TIBA 10 BORA ZA
MAHUSIANO
1. Upendo ni chaguo. unatakiwa kuwajibika kwenye chaguo lako. Hakuna asiyejua
kupenda. Mapenzi na vivutio ni vitu viwili tofauti, unaweza kuvutiwa na mtu
lakini mapenzi yakafifia mapema.
2. Furaha yako, utimilifu wa furaha unakutegemea wewe, kwa maana nyingine
usiruhusu mtu yeyote kukuamulia furaha yako wakati wewe unapaswa kuwa na furaha
yako kwaajili ya maamuzi yako, Kuwa huru kihisia. Usiwekeze hisia zako kwa mtu
yeyote bila kumtambua vizuri, kumbuka kwenye chaguo lako unapaswa kuwajibika
kfanya maamuzi yako mwenyewe
3. Kukabiriwa na changamoto. Watu wengi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali
katika mahusiano/ndoa zao kwa sababu ya hadithi nyingi za uongo, kupitia filamu
za Nollywood, Hollywood na Korean romance, kwanza mule kwenye filamu hakuna
ushahidi maalum juu ya wanachigiza Kumbuka hawa watu wanaoigiza kwa kutumia
script ya mtu, wakati mwingine huwa sio ukweli sasa bro, amka mapenzi
hayafananishwi na sinema.
4. Jiulize
Kwa nini unataka kuwa kwenye mahusiano hayo?
Kwa nini unataka kuolewa/kuoa?
5. Mpende utakayefunga naye ndoa, jifunze kuendesha gari aina ya upendo katika
mahusiano yako. Kumbuka, ukosefu wa mawasiliano sahihi huharibu mahusiano,
6. je huwa Unazungumzia nini katika mahusiano yako?
kila siku huwa unamwambia mpenzi wako maneno haya au ndiyo huyajuihebu mwambie
maneno haya basi nakukumbuka au unakuja lini umemis kuniona au umekula?
tafadhari kula kwa ajili yangu
7. Eleza maono yako, jadili ndoto zako, panga maisha yako ya baadaye na
unayempenda.
8. Usifanye mahusiano yako kuwa Miungu wako, Daima tengeneza ratiba
9. Usisukumwe kwenye mahusiano yako na vitu unavyoviona. Ndoa au uhusiano
hautasuluhisha shida zako, badala yake utakutana na shida zaidi ya hizo
ulizonazo (kama una shaka soma 1 Kor 7
10. Hakuna mwanaume/mwanamke anayetaka kuoa dhima hivyo usijifanye kuwa mmoja.
wakati mnatakiwa kuishi wawili
Kumbuka: Unawajibika kwa mustakabali wako kwa mwenyewe idhibiti wa maisha yako
.
USITEGEMEE MTU KWA
HISIA, FAHAMU SANA JUU YA HILO