Wanawake wengi wanajulikana kwa msingi wa maamuzi yao ya ndoa juu ya mambo
ambayo hayatadumu maishani. Haya makosa wameyafanya wengi wao kuingia kwenye
ndoa zisizo sahihi na kugeuka kuwa watumwa wa maisha ya ndoa. Tunahitaji
kutambua na kukabiliana nayo:
1) UREFU:
Ndoto ya kila msichana leo hii duniani ni kuolewa na mvulana mrefu, mweusi
mwenye sauti ya baritone, nashangaa walipata wapi wazo la kuwa wavulana warefu
ni bora zaidi kuliko wengine kwenye ndoa. Halo Wasichana, mtu mrefu anaweza
kukupa shida ndefu; urefu sio kitu muhimu lakini cha mhimu mtu awe na kina cha
utu na ubinadamu katika kumcha Mungu na tabia tabianzuri.
2) MISULI:
Wavulana wenye sura ya misuli na miili mikubwa maarufu kama vidali pia hawa nao
wana bahati kwenye ulimwengu wa ndoa, wanaonekana kuwa wachumba wazuri, na
wasichana husema wanaonekana wanaume. wanaonekana kama wanaume halisi. Poleni
sana Wasichana, misuli haifanyi mwanaume awe halisi, na mwenye uhusika na uwezo
wa kubeba majukumu kama mume. kwasabau Mvulana akiwa na misuli bila kuwa na
tabia njema atatumia misuli yake kukabiliana na wewe na kila siku badala
kukulisha chakula kizuri uzidi kunawili atakulisha kipigo mwisho atabaki kama
mbwa koko uliyekosa mfugaji na kuharibu uzuri wako.
3) NYUMBA NZURI:
Mvulana mwenye nyumba nzuri basi mvulana huyu ni ndoto ya kila msichana.
Wasichana wengi watatupa shida sana upeo wao mfupi ni kuwa na mwanaume
aliyejenga nyumba yenye ukubwa wa ikulu ya Mfalme; yenye Seti nzuri za
Kiitaliano, jiko la umeme, friji lenye vinywaji vingi, ukumbi wa michezo wa
nyumbani, jokofu, jiko la gesi, Plasma TV, kitanda 6 kwa 6, Jikoni, meza ya
dining, mashine ya kufuria, washer wa sahani, n.k. kwa wasichana wenye mawazo
haya Poleni sana, nyumba iliyowekwa vizuri ni nzuri kweli lakini kuna muda
nyumba hii hubadirika na kuwa shida iliyopambwa vizuri ikiwa mvulana sio mtu
mwenye tabia njema na mcha mungu huko adabu naa busara, ataifanya nyumba iwe
kama uwanja wa gereza kwenye maisha yako.
4) AKAUNTI YA BANK:
Wasichana wanapenda kuwa na mvulana aliye na utajiri kwa kumuangalia akiwa na
simu nzuri na account za benki. wasichana wanaamini kuwa wataishi maisha ya
furaha kuolewa na mvulana mwenye pesa hasa pale wakati wanapogundua kuwa
mvulana huyo ni tajiri sana. wasichana Hawataki kujua pesa na utajiri huyu
bwana unavitoa wap hata hawataki kujua huyo jamaa anafanya kazi gani.
Kinachowahusu wasichana ni pesa zinazopatikana kwa wakati huo ni kutumia tu.
kuna Wasichana wengi waliishia kujikuta wameingia kwenye maisha ya aina hii
lakini wakageuka kuwa watumwa wa ndoa zao kuna wakati pesa hii hugeuka udhaifu
kwako na mwanaume akakufanya atakavyo hata kuleta mwanamke mwingine chumbani
kwako, usiweke ndoa yako iwe kwenye CHOYO, ndoa yako itageuka kuwa nyekundu
kama bahari ya damu.
5) MAHALI PA KAZI:
Baadhi ya wasichana wetu wana mazoea ya kufanya maamuzi ya ndoa kulingana na
mahali ambapo mvulana anafanya kazi. Huthubutu kuwatamani kuhusu ndoa hasa
ikiwa wewe ni Mwalimu au mtumishi wa serikali. Huwezi kuwaksa wadada wenye
ndoto za kuolewa na wafanya kazi za serikali lazima wajipendekeze lakin
ukifanya kazi ndoto hutawaona hao, au biashara ya mtu ndogo. usiombe Wasichana
wagundue kuwa, mvulana anafanya kazi ACCESS BANK haimaanishi kuwa mwanaume wa
namna hiyo atakupa upendo wa moyo wake au utulivu wa akili. Mvulana anayefanya
kazi SHELL anaweza kufanya maisha yako yakawaka moto kama SHELL iliyolipuka
milele, wewe sio wa KWANZA katika maisha ya kijana anayefanya kazi BANK kuna
wenzio 30 walipotea njia kama wewe leo na upeo wako mfupi, kijana anayefanya
kazi BANK hawezi kukuhakikishia maisha yako ya baadaye akiwa anamaanisha toka
moyoni. Anaweza kuwa anafanya kazi NESTLE lakini asiwe MTULIVU nyumbani, Kwa
hiyo ndoa haihusu anafanya kazi wapi bali ni nani anayemaanisha kutoka moyoni
kwenye ndoa yake kumbuka kuna anayefanya kazi inayobarikiwa na mikono ya mungu
na yule anayefanya kazi kwa kushirikiana na shetani.
