JINSI YA KUMFANYA MWANAUME AKUPENDE
Je, umechoka kuchukizwa na wanaume? Wanakuchumbia tu halafu wanakuacha? Haya ni
mambo unayoweza kuyafanya ili kumfanya mwanaume akupende na hata kukuchumbia,
kukuoa na kushikamana nawe milele...
1. HESHIMA:
Jifunze kuwaheshimu wanaume kutoka ndani ya moyo wako. Hakuna mwanaume
anayeweza kumpinga mwanamke anayemuonyesha heshima na nidhamu kubwa.
2. SHUKRANI:
jifunze kuthamini kila jambo jema ambalo wanaume wanakufanyia. Mwanamke
anayejua jinsi ya kumthamini mwanamume
3. UPENDO WA DHATI:
wanaume wanapenda kusifiwa. kuhusu Akili yake, mafanikio, sura nzuri na kazi
ina maana kubwa kwake
4. SIFA:
kila anapofanya jambo la kawaida, msifu sana. Usimbembeleze, wanaume wanachukia
kubembelezwa kupitiliza, wanapendani nidhamu.
5. MALENGO:
Usiwe na tamaa sana ya kuolewa. Wanaume wajanja sana wanaweza kunusa kwa mbali
na kukusoma lengo lako na watakukwepa watakaa mbali na wewe. Hakuna anayetaka
mwanamke anayekata tamaa.
6. KUJIAMINI :
Njia moja ya uhakika ya kumfanya mwanaume akufuate ni kujiamini. Wanawake
wanaojiamini huwafanya wanaume wapende kuwa nao. kuna muda Unajifanya kama
zawadi kubwa ambayo inahitaji juhudi za ziada ili kuipata. Wanaume wanapenda
vitu vigumu ili wavipate kwa kishindo. Kujiamini kwako kunamfanya atake
mwanaume atamani "kushinda" juu yako wewe.
7. MAISHA:
kuwa na kazi, biashara, maono, malengo, ndoto nzuri. Wanaume hupenda wanawake
wanaofanya kitu cha thamani huku maisha yao yanasonga usipende kuendekeza
urembo kila saa usipende kulala huku ukingoja vya kuletewa. Hakuna mtu
anayetaka kuoa mwanamke wa namna hiyo
8. URAFIKI:
wanawake wenye urafiki na wanaume huwavutia wanaume kwa urahisi. Jifunze
kucheka, fanya ucheshi wakati mwingine, shiriki mazungumzo ya watu wenye akili
na ikiwa kucheka basi cheka kweli., usiyachukulie maisha kwa uzito sana. Kuwa
na furaha mara nyingi
9. UJANA:
Ukiendelea kujiweka kama mzee. Utakuwa single kwa muda mrefu bila kupata mwenzi
wako.
10. UREMBO:
Unatakiwa kuwa kuwa kama akina Agbanidarego, Aishwarya Rai, Kim Kardashian,
Omotola Jolade Au Angelina Jolie kabla ya kuonekana mrembo. Kuwa msafi kwanza,
vaa nguo zinazokutosha, ondoa harufu mbaya mwilini. nywele zako ziwke kwenye
mtindo unaofaa ambayo unaendana na kichwa chako sio. Epuka midomo kuicha iwe
mikavu. Jifunze kupunguza mwili na kupiga mswaki nyusi zako, epuka harufu ya
mdomo, tumia manukato sahihi. Jifunze kuonekana mtamu na mzuri wakati wote.
11. MWANAMKE:
kuwa kama anavyotakiwa kuwa mwanamke na sio kama Tomboy. Jifunze kukaa kimya,
kuzungumza, kutembea na kucheka kama mwanamke. Kuwa wa kike, kuwa msichana, ili
mwanaume ajisikie kama yuko na mwanamke, sio mwanaume!
12. NAFSI:
Usijilazimishe kuiga maisha kwa watu. maana Uongo na udanganyifu unaumiza
haraka kuliko kitu kingine chochote. Kuwa mhalisia. Ikiwa mwanaume amakupenda
basi atakupenda jinsi ulivyo.
13. TENDO LA NDOA:
Bado utakutana na mwanamume ambaye atataka penzi mapema kbla hamjajuana zaid,
hapa ndiyo unatakiwa ujiamini, mwenye akili na msafi kingono. Jifunze kuuzuia
wako kwenye matamanio kuwa na heshima. Kataa kuguswa mapema na mwanaume. hii
Itaongeza heshima yake kwako na atakuona kama mwanamke anayestahili kuwa naye,
anayestahili kumpata kwa kishindo, anayefaa kufuatiliwa na anayestahili kuolewa
naye.