AWatu wawili wanawezaje kuongozana pamoja wasipopatana? Ukweli ni kwamba, ndoa
nyingi huharibika kwa sababu ya kutoelewana pande zote mbili. Kutoelewana
kunaletwa ukosefu wa maelewano ya kushughulikia masuala yanayoathiri kila ndoa.
Kushindwa kukubaliana kutapelekea mume na mke kutafsiri mambo kwa njia tofauti
na kusababisha kuumiza hisia
Kubaliana na mwenzi wako kuhusu cha kufanya na usichofanya. Kuwa na sheria
hizi.
1. SHERIA ZA TENDO LA NDOA
Kubali kwamba unaweza kufanya tendo la ndoa kwa njia yenye msimamo, lakini pia
ukubaliane juu ya kile ambacho hautajaribu kufanya. Kwa mfano; hakuna ngono ya
kinume na maumbile, au kutopiga punyeto unapokuwa na wenzako, au hamtumii
filamu za ngono, kutofanya mapenzi wakati mwenzako yupo kwenye hedhi Kila
wanandoa wanapaswa. Kukubaliana juu ya kuwa na mipaka
2. SHERIA ZA SIMU
Kukubaliana jinsi ya kushughulikia mambo ya simu. Kwa mfano, hakuna kuzungumza
na watu wengine ifikapo saa 5 usiku kwa maana hiyo ni mida ya wewe kuwa karibu
na mwenzio, na hakuna usiri, hakuna haja ya kuondoka na kwenda kupokelea simu,
nje mjulishe mwenzi wako nani aliyepiga simu hiyo.
3. SHERIA ZA PESA
Kukubaliana jinsi ya kutumia pesa. Je, mtakuwa na akaunti ya benki ya pamoja?
Ni asilimia ngapi kila mmoja anaweza kutumia bila hitaji la kumjulisha
mwenzake? Nani wakulipa bili? Kuhifadhi. Kuwekeza. Hakuna kutoa pesa kwa wakwe
bila ridhaa ya pamoja
4. SHERIA ZA KUJA NYUMBANI
Unapaswa kufanya nini ikiwa utachelewa kurudi nyumbani? Kupiga simu? Je,
umechelewa kiasi gani kurudi nyumbani? Mwenzi wako hajali wewe kuchelewa kurudi
nyumbani mradi tu wamekubali. Ndoa sio ubinafsi bali ni ninyi wawili mnapaswa
kushiriki
5. KANUNI ZA KIJAMII
Kubali kutambulishana kwa marafiki zanu. Kubalianeni yakuwa na marafiki wa
karibu wa jinsia tofauti. Kubaliana ni marafiki gani wanafaa kubaki kwenye
maisha yenu. Kubalianeni ni mara ngapi marafiki wanaweza kuwatembelea. Nyumba
kwenu haipaswi kuja kwa kuvamia na marafiki. Kuna haja ya kuwa na mipaka
6. KANUNI ZA HABARI
Kubalini kutarifiana mahali kila mmoja alipo, hata ikiwa kwa maandishi rahisi
tu au meseji. Kubalianeni juu ya hitaji la kuambiana ratiba zenu binafsi kwa
siku. kila mtu amjulishe mwenzie
7. KANUNI ZA HASIRA
Kubalianeni juu ya nini cha kufanya wakati nyote wawili mnapokuwa mmekasirikia.
Je, unampa mwenzio nafasi? Ungependa kuondoka eneo la ugomvi kwa dakika kadhaa?
Je, unashughulikia suala hilo haraka? Kila mmoja Hakuna kwenda kulala bila
kuelewa na kupata mbinu ya Utatuzi wa migogoro yenu
8. KANUNI ZA KAZI NDANI
Kukubalianeni juu ya nani anafanya nini ndani ya nyumba. Hii itazuia yeyote
kati yenu kuhisi kama anafanya sana kazi kuzidi mwenzio
9. KANUNI ZA MITANDAO YA KIJAMII
Kubalianeni juu ya mambo ya kufanya na yasiyofaa ya mitandao ya kijamii. Kwa
mfano, kutokuwa na urafiki kwenye Facebook na mpenzi wako wa zamani, kutotoa
maoni mitandaoni kwa njia ya kuchukiza kwenye chapisho la watu wengine,
kutokuwa na tabia chafu, kutotangaza masuala ya nyumbani kwenye mitandao ya
kijamii.
10. KANUNI ZA KAZI
Kukubaliana juu ya mipaka ya kazi. Kwa mfano, ukirudi nymbani usilete kazi za
ofini kwako nyumbani, nini cha kufanya wakati kazi zako zinagongana? Nini cha
kufanya unapokuwa na saa tofauti za kazi? Wakati wa kuchukua likizo au siku za
kupumzika?
11. SHERIA ZA UZAZI
Kukubaliana jinsi ya kuwaadhibu watoto, nani anafanya nini, nani atawajibika
maswala ya Wazazi shuleni, je! watoto watakula chakula cha aina gani?
12. KANUNI ZA NAFASI ZA MTU
Kubalini kwamba wakati fulani kila mmoja wenu atataka muda fulani awe peke yake,
kufanya kazi au kutafakari au kupumzika tu. Kubali jinsi ya kumjulisha mwenzi
wako unapotaka dakika chache kwako. Mwenzi wako atakupa nafasi ikiwa unahitaji
Kukubaliana juu ya masuala haya muhimu huleta utulivu, amani na umoja.
Ikiwa ndoa yako ina machafuko kwa sababu ya ukosefu wa utaratibu. Bado
hujachelewa kufanya mazungumzo yatakayoleta makubaliano kuhusu masuala haya.