6) UPENDO:
Mwanadada mmoja alisema, Mvulana huyu anamvuto wa kimapenzi, wamoto na
mtanashati, nitaolewa nae. Dada acha mawazo hayo, Mapenzi pekeake hayatoshi
kuwa ndoa. Ukweli ni kwamba, watu wengi wanaoitwa wavulana wenye mvuto wa
kimapenzi huwa hawabaki njia kuu hasa ikitokea wamesifiwa hata wakioa. Olewa na
mvulana kulingana na sifa ambazo zitadumu milele, mapenzi huwa hayadumu milele
ila ndoa huwa inadumu sasa ukitaka kudumisha mapenzi kwanza dumisha ndoa, nenda
kaulize wanawake waliokutngulia kuolewa.
7) MAGARI:
Wasichana wengi watashawishiwa na mvulana anayeendesha gari kubwa na la gharama
kubwa. Wengine hawana ndoto za kuwa na mtu ambaye hana gari. Ikiwa unataka
kujisumbua na ukose kupata wadada wazuri basi panda au endesha baiskeli kwenda
siku ya kwenda kumchumbia mwanamke unayempenda, utasikia. Wanawake wakisema
kama kaja na baiskeli ujue wewe utaishia kwenye mkokoteni, lakini ukweli ni
kwamba kijana ambaye ana GARI anaweza ASIKUJALI kabisa, kwababu maisha sio
GARI, ni kuolewa na mtu ambaye ATAJALI maisha yako ya baadaye.
8. PASPOTI
Wasichana wengi wanaolewa kwa urahisi na mtu yeyote aliye na pasipoti za
Marekani au Uingereza, Wasichana wengi wameharibu maisha yao katika harakati za
kutafuta mtu mwenye pasipoti ya kigeni wanaamini ndiye anayefaa kuoa.
9) UIMBAJI NDANI YA KWAYA:
Inachekesha baadhi ya wanawake wapo tayari kuolewa na baadhi ya wavulana kwa
sababu ni wazuri sana kwenye kuimba kwaya, au wale wanaoweza kupiga Sax foni,
keyboard, ngoma, tarumbeta na kuimba tenor na kupiga gitaa la Bass vizuri sana.
sijui kama wanataka kuanzisha bendi ya kwaya katika nyumba zao.
10) WATOTO WA MATAJIRI:
Watoto wenye wazazi Tajiri ni walengwa rahisi sana kwa wasichana wengi wachanga
si kwa sababu wanapendana nao hapana, ni kwasababu wanajua watapata pesa kwenye
uhusiano huo. Wengi wa wavulana hawa wanaotoka katika malezi tajiri ni watu wa
kustaajabisha sana, wanakuwa wajanja, wenye majivuno na huwa wanakuwa waume na
baba wabaya na wasiowajibika kwenye majukumu yao lakini wasichana hata hawajali
hilo, Wengi wa wasichana hawa huishi kwa kujutia uamuzi wao mbaya.
Usiolewe na mtu yeyote kwa sababu tu wazazi ni matajiri, oleweni
na mtu kwa jinsi alivyo na upendo wake wa kweli.
11) UONGOZI WA USHARIKA: Wanawake wengi wa Kikristo wako tayari kufa ili tu
waolewe na ndugu walio katika wasimamizi wa usharika wao wa Campus za kidini.
Wanapigana mpaka kuong'oa jino na kucha ili kupata usikivu wa ndugu hawa,
wengine hufikia hatua ya kutoa miili yao. Wengi wa wanawake hawa wanafikiri
kwamba wanaume bora kuliko wote ni watendaji wa Campus za kidini , wamesahau kwamba
RAISI WA USHARIKA HUENDA ASIWE NA MAKAZI HUKO MBINGUNI.
12) UTAALAMU CHUMBANI:
Mojawapo ya njia ya kijinga zaidi ya kufanya uamuzi wa nani wa kuolewa nae
wanawake huzingatia jinsi jamaa alivyo sura ya kuvutia au jamaa alivyokuwa bora
chumbani. Ukiegemeza uamuzi wako wa ndoa kwenye uwezo wa kupiga show wa
mwanaume; unaweza kujikuta unaishi kwenye ndoa na mwanaume play boy au malaya
badala ya kupata Mume aliye bora. Unaweza kuishia kuolewa na mwindaji wa
mademu, badala ya mpenzi wa kweli. Utaishia kuolewa na mgawaji wa mbegu za
kiume kwa wanawake wote na mwanaume wa jinsi hii ipo siku atalala na dada yako,
mfanyakazi wa ndani, marafiki zako wa karibu, wasichana wa jirani, sekretari
wake na chochote kile kinachovaa sketi.