamke haujui mipaka yako ndiyo maana
umegeuka mama mzazi kwa mwenza wako.
mwanaume simama sehemu yako vilevile Mwanamke simama sehemu yako hauwezi
kuumizwa na mapenzi,ikiwa wewe mwanaume umeacha uanaume wako utasumbuliwa na
mapenzi, vilevile Mwanamke ukiacha hulka yako ya kike na kuanza kuwa mwanaume
ndani ya mwili wa Mwanamke utaona mwanaume anakuwa jeuri.
5. KUJIWEKEA MIPAKA HUSAIDIA KUBORESHA MAHUSIANO
Mwanaume ndiyo kiongozi katika familia,ikiwa mwanaume hawezi kumuonya
mwanamke,hawezi kumpangia sheria,mwanaume hawezi kumuongoza mwanamke,mwanaume
hawezi kumpa maagizo Mwanamke ujue kwamba huyo mwanaume hajui majukumu yake na
vilevile Mwanamke hajui majukumu yake.
kama haujaweka mipaka katika mahusiano yako utaona mwenza wako anakula
chochote,anavaa nguo yoyote,anakwenda kutembea mahali popote,anatumia fedha
kiasi chochote bila kujali athari za kufanya hivyo.
mwenza wako akiona hauna mipaka ataanza kwa kuonyesha dharau,atakuwa
jeuri,atakufokea, kukutukana, kukudhalilisha, kukujibu vibaya, kutishia
muachane,, kukugombeza, kukutoa dosari za muonekano mara kwa mara atafanya haya
kwa sababu anajua hauwezi kumuacha wala hauwezi kuishi bila yeye.
mwanaume ndiyo anaonyesha njia ya mahusiano kupita siyo Mwanamke,ikiwa mwanaume
hajielewi hapo Mwanamke atashika usukani lakini ugomvi na migogoro itaibuka
mara kwa mara kwa sababu mwanaume huwa hakubali kuwa chini ya Mwanamke.
Mwanamke anapotaka kuwa kichwa huwa ni ishara ya dharau kwa mwanaume wake kwa
sababu anakuwa anajiona mzuri sana,anajiona mwenye akili sana,anajiona mwerevu
sana.
jambo la kuzingatia ni kwamba ikiwa mwanaume hawezi kumuongoza mwanamke kwenye
njia sahihi Mwanamke atalazimika kusimama ngangari,atakuwa mbabe,atakuwa na
misimamo mikali sana,atakuwa hataki kuambiwa makosa,atakuwa haambiliki,
hashauriki, anakuwa na hasira kupitiliza hapo mahusiano kuvunjika ni rahisi.
Mwanamke akiwa mbabe anakuwa maalumu kwa ajili ya waume za watu pamoja na
player ambao wanampa ujauzito na kumtelekeza.
mwanaume akiwa mstaarabu sana kuliko Mwanamke lazima ugomvi na migogoro itazidi
kuongezeka kwa sababu sifa za upole, huruma, kujali, kunyenyekea, kusamehe
makosa, uvumilivu ni sifa za wife material sio sifa za mwanaume.
mwanaume Rijali sifa zake ni kiongozi mkuu wa familia,anatoa maagizo,anatoa
onyo,anahakikisha usalama wa familia,anahakikisha chakula,nguo, matibabu na
pesa za matumizi madogo madogo zinapatikana kwa wakati.
kisha tabia njema ya Mwanamke inalinda amani ya nyumba.
Ikiwa Mwanamke hana tabia njema basi ujue mwanaume yupo na tatizo.Ukiona
mwanaume hajielewi vilevile Mwanamke hawezi kuishi kwa amani, utulivu na furaha
kwa sababu furaha ya Mwanamke ipo kwenye uimara wa mwanaume.