1. Epuka kuzungumza naye kwa ukali. Usimfanye ajisikie kama unashindana naye
2. Akikosea Usimseme kwa ukali kufanya hivyo ni kuhatarisha penzi lako
3. Mpe nafasi na muda wa kuzungumza. Usitawale mazungumzo, muda wote
4. Kuwa mkweli. Usiwe mwanamke wa kumsema maneno makubwa na kutukana. Matusi
yako yataghairisha mahusiano
5. Angalia sauti yako. Unaweza kuwa unasema jambo sahihi lakini sauti yako
ikawa haipo sahihi. Wakati mwingine ujumbe wako haupokelewi vyema kwa sababu ya
uwasilishaji wako
6. Usitoe mahaba ya kimya, hii huwa inamsukumo wa mbali
7. Usiwe mtu wa kutoa amri na maelekezo kama bosi wake kazini , atashindwa
kukuvumilia.
8. Dumisha furaha katika mazungumzo yako, hali hii humfanya abaki katika
mazungumzo yenu na mtaelewana
9. Zungumza naye mambo yanayochangamsha akili yake, yanayomfanya ajifunze; hali
hii inamfanya afurahie kuzungumza nawewe. namaanisha Mazungumzo ya watu wazima
10. Kamwe usiwe na mazungumzo ya kumsifu mtu mwingine kitendo hiki kitamshushia
hadhi hasa ukimzungmzia ex wako, baba yako, mchungaji wako, mtu mashuhuri au rafiki