JINSI YA KUWA MKE MWENYE UPENDO NA BORA
1. Kumbuka kwamba mapenzi si jukumu la mume peke yake
2. Mpongeze mumeo akiwa amevaa vizuri na ananukia vizuri
3. Gusa paja la mumeo wakati anaendesha gari au ameketi karibu hasa unapotaka
kumwambia jambo.
4. Wakati mwingine jaribu kutumia simu kumchombeza kwa maneno ya chumbani
kiuchokozi
5. Chezea vidole vyake wakati nyinyi wawili mna mazungumzo ya kwenu binafsi na
kujadiri maisha
6. Jaribu Kumbembeleza na kuweka kichwa chake kifuani mwako mkiwa wawili
kitandani
7. Weka mkono wako kwenye mikono yake kama Malkia anayejua msimamo wake kwenye
ndoa
8. Wakati mwingine vaa Mavazi yanayoweza kumsisimua mumeo hasa akiukuona umevaa
katika chumba cha kulala
9. cheza nae ikiwa muziki basi cheza kwaajili yake na pia usisahau kumtania
10. Mwambie mambo yote ya chumbani unayoyapenda pamoja na mitindo unayoipenda
ya mapenzi na ile unayotaka kumfanyia
11. jaribu kumsifia kwa ustadi wake akiwa kifuani kwako wakati wa mizagamuano
na jinsi alivyofundi wa mapenzi anayofanya yanayokupa raha. Mwambie jinsi
anavyokutia wazimu
12. Mtoe out kwa tarehe, usisubiri kila wakati apange yeye na sio kila siku
mpate chakula nyumbani akti mwingine mnaenda kula nje
13. kumbusu, sio tu kwenye midomo bali pia kwenye mashavu yake, paji la uso
wake, vidole vyake.
14. Jitolee kumtumikia kila saa uwe na tabasamu usoni na umtunze
15. Mwite majina maalum "Mfalme wangu", "Mpenzi",
"Asali"
16. Jiamini na kuwa wewe mwenyewe, fanya mambo makubwa ukiwa mtu binafsi.
Itamsisimua atajivunia kuwa na wewe
17. Mzungumzie sana hadharani, mtie moyo faraghani anapokuwa kwenye nyakati
ngumu
18. Tafuta nafasi jinsi anayopenda akiwa kwenye michanganyo na umfanyie
hivyohivyo mara kwa mara
19. Msaidie kuvaa na kuvua nguo zake, tai yake, koti lake na viatu
20. Wakusanye watoto na umsemee maneno mazuri kwa watoto katika kumthamini,
mfanye ajisikie kuwa wa thamani akiwa nyumbani kwake bila kujali hali yake ya
kifedha
21. Ukiwa na chochote Mnunulie zawadi anazozipenda
22. Andaa chakula anachopenda au muulize angependa kula nini
23. Mwambie unampenda. Wanaume wanapenda kuthibitishwa pia. Mwambie pia kile
unachopenda kwake
24. Muulize siku yake imekuwaje? au ameshindaje kazini? Onyesha jinsi
unavyomthamini na kumtunza
25. Fanya harakati za kuanzisha uchokozi mkiwa kitandani usisubir aanze yeye
kila siku
26. Muombee dua kwa mungu abarikiwe. Wanawake wa maombi ni wa kimapenzi
27. Hudhuria mahitaji yake bila yeye kumuuliza kama vile kumtengenezea kikombe
cha chai/kahawa anapofanya kazi.
Kwa sababu mmekaa pamoja kwa miaka mingi haimaanishi kwamba utaacha kumfanya
ajisikie wa pekee. Ulimvutia na kumfanya ajione wa thamani na ndiyo maana
akakufuata ili akupate, uendelee kuvutia na kumthamini ili uendelee naye;
unapofanya hivyo, atatamani uwepo wako na kukupa kilicho bora zaidi. Mwanamke
anayempenda mumewe, hujenga nyumba yake