1. Wanawake huwa hamjali mwanaume anayempenda na kumheshimu mama yake,
mnachofanya ni kumuona kama akili ya kitoto au humuita mtoto wa mama fahamu
kuwa kuwaheshimu wazazi wako hapa duniani ni daraja kubwa sana kuliko
udhaniavyo wewe
2. Wanaume tumeshau uungwana na kuchukulia kawaida bila kujali kuwa mwanamke
kuna muda anatakiwa anunuliwe make up na na avae vizuri, tunachofanya ni
kumfanya mwanamke aonekane kama hana akili timamu na asiye na maana na kusahau
kuwa anathaman kuliko mali tunazozikumbatia kikubwa unachotakiwa kufanya ni
kumtunza na kuthamin umbile lake na mwili wake.
3. Kweli dunia imeisha kuna Wanawake siku hizi sijui wameibukia wapi wao
hawajali waume zao hasa wale waume wanaopenda mpira au siasa, wanawake
wanachofanya ni pale mwanaume anapokuwa yupo bize na siasa au mpira wao hukaa
chini na kupanga mbinu za kutawala maisha ya waume zao ili tu wawe juu ya waume
zao.
4. Wanaume hatujali mwanamke anapopata mafanikio zaidi, tunachofanya ni kutumia
akili pale mwanamke akisha pata utajiri huwa tunafikiri kuwa pesa za mwanamke
tuhaki nazo ya kuwa huwa tunaamini huenda kahongwa na bwana mwingine huwa
hatuamini kuwa mwanamke naye anaweza kupambana na kuishia kuwadhalilisha wake
zetu.
5. Wanawake huwa hawajali mwanaume anayejiamini kwenye maisha, wanachofanya ni
pale ujasiri wa mwanaume unapochanganyikana na kiburi wao huwa hawezi kuamini
kuwa anaweza kujirekebishwa au kusema samahani akikosea.
6. Wanaume huwa hatujali wanawake wanaopenda kutazama sana vipindi vya
Televisheni na video za Instagram, maana wanawake hawa wanachofanya ni pale
wanapojizima data na kutaka kuishi maisha kwa kukopi wanachokiona kwenye TV au
mtandaoni.
7. Wadada wengi siku hizi hawajali wanaume zao hasa wakitaka penzi,
wanachofanya kila siku siku visingizio visivyo na pua wala mguu.
8. Wanaume hatujali mwanamke anayekuwa na marafiki wa kike, tunachofikiri ni
kwamba mwanamke huyo atakuwa anafichiwa siri zake za mahusiano yake na mashoga
zake hasa kupeana siri za uhusiano/ndoa yake na kudanganywa jinsi ya kutembea
na wanaue wengi.
9. wanawake hawajali mwanaume mwenye akili timamu na anayejielewa zaidi kuishia
kupendana na vjana wahuni vijana wa hovyo
10. mume/mke wako leo hii hajali wewe kuwa una imani flani muislam/mkristo,
mawazo ya mwenzi wako yanaweza kugeuza kila kitu kizuri cha neema kwenye
ndoa/mahuiano kama kati yenu kuna mwenye imani na kumtazamia Mola