(A) MBUSU MKEO NA KUMWAMBIA MANENO HAYA
“Mke wangu, asante kwa kuvumilia udhaifu wangu.
Asante kwa kuvumilia shida na matatizo yangu.
Asante kwa kufufichaa aibu zangu kwa watu.
Asante kwa kutokubaliana nami wakati mapendekezo yangu yapokuwa hayapo sahihi.
Asante kwa kutazama mpira pamoja nami ingawa wewe si shabiki wa mpira.
Asante kwa kushirikiana na mimi kwenye mambo ya kifedha tangu tulikipokuwa na
hali ya chini.
Asante kwa kujiweka katika hali ya kufanya tendo la ndoa hasa nikikuvutia
kingono. huwa Hunikatai.
Asante kwa kujaribu nafasi tofauti za mitindo tofauti ya kufanya mapenzi na
zile ninazozipenda na japo kuna wakati huwa haupendi vitu vipya tunavyofanya,
asante kwa kuwa mkweli kwangu.
Asante kwa kuniombea dua kwa mungu bila mimi kukuomba uniombee.
Asante kwa kusimamia nyumba yetu vizuri.
Asante kwa kuwa mama bora kwa watoto wetu.
leo Mimi ni mtu bora mbele ya watu kwa sababu yako Malkia wangu"
(B) MBUSU TENA MUMEO NA KUMWAMBIA
“Mume wangu nashukuru kwa kunipenda hata nikiwa nina kiburi.
Asante kwa kunipa msukumo kwenye maisha mpaka nakuwa mwanamke bora zaidi na kwa
kuniamini kuwa ninaweza kuwa.
Asante kwa kuniambia ukweli hata kama ni mchungu.
Asante kwa kuelewa na kuzitambua hisia zangu na kuwa mkono thabiti wakati wa
tendo.
Asante kwa kunipa moyo nisikate tamaa katika maisha yangu kipindi ninapohisi
kuchoka.
Asante kwa kurudi nyumbani kwa wkati hata wakati tunakuwa na hali ya
kutoelewana.
Asante kwa kunipa penzi hata kama staki najihisi ninataka.
Asante kwa kunifanya nijisikie kutamani tendo la ndoa.
Asante kwa kuwa mwanaume wa kutimizia mahitaji bila kukuomba.
Asante kwa kuwa baba bora kwa watoto wetu.
Asante kwa kutoifanya ndoa iwe kama jela kwangu.
Asante kwa kusikiliza hadithi zangu nyingi na kuwa rafiki yangu mkubwa.