1. Mthamini mwanaume anayempenda mama yake mzazi hii inamaana. Amelelewa vizuri
huko alikotoka
2. Mthamini mwanaume anayependa kusoma, maana atashinda kila aina ya mitihani.
huyu ni mwenye hekima
3. Mthamini mwanaume mcheshi. Hutajuta kuishi nae maana hachoshi
4. Mthamini mtu anayewajari wageni na wasio wageni bila kujari huyu ni nani
anacheo ganina huyu anaheshima. na moyo mwema
5. Mthamini mwanaume anayekupa muda wa kukusikiliza. utakuwa unaeleweka kila
wakati kwake
6. Mthamini sana mwanamume ambaye wazo lake la kujifurahisha kwako linajenga.
huyu anakuwa Amekomaa kiakili
7. Mthamini mwanamume anayewajibika kifamilia na yupo tayari juu ya kile
unachotaka wewe. Muda wako hautapotea bure
8. Mthamini mtu anayemheshimu baba yake mzazi bila kujali jinsi baba yake
alivyo. huyu Amejifunza uanaume wa kweli
9. Mthamini mwanaume ambaye hamtusi ex wake au ex wako hata kama mliachana kwa
fujo. huyu Ni mtu anayeingia kwenye mapenzi kwa sababu sahihi
10. Mthamini mwanaume anayekuhitaji. hatakuacha njiani
11. Mthamini mwanaume anayeupa sababu ya kumpenda, anatunza siri juu ya kuona
uchi na udhaifu wako. huyu Anakuamini
12. Mthamini mtu anayekubali kurekebishwa na kubadilisha mfumo wake akikukosea.
Atakuwa mtu bora wa kukupenda
13. Mthamini mwanaume anayekuombea. Anajua wewe ni zawadi toha kutoka kwa Mungu
14. Mthamini mwanaume anayewaheshimu wanawake wengine. huyu Atakuheshimu zaidi
15. Mthamini mwanaume anayewapenda watoto wako huyu ni mfano wa baba bora. Mtu
huyu atakuwa na urithi wa heshima
16. Mthamini mtu mwenye maono. Atakupa changamoto na kukujenga, huyu anajua
anakokwenda
17. Mthamini mwanaume mwenye marafiki wazuri. Unaweza kuijua tabia ya mwanaume
wako kupitia marafiki zake.
18. Mthamini mwanaume anayethamini urafiki kuliko penzi. huyu Atakuwa mwaminifu
kwako
19. Mthamini mwanaume anayevutiwa na ndoto zako. huyu Anajali maisha yako ya
baadaye
20. Mthamini mwanaume anayeheshimu maamuzi yako asiye kurupuka. huyu Anakuona
kama mwenzi wa maisha yake
21. Mthamini mwanaume anayekusahihisha unapokosea na kukutia moyo na kukupa
msukumo unapofanya jambo zuri. Anaona uwezo wako na hatapumzika hadi uwezo wako
utimizwe. Mtu huyo ni mlinzi wa maisha yako
22. Mthamini mtu ambaye amekuwa thabiti kwenye mtazamo wake. huyu Unaweza
kumtegemea
23. Mthamini mtu anayefanya kazi kwa bidii, anajituma na ana bidii hata akiwa
na kidogo. Huyo mwanaume anaenda sehemu na siku moja atakufanya ujivunie
24. Mthamini mwanaume ambaye haopotoshwi na wanaume wengine wanapoona uzuri
wako na kukutamani. huyu Ni mtu salama kwako